Waraka wangu kwa viongozi wa CHADEMA

....Mkuu Mkandara hata vyama vikongwe duniani kama Democrats na Republicans vina mapungufu mengi tu ndani ya vyama vyao. Kule Republicans mapungufu hayo yakasababisha kuzaliwa kwa Tea Party. Pamoja na hayo mapungufu shughuli muhimu za vyama hivyo hazisimamishwi ili kuyafanyia kazi mapungufu hayo.

Mie puyngufu kubwa nililokuwa nikiliona ambalo lingweza kabisa kunyima CDN nafasi ya kuchukua dola ni lile la kutokwenda kujitangaza vijijini ambako ndio asilimia kubwa ya Watanzania wanaishi. Hili sasa linafanyika tena kwa juhudi kubwa sana. Kwa hiyo hayo mengine yanaweza kushughulikiwa taratibu huku shughuli nyingine mihimu za CDM zikiendelea.

Unasema magamba wameongoza katika mageuzi ya kiuchumi. Mie sioni mageuzi yoyote kwenye uchumi wetu zaidi ya uchumu huo kuendelekea kupokwa na mafisadi ndani ya Serikali na wale wanaojifanya ni wawekezaji.

Kuhusu umiliki wa vyombo vya habari si kweli kwamba vyombo vyote vinamilikwa na magamba. Na hili linathibitishwa na mambo mengi ya kuhusiana na ufisadi ambayo tumeyafahamu kupitia vyombo huru vya habari kama vile Mwanahalisi, Mwananchi, This Day (sasa halipo tena) Tanzania Daima na hata baadhi ya TV stations ambazo bado ziko nyuma ukilinganisha na magazeti. Kama utakumbuka gazeti la Mwanahalisi hivi karibuni lilifungiwa kwa kuandika ukweli kuhusiana na kutekwa kwa Dr Ulimboka.

Magamba hawana uchumi mkubwa wowote. Pamoja na kulipwa mabilioni ya ruzuku kila mwaka bado wanakupua mabilioni chungu nzima kutoka hazina ili kugharamia shughuli mbali mbali za magamba ikiwemo kampeni za uchaguzi. Katika uchaguzi wa 2010 walikupua mabilioni ili kugharamia kampeni zao. Katika uchaguzi wa 2005 walitumia EPA, Meremeta na Kagoda kukupua nambilioni ya pesa za Watanzania na kuzijaza katika bank accoints zao nchi za nje na pia kulipia gharama za kampeni.

Hilo la katiba kuipa nguvu CCM wala silishangai ndio maana walipinga sana kuandikwa katiba mpya ambayo itapunguza kwa kiasi kikubwa nguvu walizonazo sasa kupitia katiba iliyojaa viraka.

Mbinu za CDM labda ni kweli haziko consistent. Hili linaweza kuwa linasabishwa na vikwazo mbali mbali vinavyofanywa na magamba wakishirikiana na vyombo vya dola, Msajili wa vyama na pia Tume ya uchaguzi.

Civil society ni kweli bado dhaifu na hili pia linasababishwa na magamba kwa kuogopa kwamba hizi zikiimarika basi madhambi yao ndio yatazidi kuanikwa hadharani na hivyo kushindwa kutimiza ndoto zao za kuitawala Tanzania milele.

Kwa kumalizia napendi nirudie tena Viongozi wa juu wa CDM wanastahili pongezi kubwa sana kwa mafanikio waliyopata mpaka sasa. Hivyo inabidi tuungane nao katika jitihada za kuhakikisha kwamba 2015 CDM wanachukua dola. Hakuna ubaya wowote kukosoa mapungufu yaliyomo ndani ya CDM lakini wakati huo huo tusisahau kupongeza pale ambapo panastahili kupongezwa.

Siku na kazi njema Mkuu.



BAK, nakubalina na wewe sana tu lakiji mwenyewe umekiri kuwepo kwa mapungufu. lakini sijakuona ukiya orodhesha. Halafu kulingana na Mchambuzi hizi ndio ngome yao, nakuomba uninyeshe ni wapi tumeweza kubomoa..


  1. CCM ndio iliyoongoza mageuzi ya kiuchumi (political reforms) Tanzania;
  2. Umiliki na Udhibiti wa Vyombo Vya habari;
  3. Uchumi Mkubwa Wa CCM;
  4. Ujamaa Bado ni Relevant (unaendana) na Maisha ya Wengi Vijijini;
  5. CCM imejenga Coalition na Taasisi zote nchini zenye nguvu kiuchumi, kijamii na kijeshi;
  6. Katiba ya Sasa ya nchi inaipa CCM nguvu kubwa kisiasa;
  7. Mbinu za upinzani zinazotumiwa na Chadema Hazipo Consistent na Coherent;
  8. Tanzania inakabiliwa na Udhaifu mkubwa wa Civil Society; na
  9. Political Culture ya Tanzania ina matatizo..
 
Last edited by a moderator:
Chadema bila kukaa na kujitafakari upya harakati zenu za kuchukuwa dola itakuwa ni stori Chadema bado wanategemea wanachama wasiotabirika wanachama wake ni wale wanaoingia wakati wa mikutano ya hadhara, hawana wanachama wa takwimu, kwa mfano Wilaya ya Masasi, au Rorya, Mirare, Ingri, leo ukimwambia kiongozi Chadema akupe takwimu hawezi kukupa.

Chadema wamekosa uhalali wa mtawanyo wa wanachama hai katika kila kona ya nchi, harakati zao za kuongeza wanachama ni ile ya mikutano ya hadhara.

Chadema mpaka sasa hawajawa na uhakika wa jinsi ya kumpata kiongozi wa juu katika nafasi ya mwenyekiti au urais kutoka kanda nyingine, nguvu ya Chadema kiuchumi na kiushawishi bado inabaki kanda ya kaskazini, hii inatokaona na ukweli kwamba waasisi wa Chadema na walezi wake wenye nguvu kiuchumi wanatoka kanda ya kaskazini.

Chadema wanatakiwa watafute ufumbuzi mgombea rais au nafasi ya mwenyekiti kutoka kanda ingine haweze kupitishwa na kamati kuu ya chama,
 
Pasco,
Shukrani sana kwa kulisasambua hilo. Tunatokaje kwenye UDINI ambalo sasa ndilo tatizo
na tishio kubwa kuliko yote. Hii SILENT CODE ya CCM walidhani ingewasaidia. Badala yake inageuka balaa kwao na NCHI yetu. Moja kati ya mambo ambayo Rais huyu wa sasa ameyasimamia kwa nguvu zake zote hasa kwenye TEUZI zake ni hii silent code. Karibu teuzi zake zote hata kwenye vyombo nyeti vya DOLA kaitumia code hii. Hivyo ndivyo ilivyo JWTZ, UwT, Police, Cabinet, maRC, maDC,..., imeshindikana tu BUNGENI ambako Spika na Naibu wake wote ni WAKRISTO.
TEUZI sasa hazizingatii kwanza UWEZO na WELEDI wa mteuliwa!
WC, hakuna tena cha seniority kwenye baadhi ya teuzi, ukimuondoa CDF, IGP alimuibua aliko muibua, Director wa TISS nao akamcholopoa huko chini, Jaji Mkuu nae vivyo hivyo, tukija kwenye taasisi ndio usiseme!. Amini usiamini, mgombea wa CCM 2015 kwa jimbo la Bagamoyo tayari yupo na hata pingwa ndani ya chama na nje ya chama furungu itatembea!. Atapewa un Deputy, 2020 full minister, 2025 magogoni!. Nawaombeni tuepuka kutaja taja majina ili kulinda hadhi ya jukwaa lete kuoneka ni kijiwe cha majungu!.
 
Chadema bila kukaa na kujitafakari upya harakati zenu za kuchukuwa dola itakuwa ni stori Chadema bado wanategemea wanachama wasiotabirika wanachama wake ni wale wanaoingia wakati wa mikutano ya hadhara, hawana wanachama wa takwimu, kwa mfano Wilaya ya Masasi, au Rorya, Mirare, Ingri, leo ukimwambia kiongozi Chadema akupe takwimu hawezi kukupa.

Chadema wamekosa uhalali wa mtawanyo wa wanachama hai katika kila kona ya nchi, harakati zao za kuongeza wanachama ni ile ya mikutano ya hadhara.

Chadema mpaka sasa hawajawa na uhakika wa jinsi ya kumpata kiongozi wa juu katika nafasi ya mwenyekiti au urais kutoka kanda nyingine, nguvu ya Chadema kiuchumi na kiushawishi bado inabaki kanda ya kaskazini, hii inatokaona na ukweli kwamba waasisi wa Chadema na walezi wake wenye nguvu kiuchumi wanatoka kanda ya kaskazini.

Chadema wanatakiwa watafute ufumbuzi mgombea rais au nafasi ya mwenyekiti kutoka kanda ingine haweze kupitishwa na kamati kuu ya chama,

Kanda ya Kaskazini ndio wapi?
 
Mmh! thread inamambo hii usipime.
Ila kwa akili zangu ndogo nilizonazo nimegundua kuwa muanzilishi wa huu anasumbuliwa na vitu 3 inside his brain.

(1) kwanza yeye ni mfia dini wa dini fulani
(2) teyari ameshakuwa muathirika wa propaganda za sumu kutoka ccm kuwa CDM ni chama cha dini fulani.
(3) ni kweli labda ni mwanachama wa CDM lakini kwa vile kilakitu anakitizama kiudini...sasa anataka watu wa dini yake
wawe nusu na wa madhehebu mengine wawe nusu i mean kuanzia wanachama,wapenzi na viungozi wa cdm...nusu nusu

Binafsi nawashauri viongozi wa CDM msitie pua zenu kwenye mnakasha huu...nyie endeleeni kupiga kazi za M4C huku na huko ili tuikomboe nchi yetu kutoka kwa wakoloni weusi. Watu wanaotaka mabadiliko kwa jicho la imani ya dini nawaombeni muachanenao kabisa. USIPOTAKA MABADILIKO KWA HIARI BASI MATENDO YA NYAKATI YATAKUBADILISHA BILA KUSURUTISHWA.
 
WC, hakuna tena cha seniority kwenye baadhi ya teuzi, ukimuondoa CDF, IGP alimuibua aliko muibua, Director wa TISS nao akamcholopoa huko chini, Jaji Mkuu nae vivyo hivyo, tukija kwenye taasisi ndio usiseme!. Amini usiamini, mgombea wa CCM 2015 kwa jimbo la Bagamoyo tayari yupo na hata pingwa ndani ya chama na nje ya chama furungu itatembea!. Atapewa un Deputy, 2020 full minister, 2025 magogoni!. Nawaombeni tuepuka kutaja taja majina ili kulinda hadhi ya jukwaa lete kuoneka ni kijiwe cha majungu!.
Tayari huyo mgombea wa Bagamoyo hana mpinzani kwenye ujumbe wa NEC wilaya hiyo. Mama Salma naye kapita bila kupingwa kule kwao Lindi. NEC ijayo tayari nafasi tatu zimejazwa, Mwenyekiti, mjumbe wa NEC-Bagamoyo na Mjumbe wa NEC Lindi. Kwa mara ya kwanza katika HISTORIA ya TANU/CCM, Baba, mama na mtoto ni wajumbe!
 
Kama mumenisoma vizuri utagundua kwamba nachozungumzia mimi ni Chadema kutokuwa na defensive strategy inayohusiana na maswala haya. Tuna silaha nyingi sana za kuishambulia CCM na Mchambuzi katupa hints ni ngao zipi CCM inajivunia leo. lakini hapo hapo hakutazama kama Chadema nayo ipo uchi sana haina ngao zake isipokuwa silaha tupu za mashambulizi. Tukishambuliwa ktk Ukanda, Udini au Ukabila mara zote huja na mifano ya Zitto.. Yaani kweli Zitto pekee ndio sababu ya kutulinda ktk Ukanda, Ukabila na Udini. Nini ngao zetu? sisi tunaweza vipi kujivunia kutoshiriki ktk hizi tuhuma za KUJUANA tofauti na CCM ambao hadi kesho tunaunga mkono baadhi ya ushirika wao wenyewe. Hatuna majibu mkuu wangu tunaulizwa kila siku hapa JF mara zote majibu hutolewa na kina Mkandara au Mohammed Mtoi.. Mimi na Mohammed Mtoi tunaweza vipi kuwa na majibu ya uongozi wa Chadema inapokabiriwa na tuhuma nzito kama hizi hata kama najua sii kweli.. sema kweli maana janvi hili ni mawazo ya mtu mmoja mmoja sio janvi la chama.

Uvumi siku zote ndio hujenga imani za watu, wanasema Chadema ni chama cha Ukanda au udini, wewe huzioni, mimi zisioni na vile vile kumbuka hata mtu wa CUF anaamini hivyo hivyo. Na sidhani kama tunaweza kuonyesha Udini wa CUF lakini Je ni watanzania wangapi wanaamini CUF sio chama cha Waislaam au Wazanibar?..wamepewa majibu gani?.. maana ukweli ni kwamba CUF wenyewe hawana ngao, hawana majibu wala defence mechanism inayo onekana isipokuwa wao wenyewe wanajiingiza zaidi ktk ukimya.. Je ktk hali hiyo unafuu na credit zinakwenda wapi - CCM, uongo! I have done my study mkuu wangu na nakuhakikishia najua nilichokiandika..

Kama mtu atashindwa kukuelewa hadi hapa basi hatakuelewa sehemu yoyote!! Lakini kwavile wengi wetu huwa hatutaki kukubali ukweli basi si ajabu nikiona hata hapa watu "watajifanya" kutoelewa ulichomaanisha!
 
Chadema bila kukaa na kujitafakari upya harakati zenu za kuchukuwa dola itakuwa ni stori Chadema bado wanategemea wanachama wasiotabirika wanachama wake ni wale wanaoingia wakati wa mikutano ya hadhara, hawana wanachama wa takwimu, kwa mfano Wilaya ya Masasi, au Rorya, Mirare, Ingri, leo ukimwambia kiongozi Chadema akupe takwimu hawezi kukupa.

Chadema wamekosa uhalali wa mtawanyo wa wanachama hai katika kila kona ya nchi, harakati zao za kuongeza wanachama ni ile ya mikutano ya hadhara.

Chadema mpaka sasa hawajawa na uhakika wa jinsi ya kumpata kiongozi wa juu katika nafasi ya mwenyekiti au urais kutoka kanda nyingine, nguvu ya Chadema kiuchumi na kiushawishi bado inabaki kanda ya kaskazini, hii inatokaona na ukweli kwamba waasisi wa Chadema na walezi wake wenye nguvu kiuchumi wanatoka kanda ya kaskazini.

Chadema wanatakiwa watafute ufumbuzi mgombea rais au nafasi ya mwenyekiti kutoka kanda ingine haweze kupitishwa na kamati kuu ya chama,
Mkuu Ritz, sisi wengine, kazi yetu ni kusema tuu, wasikie wasikie, watende wasitende, kitu ambacho sitaki kukisikia ni visingizio!, katiba mpya by June 2014, itakuwa imeweka miongozo yote, wakishindwa ndio basi tena!.

Niliwashauri lazima waivunje ngome yao ya Kaskazi, nikashauri ZZK awe No.2, mkwe wa muasisi abaki CDM kama mshauri. Viti maalum wacheze nusu kwa nusu ili kujenga base kwenye maeneo ya kina yakhe!. Safari alipojiunga, nilisema hii ni Hazina, kwa vile watu wana hates zao kwa ZZK, then Safari apande pale juu, Dr na ZZK wabaki walivyo!. Mwenyemasikio na asikie!.

2010 niliandika hivi kuhusu CCM wakati nikiwaambia "CCM Imechokwa!"
Wanabodi,

Nasisitiza CCM imechokwa, na ule ushindi wa kishindo wa toka Asilimia 80% niliyohakikishiwa na mwana CCM mwandamizi mpaka asilimia 60% ni uthibitisho tosha, Watanzania wameichoka CCM ila pia hawakuwachagua wapinzania kwa wingi zaidi, kwa sababu wapinzani hawajaonyesha wako tayari kukamata dola.

Najua kwa dhati, japo JK anafurahia ushindi kwa furaha ya machoni, lazima atakuwa na huzuni moyoni kwa kukataliwa na hiyo asilimia 20% kukataliwa ni kukataliwa tuu, kunauma. Hivyo CCM lazima watakaa na kujiuliza kulikoni, huenda wakajipanga upya na kuja kwa mbinu mpya, ila kwa vile CCM imechokwa, hata ijipange upya vipi, safari ya kwaheri ndio imeanza, there is nothing to stop it from failing down!.

Dawa pekee ya kuitibu CCM, ni kuirevamp CCM completely, task nambari moja ni Makamba should go first with his old guards team. Msisubiri mpaka uchaguzi mkuu wa chama chenu, miaka miwili ijayo (2012), itakuwa too late. If you are to du anything, doi it now and fast!. Leteni fresh blood kina January type, Kippi, Nape type and the like ambao wanaweza siasa za kisasa za dot com type.
Wana CCM waliomo humu hawakujibu chochote, walijinyamazia kimya!, less than a year Makamba alipigwa chini, Nape na January wakaingia, simaanishi kuwa ni lazima waliutumia ushauri wangu, it was just a mare coincidence nimeshauri piga chini Makamba sn na lete on board Makamba jn na Nape type ndio hao kina Mchemba tunaowaona!.

Chadema niliwaambia "hamjajipanga!, nilitukana mpaka basi!, ila nikasema sioni shida kutukanwa kwa dhambo ni la ukweli na siku ya kilio cha kusaga meno ikifika, tutawakumbusha "tuliwaambia kabla".

Pasco.
 
Chadema bila kukaa na kujitafakari upya harakati zenu za kuchukuwa dola itakuwa ni stori Chadema bado wanategemea wanachama wasiotabirika wanachama wake ni wale wanaoingia wakati wa mikutano ya hadhara, hawana wanachama wa takwimu, kwa mfano Wilaya ya Masasi, au Rorya, Mirare, Ingri, leo ukimwambia kiongozi Chadema akupe takwimu hawezi kukupa.

Chadema wamekosa uhalali wa mtawanyo wa wanachama hai katika kila kona ya nchi, harakati zao za kuongeza wanachama ni ile ya mikutano ya hadhara.

Chadema mpaka sasa hawajawa na uhakika wa jinsi ya kumpata kiongozi wa juu katika nafasi ya mwenyekiti au urais kutoka kanda nyingine, nguvu ya Chadema kiuchumi na kiushawishi bado inabaki kanda ya kaskazini, hii inatokaona na ukweli kwamba waasisi wa Chadema na walezi wake wenye nguvu kiuchumi wanatoka kanda ya kaskazini.

Chadema wanatakiwa watafute ufumbuzi mgombea rais au nafasi ya mwenyekiti kutoka kanda ingine haweze kupitishwa na kamati kuu ya chama,
Ritz,
Unawaonea CHADEMA. Kwa chaguzi kuu hizi mbili zilizopita ni CHADEMA pekee imeweza kubadili mgombea kwenye nafasi ya Urais wa JMT. CUF tangu mwaka 1995 mgombea wao JMT na Zanzibar ni walewale. Na jana kwenye mkutano wao wanatajwa walewale 2015! CCM ni KATIBA ya JMT inawasaidia kubadili wagombea. Vinginevyo hadi leo tungekuwa na AH Mwinyi kama Rais. Suala la Kanda hata sielewi mnalitoa wapi mapema namna hii. Hivi kweli ndani ya CHADEMA kulikuwa na mgombea mzuri zaidi ya Dr Slaa uchaguzi uliopita? Suala la Kanda kama lile la Ukristo mnalikuza tu.
 
Mkuu Ritz, sisi wengine, kazi yetu ni kusema tuu, wasikie wasikie, watende wasitende, kitu ambacho sitaki kukisikia ni visingizio!, katiba mpya by June 2014, itakuwa imeweka miongozo yote, wakishindwa ndio basi tena!.

Niliwashauri lazima waivunje ngome yao ya Kaskazi, nikashauri ZZK awe No.2, mkwe wa muasisi abaki CCM kama mshauri. Viti maalum wacheze nusu kwa nusu ili kujenga base kwenye maeneo ya kina yakhe!. Safari alipojiunga, nilisema hii ni Hazina, kwa vile watu wana hates zao kwa ZZK, then Safari apande pale juu, Dr na ZZK wabaki walivyo!. Mwenyemasikio na asikie!.

2010 niliandika hivi kuhusu CCM wakati nikiwaambia "CCM Imechokwa!"

Wana CCM waliomo humu hawakujibu chochote, walijinyamazia kimya!, less than a year Makamba alipigwa chini, Nape na January wakaingia, simaanishi kuwa ni lazima waliutumia ushauri wangu, it was just a mare coincidence nimeshauri piga chini Makamba sn na lete on board Makamba jn na Nape type ndio hao kina Mchemba tunaowaona!.

Chadema niliwaambia "hamjajipanga!, nilitukana mpaka basi!, ila nikasema sioni shida kutukanwa kwa dhambo ni la ukweli na siku ya kilio cha kusaga meno ikifika, tutawakumbusha "tuliwaambia kabla".

Pasco.
Pasco,
CHADEMA ngazi ya KITAIFA ndani ya chama chao wamejipanga vizuri tu. Hili la Ukanda halina mashiko hata kidogo. Dr Slaa, Mbarbaig, na Mbowe, Mchagga, au Arfi Mwarabu koko wa Katavi wapi na wapi? Hili la kujipanga kwa DINI sio zuri hata kwa CCM sasa hivi. Semeni tu kuna watu mnataka kuwaona waking'ara pale juu.
DINI zinataka kututesa hivi kwa sababu gani? Mungu mwenyewe dini hana. Hata Yesu na Mtume Mohamed (S.A.W) hawana madhehebu. Kwa nini turuhusu dini hizi za kuletwa zitutese hivi?
 
Mkandara,

Umenifanya nirudi JF maana nilishaanza kupoteza interest ya kusoma na kuchangia humu jamvini. Kama unakumbuka kipindi cha nyuma niliwahi kusema kwamba Chadema bila ya kucounter attack arguments za ukristo na chama na kujinasua katika influence ya kanisa haitakaa ishinde hata siku moja uchaguzi wa urais Tanzania. Binafsi nimepita maeneo waliyofanya uchaguzi Chadema na slogan ya M4C hasa mikoa yenye waislamu na wengi walikuwa wanasema ah hicho ni chama cha kanisa wala hawataki kukisikia. Chadema ni vizuri ikawa inapita sekta zote za jamii na huku ikiwa inakubali ya kuwa Tanzania ni jamii ya watu tofauti. Bila ya hivyo haitafika mahala popote kama chama cha kisiasa.

Pili umezungumzia udini, binafsi nadhani tuwe wakweli kama unakumbuka ijumaa iliyopita Waislamu walifanya maandamano ya kustukizia pale jijini Dar. Wachangiaji wengi ambao wengi wao ni wanazi wa mapenzi ya Chadema walikuwa wakitoa maneno mengi ya kashfa na dharau kuwadhihaki waislamu waliokuwa wakiandamaana kwa madai yao ya msingi. Vile wanasahau kuwa waislamu wanapoandamana hawana tofauti na wakristo au wapagani kwani wanatumia haki yao ya msingi ya kikatiba kufanya maandamano ya amani. Je ni akina nini wadini? Hapo ndio tunakuja kwenye maudhui ya nini udini na nani mdini. Ukiwa hukubaliani na ukristo na unatetea dini isiyokuwa ukristo wewe ni mdini but vyenginevyo wewe sio mdini? Religious tolerance imepotea na hapo ndio tunakuja kujiuliza kwanini hiyo hali imekuwa hivi na why?

Hayo yanatokana na mazingira ambayo yapo Tangu hapo nyuma. Tukiangalia kiundani zaidi hiyo haitokani na sababu ya msingi isipokuwa ni UBINAFSI (GREEDY). Kuna kundi moja la dini lenyewe linajiona linatakiwa kuhodhi mamlaka, rasilimali za nchi na kuwa na maendeleo wakati wengineo wanatakiwa kuwa maskini na mafukara. Zaidi, kuna wachangiaji humu wanadiriki hata kutetea mambo mengine just for the sake of defending their religous institution. Mfano hai ni Memorandum of Understanding (MOU) ya Kanisa na Serikali, ule mkataba ni ufisadi na wizi wa mchana no matter how much you try to defend it. But wengine utawakuta mapovu yanawatoka wakija hoja dhaifu kabisa wakitetea wizi huo. Hayo yote yanatokana na ubinafsi ndani ya mioyo na vichwa vyao wakiamini kundi la wateule hao wanatakiwa wawe wao ni watawala na wenye kufaidi rasilimali za nchi hii na wengine waendelee kuwa ni mafukara na maskini.

Mkandara umeleta mjadala mzuri sana ila Chadema pamoja wazee wao wanatakiwa wajiangalie vizuri na mwelekeo wao. Vyenginevyo chadema itaishia kufa kama inavyokufa CUF. Baadhi tuliamua kujitoa CCM, ila tumekosa pa kwenda tunabakia hatuna chama kwani bado Tanzania hakuna chama mbadala baada ya CCM.

Nilikuwapo!
 
Mheshimiwa Mwenyekiti, katibu mkuu wa chama, viongozi wa chama ngazi ya Taifa, mikoa na wajumbe wa mabaraza yote ya chama ngazi zote.. leo nachuua nafasi hii kuwapa summary ya mjumuiko wa utafiti wangu kuelekea uchaguzi wa mwaka 2015 kuzungumzia hali halisi. Yamkini waraka huu umelenga jambo moja tu muhimu sana ktk mapitio yangu ya siasa za Tanzania na hasa mapenzi yangu ya dhati kwa chama cha Chadema na uongozi wake kutika maendelezo ya kukijenga chama hasa ktk wakati huu kuelekea uchaguzi wa mwaka 2015.

Ni baada ya kusoma mada kadhaa humu JF ambazo binafsi yangu nimezisoma kwa umakini mkubwa ktk kutazama fikra za wananchi mbalimbali ikiwa ni pamoja na hoja, maoni na mitazamo wa wanajanvi nimekuja na waraka huu makusudi kukinusuru chama hiki kuepukana na umaarufu wa muda. Waheshimiwa, tujihadhari sana na umaarufu wa muda ama kutukuza wingu hili la umaarufu wa muda kwa sababu lengo kuu la ujenzi wa chama hiki ni kupigania dhamana ya wananchi kuwapa mamlaka ya kuongoza nchi yetu na watu wake. Tukumbuke tu ya kwamba ngoma ikivuma sana mwisho wake hupasuka.

Hivyo basi mada nilizozitazama na kuzipa uzito mkubwa ni kama zifuatavyo:-
1. Mchambuzi Bofya
2.
Profesa Bofya na
3. Ibambasi Bofya

Waheshimiwa,
Mada hizi nimezipa uzito kutokana na nafasi ya chama kuelekea uchaguzi wa mwaka 2015. Zote hizi zimebeba uzito mkubwa sana wa tafiti zangu ktk jukwaa hili la Siasa pamoja na mkusanyiko wa hoja na mawazo ya wadau ambao kwa kuelewa ama kutoelewa wameweza kuonyesha wazi tofauti zao za kisiasa, kiimani na hata kujenga matumaini hasi japokuwa chama hiki hakitakiwi kabisa kupoteza dira yake kwa manufaa ya mtu ama baadhi ya watu.

Ikumbukwe tu kwamba wananchi wa nchii hii pamoja na tofauti zao bado ni Watanzania wenye kuthamini mila na desturi zao, wanaothamini imani zao za dini, UTU wao na wanaotukuza Ujamaa kama msingi bora na wajibu wa kila mmoja wao kulingana na hali na mali hivyo kufikia kuwapeni dhamana kubwa ya kusimamia UHURU, HAKI na USAWA kwa wawananchi wote wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Tunapodharau vitu hivi kama chimbuko la WATU wenyewe kwa kuaminishwa kwamba tunaweza kuwazuia WATU kutoamini (exclusive) badala ya kuwawezesha wao kutumikia imani zao kama sehemu ya jamii yetu (inclusive) basi tuondoe tumaini la ushindi ifikapo 2015.


Waheshimiwa,
Toka kujiunga kwangu JF nimejifunza mengi sana na nimepanua kiwango changu cha ufahamu wa Mtanzania hasa ktk hali ya Umaskini, Ujinga na maradhi. Nimeweza kuzifukua nyoyo za watu katika maabara ya fikra, hisia na kutazama tatizo hasa linatokana na ukweli upi. Hivyo kama saini yangu (signature) miaka yote hapa JF isemavyo (signature) ni wajibu wangu kuendeleza kile nachokiamini ktk ku explore reality, na nimegundua rasilimali kubwa ambayo chama kinachotaka kuongoza kitakumbana na vikwazo gani na kwa gharama gani. Hivyo kughairi haya ni sawa na kutafuta dhahabu, mafuta au gasi ktk nyanda za mbuga tupu au jangwani..

Hata wachimba Dhahabu, mafuta au gasi nchini huanza na exploration wakajua maliasili hizi zinapatikana wapi precisely, kisha ndio shirika la uchimbaji huchukua report hiyo na kuifanyia kazi.. Hii ndio kazi yangu kwa leo. Kazi yangu ni kuwapa ushauri viongozi wa Chadema tokana na utafiti wa mijadala mbalimbali na hapa JF na nje ya ukumbi huu ktk mkusanyo wa fikra mbalimbali zinatujenga jamii hii ya Kitanzania.



Waheshimiwa,
Kama tulivyowahi kuzungumza awali kuhusu nafasi ya Chadema ktk utawala na maandalizi ya chama kugombea mwaka 2015, bado nina imani kubwa na chama lakini bado kabisa chama chetu kimeshindwa kupasua ngome ya CCM ipaswavyo na kujenga imani za wananchi kwa chama hiki. Kinachotokea ni kujaribu kwa chama chetu kuwavuta wanachama wa CCM zaidi ya kuwavuta wananchi kuichagua Chadema. Kauli mbiu kama VUA GAMBA vaa GWANDA ni moja ya kauli nyingi zilizoonyesha wazi vita ya chama hiki ni kupambana na uongozi wa CCM badala ya kupambana na sera za CCM zilizotufikisha hapa tulipo.

Ebu tutazame Mchambuzi ktk mada yake utagundua kwamba Chadema inajaribu sana kufanya wajibu wake ‘Do the right thing’ kukemea Ufisadi, utawala wa mabavu, mapungufu ya JK na kadhalika lakini tumeshindwa kuyafanya ipaswavyo ‘Do things right’ hivyo tunashindwa kujenga uaminifu kwamba Chama hiki kitaweza kurekebisha kero za wananchi. Na hivyo wale walioko vyama vingine mbali na CCM wamekosa tujmaini, wale wasiokuwa na mapenzi ya siasa hawana imani na vuyama mvyote na hata wale wanaokichuka chama CCM hatuwapi matumaini isipokuwa kujiunga chama uanachama..

Waheshimiwa, sio mwanachama atakaye tupa ushindi mwaka 2015, bali mwananchi mlalahoi anayetakiwa kwenda ktk sanduku la kupiga kura siku ya Uchaguzi na kutupa imani yake kwenye kipande cha karatasi kama tumaini lake kwa miaka mitano ya uongozi wa nchi hii..


Ndugu Mchambuzi kaorodhesha mambo tisa na haya yana umuhimu wake ktk kumtambua adui yako ngao zake.. Japokuwa ngao hizi haziwezi kuwapa ushindi pasipo mashambulizi ya nguvu ambayo yanategemea na silaha walizonazo..Hivyo katika mada nzima ya Mchambuzi tumeona ngao kubwa za chama CCM ambazo zinaweza tu kutupa matumaini ya ushindi ikiwa tutaweza kuwa na silaha za kuzibomoa.

Hapo hapo tukumbuke tu kwamba nasi tuna ngao gani ambazo zinaweza kuvumilia makombora ya CCM maana ushindi wa vita hii hautokani na kushambulia tu.. Ukweli ni kwamba Chadema hatuna defence zaidi ya kushambulia na kwa bahati mbaya mara kwa mara hushindwa hata kujitetea isipokuwa wa tu kukimbia kimbia maporini kama wakimbizi wa vita au insurgents.


Na kwa nini basi tumeshindwa kuwa na ngao ktk mashambuliz makali yanayoelekezwa kwetu?. Jibu nalipata kwa Mchambuzi tena akisema hivi:- Leo hii masuala ya Uongozi na siasa yametawaliwa sana na misingi ya UKANDA, UKABILA na UDINI. Mheshimiwa hili tupende tusipende ndivyo watanzania watawahukumu viongozi wetu kwa sababu ndivyo siasa za nchi hii zimejikita iwe kutokana kupoteza dira ya Kitaifa, kuwepo kwa vyama vingi ama hisia na wajibu wa viongozi wenyewe kuwajibika ktk makundi ya watu wanaowawakilisha.

Waheshimiwa,
Hii ni tahadhari kubwa sana kwa chama na hasa vyama vya Upinzani ambavyo vimetokana ama kuasisiwa na watu waliopingana ndani ya utawala wa CCM hivyo kuanzisha fikra mpya kinzani ili mradi kujaza ubao wakati nyuma ya pazia hilo kuna KUJUANA..Ni rahisi kusema CCM imeshindwa kutuongoza kwa miaka 50 na watu wakakuelewa lakini ni vigumu sana kuwavuta wananchi ikiwa wataona chama kimeshindwa kupambana na siasa za KUJUANA ndani yake hivyo nje wataweza vipi?.. maana tunawalaumu CCM kwa kujuana lakini pia vyama vyote nchini vinafanya mambo yake kwa KUJUANA.. na pale ngome hii inaposhambuliwa vyama hivi hushindwa kujitetea.


Naye Profesa anawekamaswali yanayowakabiri wananchi wengi sana naomba ninukuu.. anasema kuhusu vyama vyetu vikuu vitatu kati ya CCM, Chadema na CUF ya kuwa –
“Nani kati ya hawa watatu ambao bila ubishi wanashikilia hatamu ya siasa za Tanzania, atatupeleka kwenye nchi yenye neema na amani kwa watu wote bila kujali itikadi, hali yao kiuchumi, kisasa, kidini au kiasili? unahitaji nini kati yao, moja wapo ya chama hiki au Kiongozi kati yao atakaebadilisha upepo na kutuepusha na mgao unaofanywa na vyama vyote hivi (kwa manufaa ya hao wanaoongoza vyama hivi kwa kuwa wanataka kuendelea kuwepo madarakani?) Huko madarakani kuna nini?

Nani atatuambia tutatokaje na siku moja itakayolengwa kwa sisi kuwa sehemu ya taifa Afrika, au Duniani imara kisiasa, kiuchumi, kiutamaduni na kimaendelo kwa ujumla (sayansi, usalama wa chakula, nafasi sawa ya elimu kwa wote, huduma za afya wote, maji safi kwa wote, ziada ya fedha, dhahabu na mafuta ambavyo tunavyo na kila mtu akimvumilia mwenzake na kumheshimu).”


Waheshimiwa,
Mawazo haya sii ya kutafanyia mzaha hata kidogo. Ni mawazo yanayofikiriwa na Watanzania wengi nchini, Watanzania ambao wanajaribu sana kutazama chama mbadala ambacho kinajaribu kwa kila hila kuwajumuisha watu wote ktk Utanzania wao pasipo kujali tofauti zao. Na hatuwezi kuwezesha jambo hili pasipo kuwaunganisha (Inclusive) kama jamii moja badala ya kuwatenga (exclusive) baadhi kwa fikra za kwamba ni wao, wale, hawa ni tofauti na sisi hivyo kama wanataka wayapendayo wafanye wenyewe hili sii jukumu la serikali au uongozi kuwavuta hawa ndnai ya jamii yetu..


Waheshimiwa,
Ndugu Ibambasi katika makala yake naye pia amehoji ushiriki wa serikali hii ktk shughuli za dini, amehoji mambo mengi japokuwa kajiweka ktk kundi la wale wasiokuwa na imani za kigeni isipokuwa za jadi zetu na kudai haki yao kikatiba ili kulindwa na kupewa fursa sawa ktk kushiriki ibada zao. Binafsi yangu pamoja na kutokubaliana juu ya tafsiri fasaha ya ibara inayozungumzia kuwa NCHI yetu haina dini isipokuwa WANANCHI wake ndio wenye dini hushindwa kuelewa nini maana ya NCHI na nini maana ya WATU ikiwa serikali haitawawezesha watu wake wenye dini zao kushiriki ktk ibada zao. Lakini ni muhimu kuyasikia maombi, mawazo kama haya na kuyapatia majibu wala sii kuyapuuza ama kuyazuia kunaweza kutupatia ufafanuzi kamili..

Nchi yetu haina dini kwa maana kwamba mihimili ya utawala wa nchi yetu haitakiwi kuundwa ama kujenga policies zinazotokana na imani ya dini moja isipokuwa serikali inawawezesha wananchi wenye ibada zao. Kuwakwaza wananchi kuabudu kama walivyofanya China na Urusi ni kuondoa ama kupokonya sehemu isemayo watu wake wana dini. Kupingana na mawazo ya kiimani kwa kutunga sheria moja kwa wote itatafsirika tu kama exclusive ama sheria ya kuwatenga wao hivyo kuzaa underground movement kupingana na sheria hiyo. Imetokea sana nchi zilizowakwaza waumini wa dini au kuwayenga makabila kama Wayahudi nchi za Ulaya.

Na Mataifa makubwa yote tokea Roman Empire hadi utawala wa Marekani leo wameanguka ama kupata mtihani mkubwa pale wanapojaribu kuwatenga watu kwa kutumia dini, kabila au tamaduni zao hivyo ni muhimu sana kwa chama hiki kuzingatia pamoja na kwamba serikali haina dini lazima tukumbuke wananchi wetu wana dini zao na makabila yao, wana maumbile yao hivo ni lazima vienziwe na sio kupigwa vita. Tunapiga vita wale wanaojaribu kukwaza wengine, wale wanaojaribu kuleta Ukabila na Udini (kudharau wengine) lakini sio wale wanaoitaka haki ya kuabudu kama alivyosema Ibambasi kwa utetezi wa waumini wa jadi..

Waheshimiwa, Inabidi nikomee hapa ktk waraka huu ambao unasisitiza zaidi kujitazama upya. Kutazama makundi ya jamii zetu kama sehemu ya Utaifa wetu badala ya kujaribu kuwabadilisha ama kuwakwaza. Chadema ktk hali hii inahitaji sana nguvu ya Watanzania wapiga kura ambao kwa nafasi zao hawawezi kushawishika na Utaifa ulojaa KUJUANA na sii rahisi wanaongoa watu wasikuwa na Imani.

Hivyo, Tuache UNAFIKI, tuache kujidanganya kwa unafiki wa wapambe wa vyama wanaotumia siasa kaa uwanja wa kujuana. Sisi sote ktk nafasi tulizopo na kutambua kwamba Utanzania wetu unajumuisha tofauti zetu za maumbile, makabila na imani za dini na yeyote atakaye jaribu kumdharau hata mmoja wetu ni kielelezo cha Ubaguzi ambao hautakiwi kupewa nafasi bali kuupiga vita. Hizi ndio ngao zetu, ndizo zinazo tu identify kama jamii ya Kitanzania na lazima tuzilinde dhidi ya siasa za chuki na uutengano. Bila utayari wa kuwajumuisha watu wote kwa tofauti zao kama sehemu ya Utanzania wetu itakuwa vigumu sana kupata ushindi mwaka 2015 maana CCM wanaifanya kazi yao ipaswavyo – Kushambulia nasi ktk kujilinda lazima tuwe na kinga zetu kwa kufanya vitu sawa – Doing things right !

Nawakilisha..

naivutia kasi.
 
Chadema bila kukaa na kujitafakari upya harakati zenu za kuchukuwa dola itakuwa ni stori Chadema bado wanategemea wanachama wasiotabirika

Chadema mpaka sasa hawajawa na uhakika wa jinsi ya kumpata kiongozi wa juu katika nafasi ya mwenyekiti au urais kutoka kanda nyingine, nguvu ya Chadema kiuchumi na kiushawishi bado inabaki kanda ya kaskazini, hii inatokaona na ukweli kwamba waasisi wa Chadema na walezi wake wenye nguvu kiuchumi wanatoka kanda ya kaskazini.

Chadema wanatakiwa watafute ufumbuzi mgombea rais au nafasi ya mwenyekiti kutoka kanda ingine haweze kupitishwa na kamati kuu ya chama,

Mkuu Ritz, kwenye uchaguzi wa Arumeru, nilisimama na kijana wa EL, Sioi, na baada ya kipigo, nilisema haya
Wanabodi,
Mara tuu baada ya Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2010, nilipandisha uzi wa "CCM Imechokwa!, Chadema Haijajipanga"!. Leo baada ya matokeo ya uchaguzi mdogo wa Arumeru, nimethibitisha kuwa ni kweli CCM Imechokwa, hivyo yale maneno yangu ya 2010, sasa yanatimia!. CCM sasa ni "sikio la kufa..." na kama ni tunda, basi ni "lakuvunda..."
Katika mada hiyo, nilisema Chadema, haijajipanga!. Ushindi wa Arumeru, sio uthibitisho kuwa sasa Chadema ndio imejipanga, no!, ni uthibitisho tuu kuwa CCM imechokwa, Wananchi wameamka na sio watu wa kuswagwa na kupelekwa pelekwa tuu kama ling'ombe!.

Ushindi huu wa Arumeru, ni uthibitisho kuwa Chadema mkiamua, mnaweza!. Ushindi huu, umewafungulia njia kuelekea 2015, yaani njia ni nyeupe!, kilichobakia ni kujipanga kwa kupanga mipango mkakati na kuunda kikosi kazi kitakachokabidhiwa malengo na kujadili utekelezaji with time frame, 2015, Ikulu ya Magogoni ni yenu!

Kuhusu ushindi wa Chadema, kuna majimbo Chadema imechaguliwa sio kwa sababi it has any tangible thing to offfer, bali Chadema imechaguliwa kwa sababu tuu CCM imechokwa!. Baada ya ushindi wa Arumeru, pia nikasema tena Chadema imeshinda sio kwa sababu imejipanga vema, bali watu wa Arumeru, wameamua kuadhibu CCM kwa kuwapelekea usultani!.

Nikashauri, ili 2015 Chadema ichukue nchi, lazima iwape wapiga kura reasons za kuichagua Chadema na sio ku bank on kura za walioichoka CCM. Nilikaa na Dr. Slaa mahali, akiwa na supposedilly Ist lady to be!, nilimweleza hitaji la Chadema kupanga safu ya 2015 mapema na sio kusubiria makapi!. Nakatolea mfano jimbo la Kinondoni, wameshamjua mgombea wa CCM ni yule yule, Kawe CCM itamsimamisha Kippi, Ubungo atasimama Nape, Nzega, atasimama Bashe etc etc, hata kama Chadema haijui CCM itamsimamisha nani jimbo gani, inahitaji kuandaa safu yake ya able people na ikijikuta haina, ina recruit na ku groom ili kuanzia serikali za mitaa, Chadema isimamishe mtu kila jimbo, kila kitongoji, kila kata na kila mtaa, exception iwe ni kuachiana breathing space na vyama vingine but not CCM!.

By now we should have identified possible candidates watakaosimama na Chadema ili kuwapika wapikike na sio kusubiria wale watakaoachwa na CCM ndipo tuokote makapi!, don't go for more Shibudas and the such. Nendeni kwa watu mka identify watu wa watu kupitia kwa watu ili muwape fursa watu hao kuwachagua viongozi wao miongoni mwao huku Chadema ikitoa uthibitisho kuwa itaunda serikali ya watu, iliyochaguliwa na watu, na kuongozwa na watu kwa faida na manufaa ya watu!.

Pasco.
 
Mkuu Mkandara, nakushukuru wewe umeliona hili, kama CCM itamsimamisha mtu safi asiye na mawaa ni kweli Chadema itakuwa na kazi kubwa 2015. Prof. Mark Mwandosya they've already done him!, Asha Rose ni msafi na hana mawaa yoyote ila binafsi yangu, sipendi asimamishwe yeye kwa sababu zile zile ambnazo sipendi simamishwe Dr. Shein. Japo mgombea wangu kwa CCM, 2015 ni EL, inside trends zinaelekezwa kwa Benard Membe!.

Nimewashauri Chadema waachane na politics of confrotations, wapunguze mashambulizi kwa CCM as an entity, waconcentrate na watu ambao ndio wapiga kura!. Nikasema determinant ya ushindi wa Chadema 2015, lies with who will stand on CCM ticket, with M4C, there is hope but msipokuwa makini, 2015 Ikulu mtaishia kuisikia tuu kwenye bomba!.

Pasco.

CCM wapo katk deadlock "Ama mgombea awe mzigo au chama kiwe mzigo na vingenevyo". Yaani kwa mtazamo wa watu juu ya CCM,mgombea mzuri hawezi gombea CCM, Na akiwa mgombea mbaya ili aweze iwakilisha CCM lazima acheze rough za ndani ya CCM ili ateuliwe kwa gharama ya kuchafuana wenyewe.Na baadaye naye anakuwa kachafuliwa hadi hafai tena kuwakilisha CCM.CCM imeonyesh wazi katk kiindi cha pili cha JK kuwa kuvunja makundi ni kugumu.So hawataweza safishana kwa muda.Kwa hiyo kwa hali zote CCM itaishia kushindwa.

Na hili la kuchafuana halina mjadala,kwani idadi ya wazee wa CCM ambao wanadhani zamu yao imefika nikubwa,na hali ya umri inaonyesha wazi kuwa atakayekosa this time ndio kakosa kabisa.Hapa wapo wengi wanaoweza komoa mgombea na hivyo chama kudhurika pia.CCM walipa advantage kuwa mara ya kwanza JK alikuwa na umaarufu sana na campaign ilikuwa ya hali ya juu sana.Kwa hiyo umaarufu wa JK ukatumika zaidi ya CCM.Mara ya pili Urais wake uliweka mazingira ya kushinda.Ila sasa hivi CCM haina superstar katika viongozi waliopo,na hata waliopo nje ya mtandao.Waliopo wamechafuka na hapahitajiki nguvu kuwamalizia, na wageniwasio maarufu sana wakiingi hawatakuwa na umaarufu wa kutosha funika udhaifu wa CCM.Na pia siasa za maji chafu kuwa kawekwa na fulani nazo zitamfikisha katk kura akiwa hoi.
 
BOLDED...mindset------
Unaamini kuwa Vyeo hupewa watu kutokana na dini zao. If you believe that then we have a problem.
Unaamini kuwa kuna watu wanakwaza. Lakini ungetaja kabisa nani wanakwazwa. Tuwe open kote, kama wewe hauwi muwazi nani anakwazwa itakuwa ni hisia kuwa unaogopa kusema ukweli.

Tufike mahali tukubali kuwa Serikali iwe haina dini wala ukabila, watu waende kanisani au msikitini na mambo yao yaishie huko huko na nyumbani kwao.

Ni kweli kabisa Chadema ni Chama Mbadala kwa Nchi hii lakini vile vile kuna matatizo; the main problems yapo kwenye public relation communication (including media relationship), intergration, intelligence etc.
Mkuu wangu sipendi kubishana saaana pasipo kuwa na mifano ama umefanya utafiti wako nje ya box na kujibu maswali haya. Kuna maswali mengi ambayo tumeulizwa/nimeulizwa na siwezi kuyaandika hapa isipokuwa nachosema ama kuandika hapa hakitokani na Mimi Mknadara nafikiri nini ama nini mtazamo wangu kwa Chadema, bali yote niliyoyaandika yanatokana na mawazo ya watu wengine ambao binafsi yangu sikuwa na majibu. Nimeweka hadi baadhi ya mada za Mchambuzi, Profesa na Ibambisi halafu nimesema baada ya kusoma hoja za watu humu na nje.. Huu ni mkusanyiko wa dhana za watu na sii kutoka kichwani kwangu..

Nini basi kilinisukuma kuandika waraka huu?.. Ni my concerned kwa chama. Kwa mfano:- Ungekuwa wewe mwanachama wa CUF halafu unakutana na hoja ya mtu anakiuliza kwa nini Profesa Lipumba na Maalim Seif ndio watu pekee waliogombea nafasi ya Urais toka mwaka 1995? Kisha unaposoma majibu unaona kabisa wanababaisha na ajabu zaidi CUF wanatangaza tena kwamba Lipumba na Seif watagombea Urais... Hivi kweli utaweza vipi kutetea hili?..Halafu itokee huna jibu, wala kusema kweli hujui sababu utafanya nini? Je ni kosa kuwashtua viongozi wa chama kwamba wananchi wanashindwa kuelwa kwa nini Lipumba na Seif pekee ndio hugombea Urais?.. Na unapofanya hivyo kwa nini ichukuliwe kuwa ni mawazo yako wewe?..

Mkuu wangu na Wanachadema tuna tatizo moja kubwa sana. hatujui kusoma between the lines.. Kila alonibishia hapa sijaona mtu aliye quote kibande cha waraka wangu na kunieleza tofauti isipokuwa wabnabisha tu ili mradi kubisha. wapo watu wanajiuliza kuhusu chaguzi ndani ya CCM, Chadema na CUF na muhimu sana tuwe na majibu yanayoridhisha kwa kuweka mifano bora. Na hizi ndio zitakuwa ngao zetu, mimi kama Mkandara kesho naweza kuzitumia kama ushahidi..Please naomba mnielewe kwanza kabla hamjakurupuka..
 
Kanda ya Kaskazini ndio wapi?

Kilimanjaro, Arusha, Arumeru...mtawanyo wa wanachama wa Chadema bado upo katika misingi ya kijiongrafia ya kikanda, utakuta kanda ya Kaskazini Mashariki wako wananchama wengi, kanda ya Kaskazini Magharibi nako kidogo kama maeneo ya Kigoma, Mara na kidogo maeneo ya Mwanza.

Hata maeneo hayo wanachama wengi wanapatikana mijini na si vijijini, kwa ujumla mtandao wa Chadema haujajikita katika kila kona kitafa.

Mkuu nadhani umenipata.
 
Pasco,
Ushauri wako ni wa ujenzi ni hiari yao Chadema waufuate au wauache.

Kimsingi Chadema haina tofouti na CCM wana virusi vya ung'ang'anizi vya kurithishana nafasi za uongozi, kwa kuwa wasisi wa Chadema wanatoka ukanda huo wa Kaskazini nao pia wamerithisha familia zao nafasi nyeti za uongozi.
 
Last edited by a moderator:
Kilimanjaro, Arusha, Arumeru...mtawanyo wa wanachama wa Chadema bado upo katika misingi ya kijiongrafia ya kikanda, utakuta kanda ya Kaskazini Mashariki wako wananchama wengi, kanda ya Kaskazini Magharibi nako kidogo kama maeneo ya Kigoma, Mara na kidogo maeneo ya Mwanza.

Hata maeneo hayo wanachama wengi wanapatikana mijini na si vijijini, kwa ujumla mtandao wa Chadema haujajikita katika kila kona kitafa.

Mkuu nadhani umenipata.
+mbeya,+iringa + Manyara+ songea+,+singida +dar sasa hembu gawanya kanda kuu za Tanzania halafu,nimabiwe wapi hakuna nguvu?
Tatizo ni watu wazima kuweka uongo bila hata haya...we jipe matumaini kwani kawaida CCM kudanganyika hata kwa vitu vilivo wazi.Tena mbaya kwa uongo waliuanzisha wenyewe.

Kwa taarifa yako mambo mengi huanzia mijini na kwenda vijijini.Chadema kina appear kama chama cha kisasa zaidi kulinganisha na CCM.Its fashionable,modern and more romantic kuwa CDM kuliko CCM.CDM wameshika majiji yote ambayo ndiyo yamebeba poputaion ya Tanzania.sasa vijiji vipi CCM wanaringia?Vile watu wapo mbali mbalia kama miti ya mbuyu?Je umeulizia pia ni kwanini vijijini wana kura?Kwa vile hakuna vijana wengi wa kulinda Kura?This Time around hata wazee watalinda kura.This time around hapatakuwa na machinery ya kutosha iba kura kwani mawakala sasa watakuwa makini.Helcopter zitakuwa nyingi zinakata anga kama Arumeru.Atakayeonekana vichakani akiana kura feki anaitiwa peoples power.Vyombo vingine vya wizi vitakuwa busy katika majimbo ya wanamtandao kuhakikisha kuwa wanashinda.Na huko napo patakuwa na funiko baya.Habari zitaenea kila kiongozi wa CCM anapoanguka, watu watakuwa na moyo wa kulinda kura zaidi na zaidi.
 
Mkandara

Nimesoma na nimejaribu kukuelewa lakini nilivyoelewa mimi tatizo ni Image appeal ya CDM, na nitaandika bila kumumunya maneno.

Mwanzo ilikuwa rahisi kukiita CDM chama cha kikanda kwa ajili klilikuwa kina wabunge kutoka upande wa kaskazini, na hii ni kutokana na ukweli kwamba kiliapata wabunge wengi kutoka kaskazini kuliko upande wowote. Sasa hivi huwezi tena kukiita chama cha kaskazini kwa ajili kimejipambanua kwenye maeneo mbali mbali, kwa maana nyingine kinayo kinga (ngao) dhini ya hii shutuma.

Kwenye swala la udini CDM bado haina ngao, bado CDM kiitwa chama cha kiikristu kujitetea ni shida sana. Sana sana watakutajia ZZK kama CUF watakavyokutajia Mtatiro. Swali je viongozi wa CDM wanafanya juhudi gani kuhakikisha wanapenya mikoa yenye waislamu wengi?

kuna mchangiaji mmoja amemwambia Bob Mkandara kuwa anataka waislamu wapewe vyeo vya bure ndani ya CDM na amepinga kitu hicho, mimi nasema hivi kama kuna muislamu ambaye unadhani ana influence kubwa na anaweza kubring in many votes, na CDM wanaweza kumsajili basi wasisiste kumsajili na kumpa cheo. CDM needs support of the muslims more now than ever before.

CDM wasirudie kosa walilolifanya CUF, lakuitwa chama cha waislamu na kutofanya juhudi zozote za kuhakikisha wanapata wakristu wengi.

Kuna wakristu wengi humu JF wanapinga hichi kitu, lakini huu ni ukweli, muslim block ni kubwa na ina control votes nyingi TZ kama wakristu wanavo control. Ni wakati wa wote (christians & muslims) na sio sisi.

Jana CUF walijaza jangwani na ukiangalia waudhuriaji wengi kutokana na mavazi yao ni waislamu, what is CDM doing kuvutia hawa watu??

CDM needs to do more to appeal to muslim voters.
Nawakilisha
Mkuu wangu nimekusoma na nakubaliana na wewe. Halafu wala sio swala la CDM kuwapa vyeo waislaam au Muislaam kuwa kiongozi bali CDM inafanya nini kupenyeza ktk ngome zao kwa kusikiliza matatizo yao pasipo kuonyesha Udini ama kutaka kuwapendelea. Hakuna Muislaam anayependa wapendelewe wao isipokuwa wao wanapewa attention gani ktk maswala ya ibada zao na jamii zao kama kina Imbabisi wenye kuabudu mila na jadi....wanachodai watu wote ni uhuru, haki na usawa sio zaidi ya hayo. Siwezi kusema mbunge wa Ukerewe yupo pale kuwapendelea Wakerewe isipokuwa kuwepo kwa tawi, viongozi na mwakilishi wa chama inatosha kabisa kuonyesha Chama kinawajali.

Mimi nisingependa sana kutumia neno Udini na Ukabila zaidi ya KUJUANA lakini nashangaa bado nasomeka vibaya kuwa nachozungumzia ni Uislaam tu kwa sababu mimi Muislaam. Kwa hili utaona jinsi akili zetu zilivyoganda ktk udini na utengano maana lipo.
Majuzi tu kuna kijana wa Chadema aliuawa ktk mikutano ya CDM na amezikwa Tanga pasipo uchunguzi kufanyika. Hii ndio imetoka hakuna mtu amesimama kudai haki ya kijana yule lakini imefuatia kifo cha mwandishi kauawa kila mmoja wetu kashtuka na kulaani serikali tena kwa jazba kubwa, lakini hivi kweli is he important au binadamu zaidi ya yule kijana?..

In fact kuna zaidi ya watu 20 wameuawa mwaka huu ktk hali za kutatanisha - Hakuna cha tume, kamati wala uchunguzi na mafaili yao yameisha fungwa.. Hizo familia za marehemu wataipenda vipi CCM au utawala ulochukua roho ya mtoto wao. Hii tabia ya kujuana ipo kila sehemu na kwa vyama vya siasa ni lazima sana kujipenyeza ktk jamii zetu na kuisimamia haki mahala popote maonevu yanapotokea..
Haya ni mawazo na mtazamo wangu..
 
Pasco,
Ushauri wako ni wa ujenzi ni hiari yao Chadema waufuate au wauache.

Kimsingi Chadema haina tofouti na CCM wana virusi vya ung'ang'anizi vya kurithishana nafasi za uongozi, kwa kuwa wasisi wa Chadema wanatoka ukanda huo wa Kaskazini nao pia wamerithisha familia zao nafasi nyeti za uongozi.

Unchelewa update database yako.Hata mukama mzee mzima anakushinda?Mbona mwasisi wa kaskazini ni Mtei tuu wengine wote wametoka nchi nzima.Napata picture kwanini Nyerere alisema CDM ni makini.Aliona walivyoanza...Mbona wazee wa TANU(leo CCM), wanadai haki yao kuwa Wao ndio waanzilishi na Nyerere alikaribishwa tuu na hakuna aliyesimama na kuthubutu kusema kuwa CCM ni ya wana MZIZIMA.Na JK kila siku anaongea nao.

CDM wameanza vizuri na wanakabilian vizuri sana na sumu za CCM.Soma thread yangu kwanini nimeaita "honey badgers" na ni favourite food yake "Snake".Aakitaka mla huanzia popote,mkiani kichwani etc, kama vile hana sumu vile.

https://www.jamiiforums.com/jukwaa-...nyoka-na-machine-za-catapiller-kwa-mlima.html

kwa ujumla mtu makini hawezi ona hatari ya sumu yako,ila watapata hruma kuwa unachelewa sana kubadili tracks.Tayari hiyo tack ni hatari kwa CCM ila wewe hujui.

By the hembutupe majibu hapa.

https://www.jamiiforums.com/jukwaa-...ivi-anasubiri-vinguvu-vidogo-kama-samsom.html
Halfu tuambie mtavuka vipi hapa?Achana na majia taka kwani hata kama CDM watapungukiwa na idadi ndogo ya kura CCM inaweza isiwepo.Waliwekeza katika uongo sasa wapo katk dead end.
 
Back
Top Bottom