Waraka wangu kwa viongozi wa CHADEMA

Kama kweli ulikuwa na nia ya dhati haya mambo ungeyapeleka makao makuu ya cdm sababu yanawahusu wao, hapa JF ni mambo ya kitaifa ndio mazuri kuyaleta kwa majadiliano ili inapotokea mtendaji wa serikali amepitia hapa apate mawazo. mimi naona kama unataka kuonyesha kwa kificho kuwa CDM ina matatizo makubwa ya kiutawala na kiutendaji ambayo watu hawafahamu kitu ambacho si dhani kama utapata majibu mazuri sana kwa sababu wananchi wa leo sio wajana na wana akili kuzidi wanaojiita wasomi na tofauti yao ni vyeti tu na nadharia walizozikariri kwa lugha ya kigeni.
 
Mkuu Mkandara, nakushukuru wewe umeliona hili, kama CCM itamsimamisha mtu safi asiye na mawaa ni kweli Chadema itakuwa na kazi kubwa 2015. Prof. Mark Mwandosya they've already done him!, Asha Rose ni msafi na hana mawaa yoyote ila binafsi yangu, sipendi asimamishwe yeye kwa sababu zile zile ambnazo sipendi simamishwe Dr. Shein. Japo mgombea wangu kwa CCM, 2015 ni EL, inside trends zinaelekezwa kwa Benard Membe!.

Nimewashauri Chadema waachane na politics of confrotations, wapunguze mashambulizi kwa CCM as an entity, waconcentrate na watu ambao ndio wapiga kura!. Nikasema determinant ya ushindi wa Chadema 2015, lies with who will stand on CCM ticket, with M4C, there is hope but msipokuwa makini, 2015 Ikulu mtaishia kuisikia tuu kwenye bomba!.

Pasco.
Pasco,
Tatizo ni kwamba CCM haina mtu safi wa kusimamisha. Na walioshika mipini ya uamuzi ndani ya chama hivi sasa wote ni mafisadi na watahakikisha wanalindana. Asha Rose si msafi kama baadhi yenu mnavyofikiria. Hebu kamuulize Lowassa anazo data za huyo mwanadada. Kama CCM wameshindwa kitu kidogo tu cha kujivua gamba, kweli wataunganaje kumpata kiongozi aliye safi?
 
Mheshimiwa Mwenyekiti, katibu mkuu wa chama, viongozi wa chama ngazi ya Taifa, mikoa na wajumbe wa mabaraza yote ya chama ngazi zote.. leo nachuua nafasi hii kuwapa summary ya mjumuiko wa utafiti wangu kuelekea uchaguzi wa mwaka 2015 kuzungumzia hali halisi. Yamkini waraka huu umelenga jambo moja tu muhimu sana ktk mapitio yangu ya siasa za Tanzania na hasa mapenzi yangu ya dhati kwa chama cha Chadema na uongozi wake kutika maendelezo ya kukijenga chama hasa ktk wakati huu kuelekea uchaguzi wa mwaka 2015.

Ni baada ya kusoma mada kadhaa humu JF ambazo binafsi yangu nimezisoma kwa umakini mkubwa ktk kutazama fikra za wananchi mbalimbali ikiwa ni pamoja na hoja, maoni na mitazamo wa wanajanvi nimekuja na waraka huu makusudi kukinusuru chama hiki kuepukana na umaarufu wa muda. Waheshimiwa, tujihadhari sana na umaarufu wa muda ama kutukuza wingu hili la umaarufu wa muda kwa sababu lengo kuu la ujenzi wa chama hiki ni kupigania dhamana ya wananchi kuwapa mamlaka ya kuongoza nchi yetu na watu wake. Tukumbuke tu ya kwamba ngoma ikivuma sana mwisho wake hupasuka.

Hivyo basi mada nilizozitazama na kuzipa uzito mkubwa ni kama zifuatavyo:-
1. Mchambuzi Bofya
2.
Profesa Bofya na
3. Ibambasi Bofya

Waheshimiwa,
Mada hizi nimezipa uzito kutokana na nafasi ya chama kuelekea uchaguzi wa mwaka 2015. Zote hizi zimebeba uzito mkubwa sana wa tafiti zangu ktk jukwaa hili la Siasa pamoja na mkusanyiko wa hoja na mawazo ya wadau ambao kwa kuelewa ama kutoelewa wameweza kuonyesha wazi tofauti zao za kisiasa, kiimani na hata kujenga matumaini hasi japokuwa chama hiki hakitakiwi kabisa kupoteza dira yake kwa manufaa ya mtu ama baadhi ya watu.

Ikumbukwe tu kwamba wananchi wa nchii hii pamoja na tofauti zao bado ni Watanzania wenye kuthamini mila na desturi zao, wanaothamini imani zao za dini, UTU wao na wanaotukuza Ujamaa kama msingi bora na wajibu wa kila mmoja wao kulingana na hali na mali hivyo kufikia kuwapeni dhamana kubwa ya kusimamia UHURU, HAKI na USAWA kwa wawananchi wote wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Tunapodharau vitu hivi kama chimbuko la WATU wenyewe kwa kuaminishwa kwamba tunaweza kuwazuia WATU kutoamini (exclusive) badala ya kuwawezesha wao kutumikia imani zao kama sehemu ya jamii yetu (inclusive) basi tuondoe tumaini la ushindi ifikapo 2015.

Waheshimiwa,
Toka kujiunga kwangu JF nimejifunza mengi sana na nimepanua kiwango changu cha ufahamu wa Mtanzania hasa ktk hali ya Umaskini, Ujinga na maradhi. Nimeweza kuzifukua nyoyo za watu katika maabara ya fikra, hisia na kutazama tatizo hasa linatokana na ukweli upi. Hivyo kama saini yangu (signature) miaka yote hapa JF isemavyo (signature) ni wajibu wangu kuendeleza kile nachokiamini ktk ku explore reality, na nimegundua rasilimali kubwa ambayo chama kinachotaka kuongoza kitakumbana na vikwazo gani na kwa gharama gani. Hivyo kughairi haya ni sawa na kutafuta dhahabu, mafuta au gasi ktk nyanda za mbuga tupu au jangwani..

Hata wachimba Dhahabu, mafuta au gasi nchini huanza na exploration wakajua maliasili hizi zinapatikana wapi precisely, kisha ndio shirika la uchimbaji huchukua report hiyo na kuifanyia kazi.. Hii ndio kazi yangu kwa leo. Kazi yangu ni kuwapa ushauri viongozi wa Chadema tokana na utafiti wa mijadala mbalimbali na hapa JF na nje ya ukumbi huu ktk mkusanyo wa fikra mbalimbali zinatujenga jamii hii ya Kitanzania.

Waheshimiwa,
Kama tulivyowahi kuzungumza awali kuhusu nafasi ya Chadema ktk utawala na maandalizi ya chama kugombea mwaka 2015, bado nina imani kubwa na chama lakini bado kabisa chama chetu kimeshindwa kupasua ngome ya CCM ipaswavyo na kujenga imani za wananchi kwa chama hiki. Kinachotokea ni kujaribu kwa chama chetu kuwavuta wanachama wa CCM zaidi ya kuwavuta wananchi kuichagua Chadema. Kauli mbiu kama VUA GAMBA vaa GWANDA ni moja ya kauli nyingi zilizoonyesha wazi vita ya chama hiki ni kupambana na uongozi wa CCM badala ya kupambana na sera za CCM zilizotufikisha hapa tulipo.

Ebu tutazame Mchambuzi ktk mada yake utagundua kwamba Chadema inajaribu sana kufanya wajibu wake ‘Do the right thing’ kukemea Ufisadi, utawala wa mabavu, mapungufu ya JK na kadhalika lakini tumeshindwa kuyafanya ipaswavyo ‘Do things right’ hivyo tunashindwa kujenga uaminifu kwamba Chama hiki kitaweza kurekebisha kero za wananchi. Na hivyo wale walioko vyama vingine mbali na CCM wamekosa tujmaini, wale wasiokuwa na mapenzi ya siasa hawana imani na vuyama mvyote na hata wale wanaokichuka chama CCM hatuwapi matumaini isipokuwa kujiunga chama uanachama..

Waheshimiwa, sio mwanachama atakaye tupa ushindi mwaka 2015, bali mwananchi mlalahoi anayetakiwa kwenda ktk sanduku la kupiga kura siku ya Uchaguzi na kutupa imani yake kwenye kipande cha karatasi kama tumaini lake kwa miaka mitano ya uongozi wa nchi hii..

Ndugu Mchambuzi kaorodhesha mambo tisa na haya yana umuhimu wake ktk kumtambua adui yako ngao zake.. Japokuwa ngao hizi haziwezi kuwapa ushindi pasipo mashambulizi ya nguvu ambayo yanategemea na silaha walizonazo..Hivyo katika mada nzima ya Mchambuzi tumeona ngao kubwa za chama CCM ambazo zinaweza tu kutupa matumaini ya ushindi ikiwa tutaweza kuwa na silaha za kuzibomoa.

Hapo hapo tukumbuke tu kwamba nasi tuna ngao gani ambazo zinaweza kuvumilia makombora ya CCM maana ushindi wa vita hii hautokani na kushambulia tu.. Ukweli ni kwamba Chadema hatuna defence zaidi ya kushambulia na kwa bahati mbaya mara kwa mara hushindwa hata kujitetea isipokuwa wa tu kukimbia kimbia maporini kama wakimbizi wa vita au insurgents.

Na kwa nini basi tumeshindwa kuwa na ngao ktk mashambuliz makali yanayoelekezwa kwetu?. Jibu nalipata kwa Mchambuzi tena akisema hivi:- Leo hii masuala ya Uongozi na siasa yametawaliwa sana na misingi ya UKANDA, UKABILA na UDINI. Mheshimiwa hili tupende tusipende ndivyo watanzania watawahukumu viongozi wetu kwa sababu ndivyo siasa za nchi hii zimejikita iwe kutokana kupoteza dira ya Kitaifa, kuwepo kwa vyama vingi ama hisia na wajibu wa viongozi wenyewe kuwajibika ktk makundi ya watu wanaowawakilisha.

Waheshimiwa,
Hii ni tahadhari kubwa sana kwa chama na hasa vyama vya Upinzani ambavyo vimetokana ama kuasisiwa na watu waliopingana ndani ya utawala wa CCM hivyo kuanzisha fikra mpya kinzani ili mradi kujaza ubao wakati nyuma ya pazia hilo kuna KUJUANA..Ni rahisi kusema CCM imeshindwa kutuongoza kwa miaka 50 na watu wakakuelewa lakini ni vigumu sana kuwavuta wananchi ikiwa wataona chama kimeshindwa kupambana na siasa za KUJUANA ndani yake hivyo nje wataweza vipi?.. maana tunawalaumu CCM kwa kujuana lakini pia vyama vyote nchini vinafanya mambo yake kwa KUJUANA.. na pale ngome hii inaposhambuliwa vyama hivi hushindwa kujitetea.

Naye Profesa anawekamaswali yanayowakabiri wananchi wengi sana naomba ninukuu.. anasema kuhusu vyama vyetu vikuu vitatu kati ya CCM, Chadema na CUF ya kuwa –
“Nani kati ya hawa watatu ambao bila ubishi wanashikilia hatamu ya siasa za Tanzania, atatupeleka kwenye nchi yenye neema na amani kwa watu wote bila kujali itikadi, hali yao kiuchumi, kisasa, kidini au kiasili? unahitaji nini kati yao, moja wapo ya chama hiki au Kiongozi kati yao atakaebadilisha upepo na kutuepusha na mgao unaofanywa na vyama vyote hivi (kwa manufaa ya hao wanaoongoza vyama hivi kwa kuwa wanataka kuendelea kuwepo madarakani?) Huko madarakani kuna nini?

Nani atatuambia tutatokaje na siku moja itakayolengwa kwa sisi kuwa sehemu ya taifa Afrika, au Duniani imara kisiasa, kiuchumi, kiutamaduni na kimaendelo kwa ujumla (sayansi, usalama wa chakula, nafasi sawa ya elimu kwa wote, huduma za afya wote, maji safi kwa wote, ziada ya fedha, dhahabu na mafuta ambavyo tunavyo na kila mtu akimvumilia mwenzake na kumheshimu).”

Waheshimiwa,
Mawazo haya sii ya kutafanyia mzaha hata kidogo. Ni mawazo yanayofikiriwa na Watanzania wengi nchini, Watanzania ambao wanajaribu sana kutazama chama mbadala ambacho kinajaribu kwa kila hila kuwajumuisha watu wote ktk Utanzania wao pasipo kujali tofauti zao. Na hatuwezi kuwezesha jambo hili pasipo kuwaunganisha (Inclusive) kama jamii moja badala ya kuwatenga (exclusive) baadhi kwa fikra za kwamba ni wao, wale, hawa ni tofauti na sisi hivyo kama wanataka wayapendayo wafanye wenyewe hili sii jukumu la serikali au uongozi kuwavuta hawa ndnai ya jamii yetu..

Waheshimiwa,
Ndugu Ibambasi katika makala yake naye pia amehoji ushiriki wa serikali hii ktk shughuli za dini, amehoji mambo mengi japokuwa kajiweka ktk kundi la wale wasiokuwa na imani za kigeni isipokuwa za jadi zetu na kudai haki yao kikatiba ili kulindwa na kupewa fursa sawa ktk kushiriki ibada zao. Binafsi yangu pamoja na kutokubaliana juu ya tafsiri fasaha ya ibara inayozungumzia kuwa NCHI yetu haina dini isipokuwa WANANCHI wake ndio wenye dini hushindwa kuelewa nini maana ya NCHI na nini maana ya WATU ikiwa serikali haitawawezesha watu wake wenye dini zao kushiriki ktk ibada zao. Lakini ni muhimu kuyasikia maombi, mawazo kama haya na kuyapatia majibu wala sii kuyapuuza ama kuyazuia kunaweza kutupatia ufafanuzi kamili..

Nchi yetu haina dini kwa maana kwamba mihimili ya utawala wa nchi yetu haitakiwi kuundwa ama kujenga policies zinazotokana na imani ya dini moja isipokuwa serikali inawawezesha wananchi wenye ibada zao. Kuwakwaza wananchi kuabudu kama walivyofanya China na Urusi ni kuondoa ama kupokonya sehemu isemayo watu wake wana dini. Kupingana na mawazo ya kiimani kwa kutunga sheria moja kwa wote itatafsirika tu kama exclusive ama sheria ya kuwatenga wao hivyo kuzaa underground movement kupingana na sheria hiyo. Imetokea sana nchi zilizowakwaza waumini wa dini au kuwayenga makabila kama Wayahudi nchi za Ulaya.

Na Mataifa makubwa yote tokea Roman Empire hadi utawala wa Marekani leo wameanguka ama kupata mtihani mkubwa pale wanapojaribu kuwatenga watu kwa kutumia dini, kabila au tamaduni zao hivyo ni muhimu sana kwa chama hiki kuzingatia pamoja na kwamba serikali haina dini lazima tukumbuke wananchi wetu wana dini zao na makabila yao, wana maumbile yao hivo ni lazima vienziwe na sio kupigwa vita. Tunapiga vita wale wanaojaribu kukwaza wengine, wale wanaojaribu kuleta Ukabila na Udini (kudharau wengine) lakini sio wale wanaoitaka haki ya kuabudu kama alivyosema Ibambasi kwa utetezi wa waumini wa jadi..

Waheshimiwa, Inabidi nikomee hapa ktk waraka huu ambao unasisitiza zaidi kujitazama upya. Kutazama makundi ya jamii zetu kama sehemu ya Utaifa wetu badala ya kujaribu kuwabadilisha ama kuwakwaza. Chadema ktk hali hii inahitaji sana nguvu ya Watanzania wapiga kura ambao kwa nafasi zao hawawezi kushawishika na Utaifa ulojaa KUJUANA na sii rahisi wanaongoa watu wasikuwa na Imani.

Hivyo, Tuache UNAFIKI, tuache kujidanganya kwa unafiki wa wapambe wa vyama wanaotumia siasa kaa uwanja wa kujuana. Sisi sote ktk nafasi tulizopo na kutambua kwamba Utanzania wetu unajumuisha tofauti zetu za maumbile, makabila na imani za dini na yeyote atakaye jaribu kumdharau hata mmoja wetu ni kielelezo cha Ubaguzi ambao hautakiwi kupewa nafasi bali kuupiga vita. Hizi ndio ngao zetu, ndizo zinazo tu identify kama jamii ya Kitanzania na lazima tuzilinde dhidi ya siasa za chuki na uutengano. Bila utayari wa kuwajumuisha watu wote kwa tofauti zao kama sehemu ya Utanzania wetu itakuwa vigumu sana kupata ushindi mwaka 2015 maana CCM wanaifanya kazi yao ipaswavyo – Kushambulia nasi ktk kujilinda lazima tuwe na kinga zetu kwa kufanya vitu sawa – Doing things right !

Nawakilisha..
Braza umejaribu kuongea kwa kirefu lakini nadhani unaelewa ila unajilazimisha kutoelewa, sitaongea sana ila nitaelezea baadhi ya main points zako,

(1) Doing things right (kuleta maendeleo shule, kupunguza umaskini, matibabu n.k.

(2) Swala la kujuana na udini na ukabila ndani ya CHADEMA, nitajibu haya machace naamini viongozi wengine watajibu mengine au watatoa maelezo yakina

(1) DOING THINGS RIGHT!! -
CHADEMA haikufanikiwa kuongoza serikari ya Tanzania, haikutangazwa Mshindi kwa mujibu wa Katiba yetu, lakini ilifanikiwa kwenye majimbo machache na kata chache ambazo baadhi yake imeunda almashauri za wilaya na majiji na uongozi wake unaenda safi na kama ikitokea kuna ibadhirifu wowote somo la kulindana chadema ilifeli hivyo hatua stahiki huchukuliwa dhidi ya yeyote aliyehusika, mfano ni Madiwani Arusha na Jana Madiwani 2 Mwanza,

Chadema hakiwezi kubadilisha hali ya uchumi wa Tanzania kwa sasa sababu serikali ya CCM ndiyo ipo madarakani na Chadema kama chama cha siasa kina pata Million 200+ kila mwezi ambazo ni ruzuku ya kazi za chama, masharti yamewekwa juu ya pesa hizi na zinatumika sawa sawa kwa mujibu wa sheria na ndio maana taasisi inayotoa haihoji

(2) UDINI NA UKABILA
CHADEMA ni ya wanachama kila mwanachama ana dini na kabila lake, hizi ni propaganda zilizopitwa na wakati, wangekuwa ni mapagani ungesemaje? labda nitakushangaa ni dini gani hasa iliyopo CHADEMA maana wapo wakristo na waislam na madhehebu mengine kadha wa kadha, haya ni kabila gani lililopo CHADEMA?

CHADEMA iliasisiwa na watanzania wenye dini tofauti tofauti na wenye makabila tofauti ila watu wa kaskazini ndio walianza kuikubali CHADEMA na kuipa imani ya kuwaongoza na kama mrengo wa chama ungekuwa ni ukabila Makao Makuu ya CHADEMA yasingekuwa Ufipa kinondoni yangekuwa Moshi au Arusha nenda kwenye safu za viongozi wa CHADEMA then angalia ratio ijapokuwa wakati wanachaguliwa wapiga kura hawaongozwi na udini, kwani Zanzibar Chadema haina wanachama wakristo? mbona viongozi wa CHADEMA kule ni waislamu tupu?

nafarijika watanzania wa leo sio wale wa miaka ilee sasa hawaogopi vitisho wapo mstari wa mbele CHADEMA tunatoa elimu ya kubadilisha fikra za mtanzania sababu hata kama SERIKALI ifanyeje wananchi wamesha choka

VIVA M4C
 
Pasco,
Tatizo ni kwamba CCM haina mtu safi wa kusimamisha. Na walioshika mipini ya uamuzi ndani ya chama hivi sasa wote ni mafisadi na watahakikisha wanalindana. Asha Rose si msafi kama baadhi yenu mnavyofikiria. Hebu kamuulize Lowassa anazo data za huyo mwanadada. Kama CCM wameshindwa kitu kidogo tu cha kujivua gamba, kweli wataunganaje kumpata kiongozi aliye safi?
Jasusi swala sio CCM isipokuwa ni CDM wamejiandaa vipi kupambana na missile za CCM na CUF maana Simba alojeruhiwa ni mbaya zaidi ya yule mwindaji..
Pasco ana point kubwa sana kama utawatazama wadanganyika kwa makini. Hao Magamba wote wanaotakiwa kuvuliwa ndio watu wanaopendwa nchini kuliko wasafi.. EL anaweza kupita uchaguzi wowote jimboni kwake au kitaifa. Chenge, Rostam hawa wote wanaweza kupita uchaguzi kwao pasipo kwa kura zaidi ya 80 fumba fumbua na hawa ni mafisadi kama tunavyowaita..

Binafsi yangu sidhani ni busara sana kutegema kuanguka kwa CCM ikiwa sisi wenyewe tunashukiwa kwa mambo ambayo tunaamini sio kweli. Unajua mkuu wangu Udini na Ukabila sii swala la kudharau kabisa. Ni sawa kabisa na kusingiziwa Ukimwi hivyo mapungufu ya CCM hayawezi kuonekana mazito kuliko haya ya Ukimwi. CCM inaweza kuwa imechoka lakini kumbuka kuchoka kunasameheka ikiwa wataweza kubadilisha Upepo.

Hivi tuseme mathlan Mh. Membe/AshaRose kasimama na kuahidi kupambana na mafisadi, akaahidi kama alivyofanya JK kuponda ya Mkapa japokuwa wako team moja. Kumbuka mkuu wangu CCM ilichoka baada ya Mkapa kuondoka. Kulikuwa na scandals nyingi wakati wa Mkapa kuliko leo tena nadhani waislaam waliichukia sana CCM kutokana na Mkapa. Kulikuwa na mvutano mkubwa ndani ya chama baina ya Salim, Mwandosya, Sumaye na Kinana wote hawa wakiwa na makundi yao ya mtandao. Lakini tazama alipochaguliwa JK tu.. Huyu hakuwa na sifa zozote unazojaribu kuzijenga hapa lakini aliondoka na asilimia 80..labda nikumbushe JK alikuwa na sifa gani hadi akapata asilimia 80 ya kura za waanchi?..

We should never underestimate CCM. Besides,l wanaopiga kura ni wananchi na muhimu zaidi Rais huchaguliwa kwa Popular vote na sio electral vote, hivyo michango yote hapa JF iwe kutoka kwa Pasco, Munishi au Ritz tuisome, tuitafakari na siii lazima tuifuate isipokuwa inatufundisha jinsi gani watu wengine wanatutazama.
 
Mkandara,ccm imekuwa kama nyani anayekufa,kama unavyojuwa,huwa nyani huyo hujaribu kukamata matawi ya miti ili kujiepusha kwenda chini kwenye safari hiyo ya kifo.

CCM,imeamuwa kuwatumia waislam kama matawi ya miti ya kujishikilia inapoanguka kwenye kifo chake.Ni wajibu wetu kuangalia ni kivipi hilo halitotokea.Ni wazi wata capitalize kwenye maeneo ya waislam ili kuzidi kuleta ile chuki pamoja na kuhaikisha wanakufa na wengine.Nguvu zao zote watazielekeza kwenye kushikilia matawi hayo(waislam).

Wanachotakiwa kufanya chadema,ni kuendeleza mapambano haya kama kawaida.Kama kunawatakaokuja na waje(waislam,wakristo,wakristu,wapagani etc),ila si vyema wajikite kwenye kujaribu kuonyesha hili ama lile ili kupata sura ya kuwafurahisha watu wa imani hii ama ile.

Kama chadema inapita nchi nzima,na kusikiliza matatizo ya watanzania,basi watakutana na maoni hayo kama yapo.

Ushahidi upo wazi kabisa na kama unakumbuka,JK kwa kupitia yule Rashid Shamte,walituma zile message zilizopanda chuki hizi.Na funny enough,kuna waliozinunuwa na kuziamini

Halafu kuna maopportunist kama mh Zitto,yeye nadhani anasikia raha sana kufikia hapo alipo bila kutumia dini yake,lakini anataka kufanikisha malengo yake ya juu zaidi kwa kutumia hilo hilo la dini.Na nilishasema huko nyuma kuwa chadema ina waislam wengi tu,la muhimu ni kuwarecruit wale ambao wana sifa za uongozi na pia wenye kuijali Tanzania na utaifa wao.Hao wako wengi tu.Cha muhimu,ni kuhakikisha si wabinafsi,maana kuna watu wanaitumia sana karata ya udini kufanikisha malengo ya binafsi na ya kisiasa.

Kwa kifupi,aliyoyasema Semilong,nilishayasema vilevile,kama chadema tayari ina waislam,basi ianze nao na si kwenda kujaribu kuwatafuta hao wasiokuwa na imani ama walioaminishwa hayo ya mafisadi wa ccm.

Ninakuhakikishia kabisa kuwa kama harakati hizi za ukombozi tutakuwa tunataka kubalnce viongozi based on religion affiliation,basi hilo linaweza kukwamisha ukombozi.Kwasababu kama tutawaondoa viongozi wenye uwezo na kupachika wasiokuwa na uwezo ili tu kuweka balance ya dini,basi hapo ni kupotoka na itakuwa sawa na kuondoa "eye on the prize",ama kwa kifupi ukombozi wa mtanzania unaweza ukawa jeorpodized,unapoweka viongozi kwa misingi hiyo.

Na kiongozi huyo akijuwa kuwa amewekwa hapo kwa misingi hiyo,basi sitoshangazwa kuona akitaka kubaki hapo kwa misingi hiyohiyo hata kama amevurunda,huko sidhani kama chadema inataka kwenda.

I'm just saying.
 
Last edited by a moderator:

Mkandara,
Kikwete aliandaliwa ndani na nje ya nchi.
 
UKANDA, UKABILA na UDINI.
Chadema wanatakiwa kuyafanyia kazi kubwa sana haya mambo matatu yanayotumiwa sana kuwashambulia.

Hoja nyingi zinazozungumzwa na WAISLAMU kuhusu maslahi yao kutoka kwa wanasiasa sio za kubezwa harakaharaka, Hatakama zinamapungufu makubwa, zina madhara makubwa kwakuwa wao pia ni sehemu ya wanachama na ni idadi kubwa ya wapiga kura kwa Chadema.ikumbukwe pia haohao waislamu wanaodaiwa kuwa wengi wao hawana elimu dunia lakina wanayosifa mkononi ya kupiga kura CDM washike dola (kwani Primary goal si ni kuingia ikulu na kukamata dola?)

Suala la tuhuma za Mfumo wa uongozi wa CDM kujaa watu WAKASKAZINI na UKABILA hata kama kuna hoja za msingi za kulitetea ni lazima litupiwe macho mawili kwa lengo Kuepusha kuwa kama silaha kubwa za mahasimu wao.Upo ushahidi pia ndani ya CDM kuna kama familia 1 ya wa wabunge;ambapo kuna Mume,Mke,Mtoto na wakwe zao kwa pamoja.

Nashauri pia hoja nyingine za kukikosoa chama ni sehemu nzuri ya kukijenga pia badala ya watu wachache ku defend kwa nguvu zote huku mambo yanaanza kuharibika polepole.Miaka mitatu bado ni mingi kwa chama kama CCM kufufuka kwa kutumia hila, zengwe, Jeshi, Fitina na Kununua viongozi njaa kutoka CDM, mauaji ya siri, na kuinfluency taasisi zake zote inazozishikilia kama Mahakama,Tume ya uchaguzi na Polisi.Na kwa hii historia ya siasa za Tanzania bado kigezo cha nguvu za ushabiki au kujaza mikutano bado sio kigezo cha kukamata dola.Kushinda kwa kura au Kutangazwa mshindi ni vitu viwili tofauti hasa kwa hizi siasa za zengwe za bara la Africa.
 
Kama kweli ulikuwa na nia ya dhati haya mambo ungeyapeleka makao makuu ya cdm sababu yanawahusu wao, hapa JF ni mambo ya kitaifa ndio mazuri kuyaleta kwa majadiliano ili inapotokea mtendaji wa serikali amepitia hapa apate mawazo. mimi naona kama unataka kuonyesha kwa kificho kuwa CDM ina matatizo makubwa ya kiutawala na kiutendaji ambayo watu hawafahamu kitu ambacho si dhani kama utapata majibu mazuri sana kwa sababu wananchi wa leo sio wajana na wana akili kuzidi wanaojiita wasomi na tofauti yao ni vyeti tu na nadharia walizozikariri kwa lugha ya kigeni.

Mkuu nimefuatilia kwa karibu sana mjadala huu tangu ulipoanza. Nimekuwa nikijizuia kusema kama ulivyosema hapa lakini nashukuru kwa kuliona hilo.

I agree with u for 100%
 
Sehemu zingine au kubwa nimeona lawama nyingi kwa cdm, kwamba wanapigana vita wasiyoijua. Kwamba wanang'ang'ana na vua gamba badala ya kupandikiza ukweli kwenye fikra za watu. Tangu operation sangara hadi m4c kweli hakuna cha maana kilichofanyika? Yani tangu 2010 hakuna ambacho cdm wamefikia? Bila nguvu ya Dola ungetaka cdm ipambane vipi zaidi? Wao wana tbc, polisi, uwt, mahakama, Bunge, n.k na ndio maana unaona kuwa ccm inashambulia. Pia naomba utufafanulie upya kuhusu kujuana
 
Mkandara,ccm imekuwa kama nyani anayekufa,kama unavyojuwa,huwa nyani huyo hujaribu kukamata matawi ya miti ili kujiepusha kwenda chini kwenye safari hiyo ya kifo.

CCM,imeamuwa kuwatumia waislam kama matawi ya miti ya kujishikilia inapoanguka kwenye kifo chake.Ni wajibu wetu kuangalia ni kivipi hilo halitotokea.Ni wazi wata capitalize kwenye maeneo ya waislam ili kuzidi kuleta ile chuki pamoja na kuhaikisha wanakufa na wengine.Nguvu zao zote watazielekeza kwenye kushikilia matawi hayo(waislam).

Wanachotakiwa kufanya chadema,ni kuendeleza mapambano haya kama kawaida.Kama kunawatakaokuja na waje(waislam,wakristo,wakristu,wapagani etc),ila si vyema wajikite kwenye kujaribu kuonyesha hili ama lile ili kupata sura ya kuwafurahisha watu wa imani hii ama ile.

Kama chadema inapita nchi nzima,na kusikiliza matatizo ya watanzania,basi watakutana na maoni hayo kama yapo.

Ushahidi upo wazi kabisa na kama unakumbuka,JK kwa kupitia yule Rashid Shamte,walituma zile message zilizopanda chuki hizi.Na funny enough,kuna waliozinunuwa na kuziamini

Halafu kuna maopportunist kama mh Zitto,yeye nadhani anasikia raha sana kufikia hapo alipo bila kutumia dini yake,lakini anataka kufanikisha malengo yake ya juu zaidi kwa kutumia hilo hilo la dini.Na nilishasema huko nyuma kuwa chadema ina waislam wengi tu,la muhimu ni kuwarecruit wale ambao wana sifa za uongozi na pia wenye kuijali Tanzania na utaifa wao.Hao wako wengi tu.Cha muhimu,ni kuhakikisha si wabinafsi,maana kuna watu wanaitumia sana karata ya udini kufanikisha malengo ya binafsi na ya kisiasa.

Kwa kifupi,aliyoyasema Semilong,nilishayasema vilevile,kama chadema tayari ina waislam,basi ianze nao na si kwenda kujaribu kuwatafuta hao wasiokuwa na imani ama walioaminishwa hayo ya mafisadi wa ccm.

Ninakuhakikishia kabisa kuwa kama harakati hizi za ukombozi tutakuwa tunataka kubalnce viongozi based on religion affiliation,basi hilo linaweza kukwamisha ukombozi.Kwasababu kama tutawaondoa viongozi wenye uwezo na kupachika wasiokuwa na uwezo ili tu kuweka balance ya dini,basi hapo ni kupotoka na itakuwa sawa na kuondoa "eye on the prize",ama kwa kifupi ukombozi wa mtanzania unaweza ukawa jeorpodized,unapoweka viongozi kwa misingi hiyo.

Na kiongozi huyo akijuwa kuwa amewekwa hapo kwa misingi hiyo,basi sitoshangazwa kuona akitaka kubaki hapo kwa misingi hiyohiyo hata kama amevurunda,huko sidhani kama chadema inataka kwenda.

I'm just saying.
Unachkosea ni pale unaposema CDM haihitaji kwenda kwa wale wasiokuwa na imani..Swala hapa sio kutafuta wanachama bali wapiga kura na hawa ndio watatuweka IKULU.. Nisome vizuri ktk waraka wangu utagubndua nachosema kuwa wanachama sio wanatuweka IKULU bali wapiga kura. Tanzania nzima CCM mina wananchama wasiozidi mil 4 na ujumla wa nyama vyote sidhani kama wanafika mil 6 wakati wapiga kura ni mil 12 pengine hesabu hiyo mitaongezeka ifikapo mwaka 2015.

Hawa watu wasioonekaa hawa, ndio wanaweza kutupa ushindi na sio wananchama ambao nguvu kubwa inatumika na vyama vyote kujaribu kupora wananchama wa vyama vingine. Kila mkutano unaouona ni wanachama wa CCM kurudisha kadi za chama.. hawa zuga tu kesho wanaweza kukuacha kama walivyoweza kuiacha CCM..
 
MH MKANDARA,
Yani unamanisha kua tatizo la chadema ni kua hawana uwezo wa kujibu/kupinga kwa hoja thabiti kuhusu mashambulizi zote za uongo/ukweli zinazorushwa kwao kutoka upande wa pili(ccm)? kama udini na ukabila na ukanda?.

Mi ninavyo ona kama adui anakushambulia kwa kukosa ushaidi thabiti kuhusu hoja usika ili ukose kile mnachogombania,basi njia rahisi ni kumbomba alete vithibitisho na akishidwa wewe ukiwa mushtakiwa unatakiwa kuibua hoja nyingi sana kuhusu mpinzani wako na kuzithibitisha kwa ndio chadema anachokifanya mpaka sasa.

KATIKA MCHEZO WA MPIRA KAMA TIMU MOJA INAWASHAMBULIAJI WAZURI WASIOLENGA GOLI(BUTU) NA MABEKI WAZEMBE (CCM),THEN TIMU PINZANI INAPASWA KUINGIZA ZAIDI WASHAMBULIAJI WAZURI WA KULENGA GOLI BILA KUWEKA MABEKI WALIO MAKINI (CHADEMA) MWISHO WA SIKU CHADEMA WANAWIN KWA MAGOLI MENGI
ASSUME: VIUNGO WOTE WAKO SAWA
 
Sehemu zingine au kubwa nimeona lawama nyingi kwa cdm, kwamba wanapigana vita wasiyoijua. Kwamba wanang'ang'ana na vua gamba badala ya kupandikiza ukweli kwenye fikra za watu. Tangu operation sangara hadi m4c kweli hakuna cha maana kilichofanyika? Yani tangu 2010 hakuna ambacho cdm wamefikia? Bila nguvu ya Dola ungetaka cdm ipambane vipi zaidi? Wao wana tbc, polisi, uwt, mahakama, Bunge, n.k na ndio maana unaona kuwa ccm inashambulia. Pia naomba utufafanulie upya kuhusu kujuana
Nisome vizuri mkuu wangu nachosema ni kwamba -The best offense is the good defence..Ngome yako ikisha ingiwa huwezi kufanya mashambulizi bali kurudi nyuma kuilinda ngome. Utashambulia mbele tu wakati nyumbani kwako kumesha chukuliwa?

Kuhusu KUJUANA ni tuhuma tunazotupiwa sisi lazima ziwekewe ngao zetu iwe kuwafikia walengwa na kushirikiana nao ama kutetea hoja pale haki yao inapopotea, hivyo hata mimi Mkandara naweza kujibu tuhuma hizo. Kuna maswali mengi Ritz na Zomba huyaweka hapa tunashindwa kuwajibu isipokuwa kuwaita wajinga na pengine kuushambulia hata Uislaam. Hawa wenzetu wapo kazini kuonyesha mapungufu ya CDM na tunapokosa majibu ndivyo wananchi wanavyotusoma. Hii haitokani na lolote zaidi ya kwamba hatuna majibu ama hatujui tujibu nini lakini kama tunayo mifano bora tunaweza kabisa kuitumia na wakatuelewa.
 
Hivi kama mimi nikisema naamini kwa Mungu mwenye nguvu ambaye kaumba hao wenye dini zao...then why waste my time kuwabalance hao wadini? Ninachojua huyu Mungu wangu huyu huyu asiye na dini atasababisha hao wadini wa pande zote kukosa mbadala wao na hivyo kuamua kumpa kura yao huyo ambaye mm ndiyo nimemwombea kibali kwa Mungu wangu mwenye uwezo hapo mnasemaje enyi wadini wa JF?

Kwataarifa yenu mtu ambaye mimi kama raia na mwenye imani thabiti kwa Mungu wangu mwenye nguvu zote ndiye atakayekuwa Rais wa nchi hii na mimi nitakuwa master mind wake wakusababisha chumi wa nchi hii uwe kwa jinsi ambayo dunia haikuwahi kuwaza kama haya yatatokea Afrika; nyie bakieni na kublance dini zenu hizo kama zitawasaidia lolote!

Mungu hahitaji demokrasia jamani maana anauwezo waku-change demokrasia to the favour wa huyo anointed one na huu ndiyo ujasiri nilionao yakwamba nimeomba sawa sawa na mapenzi yake naye amekwisha nionyesha atafanya zaidi ya yale niwezayo kuomba ama tamani....
 
Dini maana yake nini?
 
MH MKANDARA,
Yani unamanisha kua tatizo la chadema ni kua hawana uwezo wa kujibu/kupinga kwa hoja thabiti kuhusu mashambulizi zote za uongo/ukweli zinazorushwa kwao kutoka upande wa pili(ccm)? kama udini na ukabila na ukanda?.

Mi ninavyo ona kama adui anakushambulia kwa kukosa ushaidi thabiti kuhusu hoja usika ili ukose kile mnachogombania,basi njia rahisi ni kumbomba alete vithibitisho na akishidwa wewe ukiwa mushtakiwa unatakiwa kuibua hoja nyingi sana kuhusu mpinzani wako na kuzithibitisha kwa ndio chadema anachokifanya mpaka sasa.

KATIKA MCHEZO WA MPIRA KAMA TIMU MOJA INAWASHAMBULIAJI WAZURI WASIOLENGA GOLI(BUTU) NA MABEKI WAZEMBE (CCM),THEN TIMU PINZANI INAPASWA KUINGIZA ZAIDI WASHAMBULIAJI WAZURI WA KULENGA GOLI BILA KUWEKA MABEKI WALIO MAKINI (CHADEMA) MWISHO WA SIKU CHADEMA WANAWIN KWA MAGOLI MENGI
ASSUME: VIUNGO WOTE WAKO SAWA
Kwa nini nitake alete vithibitisho ikiwa mimi mwenyewe sina vithibitisho vya madai yangu juu ya CCM na CUF.. Mkuu fahamu kwamba Uongo ukisemwa sana huaminika na wananchi hawahitaji ushahidi maana hatupo mahakani. Yule atakaye amini tuhuma hizi kutokana na siis kushindwa kujihusisha na jamii zetu kwa kufikiria kwamba kuishambulia CCM pekee kutaongeza tumaini la watu kwetu ni kujidanganya. Utamaduni wa Mtanzania siku zote umejengeka ktk fitna, Udaku na hadithi hatuna hii kitu ushahidi isipokuwa kinachoaminika. Reasoning zetu zinaenda kwa ushawishi tu kama tunavyochagua imani zetu za dini, ushabiki wa Simba na Yanga ndivyo ilivyo hata kwenye siasa.
 
Dini maana yake nini?

Unaniulizaje vocabulary ambayo haipo kwenye luga yangu? Kwenye dictionary ya luga ninayoongea mm hakuna neno linaitwa dini so may be a wrong person to be asked of such a question...
 
Hivi kama mimi nikisema naamini kwa Mungu mwenye nguvu ambaye kaumba hao wenye dini zao...then why waste my time kuwabalance hao wadini? Ninachojua huyu Mungu wangu huyu huyu asiye na dini atasababisha hao wadini wa pande zote kukosa mbadala wao na hivyo kuamua kumpa kura yao huyo ambaye mm ndiyo nimemwombea kibali kwa Mungu wangu mwenye uwezo hapo mnasemaje enyi wadini wa JF?

Kwataarifa yenu mtu ambaye mimi kama raia na mwenye imani thabiti kwa Mungu wangu mwenye nguvu zote ndiye atakayekuwa Rais wa nchi hii na mimi nitakuwa master mind wake wakusababisha chumi wa nchi hii uwe kwa jinsi ambayo dunia haikuwahi kuwaza kama haya yatatokea Afrika; nyie bakieni na kublance dini zenu hizo kama zitawasaidia lolote!

Mungu hahitaji demokrasia jamani maana anauwezo waku-change demokrasia to the favour wa huyo anointed one na huu ndiyo ujasiri nilionao yakwamba nimeomba sawa sawa na mapenzi yake naye amekwisha nionyesha atafanya zaidi ya yale niwezayo kuomba ama tamani....
Mkuu wangu sio swala la dini ndani ya chama isipokuwa chama kutambua inataka kuongoza watu wenye tofauti zao. Huwezi kuongoza kundi la mbuzi na kondoo usijue kama kuna mbuzi na kondoo kwa kusema wote hawa ni wanyama. Pamoja na Utanzania wetu kuna makundi yetu wapo wakulima, wafugaji na wavuvi huwezi kuwafikiria wote kuwa ni kitu kimoja tu. Kuna wanawake na watoto, vilema na kadhalika hawa wote lazima kiongozi uonyeshe umuhimu wao ktk jamii.

Unaweza sana kudharau ya Udini lakini binafsi yangu nimetazama mijadala hapa JF na kugundua kwamba jamii yetu inathamini sana dini zao kuliko hata makabila na wapo radhi kukichagua chama kwa sura ya Udini. Hivi kwa nini kila mheshimiwa akisimama kuhutubia huanza na Asalaam Aleikum kisha Bwana asifiwe.. kuna umuhimu gani wa maneno haya kwa mwanasiasa kuyatumia?. CCM sio wajinga kutumia Udini baada ya kujaribu fitna za kila aina wakashindwa lakini walipofika hapa wamefanikiwa sana kwa sababu ndipo vyama vingi vya Upinzani havikujiandaa. It's just a wake up call.
 
Pasco,
Tatizo ni kwamba CCM haina mtu safi wa kusimamisha. Na walioshika mipini ya uamuzi ndani ya chama hivi sasa wote ni mafisadi na watahakikisha wanalindana. Asha Rose si msafi kama baadhi yenu mnavyofikiria. Hebu kamuulize Lowassa anazo data za huyo mwanadada. Kama CCM wameshindwa kitu kidogo tu cha kujivua gamba, kweli wataunganaje kumpata kiongozi aliye safi?
Mkuu Jasusi, hapa ndipo mimi ninapotofautianaga members wengi humu hatimaye kupelekea kuitwa gamba!. "truth", nothing but the truth!. Jasusi, kuna "ukweli halisi" na "ukweli wako"!. Ukweli halisi ni ile "plain truth" yenyewe amnao ndio ukweli wa ukweli, na "ukweli wako" ni ule "your truth" kwa mujibu wa what is fed on your brain!.

Sasa hii hoja kuwa CCM haina mtu safi wa kumsimamisha kwenye urais, "its your truth" but not the "plain truth"!. Kukweli halisi, Si kweli kuwa CCM haina mtu safi wa kumsimamisha!, ukimuondoa Asha Rose, hivi CCM ikiamua kumsimamisha Dr. Shein, mtasimama majukwaani na kumchambua kwa uchafu upi?. Japo Asha Rose namkubali kwa usafi wake, kwenye chaguo langu la presidential materials from CCM, yeye hayupo!, hivi akisimama mtu ka Prof. Tibaijuka, mtam discredit kwa uchafu gani?.

CCM inao watu safi wengi tuu ambao wakisimamishwa Chadema itakuwa na kibarua cha ziada!. Ni kweli CCM imeoza kwa rushwa na ufisadi, na CCM inaongozwa na mazimwi!. Whoever ambaye Chadema watamsimamisha, obvious atakuwa sii malaika, hivyo na yeye atakuwa na uzimwi wake!. Wapiga kura watakapo kuwa na choice betwen masimwi mawili, wanayo chance ya kulichagua zimwi likujualo "CCM" kuliko zimwi lisilo kujua "Chadema". "Beter choose a devil you know than a devil you don't know!". ndio maana katika debe langu kwa mgombea wa CCM, nasimama na EL, he is a devil!, but he is a devil we know!, and between the two devils, choose the lesser!, EL akisha safishwa. ni mwana Chadema gani anaweza kusimama nae?!.
 
Back
Top Bottom