Warioba: CCM ijiandae kuwa chama cha Upinzani

Mh CCM ndio chama pekee nchi hii hata kada wenu wa chadema amekubali hilo , wewe hukumsikia Shibuda?

Acha pombe za mchana wewe, Shibuda yule ni gamba tu kama ulvyoo magamba sugu wewe msiyeamini CCCMMM imekwisha poteza uelekeo , ajali ya ccccmmm hiyoo inakujaa!!!
 
Ni ccm na mawazo yao. Mwl. Nyerere aliwahi sema: If u break a principle that same principle shall break u. Ccm know this better than any one of us.
Let ccm die n leave us living in peace n not in pieces. I do not know anybody within ccm who can be our Musa 2 get us out of the hands of Pharao.
 
Ni ccm na mawazo yao. Mwl. Nyerere aliwahi sema: If u break a principle that same principle shall break u. Ccm know this better than any one of us.
Let ccm die n leave us living in peace n not in pieces. I do not know anybody within ccm who can be our Musa 2 get us out of the hands of Pharao.

Huo ndio ukweli, na tatizo wameshachelewa. Wangechukua hatua tangu hayati Kolimba alipoangalisha kwamba CCM imepoteza dira haya yanayotokea leo yasingekuwepo.
 
Acha pombe za mchana wewe, Shibuda yule ni gamba tu kama ulvyoo magamba sugu wewe msiyeamini CCCMMM imekwisha poteza uelekeo , ajali ya ccccmmm hiyoo inakujaa!!!


Anayefikiria porojo za Shibuda nampa pole, maana Shibuda anafahamika ni vuvuzela, ndio maana viongozi wa Chadema wanadharau kauli zake, ni kupoteza muda kuhangaika na kauli za Shibuda badala ya kuhangaika na uimarishaji wa chama.
 
CCM yanusa anguko 2015
Baada ya Halmashauri Kuu ya Taifa (Nec) ya CCM kubariki mjadala wa kuhoji mahakamani matokeo ya uchaguzi wa rais, wasomi wameibuka na kudai kuwa hali hiyo imetokana na chama hicho kusoma alama za nyakati sambamba na kuanza kunusu harufu za anguko lake.

Mbali na kuridhia kuhoji mahakamani matokeo ya rais, kikao cha Nec, kilichomalizika mwanzoni mwa wiki iliyopita mjini Dodoma chini ya Mwenyekiti wake, Rais Jakaya Kikwete, pia kilibariki majadala wa mgombea binafsi, madaraka ya rais, utaratibu wa uchaguzi wa Rais wa Jamhuri ya Muungano pamoja na mambo yanayosababisha kuwepo kero za Muungano.

Baraka hizo za Nec zinaashiria kuwa chama hicho tawala kimesoma alama za nyakati na kutambua kuwa ipo siku kinaweza kung'oka madarakani na kuwa chama cha upinzani, hivyo kuwa na haki ya kikatiba kulalamikia matokeo ya rais au vyovyote vile.

Kwa muda mrefu, vyama vya siasa, wanaharakati na watu wa kada mbalimbali, wamekuwa wakihoji kinga hiyo ya rais inayomfanya asiweze kushitakiwa wakati akiwa madarakani na hata baada ya kumaliza muda wake.

Lakini jana, wakati wakizungumza na Mwananchi Jumapili kwa nyakati tofauti, wasomi hao wamesema kuwa huenda ubadhirifu wa mali za umma na matendo mengine yasiyo ya kizalendo, yakapungua kwa kuwa kama suala hilo likijadiliwa na Watanzania wakaridhia liingizwe katika katiba mpya, rais atakuwa makini zaidi katika utendaji wake wa kazi.

Vile vile, wamesema kuhoji madaraka ya rais kutaongeza uwajibikaji na uzalendo kwa rais atakayekuwa madarakani au atakayemaliza muda wake kwa kuhofia kuburuzwa mahakamani.

Hata hivyo, walionya kuwa lazima kuwe na utaratibu maalumu ili kuzuia kila mtu kumshitaki rais aliyemaliza muda wake.

Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Dk Kitila Mkumbo, alisema kuwa kitendo cha CCM kuridhia kuwepo mjadala huo, kinaonyesha wazi kuwa chama hicho tawala kimeshasoma alama za nyakati na kwamba kuna siku kitakuwa cha upinzani.

"Labda wamesoma alama za nyakati, jambo hili kwa muda mrefu limekuwa likilalamikiwa na wapinzani. Chama chochote cha siasa kinaweza kuwa cha upinzani hakuna mwenye hati miliki katika utawala wa nchi," alisema Dk Mkumbo.

Mhadhiri mwingine wa UDSM, Profesa Gaudence Mpangala, alisema kuwa suala la rais kutoshitakiwa, liliibuka zaidi baada ya kushamiri kwa mfumo wa vyama vingi na kwamba ilikuwa hivyo ili kuepusha migogoro ya kisiasa.

Alisema kuwa katika misingi ya kidemokrasia, rais anaweza kushitakiwa kwa kuwa wengi wamekuwa wakifanya mambo kinyume na taratibu za nchi husika na kwamba kitendo cha kuwepo sheria ambayo itawafanya washitakiwe, kitasaidia kuwajibika zaidi.

"Kinga kwa rais ina uzuri wake na kama nchi inaamua kuwa na sheria hiyo basi lazima kuwe na sheria ya kulinda ushindani wa kisiasa…, hii itasaidia kwa kuwa hali ikiwa tofauti kila mtu atakwenda mahakamani," alisema Prof. Mpangala.

Alisema kuwa mfumo wa vyama vingi umejaa vurugu za kila aina, kwamba demokrasia ya mfumo wa vyama vingi inatakiwa kuboreshwa ili kwenda sambamba suala hilo.

Prof. Tolly Mbwete wa Chuo Kikuu Huria cha Tanzania (OUT), alisema kuwa hali hiyo itasaidia kwa kuwa itakuwa vigumu kwa rais kufanya madudu wakati wa utawala wake.

"Hii itasaidia kwa kuwa hawatafanya tena madudu…, hawatakuwa wakivurunda tena katika utawala wao kwa kuhofia kuhukumiwa na sheria hii, ni utaratibu mzuri" alisema Prof. Mbwete.

Mambo mengine ambayo Nec ilibariki yajadiliwe ni Muundo wa Bunge na Baraza la Wawakilishi, uwepo wa Baraza la pili la Kutunga Sheria, ukomo wa idadi ya wabunge, mfumo wa Mahakama na nafasi ya Rais wa Zanzibar katika uongozi wa Jamhuri ya Muungano.
 
CCM kimeanza kuweka mazingira ya kuwa chama kikuuu cha upinzani bungeni kuanzia uchanguzi mkuu 2015. Katika harakati hizo, mbinu mbali mbali za kujiandaa kuwa boss wa pande ya upinzani zimeeendelea kuwa wazi ikiwa ni pamoja na kujiandaa kimtindo kuja kupinga matokeo ya urais 2015 mara tu baada ya CDM kutua pale mjumba mkuu na mtakatifu wa matakatifu wa nchi hii(Ikulu).






Source: MwanaHalisi
 
na kule zenji CUF wanasema hawakubali. sasa magamba watakimbilia wapi jaamani, nawaonea huruma sana. na wakikaa vibaya CUF wanaweza kuwapiku hata huku Tanganyika. JIWE WALILOLIKATAA WAASHI LIMEKUWA JIWE KUU LA PEMBE.
 
Heeh! ..wajiandae tu make maamuzi ya mwisho na mahakama kubwa kuliko zote ni nguvu ya umma.
 
Watanzania tumeendelea kuwa maskini na hali nchi yetu ina kila rasilimali. CCM siku zao zinahesabika ndugu zangu.
 
CCM inapofanya kazi ya chama cha upinzani, nani atafanya kazi ya chama tawala?

Kitila Mkumbo

Toleo la 243
13 Jun 2012













KATIKA mfumo wa demokrasia ya vyama vingi, kazi ya chama tawala na vyama vya upinzani zinatofautiana sana. Kazi kubwa ya chama tawala ni kuisimamia serikali yake itekeleze yale iliyoahidi kwa wananchi wakati wa kampeni za uchaguzi na kuhakikisha kwamba mambo yaliyomo katika ilani yake ya uchaguzi yanaingia katika mfumo wa kisheria na sera za nchi.
Kwa hiyo katika majukwaa ya kisiasa chama tawala hujitahidi kuonyesha kwamba wanatekeleza waliyoahidi na huonyesha kwamba kweli mambo yanaenda vizuri kuliko kabla hakijaingia madarakani. Kwa hiyo, kazi ya chama tawala baada ya uchaguzi ni kutenda kwa sababu wana nyenzo za kutendea kazi, yaani serikali.
Kupitia utekelezaji wa mambo mbalimbali yaliyopo katika ilani yake, chama tawala hujitahidi kuonyesha mafanikio na kujenga hoja ya kuwafanya wananchi waliokichagua kuendelea kujivunia na kufurahia chaguo lao, wakati huo huo kikionyesha kwamba kama wangechagua wapinzani mambo yangekuwa mabaya.
Kwa hivyo, kazi ya chama tawala ni kusimamia utekelezaji na huhukumiwa kwa vitendo vya serikali yake. Chama tawala wakati wote huhakikisha kuwa harakati za vyama vya upinzani haziwatoi nje ya mstari wa kutekeleza sera zake.
Chama cha upinzani, kwa upande mwingine, kazi yake kubwa ni kuweka wazi udhaifu wa chama kinachotawala kwa kuonyesha wananchi kwamba mambo hayaendi kama walivyoahidiwa na kwa hivyo, walidanganywa.
Kwa kifupi, ni kazi ya chama cha upinzani kuwafanya wananchi wajutie kukichagua chama kilichopo madarakani na kuwajengea uelewa, ufahamu na ujasiri wa kukitoa chama tawala katika uchaguzi mwingine utakaofuatia. Chama cha Upinzani hujitahidi kuonyesha kwamba kama wangechaguliwa wao mambo yangekuwa mazuri zaidi kuliko ilivyo sasa.
Kwa hivyo, kazi ya chama cha upinzani ni kuuza maneno na huhukumiwa kwa maneno wanayoyasema. Wakati wote wakisubiri uchaguzi mwingine chama cha upinzani hujitahidi kupita huku na kule kuonyesha udhaifu wa serikali iliyopo na kuonyesha kwamba, kina sera na mipango bora zaidi ya kuipeleka nchi mbele zaidi.
Ni kazi ya chama cha upinzani kuhakikisha kwamba chama tawala kinatoka nje ya mstari na kuanza kuhangaika kujitetea. Dalili za mafanikio ya chama cha upinzani ni pale ambapo unaona chama tawala kinaanza kulialia na kujitetea.
Kama wewe ni mgeni katika nchi hii na kama uliingia nchini kwa mara ya kwanza siku ambapo CCM walifanya mkutano pale Jangwani (Jumamosi ya Juni 9, 2012), ungeamini kwamba chama hiki tawala ama ndio kwanza kilikuwa kimeingia madarakani kwa mara ya kwanza au kilikuwa kinaomba ridhaa ya kuchaguliwa.
Mawaziri waliendeleza kasumba sugu ndani ya CCM ya kumwaga ahadi ambazo wanajua hazitekelezeki. Mwakyembe anautangazia umma kwamba anaomba apewe miezi mitatu tu ili aweze kumaliza matatizo yaliyopo katika Wizara ya Uchukuzi.
Mwakyembe anataka tuamini kwamba suluhu ya matatizo ya sekta ya uchukuzi anayo mtu mmoja tu anayeitwa Waziri, na kwamba mawaziri wote waliopita katika wizara hii walishindwa kutatua matatizo yale isipokuwa sasa tumepata ‘mwarobaini’ na mambo yatakuwa mazuri. Anataka tuamini kwamba, Mwakyembe ndiyo wizara na wizara ndiyo Mwakyembe!
Mwakyembe anaelewa vizuri kwamba ujenzi wa reli katika nchi hii umekwamishwa na serikali kushindwa kuwekeza fedha za kutosha katika sekta hii, na sote tumesikia taarifa kwamba katika mwaka wa fedha unaoisha ni chini ya asilimia 40 tu ya fedha iliyotengwa kwa ajili ya kuendeleza miundombinu ya reli ndiyo iliyotolewa na hazina.
Sasa Mwakyembe ana miujiza gani ya kutatua matatizo ya wizara hii katika miezi mitatu aliyoomba apewe? Mwakyembe na mawaziri wengine wapya wanaelekea kuamini kwamba ili waonekane wanachapa kazi ni lazima wafukuze watu kazi na watangaze kwa sauti kubwa kwamba tumewafukuza!
Tunarudia tena kuwaasa kwamba matatizo ya kiutawala katika nchi yetu na nchi nyingine kadhaa za kiafrika ni ya kimfumo na hayawezi kutatuliwa kwa kufukuza wafanyakazi tu. Tatizo letu ni kwamba tumekuwa tukifanya bidii ya kuimarisha watu badala ya kuimarisha mifumo ya kuwadhibiti viongozi.
Matokeo yake kiongozi mmoja anaweza akaja na jambo jema lakini likafa mara yeye atakapoondoka katika wizara husika. Na bahati mbaya mawaziri wa CCM hawakai muda wa kutosha katika wizara moja kabla hawajanyang’anywa uwaziri au kuhamishiwa wizara nyingine.
Tunamkumbusha Mwakyembe kwamba miezi mitatu aliyoomba itaisha mwezi wa tisa mwaka huu, na tutawaomba wabunge wamkumbushe kutoa taarifa yake katika Bunge la Novemba.
Mawaziri na viongozi wengine wa CCM walijikita katika kukipiga vijembe chama kikuu cha upinzani nchini, CHADEMA. Kimsingi wengi walikuwa wanajitetea na kulialia. Kwamba ugumu wa maisha umesababishwa na kupanda kwa gharama za mafuta duniani kote na kwamba CCM haipaswi kulaumiwa kwa hilo ni utetezi usio na maana yeyote.
Hakuna mtu anayesema kwamba ni lazima utatue matatizo uliyosababisha wewe tu. Matatizo ni matatizo tu, na unapokuwa kiongozi yakupasa kujua kwamba upo hapo ulipo kwa ajili ya kushughulikia matatizo, sio kujitetea.
Kuilaumu CHADEMA kwa kuibua matatizo yaliyopo na kuonyesha udhaifu wa serikali iliyopo ni kujaribu kuwazuia wasifanye kazi yao ya kuwa chama cha upinzani. Ni muhimu kusisitiza hapa pia kwamba kazi ya chama cha upinzani sio kuisaidia serikali ijirekebishe.
Chama cha Upinzani kikiamua kufanya kazi ya kuirekebisha serikali maana yake ni kwamba kimeamua kuendelea kuwa chama cha upinzani milele. Kazi ya kuirekebisha serikali ni kazi ya taasisi za kiraia (NGOs) ambazo hazina malengo ya kutawala. Na isitoshe serikali ina vyombo tele vya kuishauri na kuirekebisha.
CCM wanapouza maneno na kulalamika barabarani badala ya kuisimamia serikali yao itekeleze ahadi zake ni kuzidi kupoteza mwelekeo, na kimsingi wanafanya kazi ya upinzani.
Kuendelea kutoa ahadi wakati upo madarakani ni kutokuelewa kazi za chama tawala. Ndiyo maana sasa tunauliza, CCM inapoamua kufanya kazi ya upinzani, nani atafanya kazi ya chama tawala? Tutafakari.
 
Asante sana kwa kujitolea bure kutoa Tuition kwa CCM, hawa mamjamaa ni viziwi, vipofu, wakaidi na wasioelimika. Lakini 2015 sio mbali, wataanza kuona utamu wa kuwa chama cha upinzani.
 
Kisa kirefu lakini hakina maana yoyote. Huyu mwandishi ameenda shule kweli?
 
Inafurahisha kama haichekeshi kuona chama kilichoko madarakani kinakuwa chama pinzani kwa vyama vya upinzani!!

Nipofurahia ni pale tu CHADEMA inapokuwa katika harakati zake zakawaida za kila siku nyuma CCM wanahaha wakijibu mapigo ya
CHADEMA inamaana CCM mmeishiwa ubunifu wakuwa na sera nzuri za kuwashawishi wananchi ili wawakubali?

Mwisho wake nabaki kufuta nyayo za mahali alipopita CHADEMA ili wananchi wasifate lakini kumbe wananchi awaangalii nyayo wafata ngurumo!!

Ukisikia kuchoka kwa siasa ndo huko......kaeni chonjo! Saa ya ukombozi inajili.
 
Back
Top Bottom