Warioba: CCM ijiandae kuwa chama cha Upinzani

ccm bila dola itakufa tu. Miaka 15 baada ya kupoteza dola ccm inaweza kuwa inasomwa kwenye historia.
Huyo anayesema miaka elfu 10 hazingatii hali ya sasa. 2015 ccm itashindwa lakini italazimisha kuwa imeshinda, kama wananchi wakichoka kuibiwa then umwagaji damu utatokea, na huo hauwezi kuchukua miaka yote hiyo. Kama 2015 wananchi watanyamaza, but 2020 hawatanyamaza
 
cc1xv.jpg

Katika kikao cha Halmasahauri Kuu CCM kilichofanyika Dodoma hivi karibuni, kimeibua mambo mapya ambayo yanapingana na msimamo wa chama hicho kuhusu masuala mazito ya kuingizwa kwenye katiba mpya ambapo hapo awali hawakulibaliana nayo.

Moja ya mambo hayo ni:

  1. Kikwete kupendekeza kuhoji mahakamani matokeo ya uchaguzi wa Rais.
  2. Mkutano kupendekeza uwezekano wa serikali tatu.
  3. Kupunguza madaraka ya Rais
  4. Tume huru ya uchaguzi
  5. Mgombea binafsi
  6. Kero za Muungano.
  7. Na baadhi ya mengine ambayo kwa pamoja yamefikia mapendekezo17.

Tafsiri ya haraka ni kwamba CCM imeshaona dalili za wazi kupoteza sifa ya kuendeleza ushindi wa kushika dola, na hivyo kukubali kuwa chama cha upinzani. Kwa kuhofia chama kingine kushika serikali, wako tayari kuafiki yale ambayo yamekuwa yakilalamikiwa na wapinzani kwa siku nyingi lakini CCM ilitetea kwa nguvu zote na kuweka pamba masikioni siku zote.

Kwa nini CCM haikuona umuhimu wa mambo hayo awali wakati yakilalamikiwa na vyama vya upinzani nchini?


CCM yanusa anguko 2015
Baada ya Halmashauri Kuu ya Taifa (Nec) ya CCM kubariki mjadala wa kuhoji mahakamani matokeo ya uchaguzi wa rais, wasomi wameibuka na kudai kuwa hali hiyo imetokana na chama hicho kusoma alama za nyakati sambamba na kuanza kunusu harufu za anguko lake.

Mbali na kuridhia kuhoji mahakamani matokeo ya rais, kikao cha Nec, kilichomalizika mwanzoni mwa wiki iliyopita mjini Dodoma chini ya Mwenyekiti wake, Rais Jakaya Kikwete, pia kilibariki majadala wa mgombea binafsi, madaraka ya rais, utaratibu wa uchaguzi wa Rais wa Jamhuri ya Muungano pamoja na mambo yanayosababisha kuwepo kero za Muungano.

Baraka hizo za Nec zinaashiria kuwa chama hicho tawala kimesoma alama za nyakati na kutambua kuwa ipo siku kinaweza kung'oka madarakani na kuwa chama cha upinzani, hivyo kuwa na haki ya kikatiba kulalamikia matokeo ya rais au vyovyote vile.

Kwa muda mrefu, vyama vya siasa, wanaharakati na watu wa kada mbalimbali, wamekuwa wakihoji kinga hiyo ya rais inayomfanya asiweze kushitakiwa wakati akiwa madarakani na hata baada ya kumaliza muda wake.

Lakini jana, wakati wakizungumza na Mwananchi Jumapili kwa nyakati tofauti, wasomi hao wamesema kuwa huenda ubadhirifu wa mali za umma na matendo mengine yasiyo ya kizalendo, yakapungua kwa kuwa kama suala hilo likijadiliwa na Watanzania wakaridhia liingizwe katika katiba mpya, rais atakuwa makini zaidi katika utendaji wake wa kazi.

Vile vile, wamesema kuhoji madaraka ya rais kutaongeza uwajibikaji na uzalendo kwa rais atakayekuwa madarakani au atakayemaliza muda wake kwa kuhofia kuburuzwa mahakamani.

Hata hivyo, walionya kuwa lazima kuwe na utaratibu maalumu ili kuzuia kila mtu kumshitaki rais aliyemaliza muda wake.

Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Dk Kitila Mkumbo, alisema kuwa kitendo cha CCM kuridhia kuwepo mjadala huo, kinaonyesha wazi kuwa chama hicho tawala kimeshasoma alama za nyakati na kwamba kuna siku kitakuwa cha upinzani.

"Labda wamesoma alama za nyakati, jambo hili kwa muda mrefu limekuwa likilalamikiwa na wapinzani. Chama chochote cha siasa kinaweza kuwa cha upinzani hakuna mwenye hati miliki katika utawala wa nchi," alisema Dk Mkumbo.

Mhadhiri mwingine wa UDSM, Profesa Gaudence Mpangala, alisema kuwa suala la rais kutoshitakiwa, liliibuka zaidi baada ya kushamiri kwa mfumo wa vyama vingi na kwamba ilikuwa hivyo ili kuepusha migogoro ya kisiasa.

Alisema kuwa katika misingi ya kidemokrasia, rais anaweza kushitakiwa kwa kuwa wengi wamekuwa wakifanya mambo kinyume na taratibu za nchi husika na kwamba kitendo cha kuwepo sheria ambayo itawafanya washitakiwe, kitasaidia kuwajibika zaidi.

"Kinga kwa rais ina uzuri wake na kama nchi inaamua kuwa na sheria hiyo basi lazima kuwe na sheria ya kulinda ushindani wa kisiasa…, hii itasaidia kwa kuwa hali ikiwa tofauti kila mtu atakwenda mahakamani," alisema Prof. Mpangala.

Alisema kuwa mfumo wa vyama vingi umejaa vurugu za kila aina, kwamba demokrasia ya mfumo wa vyama vingi inatakiwa kuboreshwa ili kwenda sambamba suala hilo.

Prof. Tolly Mbwete wa Chuo Kikuu Huria cha Tanzania (OUT), alisema kuwa hali hiyo itasaidia kwa kuwa itakuwa vigumu kwa rais kufanya madudu wakati wa utawala wake.

"Hii itasaidia kwa kuwa hawatafanya tena madudu…, hawatakuwa wakivurunda tena katika utawala wao kwa kuhofia kuhukumiwa na sheria hii, ni utaratibu mzuri" alisema Prof. Mbwete.

Mambo mengine ambayo Nec ilibariki yajadiliwe ni Muundo wa Bunge na Baraza la Wawakilishi, uwepo wa Baraza la pili la Kutunga Sheria, ukomo wa idadi ya wabunge, mfumo wa Mahakama na nafasi ya Rais wa Zanzibar katika uongozi wa Jamhuri ya Muungano.
 
Tatizo la ccm wana uroho wa madaraka. Tuliwashauri hapa wakati wa uchaguzi 2010 kuwa kama wanataka kubaki kama chama cha siasa basi wangeendesha uchaguzi wa haki na kuachia madaraka. Its too late for ccm to remain as party beyond 2015. Ya KANU yameshawafika!
 
labda 2050, wapinzani wenyewe wamegawanyika, cdm kask, CUF kus, waunganishe wapiga kura.
 
wamegundua kwamba hawatashinda hivyo wanataka kupinga matokeo mahakamani. Pia mahakama ikiwatupia mbali basi rais ajaye asijaze watu wa chama chake kama wao wanavyofanya. Mbona suala la wakuu wa wilaya na mikoa na wilaya? Mbona hawajazungumzia kumshitaki rais aliyetumia ofisi ya umma kwa manufaa yake na familia yake? Mbona hawajaweka kipengele cha wastaafu ie rais asihusike kwenye siasa kama anataka kupata mafao? Hata mgonjwa anayekaribia kufa huwa madudu yote aliyoyafanya.
 
Nakubaliana na wewe mkuu! Wanajua watakaa benchi kwa hiyo mkakati wa kwanza ni kuweka uwezekano wa kumpinga mahakamani huyo rais wetu atakayechaguliwa (ambaye hatatoka ccm). Wanajua Tume yao sio huru kwa kuogopa kivuli chao (madudu yao) wanadhani rais atakayekuja atafanya kama wao. Hoja ya serikali 3 ni kutaka kuwapokonya wapinzani ili wakati wa uchaguzi na kama katiba itakuwa imeshakuwa tayari (kama JK alivyoahidi), basi wataibeba hoja hiyo kwenye kampeni za 2015. Ili kuzuia utitiri wa kuhamia CHADEMA kwa watakaotemwa kwenye mchujo, basi hoja ya mgombea binafsi imeandaliwa. Ikionekana ana mvuto basi mafisadi wa ccm watam-finance mpk ashinde kisha aonekane bado ni ccm.
 
wamegundua kwamba hawatashinda hivyo wanataka kupinga matokeo mahakamani. Pia mahakama ikiwatupia mbali basi rais ajaye asijaze watu wa chama chake kama wao wanavyofanya. Mbona suala la wakuu wa wilaya na mikoa na wilaya? Mbona hawajazungumzia kumshitaki rais aliyetumia ofisi ya umma kwa manufaa yake na familia yake? Mbona hawajaweka kipengele cha wastaafu ie rais asihusike kwenye siasa kama anataka kupata mafao? Hata mgonjwa anayekaribia kufa huwa madudu yote aliyoyafanya.

Mojawapo ya mapendekezo yao ni kuundwa kwa seneta ambayo itawaingiza marais wa awamu zilizotangulia. Hii ni njia ya kuwapa nafasi kuingia serikalini kwa mlango wa nyuma. Lazima kuwa macho na pendekezo hilo.
 
Nakubaliana na wewe mkuu! Wanajua watakaa benchi kwa hiyo mkakati wa kwanza ni kuweka uwezekano wa kumpinga mahakamani huyo rais wetu atakayechaguliwa (ambaye hatatoka ccm). Wanajua Tume yao sio huru kwa kuogopa kivuli chao (madudu yao) wanadhani rais atakayekuja atafanya kama wao. Hoja ya serikali 3 ni kutaka kuwapokonya wapinzani ili wakati wa uchaguzi na kama katiba itakuwa imeshakuwa tayari (kama JK alivyoahidi), basi wataibeba hoja hiyo kwenye kampeni za 2015. Ili kuzuia utitiri wa kuhamia CHADEMA kwa watakaotemwa kwenye mchijo, basi hoja ya mgombea binafsi imeandaliwa. Ikionekana ana mvuto basi mafisadi wa ccm watam-finance mpk ashinde kisha aonekane bado ni ccm.

Nimekupata vizuri, ni dalili kwamba wanaandaa mazingira ya kugombea binafsi kwa vile chama chao hakina mvuto tena, na kuna baadhi walivyowatukana na kuwadharau wapinzani eti ni kokoto, vyama vya msimu nk wanaona aibu bora kugombea binafsi kwa vile pesa walizoiba zinatosha kufanyia kampeni.
 
Wanajiandalia mazingira mazuri ya maisha ya upinzani! Wanaona wapinzani wanavyotaabika hivyo wanajipanga yasije kuwakuta!
 
Kujifunza ni kwa namna nyingi. I wish I could see Philip Marmo na kujitutumua kwake wakati anazima hoja ya mgombea binafsi mwaka 2010. Mara nyingine tunaongea kama tuna own future...
 
Back
Top Bottom