Warioba amshangaa Kikwete kusema mpasuko ndani ya CCM ni kidogo

Final Score: Waryoba 89%, na Makala 9%

Waryoba anasema ukweli ila anazungumza ukweli huo akiwa vichochoroni badala ya kuusema ukweli huo akiwa huko kwenye NEC ambako yeye ni member kutokana na kuwa Waziri Mkuu wa zamani.


Makala hana busara kabisa na hiyo inaonyesha jinsi gani chama kile kilivyo na viongozi wababaishaji. Anataka kusema kuwa kwake yeye watanzania wenye haki ya kuisema serikali ni wale waliompigia Kikwete tu wengine hawana lao. Huo siyo uongozi kwani hata katika maandiko matakatifu tunafundishwa kuwaangalia tunaonwaongoza wote kwa hakli sawa. Biblia ina hadithi ya mchunga kondoo aliyewaacha kondoo kumi ili kumfuata kondoo mmoja aliyepotea na kumrudisha kundini; hiyo ndiyo filosofi ya uongozi siku zote.
 
*Wasomi, Wazee wa CCM waonya

raiskikwete.jpg

Rais Kikwete: Kauli za viongozi waandamizi wastaafu zinasemekana kutikisa serikali yake

Na Waandishi wetu
Mwananchi
10/3/2009


MAWAZIRI wakuu wa zamani, Jaji Joseph Warioba na Dk Salim Ahmed Salim walikuwa wakizungumza siku moja wakiwa maeneo tofauti, lakini kauli zao kuhusu uendeshaji nchi wa serikali ya awamu ya nne zilifanana na hakuna shaka kwamba, zimeutikisa utawala wa Rais Jakaya Kikwete.

Wote wawili walitoa kauli zinazoonyesha kuwa nchi inayumba na kwamba vita inayoendelea dhidi ya rushwa haiwezi kufanikiwa kama serikali haitapambana kuuondoa mfumo ambao unalea rushwa, huku wakimuelezea Rais Kikwete kuwa anashauriwa vibaya.

Mara baada ya vyombo vya habari kuchapisha habari ya vigogo hao, mweka hazina wa CCM, Amos Makala alijibu kwa maneno makali, akielekezea shutuma zake kwa Warioba ambaye alimtuhumu kuwa hajawahi kuzungumzia mazuri ya Kikwete na kwamba hata wakati akishikilia nafasi ya waziri mkuu, kulikuwa na matatizo.

Kauli ya Makala ilifuatiwa na kauli ya makamu mwenyekiti wa CCM, Pius Msekwa ambaye alisema Warioba na Dk Salim wanao uhuru wa kutoa maoni yao dhidi ya serikali kama ilivyo kwa wananchi wengine.

Wasomi na wanasiasa walioongea na Mwananchi Jumapili wameeleza bayana kuwa kauli hizo za vigogo hao zinaashiria kuwa serikali ya Kikwete inakwenda kombo.

Wanaona kuwa hali hiyo inatokana na serikali kukosa mwelekeo wa baadhi ya viongozi waliopo serikalini na utashi wa kisiasa.

Mkuu wa Kitivo cha Sayansi ya Jamii ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Profesa Bertram Mapunda aliiambia Mwananchi Jumapili kuwa viongozi wa nchi hawana mwelekeo na hawajui pa kuipeleka nchi.

"Viongozi wanatakiwa wawe na vision (uwezo wa kuono mbali). Kwa sasa tunaendaenda tu; hatuna mwelekeo; kiongozi anatakiwa akae chini kufikiria baada ya kupewa madaraka ajue ataipeleka wapi nchi.

Wakati mwingine inatakiwa hata ikibidi achukue likizo ili ajipange namna ya kutekeleza ahadi alizotoa wakati wa kampeni," alisema Profesa Mapunda bila ya kufafanua kauli yake kuihusisha na matamko ya mawaziri wakuu hao wa zamani.

Naye katibu mkuu wa Chadema, Dk Willibrod Slaa alidai serikali ya Rais Kikwete haina uongozi mzuri na ndio sababu nchi inaelekea kubaya na akawamwagia sifa Warioba na mkurugenzi wa Taasisi ya Mwalimu Nyerere, Joseph Butiku kwa kauli zao.

Alisema kitendo cha vigogo hao kuamua kuzungumzia hadharani hali na mwelekeo mbaya wa nchi kutokana na kushamiri kwa vitendo vya ufisadi na rushwa, ni dalili njema na kwamba hiyo inaonyesha wazi kuwa hata wao wameanza kukerwa na wanajiunga na kambi ya wanaharakati katika kutetea haki za wanyonge.

Dk Slaa aliliambia Mwananchi Jumapili jana kuwa kukosekana kwa uongozi mzuri ndiko kunakofanya watendaji wafanye kazi zao kiholale na kuendeleza vitendo vya kifisadi kwa kuwa hawana mtu wa kuwafokea.

Alisema yeye binafsi amekuwa akipiga kelele juu ya kushamiri kwa vitendo vya ufisadi na rushwa hapa nchini, lakini hakuna hatua zinazochukuliwa na hivyo akasema kitendo cha Warioba na Butiku kusimama kidete kusema hadharani udhaifu huo ni dalili njema kwao kwani kilio chao kimesikika.

"Kitendo cha wazee waliowahi kushika nafasi za juu serikalini na ndani ya chama tawala, kuzungumzia hayo hadharani ni dalili njema kwamba, sasa watu wameanza kuona ukweli," alisema Dk Slaa, ambaye ni mbunge wa Karatu.

Dk Slaa alishangazwa na kitendo cha serikali kushindwa kuchukua hatua kwa watuhumiwa wa kashfa ya ununuzi wa rada na kuiachia Serikali ya Uingereza pekee kufanya kazi hiyo.

"Hawa watuhumiwa watashtakiwa kwa sheria za Uingereza wakati Tanzania ni taifa linalojitegemea," alisema.

"Niliwahi kutoa mapendekezo kuwa John Chenge na Dk Idris Rashid wafikishwe mahakamani kutokana na tuhuma za ufisadi, lakini serikali iko kimya hadi taasisi ya nje ya SFO (ya kuchunguza jinai kubwa) imekamilisha kazi zake.

"Sasa kama itawafungulia kesi watuhumiwa, watashtakiwa kwa sheria za Kiingereza ambazo hazitakuwa na manufaa kwetu."

Naye Mwenyekiti wa CUF, Profesa Ibrahimu Lipumba amewataka Jaji Joseph Warioba, Dk Salim Ahmed Salim na Joseph Butiku kuvaa ujasiri wa baba wa taifa Mwalimu Julius Nyerere kwa kueleza kiini cha matatizo ya kuyumba kwa nchi.

Akizungumza katika mahojiano maalum na Mwananchi, Dk Salim ambaye pia ni mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM, alisema mfumo wa serikali umeoza kwa rushwa pamoja na kwamba serikali inajitahidi kupambana nayo.

"Rais Kikwete anajitahidi na ana nia ya kupambana na rushwa, lakini bado 'system' (mfumo) haijajitayarisha vya kutosha kupambana rushwa," alisema Dk Salim ambaye aliwahi kuwa katibu mkuu wa Umoja wa Afrika (OAU).

Kuhusu uchaguzi ujao, Dk Salim alisema kuwa wanachama wa chama hicho wanaotaka kugombea urais sambamba na Jakaya Kikwete, waachwe wapambane naye, lakini akasema hawatamuweza.

Lakini Dk Salim alisema Wanachama wa CCM wana haki ya kupambana na Kikwete kuwania kuteuliwa kugombea urais kwa tiketi ya chama hicho tawala.

Naye Warioba aliwaambia waandishi wa habari kuwa nchi inaelekea kubaya anapoangalia jinsi mambo mbalimbali yanavyoendeshwa, huku akisema kuwa serikali haitaweza kushinda vita dhidi ya rushwa iwapo haitaelekeza nguvu zake katika kupambana na mfumo unaolea tatizo hilo.

Warioba, ambaye alishika nafasi hiyo ya mtendaji mkuu wa serikali kwenye miaka ya themanini, alisema kwa sasa taifa linakabiliwa na matatizo mengi kuanzia ya ukosefu wa maadili ya uongozi, rushwa na hata utaratibu mzima wa kuendesha mambo na kubainisha kuwa kuna pengo kubwa katika kuaminika kwa serikali.

Jaji Warioba alisema hivi sasa kuna dalili ya umoja wa Watanzania kusambaratishwa, watu kugawanywa makundi kwa udini na ukabila pamoja na kuwepo kwa matabaka ya matajiri na maskini.

Naye Butiku wiki hii alipigilia msumari mwingine aliposema utawala wa awamu ya nne bado una kazi kubwa katika mapambano dhidi ya rushwa pamoja na jitahidi za kupambana nayo.

Butiku alisema licha ya serikali kutumia mbinu mbalimbali bado rushwa imeendelea kushamiri kwenye chama na serikali na kwamba sasa imevuruga mfumo wa nchi. Imeandikwa na Elias Msuya, Fedy Azzah na Geofrey Nyang'oro.
 
And so the race begins for 2010! Mi naona ni dalili nzuri, we need honest dialogue, inabidi tuache unafiki na tuwe wawazi. The only problem is that the powers that be will try to clamp down harder on free speech and right to express ourselves.

How much time before they will start vicious attacks on Salim, Warioba and Butiku? Even jamiiforums will be again targeted. We have to ensure that we keep the conversation going.

Sasa natumaini wapambe hawaji kui-hijack topic hii with trivialities....
 
Jk naona analekea kuwa kama mzee ruksa bado tu kuliweka wazi hili anatakiwa kuchukua hatua kama kiongozi na kufanya kazi kwa ujasiri zaidi nadhani hata Mkapa alipata mafanikio kidogo na kuiweka nchi mahala pazuri kidogo kwa vile alikuwa na maamuzi binafsi tofauti na JK.

Angakuwa huwa anapita hapa JF nimemshauri apunguze safari za nje ambazo binafsi naziona hazina tija kwa Watanzania zaidi ya yeye kufanya utalii zaidi,kwa dunia ya sasa huwezi kujisifu kwa jinsi unavyoweza kupata misaada toka nje ila unaweza ukajisifu kwa mikakati bora ya kuzalisha na kukuza uchumi bila kutegemea nchi wahisani.

Nadhani kama atakaa ofisini na kupitia matatizo ya wananchi kwa umakini anaweza akaja na mipango ya kuipeleka nchi mahala pazuri na si kuifuata zimbabwe uliko au kuwa mzee ruksa.
 
aliutikisa huo utawala wa jk ni salim,
warioba wamemzoea kuuponda utawala wa jk,
salim hawakutegemea.....
 
.................."Naomba niseme tena namheshimu sana Mzee Warioba, na si kweli kama mimi nimemtukana ila Mzee Warioba ni miongoni mwa wazee wasiopenda kupingwa wala kukosolea na anapenda hoja yake ichukuliwe ni fikra sahihi ambayo kila Mtanzania anapaswa kuiheshimu.
Kijana hii ni tuhuma ninayoisikia kw amara ya kwanza kuhusu huyu Mzee


"Ninamwomba kama kweli yeye ni mwana CCM thabiti tena Waziri Mkuu mstaafu, anashindwaje kutumia uzoefu wake kutoa ushauri kwa viongozi wa chama na Serikali katika vikao vyao, au kuwaona moja kwa moja maofisini, awe Rais , Waziri Mkuu na viongozi wa juu katika chama?

Kijana ulishawahi kuisoma ripoti ya Warioba kuhusu Rushwa?

" Je fursa hizo kwake yeye anaona zimeshindikana na anaona ni vema ashauri kupitia vyombo vya habari? Au ni busasra gani ya kushauri Serikali kwa kuita waandishi wa habari? Kwanini yeye anapenda kukosoa kupitia vyombo vya habari? " Alihoji Bw. Makalla.

Kuna ubaya gani, akati mwingine mnashauriwa, lakini mafisadi wanawakamata kisawasawa kiasi kwamba mnashindwa kufuata ushauri wa Wazee kama hawa.....wacha wananchi tusikie ili tujue matatizo ya kifisadi mliyonayo............nyie mnataka kuficha maradhi eehh



"Mimi sijajipendekeza kwa Kikwete kama anavyodai yeye mimi ni wajibu wangu kama mwana CCM na kiongozi kutetea chama changu na Serikali ya CCM . Yeye mwenzangu ameamua kutafuta umaarufu wa kuikosoa Serikali ya chama chake hadharani kwa maslahi binafsi, "

...........Sidhani kama Mzee Warioba anatafuta umaarufu hapa, (alishakuwanao tangu zamani), ila wewe ndio unajaribu kutafuta umaarufu kwa kujibishana na Mzee Warioba............


" Namshukuru amekiri kwa mara ya kwanza wazi wazi kuwa alikuwa kwa Salim 2005. Hivi kama inajulikana hivyo, sasa tutegemee nini unapolaumu Serikali hata jambo moja la kusifia hana kwanini nisiamini kuwa anaendekeza makundi.?

Hivi ni ajabu kum-support mtu kwenye uchaguzi hata kama mko chama kimoja?....baada ya mchakato si mnakuwa kitu kimoja.....ubaya uko wapi.........boy are you really a politician?

"Hivi anataka nimkumbushe kuwa siku ya mkutano wa kupata mgombea urais 2005 yeye tayari alishavaa shati lake safi la CCM lenye nembo ya Bendera ya Taifa huku akiiamini kuwa Salim akishinda anakuwa mgombea mwenza! Kwanini nisiamini kuwa Salim alishakubali kushindwa lakini yeye akikumbuka umakamu basi hasira zake ndiyo kushambulia Serikali, tukimkosoa anasema ametukanwa!..............

Kumbe ni kweli unaendekeza siasa za makundi eeh........


" Nachelea kuamini kama uzee ni dawa, lakini si kila mzizi ni dawa ipo mizizi mingine ni sumu.

Nenda kajiunge na vikundi vya mipasho ili tujue moja

"Nimemlaumu kwa kulaamu pasipo kutoa majawabu. Namtaka Mzee Warioba na Watanzania wote tushirikiane na Serikali kujenga nchi yetu, tuache siasa zitakazobomoa umoja wetu na amani tuliyonayo," alisema Bw. Makalla .

majibu mnayo hamtaki kuyafanyia kazi (List ya wala rushwa, list ya wauza unga and so on ).........kwa kuwa mnawaogopa mafisadi
 
Warioba is also part of the problem (mnafiki)...anaendeleza makundi vilevile jino kwa jino wacha walumbane tunawaita walewale (agenda zao zinafanana) wamejificha kwenye nyasi fupi.

To the contrary, I support all this CCM gibberish and hypocrisy. Let them hang all their dirty linens in public. After all, dirty is who they are.

Now we will get to realise the kind of leaders we have and how stupid we all have been. Perhaps we will maintain some sense of sanity next time we go to the polls and rid ourselves from all this, once and for all.
 
Angakuwa huwa anapita hapa JF nimemshauri apunguze safari za nje ambazo binafsi naziona hazina tija kwa Watanzania zaidi ya yeye kufanya utalii zaidi,kwa dunia ya sasa huwezi kujisifu kwa jinsi unavyoweza kupata misaada toka nje ila unaweza ukajisifu kwa mikakati bora ya kuzalisha na kukuza uchumi bila kutegemea nchi wahisani.

Tatizo tulilonalo kwa mkuu wetu ni kuwa hajielewi kuwa yeye mwenyewe (i.e. mitizamo yake kama huo) ni moja ya tatizo.........tufanyeje ili ajielewe mwenyewe......maana naona washauri wameshindwa kazi.....wameamua kula sambamba na posho za safari.....damn
 
Warioba asitake kujifanya anajua sana kukosowa wenzake, yeye kashfa ya mwananchi gold zinamsubiri.

Vile vile mbona hakuifanyia lolote nchi hii alipokuwa waziri mkuu!!! Yeye ni mwanachama hai wa CCM, je amekishauri nini chama chake ili kutatua matatizo ya sasa?

Jamani hapa nini Warioba alilololisema sio kweli?Utatoa ushauri gani kwa viongozi wa CCM ambapo kwao ukweli kwao majungu na majungu kwao ukweli?????Nini kilichotokea katika kikao NEC Dodoma?Badala ya ya kuwaunga mkono wanaojaribu kupambana na ufisadi wanawalaumu nakuwatia mikwala.Viongozi wengi wa CCM na serikali wanalinda masilahi yao binafsi na sio ya walala hoi,wamelewa madaraka.Naimani yangu kua wakina Mzee salim Ahamed Salim,Warioba Butiku n.k.Wamekua wanatoa ushahuri lakini ushauri wao unakua ni kumpigia mbuzi gitaa.Kweli nchi inakwenda kubaya,hatua zao wazee hao ni za kijasiri na kufikisha ujumbe kwa walalahoi ili waelewe ya kua ndani ya CCM sio wote waliooza kunawatu ambao wanamawazo tofauti na ambao hawaridhiki na nchi inavyo endeshwa hii itasaidia kunyanyua au kuleta mwamko kwa lalahoi kupambana na hali hii.Kwa hali ilivyo kwa uongozi wa sasa Wa CCM na serikali hakuna mshauri yeyota wanaweza kumsikia.Nia za pekee ni shinikizo toka wa wafadhiri na msukumo kutoka kwa walalaho kwa kusema sasa basi tumechuka kuburuzwa,tumechoka kuibiwa,tumechoka kunyanyaswa.MUNGU IBARIKI TANZANIA
 
kiukweli JK anakazi kubwa sana. Mwenyewew anawezekana ana dhamira njema kabisa lakini timu yake ndo mbovu. kitendo cha hawa wazee kutoa ushauri hadharani ni kielelezo kwamba hata wao wanakerwa na jinsi mambo yanavyoendeshwa hususani kwenye vita hizi za ufisadi. na inaonekana hakuna dhamira ya kweli kupambana na Rushwa na hizi kesi ni kama kiini macho na mtaji wa kampeni 2010. Lakini KWELI uwa inashinda daima kama alivosema SHABAN ROBERT.
 
Serikali nayo ijirekebishe kwani watu wamechoka jamani.
Hayo mambo ya Salim kuwa Hizbullah ni scaremongering za CCM Zanzibar wasiomtaka Salim kwa sababu ni Mpemba.

JK and his sidekick Pinda are effin lightweights ambao wasingefaa hata kuwa manaibu waziri, ukiona mpaka Salim anaongea ujue makubwa yamejificha hatuyajui, haya tunayoyajua na yanayosemwa ni "tip of the iceberg" tu.
 
wametoa kauli zinazoshabihiana wakiwa maeneo tofauti!? Isije ikawa ni ndogo ndogo za 2010, maana 2005 hawa watu ilikuwa wawe Rais na Makamu wake. I hope kauli zao zinathibitika kisayansi, isije kuwa ni maneno tu ya watu dhidi ya utawala wasioupenda kwa sababu binafsi. Aidha, ni heri kauli zao zingekuwa ujumbe tosha kwa watanzania woote, ili watambue tulipo na kuchukua hatua stahili, maana fursa ya kufanya hivyo iko karibu.
 
Jamani, sasa hii siasa inatupeleka pabaya hata adabu tunakosa. Kuanzia sasa hadi apatikane Rais wa Tanzania (najua wagombea watakuwa wengi)kwenye uchaguzi mwaka kesho tutasikia mengi.

Amos Makalla yule Mweka Hazina wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) ameibuka akiwa London na kusema hadharani kuwa ni wakati wa Jaji Joseph Sinde Wariaoba kukaa kimya eti kwa kuwa hayumo na hakuwemo kwenye boti ya ushindi wa JK tangu awali.

Eti kwa kuwa yeye alikuwa ni mpiga debe wa Dk. Salim Ahmed Salim (SAS) kwenye kinyang'anyiro cha uchaguzi ndani ya CCM mwaka 2005, basi hana nafasi ya kumzungumzia na akizungumza anafanya hivyo kwa kuwa alishindwa pamoja na mgombea wake.

Makalla anasema kuwa Warioba siku ya uchaguzi kuteua mgombea wa urais kutoka kwa wanaCCM watatu- Kikwete, Salim na Mwandosya, alikuwa na uhakika wa mgombea wake SAS kupata nafasi hiyo kwa hiyo alikuwa amejiandaa vilivyo kwa nguo za kuvutia kwani alikuwa amejiaminisha (au kuelezwa mapema) kuwa ndiye angekuwa mgombea mwenza, lakini haikuwa hivyo.

Sasa hapo Makalla ndiyo anaibuka na kusema Warioba anamuonea gere Kikwete kwa mafanikio aliyoyapata tangu aingie madarakani, ndiyo maana eti anazomoka kwa ubaya dhidi ya JK ambaye ni kiongozi wake wa nchi, chama na zaidi sana ni rafiki yake wa karibu.

"Tanzania, Tanzania, nakulilia mama Tanzania. Mungu akubariki uendelee kumea na kustawi kwa neema ya watu wako"
 
"Tanzania, Tanzania, nakulilia mama Tanzania. Mungu akubariki uendelee kumea na kustawi kwa neema ya watu wako

waacheni wafu wazike wafu wao....na bado hiyo trela wanaanza
 
Hii Nchi Bana, unaweza ukashangaa eti Siku moja Makalla akawa Raisi wa Nji hii
 
And so the race begins for 2010! Mi naona ni dalili nzuri, we need honest dialogue, inabidi tuache unafiki na tuwe wawazi. The only problem is that the powers that be will try to clamp down harder on free speech and right to express ourselves.

How much time before they will start vicious attacks on Salim, Warioba and Butiku? Even jamiiforums will be again targeted. We have to ensure that we keep the conversation going.

Sasa natumaini wapambe hawaji kui-hijack topic hii with trivialities....

Ulipotelea wapi ndugu yangu!? Nafurahi kukuona I hope this time you'll stay at least until November 2010 ha ha ha ha :) ili tufaidike na michango yako iliyojaa hekima na busara tele.
 
Hapa kuna chuki ya ajabu.Kinachoonekana Warioba hawezi kukaa pamoja na kikwete akamshauri kitu, hili halijaanza leo, Kikwete mwenyewe ameshindwa kumweka Warioba kama mshauri wake mkubwa..Kikwete ni mtu wa vizazi kwa hiyo Makalla asijitie unafiki wa kumlaumu Warioba as if hata kama angefanya hivyo angesikilizwa.Ila kinachonistua sana ni majibu ya kebehi na utovu wa nidhamu aliyotoa Makalla.
Well all in all wacha wagombane wenyewe, hatuitaki C.C.M mwakani..hii ni nafasi nzuri kwa upinzani kupata members muhimu wa c.c.m
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom