- Thread starter
- #21
Sikuelewi hapa. Nilichosema siwezi kuandika kwa uchache ili kila mtu asome wakati waraka wangu umelenga kuyasema yote yalokuwa kichwani kwangu. Kwa nini nifiche? au niyakatishe pasipo kutoyatoa fully. Kwa nini JF wayakate maelezo yangu vipande kwa sababu kuna watu hawana muda wa kuyasoma yote, wakati wapo wanaopenda kuyasoma yote? kosa ni lipi mkuu wangu...Hiki ndo nachokikataa mimi na ninapogundua kuwa we ni mtu wa namna gani katika kunena lakini ukashindwa kuonesha unachokinena kwa matendo ni ushahidi tosha kuwa ni mtu mnafiki.
Ngoja nikwambie kwa nini nimesema hivyo; waraka wako uko wazi kwa kusisitiza umuhimu wa kuwa mtu wa watu wote kama kiongozi. Na tafsiri ya uongozi hapa ni kuwa kila binadamu mwenye akili timamu ana sifa za uongozi. Umetuo ushauri wa kiuongozi lakini umeshindwa kuonesha tabia za kiungozi.
Katika jibu lako hilo umebagua, umesema una watu wako kwamba uliyemjibu sio sehemu ya kusudio lako maana kuna watu umewalenga. Sasa utawezaje kuhubiri kitu kuhusu kuthaminiana wakati wewe hujathamini?!
Teh teh teh Tanzania bhana.
Kwa ufupi, waraka wako una madhaifu mengi. Nayafanyia kazi halafu nitakujibu.
Nicholas,
Mkuu wangu mimi nimeandika waraka huu kwa uchunguzi wangu niloufanya na wewe umechukulia unayoyafahamu kuwa ndio kinga ya Chama hivyo waendelee na haya wanayoyafanya pasipo kuzingatia yangu kwa imani kwamba watakao athirika ni CCM na CUF, hii ni dhana tu huwezi kuweka dhamana juu yake.
Mimi nasema hivi haya ni mawazo yako na unasema upendavyo kwa sababu hujui lolote kuhusu CCM wala CUF na mbinu wanazozijenga na kuzitumia ktk mashambulizi yao. Hujui athari yake kwa chama unless utawafikia wananchi wenyewe wapiga kura na kufanya utafiti..
Sasa nakuomba hivi:- Wasimamishe watu njiani (one oon one) na waulize imani zao kwa Chadema, nini wasiwaisi wao na wapi wanaona bado chama kinashindwa kuwapa majibu sahihi na kama watakichagua chama hiki mkuongoza mwaka 2015 au itategemea nini?. Nakuhakikishia watu wengine hawana imani kama chadema inaweza kuwa tofauti, wameaminishwa mengi sana usiyoyaona wewe na kibaya zaidi utagundua kwamba Waislaam wengi hawana imani na chama hiki kutokana na Tuhuma za CCM na CUF ambazo hazina majibu.
Unachoshindwa kuelewa ni kwmba Chadema leo hii inashambuliwa na vyama karibu vyote utafikri nwapo madarakani na wasipo jiweka sawa kulinda huu umaarufu wa muda, trust me tutasema mengine hapa kijiweni ifikapo January 2016..