Warioba amshangaa Kikwete kusema mpasuko ndani ya CCM ni kidogo

Kevo,

Napenda wambia Ikulu is an institution ambayo ina watu waano wajibika kwa kumshauri Rais na kama hawafuatilia mambo ya wananchi wao kiunda na kumpa report mbovo basi hapo rais wetu ana kazi ya ziada ya kuwa na kitengo chake cha siri cha kumhabarisha direct maana kuna mijitu mingine humo sijui kama kweli yana uchungu na nchi yetu hii au wako tu basi siku iwe imepita

Naona The Citizen ya Leo wanaliendeleza libeneke la kauli za Dk Salim na Warioba kwa Kusema Jk Should be held responsible for govt weaknesses
 
Kevo,

Napenda wambia Ikulu is an institution ambayo ina watu waano wajibika kwa kumshauri Rais na kama hawafuatilia mambo ya wananchi wao kiunda na kumpa report mbovo basi hapo rais wetu ana kazi ya ziada ya kuwa na kitengo chake cha siri cha kumhabarisha direct maana kuna mijitu mingine humo sijui kama kweli yana uchungu na nchi yetu hii au wako tu basi siku iwe imepita

You are very right Jethro about Ikulu being an institution lakini Rais naye anayo madaraka ya pekee akiwa kama Rais na ndio maana JK alitamka kwamba urais wake hauna ubia. Kwa maana hiyo anao uwezo wa kuchambua kila analoshauriwa ili kutenganisha pumba na mchele na kuchukua hatua kutokana na maamuzi yake binafsi.

Kwa maoni yangu, Rais wetu ameelemewa. Kwanza; labda alipokuwa anakazana kuunda mtandao ili aweze kuingia Ikulu hakuelewa uzito wa kazi ya urais. Vile vile inawezekana pia alikuwa anaelewa na sasa anaelewa zaidi uzito wa kazi hiyo ulivyo, lakini anashindwa kuwa na ujasiri wa kuweza kuchukua hatua ambazo sisi sote tunadhani anapaswa kuchukua kuhusu masuala mbali mbali ya uendeshaji nchi. Pia, zipo sababu zinazofanya ashindwe kuwa jasiri wa kuchukua hatua kali, moja ya sababu ni kushindwa kutenganisha uswahiba na majukumu yake kama Rais wa nchi!

Mimi nilikuwa mmoja wa wananchi walio 'danganyika' wakati Rais wetu anaingia madarakani. Alipoanza kuzungukia wizara na kutoa maagizo na maelekezo, na hotuba yake ya kwanza Bungeni, nilipata imani kwamba LABDA sasa tumepata 'JK mdogo'! Lakini wapi.

Kwa hulka yetu Watanzania na kwa malezi tuliyolelewa na Baba wa Taifa JKN, kama tulivyoweza kumvumilia (kwa wale waliokuwa wanamuona haendeshi nchi wanavyotaka wao), tukaweza kumvumilia RUKSA, tukajamvumilia MBABE Mkapa, yatupasa vivyo hivyo tuwe wavumilivu na kumpa nafasi Rais wa sasa amalize muda wake kwa amani bila kufanya vurugu. La msingi lililo mbele yetu sasa ni kuunganisha vichwa - ku brain-storm kuweza kubaini tunataka nchi yetu iweje (kama itabaki kuwa nchi) tunataka nani awe kiongozi wa awamu ya Tano ili watoto wetu na wajukuu zetu waweze kujivunia kuwa Watanzania.

Mungu Ibariki Tanzania!
 
Lampart,

Ukikanywa na kukumbushwa yaote ni kuambiwa kuwa jitizame kuna kasoro sasa unaposema ana Jaribu kusaidia au ku destroy TZ sijakuelewa hapo,

Tatizo letu na viongozi wetu tukiambiwa kitu au kukoselewa kwanza huanza niambie wewe hujioni jamani tuwe na kasumba ya kuangalia jambo uambiwalio au ukosolewalo na ulipime pia na ulitendee kazi ila sisi tu wabishi sana as if tuta ishi milele dunia hii


Kama kweli unataka kumkanya mwanao basi huendi kwa jirani kumsema, utamwita na utamuweka chini na utamueleza ukweli. Warioba kama kweli anayo makanyo na kama bado ni mwana-ccm, then, he knows where to go and sio kwa waandishi wa habari. Waandishi wa habari watasaidia nini? Hii ni sawa na ile ya Nyerere kuenda pale Kilimanjaro Hotel kumtukana Mwinyi. For the first time Nyerere never helped this nation at all. Salama Mwinyi ni muungwana or to be precise tumshukuru Thabit Kombo. Nyerere was supposed to go to State House and talk to Mwinyi and his ministers, guide them and show them the way. Lakini yote ilikuwa ni babaisha ***** tu ili wananchi wafurahi na huyu Warioba ndio yupo kwenye njia hio hio na wala hana lolote lile la maana la kusema kuhusu CCM na serikali yake. Zaidi labda anataka kuweka kizingiti ili asifuatwe fuatwe kuhusu hizo shituma juu yake za ufisadi na hio kampuni yake. Hata kama alisaidia sana huko nyuma he is now slowly slipping into oblivion in the usual bongo way!
Maanake Bongo mpaka ukose wadhifa hapo tena ndio utaanza kuikosoa CCM au utaingia chama cha upinzani!
Anaweza kujiunga CUF kwani wote wana-ccm wakongwe waliopo nje ya madaraka wapo huko.
Sidhanii kama CCM inahaja ya watu wanaoropokwa ovyo. A man of his status can at any time meet JK and talk sense to him instead ya kuwasaidia wapinzani.
 
kama kweli unataka kumkanya mwanao basi huendi kwa jirani kumsema, utamwita na utamuweka chini na utamueleza ukweli. Warioba kama kweli anayo makanyo na kama bado ni mwana-ccm, then, he knows where to go and sio kwa waandishi wa habari. Waandishi wa habari watasaidia nini? Hii ni sawa na ile ya nyerere kuenda pale kilimanjaro hotel kumtukana mwinyi. For the first time nyerere never helped this nation at all. Salama mwinyi ni muungwana or to be precise tumshukuru thabit kombo. Nyerere was supposed to go to state house and talk to mwinyi and his ministers, guide them and show them the way. Lakini yote ilikuwa ni babaisha ***** tu ili wananchi wafurahi na huyu warioba ndio yupo kwenye njia hio hio na wala hana lolote lile la maana la kusema kuhusu ccm na serikali yake. Zaidi labda anataka kuweka kizingiti ili asifuatwe fuatwe kuhusu hizo shituma juu yake za ufisadi na hio kampuni yake. Hata kama alisaidia sana huko nyuma he is now slowly slipping into oblivion in the usual bongo way!
Maanake bongo mpaka ukose wadhifa hapo tena ndio utaanza kuikosoa ccm au utaingia chama cha upinzani!
Anaweza kujiunga cuf kwani wote wana-ccm wakongwe waliopo nje ya madaraka wapo huko.
Sidhanii kama ccm inahaja ya watu wanaoropokwa ovyo. A man of his status can at any time meet jk and talk sense to him instead ya kuwasaidia wapinzani.


ngida, you made my day!!!!
I hope nd. Jethro will read your posting. This is exactly what i had in mind but couldn't put it down so vividly when i wrote that warioba was not helping anybody.
Again, thank you ngida for your detailed explanation!!!

thank u, thank u, thank u!!!
 
Kama kawaida yao wanachofanya mchana kutwa ni kuita vyombo vya habari na kutoa porojo tu. Tunataka vitendo vionekane sio maneno tu. Wote ndio hao hao!!
 
Kuna umuhimu wa kuwa na watu wenye ujasiri wa kusema yale wanayoona yanaisibu nchi.Wanaosema Warioba akae kimya kwani anakesi ya kujibu ya Mwananchi Gold , kwanini basi hamumpeleki mahakamani na yeye alishawaambia fanyeni hivyo haraka!! Watu wenye hekima lazima waseme pale wahuni wanapotaka kuiangamiza nchi!! CCm ni lazima wanachama wake waamke sasa na kukubali kuzitosa taratibu zilizopitwa na wakati kama vile kusema maadam Rais amepewa kipindi kimoja cha kuongoza ni utamaduni wetu kumpa kipindi cha pili hata kama performance yake ni mediocre; mbona tunazipiga vita mila potofu za ukeketaji si kwa vile zimepitwa na wakati!! Huu utamaduni wa kulea uozo ndani ya taratibu za ccm pia umepitwa na wakati.
 
Dear Nd. Boramaisha,
>yatupasa vivyo hivyo tuwe wavumilivu na kumpa nafasi Rais wa sasa amalize muda wake kwa amani bila kufanya vurugu.<


No!!! No!!! No!!!
Hatuwezi kuvumilia tena.
Kama kule ZNZ wangelikuwa kila mwaka wanavumilia, basi mpaka leo wangelikuwa chini ya Sultani.
The time is ripe right now to remove these Sultans from power by any means - even through an armed uprising! What else can a people whose quest for development in their country always remain trampled upon by Mafisadis do? Where all ways fail, a people's insurrection becomes the only alternative for a people oppressed by Mafisadis such as us in order to redeem themselves.
Let's take the State House by force!
Let's take the street of DSM by force!
Let's remove these guys now! We cannot afford to wait a second more!!!
The time for such an insurrection in Tanzania is now. It will be suicidal to wait a second more!!!
Hatuwezi tena kuwavumilia akina JK na wenzake! Wanatusaliti kila siku!
Watoke haraka, kwani wameshindwa.
Ari yao Mpya, Nguvu yao Mpya na Kasi yao Mpya itazidi kila siku kutudidimiza kwenye umaskini daima!
 
Kama kweli unataka kumkanya mwanao basi huendi kwa jirani kumsema, utamwita na utamuweka chini na utamueleza ukweli. Warioba kama kweli anayo makanyo na kama bado ni mwana-ccm, then, he knows where to go and sio kwa waandishi wa habari. Waandishi wa habari watasaidia nini? Hii ni sawa na ile ya Nyerere kuenda pale Kilimanjaro Hotel kumtukana Mwinyi. For the first time Nyerere never helped this nation at all. Salama Mwinyi ni muungwana or to be precise tumshukuru Thabit Kombo. Nyerere was supposed to go to State House and talk to Mwinyi and his ministers, guide them and show them the way. Lakini yote ilikuwa ni babaisha ***** tu ili wananchi wafurahi na huyu Warioba ndio yupo kwenye njia hio hio na wala hana lolote lile la maana la kusema kuhusu CCM na serikali yake. Zaidi labda anataka kuweka kizingiti ili asifuatwe fuatwe kuhusu hizo shituma juu yake za ufisadi na hio kampuni yake. Hata kama alisaidia sana huko nyuma he is now slowly slipping into oblivion in the usual bongo way!
Maanake Bongo mpaka ukose wadhifa hapo tena ndio utaanza kuikosoa CCM au utaingia chama cha upinzani!
Anaweza kujiunga CUF kwani wote wana-ccm wakongwe waliopo nje ya madaraka wapo huko.
Sidhanii kama CCM inahaja ya watu wanaoropokwa ovyo. A man of his status can at any time meet JK and talk sense to him instead ya kuwasaidia wapinzani.

My dear friend you are being driven by biasness. Kusoma uliyoandika nimeshabaini kwamba wewe ni mmoja wa mafisadi wanaonufaika na status quo ama inawezekana wewe ni ndugu ya Rais Mwinyi na una 'uswahiba' na kiongozi wa Awamu hii. Hapa we are trying to be objective kwa manufaa ya nchi yetu. Unaanza kuleta habari za kumfuata mtu kumkanya na za Nyerere kumsema Mwinyi hadharani. How sure are you kwamba Mwalimu hakuwahi kuzungumza na Mwinyi kuhusu hali ya nchi ilivyokuwa wakati ule na jinsi inavyoweza kuathiri mustakabali wa nchi yetu na kuharibu yote yenye manufaa ambayo awamu ya kwanza ilijaribu kuyajenga?

Kwanza nianze na hilo la Nyerere kumtukana Mwinyi as you put it! Lazima umtendee haki marehemu. Mwalimu Nyerere tunaweza kabisa kusema kwa uhakika na kujiamini alikuwa MZALENDO nambari wani wa nchi hii. Kwa hiyo Mtanzania yeyote ambaye hana maslahi 'binafsi' anaelewa wazi kwamba Mwalimu hakumtukana Mwinyi kwa lolote lile. RUKSA ya Mwinyi ilikuwa kero kwa mustakabali wa nchi, ilikuwa inalipeleka pabaya taifa letu. Mwalimu alikuwa akielezea umuhimu wa kuwa kiongozi bora na mwenye msimamo - jambo ambalo leo hii ndilo linatufanya tulumbane humu. Angelikuwepo Mwalimu naamini (kwa kutumia lugha yako) 'angetukana' sana uongozi uliopo sasa na angemtukana Mkapa ambaye alitoka kwenye u-Mr. Clean akawa Mr. Dirty kwa ajili ya 'vipande vya fedha', ambao kwa pamoja wameifikisha nchi kwenye uchafuzi mkubwa wa hali ya hewa ulioletwa na lindi la ufisadi.

And by the way, unadhani uungwana wa MWINYI usingalikuwepo angelimfanya nini MWALIMU? Thubutu! Tena si Mwalimu ambaye ange-lift his fingure kujibu mapigo. Pangelikuwa hapatoshi maana Watanzania wangelimshukia Mwinyi kama tai kama angelijaribu kumgusa Mwalimu! Tuache ushabiki uliojaa ubinafsi tuangalie zaidi mustakabali wa Taifa letu vinginevyo, mark my words Taifa hili tunalodhani haliwezi kupata dhoruba yoyote, litasambaratika tukiendekeza siasa za ubinafsi na kujali zaidi 'vipande vya fedha' kuliko mustakabali wa Taifa!

Tukija kwenye suala la Warioba kuongea kwenye media kutoa dukuduku lake. Hivi Wana - CCM kama Mzee Makamba, Amos Makala (Mhasibu/Bwana fedha tu wa Chama) na wengine wa aina yao hata kama ni wajumbe wa Halmashauri Kuu wao tu ndio wanaoruhusiwa kuongea na Media lakini si Warioba? Jambo moja ambalo watu wa aina yako waliojaa mawazo ya ubinafsi wanasahau kwamba Warioba alikuwa ni Waziri Mkuu wa nchi hii - Kiongozi mwandamizi wa cheo cha juu kabisa nchini mwetu. Iweje akina Makamba ambao ni makatibu wakuu tu wa Chama wawe na uwezo na haki ya kuongea kwenye vyombo vya habari na Warioba (Waziri Mkuu) asiwe na haki hiyo? Ni mawazo potofu kabisa kwamba eti mtu aliyekuwa kiongozi akimaliza muda wake basi afunge mdomo wake, hana haki ya kusema lolote kuhusu mustakabali wa nchi. Wenzetu wanaojua hazina ya viongozi Wastaafu wanawaheshimu na kuwafanya washauri wakuu, Sie tunawafanya maadui!!! UBINAFSI usio na kipimo!

Labda nikuulize suala moja ndugu yangu, hivi hivyo vikao vya Chama unavyovizungumzia vimekuja na lipi la maana kwa Taifa letu katika kipindi hiki? Juzi juzi tu tumetoka kuona jinsi ambavyo CCM ngazi ya Taifa imekuwa na 'midomo miwili' - leo wanaamua kuwajadili na kuwatishia kunyang'anya kadi wanachama VIONGOZI WAANDAMIZI kama Spika na Wabunge wanaoamua kulikabili tatizo la ufisadi. Kabla hata mate hayajakauka, wale wale waliotaka kuwanyang'anya kadi viongozi hao, wanaenda mbele ya media na kusema kwamba viongozi waliokuwa wanataka kunyang'anywa kadi na Chama wanaungwa mkono na chama hicho hicho kwa 'kosa' lile lile ambalo lingewafutia uanachama!

Kwa nini Watanzania hatutaki kuwa wakweli ili kuinusuru nchi yetu?
 
I say, huyu mzee namuonea huruma? Is he trying to help CCM or destroy Tanzania?
Kukosa ukubwa ni mbaya kweli! Mzee wa watu huyu anaadhirika ovyo!

From what I can gather all comments are from CCM zealots! Mbona tunambeza hivyo? Hata kama mtu ana madhambi au mapungufu yake haina maana kwamba hapaswi kutoa mawazo yake. Mzee Warioba ni mtu huru kama wengine katika nchi yake. Utawala uliopo unamgusa yeye kama sisi wote tulivyo hata kama inasemekana kuna madudu ya Mwananchi yanamsubiri.

Hata hivyo mzee Warioba alishaelezea upande wake kuhusu Mwananchi Gold Project katika mahojiano na Gazeti la Raia Mwema katika siku za nyuma. Sijaona mtu akimpinga kwa hoja zake alizotoa kuhusu ilo. Vile vile sioni ubaya wa Mzee Warioba kutoa ushauri kwamba Rais wetu (JK) asijiingize katika mambo ya kesi hasa zikiwa katika ngazi za mwanzo kabisa. Ametoa mfano wa jinsi Rais Nyerere alivyoingilia mwenendo wa "uhujumu uchumi" miaka ya 1980 na jinsi serikali ilivyolipa hela nyingi baada ya kukurupuka kupeleka "wahujumu uchumi" mahakamani na kushindwa kesi.

Mfano mzuri ni ule wa sakata la EPA. Mzee anaona kama Rais alishauriwa vibaya kuwapa muda mafisadi wa EPA kurudisha pesa na hata baadhi wakarudisha. Je sasa ikitokea wakishinda kesi mahakami itakuwaje wakati pesa zenyewe zimeshapangiwa matumizi? Kuna ubaya gani katika ushauri kama huo?

Hivi ukikuta nanasi nzuri imeota katikati ya miiba utaacha kuivuna? Basi mawazo au ushauri ya watu kama Mzee warioba tuuchulie kama nanasi ilyoota katikati ya miiba. Basi tuvune nanasi tuachane na miiba.
 
Nd. ByaseL na Nd. Boramaisha,
Kwanza tusijifanye kama sisi Watanzania ni kweli mashujaa (japokuwa kidogo Waznz ni mashujaa kutokana na hayo Mapinduzi yao matukufu ya January12, 1964), kwasababu kama tungelikuwa mashujaa basi yasingelitufika haya yanayotufika kila siku. Unapozungumzia ushujaa ni kuzungumzia watu kama vile wa Philippines who rose up in arms and overthrew Fisadi Marcos. Sisi tutatiwa vidole vya macho kila siku na hakuna kimoja tutakachokifanya.
Kumfanya Nyerere Mungu Mtu pia haisaidii kitu. Hakuna anaekataa kama hakutugomboa – he liberated us and at the same time mentally colonized us with his socialist ideals which never worked! Nyerere kafanya makosa tele akiwepo madarakani na nje ya madaraka. Bila ya Mwinyi leo mimi na nyinyi tusingeliweza kuandika haya tunayoyaandika. Mwinyi liberated us politically and economically. Nyerere created Tanzania and later destroyed it. Nobody in his proper senses would deny that.
Pili, hatusemi kama Warioba asiseme kitu. Tunachosema ni kuwa Warioba sio mkweli na haitakii hii nchi la maana, kwasababu kutokana na wadhifa wake angeliweza kufanya mengi leo japokuwa yupo nje ya madaraka, lakini hataki na analotaka ni kujitangaza tu kwa wananchi kama wanavyofanya wote waliopita - japokuwa yeye hakujitangaza Kilimanjaro Hotel lakini kajitangaza nyumbani kwake!
Hatutaki jamani kumpunguzia uhuru wake wa kusema yeye au Mtanzania mwengine yoyote yule. Uhuru wa kusema (thanks to Mwinyi) has today in Tanzania become the cardinal right of every Tanzanian. This right was not there under Nyerere.
Tusichotaka ni kwa Warioba leo kutaka kuikosoa CCM while at the same time he flocks with the same people all the time. Kama kweli anataka kuwaeleza ukweli CCM kwanini anapokutana nao hafanyi hivyo na anapiga kelele magazetini tu? Au Nd.Maishabora utanieleza kuwa unajuwaje kama hawaeelezei hayo wakikutana? Narejea tena kusema kuwa, wewe kama unauchungu na mwanao kwasababu unamuona anaelekea kubaya, kweli utakuenda kwa jirani kupiga kelele?
Warioba should do well to understand that he can fool nobody in Tanzania today with his empty harangues and that no amount of dilly-dallying on his part will extricate him from the quagmire of Mwananchi Gold in which he is deeply entrenced!
 
Nd Boramaisha wrote and I quote:…”Pangelikuwa hapatoshi maana Watanzania wangelimshukia Mwinyi kama tai kama angelijaribu kumgusa Mwalimu!”
My dear countryperson, what are you talking about? Please, don’t stoop that low. Umeona tumempiga kofi mzee wa watu na hakikutokea kitu sasa una-vision mambo mengine. Kwanini? Kwasababu huyu mzee katufungua midomo au kwasababu huyu mzee wa watu katupa uhuru huu wa kusema tuliyokuwa nao leo?
Kama sio huyu tuliempiga kofi tungelikuwa wapi leo? Nani hao ambao wangelimshukia Mwinyi kama tai? Kama tunaweza kweli kumshukia mtu kama tai, mbona tunashindwa kumshukia JK? Mbona tumeshindwa kumshukia Mkapa wakati sote tunajua madhambi aliyoyafanya? Mbona tulishindwa kumshukia Komando wakati wa enzi zake? Your statement was very disrespectful of the very person who liberated us! Yes, Mwinyi is indeed a LIBERATOR to Tanzania. We were deep down in the s…!!!
Kama angelimgusa Mwalimu!!!! Unakusudia nini? Ulitaka uzione ndondi? In politics it is different from what is taking place in the World Wresting Entertainment – katika siasa watu wanapigana chinichini na hawapigani ngumi unazozijua wewe, bali mapigano yao yanakuwa ni change of policies.
Ziko wapi leo siasa za Ujamaa na Kujitegemea? Zipo wapi leo siasa za watu wote kuishi kijiji kimoja? Huoni hilo ni pigo kwa Mwalimu na siasa zake? Hao tai mbona hawakushuka? Boramaisha wanichekesha kweli. Mwinyi kuiua siasa ya Ujamaa na Kujitegemea huoni hapo kamgusa Mwalimu? Au ulitaka amguse kwa kumpiga kofi kama alivyopigwa yeye, - hapo tena ndio tai mngeshuka?????? .
Nd. ByseL nae aliandika kuwa:…..” Hata hivyo mzee Warioba alishaelezea upande wake kuhusu Mwananchi Gold Project katika mahojiano na Gazeti la Raia Mwema katika siku za nyuma. Sijaona mtu akimpinga kwa hoja zake alizotoa kuhusu ilo".
Kwavile hujaona mtu akimpinga kwa hoja zake alizotoa that does not at all exonerate him. Waswahili wanasema: ”Msema pweke……. (malizia mwenyewe)”.
Hivyo kwani uliona mtu akimpinga Mkapa kuhusu yale machimbo ya mawe isipokuwa mimi na wewe? Je, Bw. Mkapa is blameless kwavile hujaona akipingwa rasmi na serikali? Ukitegemea mtu gani ampinge Bw. Warioba na hizo hoja zake? Ulitegemea apingwe na JK? Ali Shein? Pinda? – hapo tena ndio ungeliamini kuwa nae yumo kwenye ufisadi?????
CCM – the very acronym of the ruling party speaks it all. Chukua Chako Mapema. Bw. Warioba keshafanya hivyo na hivi sasa bora afunge mdomo wake na hatatokea mtu yoyote atakaesema zaidi juu yake – if anything else the government will just purchase the company from him in order to close the issue for ever. This is the true meaning of CCM and we all know that.
 
Imeandikwa na Shadrack Sagati;
Tarehe: 1st October 2009

Habari Leo

WAZIRI Mkuu Mstaafu Jaji , Joseph Warioba, amesema, Katibu wa Uchumi na Fedha wa Chama Cha Mapinduzi(CCM), Amos Makala, ni mbaguzi na amemtaka aache tabia hiyo.

Warioba amesema, Makala anaendeleza makundi katika chama hicho na anajipendekeza kwa Rais Kikwete.

Amemtaka Makala atambue kuwa yeye ni kiongozi wa chama kitaifa hivyo asifikiri umri wake mdogo unaweza kumpa kinga ya kutoa kauli zisizo za busara.

“Sisi tulipewa madaraka tukiwa wadogo na ukishakuwa kiongozi ni lazima uwe na busara hivyo umri mdogo sio sababu.”

Warioba amesema, kauli za Makala zinadhihirisha asivyowathamini wana CCM ambao hawakumuunga mkono Rais, Jakaya Kikwete, wakati wa mchakato wa kumpata mgombea urais kupitia chama hicho.

Kiongozi huyo alisema jana kuwa, kauli ya Makala kwamba yeye (Warioba) alikuwa anamuunga mkono Dk Salim inaonyesha kiongozi huyo alivyodhamiria kuendeleza makundi na kuleta mpasuko ndani ya chama.


Warioba amesema, kauli ya Makala pia ina maana kwamba,wana CCM ambao hawakumuunga mkono Rais Kikwete wakati wa mchakato huo hawana nafasi ya kutoa maoni yao kuhusu uendeshaji wa Serikali ya Awamu ya Nne.

Amesema, ni hatari kama Makala haoni matatizo yaliyopo, na amemtuhumu kuwa kiongozi huyo wa CCM anajipendekeza kwa Rais Kikwete aonekane ni mtetezi wake.

“Huyu ni mwanamtandao kwa hiyo haheshimu mwana CCM mwingine ambaye hakumuunga mkono Rais Kikwete…wana mtandao ni tatizo na ndio wanaoendeleza mpasuko katika chama chetu,” amesema Warioba.

“Makala ni kiongozi wangu ndani ya chama kwa nafasi yake namheshimu lakini anaonekana ni mbaguzi wa wana CCM…huyu kwa nafasi yake hapaswi kuendeleza malumbano ya mtandao wakati sisi tunataka mtandao uondoke.” amesema kiongozi huyo ambaye amewahi kuwa Makamu wa Kwanza wa Rais, Tanzania.


Warioba amesema, Makala alipaswa kujibu hoja alizozitoa kuhusu matatizo yaliyopo kwenye jamii kama ya udini, matabaka, ukabila na chama kukumbatia utajiri na si kumtukana kwamba ni mchochezi na ni mfuasi wa Dk Salim Ahmed Salim.

Amesema, wakati anazungumza juzi na wanahabari, hakuishambulia Serikali wala Rais Jakaya Kikwete, ila alielezea mambo anayoona ni tatizo na yanaweza hatarisha umoja wa kitaifa.
“Makala badala ya kujibu hoja hizo, alichofanya ni kunitukana kuwa mimi ni mchonganishi…nataka Makala aniambie ninaposema kuna udini ni uongo? Ninaposema kuna tabaka la matajiri na masikini ni uongo?

“Nilitaka ajibu hoja hizo na sio akwepe na kukimbilia kunishambulia kuwa nalaumu kwa vile nilimuunga mkono Dk Salim (Salim Ahmed) wakati wa mchakato,” alisema Warioba.

Alikiri kuwa wakati wa mchakato wa kumpata mgombea urais wa CCM alikuwa anamuunga mkono Dk Salim, lakini baada ya Rais Kikwete kushinda alishiriki kumfanyia kampeni mgombea wa CCM.

“Mimi sio mtendaji ni mshauri tu. Ninaposema umoja wetu uko hatarini unataka nifanye nini zaidi ya kusema?" amesema wakati anajibu tuhuma kwamba amekuwa akisema tu bila kutoa suluhisho.

“Ninaposema tumeanza kukumbatia udini, utajiri, ukabila, unataka nifanye nini zaidi ya kusema na watendaji walioko madarakani ndio wanapaswa kutafuta njia ya kuondoa tatizo,” alisema kiongozi huyo.

Amesema, wakati anatoa maoni yake alikuwa anawaeleza watanzania wote na wala si wana CCM tu hivyo amemtaka kamtaka Makala aache kuwa mbaguzi, na azifanyie kazi hoja ambazo aliziainisha kwenye mazungumzo yake.

“Sijui anamchukia Dk Salim maana hii si mara ya kwanza kusema, kuna wakati Butiku (Joseph) alitoa maoni yake huyu Makala akasema analaumu kwa vile ni mfuasi wa Dk Salim,” alisema.

Makala katika taarifa yake alimlaumu Jaji Warioba kuwa ni sehemu ya matatizo yanayoendelea nchini kwa kuwa analaumu bila kuonyesha njia ya kuyatatua.
 
someone told me anachosema makala ni views za mkuu wa kaya.
kwa hiyo katika hili ni wazi hakukurupuka bali amemjibia mzee, what pertubs me however ni kwamba huyu dogo atajimaliza kwa kuendeleza siasa za makundi. tayari anajiona ni 'matawi ya juu' kwa nafasi yake kichama na ni mdau mzuri wa mafisadi kwani ndio sehemu kubwa ya wanaounda mtandao.
 
[FONT=&quot;]Makala katika taarifa yake alimlaumu Jaji Warioba kuwa ni sehemu ya matatizo yanayoendelea nchini kwa kuwa analaumu bila kuonyesha njia ya kuyatatua.[/FONT]

Hio ni kweli kabisa.

Warioba japokuwa sio mtendaji tena serikalini, lakini kama ni mwenye ushauri anaweza moja kwa moja akautoa huo ushauri wake kwa hao wanaohusika na hatua zikachukuliwa. Warioba sio mimi na wewe, ni mtu anaeheshimika mpaka leo, kwahivyo, sio mtu wa kupiga kelele magazetini. Kama anaona kuna ubaya fulani unatendeka anaweza kumuona hata Rais JK at any time. Kwanini hafanyi hivyo na anabakia kupiga kelele pembeni tu kama vile ni mlalahoi? Au anataka sisi wananchi tumsikie na tusahau juu ya Mwananchi Gold?

Kama wapinzani wanapiga kelele magazetini tunafahamu, lakini sio yeye. Japokuwa kastaafu bado heshima yake ipo pale pale. Ikiwa sote siku zote tutakuwa tunalaumu tu, sasa nani atatusaidia kutatua haya matatizo? Kwani hao watendaji serikali ni wenye ufumbuzi wa kila kero hata tunawasukumia wao kila kitu?

Kila mtu anajua kuwa udini, ukabila, utajiri, ufisadi, etc etc ndio kero zetu leo katika serikali hii ya awamau ya 4. Kwahivyo, kusema tena na tena juu ya mambo ambayo kila Mtanzania anayajua haisaidii kitu! Mimi na wewe tunaweza kupiga kelele kila siku lakini sio Warioba. Tukitaka kusaidia ni lazima tutowe mbinu za kutatua matatizo. Ni nchi yetu sote sasa kwanini hatutaki kutatua matatizo yetu kwa pamoja na tunajiweka pembenei kila wakati? Mimi na wewe hatutofika mbali, lakini Warioba atafika na atasikilizwa!

In fact, some of these problems that we are facing today in Tanzania have been created during his reign. Haya sio mambo yalioanza jana na leo - hasa huo udini. Au hajui hilo? Wakiwafanyia nini waisalamu katika utawala wao? Is it not right now kwa awamu hii to undo those wrongs?

I hope Warioba will realize that he is doing more harm to this nation by talking to the press than good - this is from the bottom of my heart. Hatutaki afungiwe uhuru wake wa kusema, lakini yeye ni mtu ambae kama angekuenda mbele na kusema basi angelisikilizwa and this nation would have benefited, lakini kama ataendelea kuropokwa kwenye magazeti tu basi hakuna atakae mchukulia kuwa yupo serious!

Au nitaulizwa ninajuaje kama hajawahi kutoa ushauri huko nyuma bila ya kusikilizwa? Kama ni hivyo atueleze!

Kwanini hafuati nyayo za Sh. Ali Hassan Mwinyi? Juzi alikuwa
katika Kata ya Ndungu, jimbo la Same Mashariki, mkoani Kilimanjaro, akiengezea nguvu juu ya kile kinachoweza kuitwa mapigano dhidi ya ufisadi. Yeye sio mwenye kulalamika tu from the corridors of his house in Upanga kuwa nchi imechukuliwa na mafisadi bali anapigana nao huko huko kwenye Kata zao. Please, Warioba, follow his example. Tunataka ukumbukwe kama ni shujaa wa awamu ile na sio mropokwaje wa awamu ile!!!
 
Mkuu Ngida, nadhani kama Serikali ina ushahidi wa kutosha dhidi ya Warioba katika ufisadi wa "Mwananchi Gold" basi wangeharakisha ili kumfungulia mashtaka na "kumziba mdomo" maana atakuwa busy kushughulikia utetezi wake katika ufisadi wa Mwananchi Gold huku wanachama wa mtandao wa ufisadi wakiongozwa na Rostam wakiendelea kupeta mtaani na mabilioni yao ya kifisadi.
 
Mkuu Ngida1, Heshima mbele.

Naomba kutokubaliana na hoja yako kwamba Jaji Warioba hakutakiwa kuzungumza kero au kutoa maoni yake kupitia vyombo vya habari.Jaji Warioba katoa maoni au ushauri kupitia vyombo vya habari kwa maoni yangu hii ni njia sahihi kwasababu ushauri ulitakiwa uwafikie wengi na si Muungwana pekee yake.

Kuna kila dalili Muungwana kashindwa kutuondolea kero za rushwa,udini,ukabila na ufisadi pengine sababu yaweza kuwa si yeye kama rais wa JMT bali kundi kubwa la wanamtandao kama Makala hawataki mabadiliko.Si siri tena wanamtandao waliompeleka Muungwana pale Magogoni wengi wao wanakabiliwa na kashfa nzito lakini kwa mshangao bado wanaendelea kushikilia nyazifa nzito ndani ya chama cha mapinduzi na serekalini.

Kamati kuu ya CCM imejaa wajumbe wenye kila aina ufisadi.Kamati kuu ni chombo cha juu kabisa cha CCM na kinategemewa kutoa mwongozo na maamuzi makubwa kwaajili ya maendeleo ya Tanzania.Kamati kuu inapokuwa na wajumbe kama Makalla,Lowassa,Chenge,Kinana,Kingunge na wengineo kibao tegemea ubabaishaji kama majibu ya Makalla kwa Jaji Warioba.



 
Last edited:
someone told me anachosema makala ni views za mkuu wa kaya.
kwa hiyo katika hili ni wazi hakukurupuka bali amemjibia mzee, what pertubs me however ni kwamba huyu dogo atajimaliza kwa kuendeleza siasa za makundi. tayari anajiona ni 'matawi ya juu' kwa nafasi yake kichama na ni mdau mzuri wa mafisadi kwani ndio sehemu kubwa ya wanaounda mtandao.

Au uenda ni knee jerk reaction kama kawaida ya court jesters kama Bwana Makala. Hawaangalii hoja na kufanya tafakuri ila wao ni kumtetea mfalme hata kama yuko "nusu uchi"! Kumkosoa JK unatangaza uadui. Kila kitu kwao ni shwari na kazi yao kubwa ni kusema sawa mzee. With friends like Makala JK does not need enemies. Wanatosha.
 
Hi Ngida,
<In fact, some of these problems that we are facing today in Tanzania have been created during his reign. Haya sio mambo yalioanza jana na leo - hasa huo udini. Au hajui hilo? Wakiwafanyia nini waisalamu katika utawala wao? Is it not right now kwa awamu hii
to undo those wrongs?>

Ni mimi mtani wako hapa. Naona hapo juu umekosea. Warioba alifanyakazi na Mwinyi na kama unataka kumlaumu katika mambo ya udini basi itabidi umlaumu Mwinyi. Pia na huyo Mwinyi huko kwenye Kata anakuenda kujitakasa tu. Yeye sie aliyewaweka akina Rastam mbele? Pia kama Mwinyi angelilishikilia Azimio La Rushwa leo tungelikuwa wapi Watanzania?
Anyway, ninafurahi kuwa makada wa CCM kumbe wamo humu kwenye mtandao na wewe ndio kweli NAMBARI ONE!!!
Anyway, usikose kuja leo saa zile zile.
 
Mkuu Ngida, nadhani kama Serikali ina ushahidi wa kutosha dhidi ya Warioba katika ufisadi wa "Mwananchi Gold" basi wangeharakisha ili kumfungulia mashtaka na "kumziba mdomo" maana atakuwa busy kushughulikia utetezi wake katika ufisadi wa Mwananchi Gold huku wanachama wa mtandao wa ufisadi wakiongozwa na Rostam wakiendelea kupeta mtaani na mabilioni yao ya kifisadi.

Dear Bubu Ataka bin Kusema,
Kumfungulia mashtaka hilo halitotokea. Kama ni kufungua mashtaka wangelifunguliwa akina Mkapa, Chenge, etc etc.
Hii ni CCM na wanaruhusu uchukue chako mapema, lakini ufunge mdomo wako tu, ili wengine nao wafanye hivyo hivyo.
 
Dear Bubu Ataka bin Kusema,
Kumfungulia mashtaka hilo halitotokea. Kama ni kufungua mashtaka wangelifunguliwa akina Mkapa, Chenge, etc etc.
Hii ni CCM na wanaruhusu uchukue chako mapema, lakini ufunge mdomo wako tu, ili wengine nao wafanye hivyo hivyo.

Kumbe unalijua hilo eh! mbona hukumuweka papa wa mafisadi Rostam katika hiyo list!? Hii Serikali yote imejaa mafisadi ndiyo maana kamwe hawatamgusa Warioba kwanza sidhani kama wana ushahidi wa kutosha dhidi yake. Pili, Warioba anaweza kabisa kuwageuzia kibao kutokana na uchafu mkubwa anaoufahamu kuhusu Serikali iliyo madarakani na pia jinsi jamaa alivyobebwa na mtandao hadi kuwa mgombea wa CCM 2005. Dar na Dodoma patakuwa hapatoshi kama Warioba akiamua kuongea.
 
Back
Top Bottom