Waraka wangu kwa viongozi wa CHADEMA

Mkandara

JF-Expert Member
Mar 3, 2006
15,772
8,958
Mheshimiwa Mwenyekiti, katibu mkuu wa chama, viongozi wa chama ngazi ya Taifa, mikoa na wajumbe wa mabaraza yote ya chama ngazi zote.. leo nachuua nafasi hii kuwapa summary ya mjumuiko wa utafiti wangu kuelekea uchaguzi wa mwaka 2015 kuzungumzia hali halisi. Yamkini waraka huu umelenga jambo moja tu muhimu sana ktk mapitio yangu ya siasa za Tanzania na hasa mapenzi yangu ya dhati kwa chama cha Chadema na uongozi wake kutika maendelezo ya kukijenga chama hasa ktk wakati huu kuelekea uchaguzi wa mwaka 2015.

Ni baada ya kusoma mada kadhaa humu JF ambazo binafsi yangu nimezisoma kwa umakini mkubwa ktk kutazama fikra za wananchi mbalimbali ikiwa ni pamoja na hoja, maoni na mitazamo wa wanajanvi nimekuja na waraka huu makusudi kukinusuru chama hiki kuepukana na umaarufu wa muda. Waheshimiwa, tujihadhari sana na umaarufu wa muda ama kutukuza wingu hili la umaarufu wa muda kwa sababu lengo kuu la ujenzi wa chama hiki ni kupigania dhamana ya wananchi kuwapa mamlaka ya kuongoza nchi yetu na watu wake. Tukumbuke tu ya kwamba ngoma ikivuma sana mwisho wake hupasuka.

Hivyo basi mada nilizozitazama na kuzipa uzito mkubwa ni kama zifuatavyo:-
1. Mchambuzi Bofya
2.
Profesa Bofya na
3. Ibambasi Bofya

Waheshimiwa,
Mada hizi nimezipa uzito kutokana na nafasi ya chama kuelekea uchaguzi wa mwaka 2015. Zote hizi zimebeba uzito mkubwa sana wa tafiti zangu ktk jukwaa hili la Siasa pamoja na mkusanyiko wa hoja na mawazo ya wadau ambao kwa kuelewa ama kutoelewa wameweza kuonyesha wazi tofauti zao za kisiasa, kiimani na hata kujenga matumaini hasi japokuwa chama hiki hakitakiwi kabisa kupoteza dira yake kwa manufaa ya mtu ama baadhi ya watu.

Ikumbukwe tu kwamba wananchi wa nchii hii pamoja na tofauti zao bado ni Watanzania wenye kuthamini mila na desturi zao, wanaothamini imani zao za dini, UTU wao na wanaotukuza Ujamaa kama msingi bora na wajibu wa kila mmoja wao kulingana na hali na mali hivyo kufikia kuwapeni dhamana kubwa ya kusimamia UHURU, HAKI na USAWA kwa wawananchi wote wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Tunapodharau vitu hivi kama chimbuko la WATU wenyewe kwa kuaminishwa kwamba tunaweza kuwazuia WATU kutoamini (exclusive) badala ya kuwawezesha wao kutumikia imani zao kama sehemu ya jamii yetu (inclusive) basi tuondoe tumaini la ushindi ifikapo 2015.

Waheshimiwa,
Toka kujiunga kwangu JF nimejifunza mengi sana na nimepanua kiwango changu cha ufahamu wa Mtanzania hasa ktk hali ya Umaskini, Ujinga na maradhi. Nimeweza kuzifukua nyoyo za watu katika maabara ya fikra, hisia na kutazama tatizo hasa linatokana na ukweli upi. Hivyo kama saini yangu (signature) miaka yote hapa JF isemavyo (signature) ni wajibu wangu kuendeleza kile nachokiamini ktk ku explore reality, na nimegundua rasilimali kubwa ambayo chama kinachotaka kuongoza kitakumbana na vikwazo gani na kwa gharama gani. Hivyo kughairi haya ni sawa na kutafuta dhahabu, mafuta au gasi ktk nyanda za mbuga tupu au jangwani..

Hata wachimba Dhahabu, mafuta au gasi nchini huanza na exploration wakajua maliasili hizi zinapatikana wapi precisely, kisha ndio shirika la uchimbaji huchukua report hiyo na kuifanyia kazi.. Hii ndio kazi yangu kwa leo. Kazi yangu ni kuwapa ushauri viongozi wa Chadema tokana na utafiti wa mijadala mbalimbali na hapa JF na nje ya ukumbi huu ktk mkusanyo wa fikra mbalimbali zinatujenga jamii hii ya Kitanzania.

Waheshimiwa,
Kama tulivyowahi kuzungumza awali kuhusu nafasi ya Chadema ktk utawala na maandalizi ya chama kugombea mwaka 2015, bado nina imani kubwa na chama lakini bado kabisa chama chetu kimeshindwa kupasua ngome ya CCM ipaswavyo na kujenga imani za wananchi kwa chama hiki. Kinachotokea ni kujaribu kwa chama chetu kuwavuta wanachama wa CCM zaidi ya kuwavuta wananchi kuichagua Chadema. Kauli mbiu kama VUA GAMBA vaa GWANDA ni moja ya kauli nyingi zilizoonyesha wazi vita ya chama hiki ni kupambana na uongozi wa CCM badala ya kupambana na sera za CCM zilizotufikisha hapa tulipo.

Ebu tutazame Mchambuzi ktk mada yake utagundua kwamba Chadema inajaribu sana kufanya wajibu wake ‘Do the right thing' kukemea Ufisadi, utawala wa mabavu, mapungufu ya JK na kadhalika lakini tumeshindwa kuyafanya ipaswavyo ‘Do things right' hivyo tunashindwa kujenga uaminifu kwamba Chama hiki kitaweza kurekebisha kero za wananchi. Na hivyo wale walioko vyama vingine mbali na CCM wamekosa tujmaini, wale wasiokuwa na mapenzi ya siasa hawana imani na vuyama mvyote na hata wale wanaokichuka chama CCM hatuwapi matumaini isipokuwa kujiunga chama uanachama..

Waheshimiwa, sio mwanachama atakaye tupa ushindi mwaka 2015, bali mwananchi mlalahoi anayetakiwa kwenda ktk sanduku la kupiga kura siku ya Uchaguzi na kutupa imani yake kwenye kipande cha karatasi kama tumaini lake kwa miaka mitano ya uongozi wa nchi hii..

Ndugu Mchambuzi kaorodhesha mambo tisa na haya yana umuhimu wake ktk kumtambua adui yako ngao zake.. Japokuwa ngao hizi haziwezi kuwapa ushindi pasipo mashambulizi ya nguvu ambayo yanategemea na silaha walizonazo..Hivyo katika mada nzima ya Mchambuzi tumeona ngao kubwa za chama CCM ambazo zinaweza tu kutupa matumaini ya ushindi ikiwa tutaweza kuwa na silaha za kuzibomoa.

Hapo hapo tukumbuke tu kwamba nasi tuna ngao gani ambazo zinaweza kuvumilia makombora ya CCM maana ushindi wa vita hii hautokani na kushambulia tu.. Ukweli ni kwamba Chadema hatuna defence zaidi ya kushambulia na kwa bahati mbaya mara kwa mara hushindwa hata kujitetea isipokuwa wa tu kukimbia kimbia maporini kama wakimbizi wa vita au insurgents.

Na kwa nini basi tumeshindwa kuwa na ngao ktk mashambuliz makali yanayoelekezwa kwetu?. Jibu nalipata kwa Mchambuzi tena akisema hivi:- Leo hii masuala ya Uongozi na siasa yametawaliwa sana na misingi ya UKANDA, UKABILA na UDINI. Mheshimiwa hili tupende tusipende ndivyo watanzania watawahukumu viongozi wetu kwa sababu ndivyo siasa za nchi hii zimejikita iwe kutokana kupoteza dira ya Kitaifa, kuwepo kwa vyama vingi ama hisia na wajibu wa viongozi wenyewe kuwajibika ktk makundi ya watu wanaowawakilisha.

Waheshimiwa,
Hii ni tahadhari kubwa sana kwa chama na hasa vyama vya Upinzani ambavyo vimetokana ama kuasisiwa na watu waliopingana ndani ya utawala wa CCM hivyo kuanzisha fikra mpya kinzani ili mradi kujaza ubao wakati nyuma ya pazia hilo kuna KUJUANA..Ni rahisi kusema CCM imeshindwa kutuongoza kwa miaka 50 na watu wakakuelewa lakini ni vigumu sana kuwavuta wananchi ikiwa wataona chama kimeshindwa kupambana na siasa za KUJUANA ndani yake hivyo nje wataweza vipi?.. maana tunawalaumu CCM kwa kujuana lakini pia vyama vyote nchini vinafanya mambo yake kwa KUJUANA.. na pale ngome hii inaposhambuliwa vyama hivi hushindwa kujitetea.

Naye Profesa anawekamaswali yanayowakabiri wananchi wengi sana naomba ninukuu.. anasema kuhusu vyama vyetu vikuu vitatu kati ya CCM, Chadema na CUF ya kuwa –
"Nani kati ya hawa watatu ambao bila ubishi wanashikilia hatamu ya siasa za Tanzania, atatupeleka kwenye nchi yenye neema na amani kwa watu wote bila kujali itikadi, hali yao kiuchumi, kisasa, kidini au kiasili? unahitaji nini kati yao, moja wapo ya chama hiki au Kiongozi kati yao atakaebadilisha upepo na kutuepusha na mgao unaofanywa na vyama vyote hivi (kwa manufaa ya hao wanaoongoza vyama hivi kwa kuwa wanataka kuendelea kuwepo madarakani?) Huko madarakani kuna nini?

Nani atatuambia tutatokaje na siku moja itakayolengwa kwa sisi kuwa sehemu ya taifa Afrika, au Duniani imara kisiasa, kiuchumi, kiutamaduni na kimaendelo kwa ujumla (sayansi, usalama wa chakula, nafasi sawa ya elimu kwa wote, huduma za afya wote, maji safi kwa wote, ziada ya fedha, dhahabu na mafuta ambavyo tunavyo na kila mtu akimvumilia mwenzake na kumheshimu)."

Waheshimiwa,
Mawazo haya sii ya kutafanyia mzaha hata kidogo. Ni mawazo yanayofikiriwa na Watanzania wengi nchini, Watanzania ambao wanajaribu sana kutazama chama mbadala ambacho kinajaribu kwa kila hila kuwajumuisha watu wote ktk Utanzania wao pasipo kujali tofauti zao. Na hatuwezi kuwezesha jambo hili pasipo kuwaunganisha (Inclusive) kama jamii moja badala ya kuwatenga (exclusive) baadhi kwa fikra za kwamba ni wao, wale, hawa ni tofauti na sisi hivyo kama wanataka wayapendayo wafanye wenyewe hili sii jukumu la serikali au uongozi kuwavuta hawa ndnai ya jamii yetu..

Waheshimiwa,
Ndugu Ibambasi katika makala yake naye pia amehoji ushiriki wa serikali hii ktk shughuli za dini, amehoji mambo mengi japokuwa kajiweka ktk kundi la wale wasiokuwa na imani za kigeni isipokuwa za jadi zetu na kudai haki yao kikatiba ili kulindwa na kupewa fursa sawa ktk kushiriki ibada zao. Binafsi yangu pamoja na kutokubaliana juu ya tafsiri fasaha ya ibara inayozungumzia kuwa NCHI yetu haina dini isipokuwa WANANCHI wake ndio wenye dini hushindwa kuelewa nini maana ya NCHI na nini maana ya WATU ikiwa serikali haitawawezesha watu wake wenye dini zao kushiriki ktk ibada zao. Lakini ni muhimu kuyasikia maombi, mawazo kama haya na kuyapatia majibu wala sii kuyapuuza ama kuyazuia kunaweza kutupatia ufafanuzi kamili..

Nchi yetu haina dini kwa maana kwamba mihimili ya utawala wa nchi yetu haitakiwi kuundwa ama kujenga policies zinazotokana na imani ya dini moja isipokuwa serikali inawawezesha wananchi wenye ibada zao. Kuwakwaza wananchi kuabudu kama walivyofanya China na Urusi ni kuondoa ama kupokonya sehemu isemayo watu wake wana dini. Kupingana na mawazo ya kiimani kwa kutunga sheria moja kwa wote itatafsirika tu kama exclusive ama sheria ya kuwatenga wao hivyo kuzaa underground movement kupingana na sheria hiyo. Imetokea sana nchi zilizowakwaza waumini wa dini au kuwayenga makabila kama Wayahudi nchi za Ulaya.

Na Mataifa makubwa yote tokea Roman Empire hadi utawala wa Marekani leo wameanguka ama kupata mtihani mkubwa pale wanapojaribu kuwatenga watu kwa kutumia dini, kabila au tamaduni zao hivyo ni muhimu sana kwa chama hiki kuzingatia pamoja na kwamba serikali haina dini lazima tukumbuke wananchi wetu wana dini zao na makabila yao, wana maumbile yao hivo ni lazima vienziwe na sio kupigwa vita. Tunapiga vita wale wanaojaribu kukwaza wengine, wale wanaojaribu kuleta Ukabila na Udini (kudharau wengine) lakini sio wale wanaoitaka haki ya kuabudu kama alivyosema Ibambasi kwa utetezi wa waumini wa jadi..

Waheshimiwa, Inabidi nikomee hapa ktk waraka huu ambao unasisitiza zaidi kujitazama upya. Kutazama makundi ya jamii zetu kama sehemu ya Utaifa wetu badala ya kujaribu kuwabadilisha ama kuwakwaza. Chadema ktk hali hii inahitaji sana nguvu ya Watanzania wapiga kura ambao kwa nafasi zao hawawezi kushawishika na Utaifa ulojaa KUJUANA na sii rahisi wanaongoa watu wasikuwa na Imani.

Hivyo, Tuache UNAFIKI, tuache kujidanganya kwa unafiki wa wapambe wa vyama wanaotumia siasa kaa uwanja wa kujuana. Sisi sote ktk nafasi tulizopo na kutambua kwamba Utanzania wetu unajumuisha tofauti zetu za maumbile, makabila na imani za dini na yeyote atakaye jaribu kumdharau hata mmoja wetu ni kielelezo cha Ubaguzi ambao hautakiwi kupewa nafasi bali kuupiga vita. Hizi ndio ngao zetu, ndizo zinazo tu identify kama jamii ya Kitanzania na lazima tuzilinde dhidi ya siasa za chuki na uutengano. Bila utayari wa kuwajumuisha watu wote kwa tofauti zao kama sehemu ya Utanzania wetu itakuwa vigumu sana kupata ushindi mwaka 2015 maana CCM wanaifanya kazi yao ipaswavyo – Kushambulia nasi ktk kujilinda lazima tuwe na kinga zetu kwa kufanya vitu sawa – Doing things right !

Nawakilisha..
 
Last edited by a moderator:
Mkandara

Kwa sehemu ndogo niliyokupata umemaanisha watu wanaojipambanua kwa dini zao wapewe nafasi ya kubembelezwa!!!!

Mimi nawaambia viongozi wangu wa chadema; ni heri kutokuingia ikulu kuliko kuingia kwa upendeleo wa wanaojitambua kwa imani zao.

Waelimisheni wajitambue kwa utanzania wao ndipo wawape ridhaa ya kuwaongoza.
Haihitajiki mistari miiiiiiiiiingi unazunguka zunguka kisa unataka waislamu wapewe aproach ya kiislamu.

kwenye ukombozi huu wanatakiwa watanzania-waislamu pamoja watanzania wa imani zingine na wala si waislamu-watanzania . . . .
 
Umesoma lakini hujanielewa na ndilo tatizo la Watanzania hamtaki kusoma isipokuwa amnajua sana kuuchonga ktk ujinga..Sijazungumzia vyeo wapewe kina nani isipokuwa kutokuwepo mfumo huo utumike maana unatumika. Swala ni kutambua uhuru, haki na usawa wa jamii zetu. Huwezi kuleta usawa mahala popote kwa kuzuia (kukwaza) isipokuwa kwa kuwawezesha. Hata katika uzalishaji hatuwezi watu wote kuwa Wakulima wa kilimo, isipokuwa wapo wafugaji, wavuvi, wafanyabiashara na Wafanyakazi , wawekezaji na kadhalika. Hawa wote wanataka kuwezeshwa na sio kukwazwa ktk nafasi zao za Uzalishaji kwa sababu kiongozi fulani anapendelea zaidi Ukulima.

Labda nikuulize wewe UTANZANIA ndio nini? nini mila na desturi zao, wanafananaje? wana mahusiano gani tofauti na watu wengine au unataa kunambia ukisha zaliwa Tanzania basi unalazimika kuwa kinyambiro kisichokuwa na identity. hata Mweneyezi Mungu katuumba tofauti kwa maumbile, makabila na kadhalika leo wewe nani wa kusema hakuna tofauti hizi.
 
Nashauri JF tuanzishe utaratibu wa kuwa na abstracts. Kuna posts ndefu mno kiasi cha kuweza kumfanya mtu afukuzwe kazi (kumbuka kuna mambers wengi wanaaccess JF wakiwa kazini).

Ukiandika post ndefu itengenezee abstract ya maneno kama 150 iweke pale juu, ili wadaua wa fasterfaster wapate picha nini kinazungumziwa...
 
Bila shaka lakini huu ni waraka wangu na nimeulekeza kwa watu wangu. Wewe soma kiasi chako, ukirudi kesho endelea halafu utafikia mahala utamaliza kisha jenga hoja. Ni mtazamo wangu tu...
 
soma acha uvivu
 
Asante mkandara. Mimi naona nguvumzaidi Za hoja zielekezwe vijiijini ambako watu Havana mbadala.nccm inatakiwa ishindwenkwa asilimia sabini hivi ndogo kujiandaa kutawala come 2015, kwanza inabidi wajeruhiwe sana 2014
 
Mkuu Mkandara kwa miaka mingi sasa nimekuwa nasikia hizi propaganda zinazofanywa na magamba kwamba CHADEMA ni chama cha kikabila na kidini lakini hadi hii leo sijaona mifano yoyote ile ambayo imewahi kutolewa ili kuthibitisha kwamba kweli CHADEMA ni chama cha Wakristo na Wachaga.

Tukiangalia ndani ya CHADEMA viongozi wajuu kama Dr Slaa, Lissu, Zitto na wengineo si wachagga na pia Zitto si mkristo. Tukiangalia Wabunge wa CDM walichaoguliwa katika uchaguzi wa 2010 pia tunaona Wabunge wa CDM wametoka katika mikoa mbali mbali si Kilimanjaro pekee hili pia linathibitisha kwamba Watanzania wamekikubali CDM na hivyo kutoona kama kuna matatizo yoyote ya kuwapigia kura wagombea wake wa nafasi ya Ubunge. Mpaka sasa hivi katika sera zote za CDM sijaona sera yoyote ile ambayo imekaa kikabila au kidini.

Ndani ya CDM pia kuna wanachama wengi na wafuasi wa CDM ambao ni Waislamu na wamekikubali chama hicho pamoja na propaganda za nguvu zinazofanywa nchini ili kukionyesha chama cha CHADEMA kama ni cha Wakristo.

Hivi karibuni hapa jamvini nimesoma bandiko la mwenzetu mmoja aitwaye mohamed Mtoi kwa kweli lilinifariji sana na kunithibitishia tena kwamba CDM si chama cha kidini kama vile ambavyo magamba wanataka tuamini.

Bandiko la Mohamed ni hili hapa:

Mimi huwa namshangaa sana Ritz! Hata kama ni muislamu wa siasa kali uislamu wetu hauna chuki na upande wa pili namna hiyo! Kwanza muislamu yoyote uislamu wake hauwezi kukamilika kama hakiri kutambua uwepo wa ukristo kama jinsi ukristo unavyotambua uwepo wa uislamu! Uelewa mdogo ndio unamfanya Ritz anakuwa mbumbumbu wa mambo ya dini kiasi hiki!

Hapa leo anawatetea ccm na kusahau kuwa ccm ndio waliichafua cuf kuwa ni chama cha udini na kigaidi, baadae haohao wakasema chadema ni chama cha wakristo lakini wao hawasemi kuwa ni chama cha dini gani! Sasa ukija hapa ukimuona jinsi ritz anavyotoa povu la udini unajua kabisa aidha uelewa wake ni mdogo au yuko hapa kwa kazi maalum ya kipato kutoka Lumumba.

Mimi ni muislamu lakini napingana sana na misimamo ya Ritz! Alisha diriki kuniambia Mohamedi na chadema wapi na wapi?! Huu ni upovu iliopiitiliza na tangu siku ile niliamua kumsamehe bure na kumkabidhi Mungu maana nimeona ni mtu ambae ana uabisha hata uislamu wenyewe.

Hapa chini sijakuelewa. Pale ulipoandika kuwakwaza wananchi kuabudu na kupingana na mawazo ya kiimani. Je, una maana CDM inawakwaza wananchi kuabudu na pia inapingana na mawazo ya kiimani? Naomba ufafanue tafadhali kama muda wako unakuruhusu kufanya hivyo.

"Nchi yetu halina dini kwa maana kwamba milihili ya utawala wa nchi yetu haitakiwi kuundwa ama kujenga policies zinazotokana na imani ya dini moja isipokuwa serikali inawawezesha wananchi wenye ibada zao. Kuwakwaza wananchi kuabudu kama walivyofanya China na Urusi. Kupingana na mawazo ya kiimani kwa kutunga sheria moja kwa wote itatafsirika tu kama exclusive ama sheria ya kuwatenga wao hivyo kuzaa underground movement kupingana na sheria hiyo. Imetokea sana nchi zilizowakwaza waumini wa dini au kuwayenga makabila kama Wayahudi nchi za Ulaya."

Natanguliza shukrani

L
Umesoma lakini hujanielewa na ndilo tatizo la Watanzania hamtaki kusoma isipokuwa amnajua sana kuuchonga ktk ujinga..Sijazungumzia vyeo wapewe kina nani isipokuwa kutokuwepo mfumo huo utumike maana unatumika. Swala ni kutambua uhuru, haki na usawa wa jamii zetu. Huwezi kuleta usawa mahala popote kwa kuzuia (kukwaza) isipokuwa kwa kuwawezesha. Hata katika uzalishaji hatuwezi watu wote kuwa Wakulima wa kilimo, isipokuwa wapo wafugaji, wavuvi, wafanyabiashara na Wafanyakazi , wawekezaji na kadhalika. Hawa wote wanataka kuwezeshwa na sio kukwazwa ktk nafasi zao za Uzalishaji kwa sababu kiongozi fulani anapendelea zaidi Ukulima.

Labda nikuulize wewe UTANZANIA ndio nini? nini mila na desturi zao, wanafananaje? wana mahusiano gani tofauti na watu wengine au unataa kunambia ukisha zaliwa Tanzania basi unalazimika kuwa kinyambiro kisichokuwa na identity. hata Mweneyezi Mungu katuumba tofauti kwa maumbile, makabila na kadhalika leo wewe nani wa kusema hakuna tofauti hizi.

mkandara umenielewa vema! Wala hoja yangu haijifichi kwenye mistari kama unavyojitahidi kuuficha uislamu kwenye riwaya yako.

Kama unataka kujua utanzania ni nini, msubiri kuna mtu toka malawi anaitwa Chiume anakuja dar. bado kitambo kidogo.
Waislamu safi wanajua kuwa uislamu ni harakati za kuwapeleka peponi ama kuwakutanisha na muumba wao, hakuna kipengele cha urais wala u-mizengo pinda kwenye kuruani, ndio maana kupitia utanzania wao ikulu inakuwa wazi kabisa.

Huendi ikulu na mashuka yako ya kimasai eti wewe nadumisha mila, kama unataka umasai wako nenda kwa laigwanani na morani huko kwenye himaya ya nyumbu.

Una matheory yasiyotekelezeka achana nayo. Usijidanganye kuwa watanzania ni wavivu wa kufikiri, mara useme ni wajinga, jifunze kuwaheshimu ndipo uwape huo ujumbe unaotaka kuwapa, na ujumbe uwe na viwango, sio paragraph nzima huna ulichosema. Tunashindwa kukutoautisha na porojo za nape.
 
Mkuu Mkandara kwa miaka mingi sasa nimekuwa nasikia hizi propaganda zinazofanywa na magamba kwamba CHADEMA ni chama cha kikabila na kidini lakini hadi hii leo sijaona mifano yoyote ile ambayo imewahi kutolewa ili kuthibitisha kwamba kweli CHADEMA ni chama cha Wakristo na Wachaga.

Tukiangalia ndani ya CHADEMA viongozi wajuu kama Dr Slaa, Lissu, Zitto na wengineo si wachagga na pia Zitto si mkristo. Tukiangalia Wabunge wa CDM walichaoguliwa katika uchaguzi wa 2010 pia tunaona Wabunge wa CDM wametoka katika mikoa mbali mbali si Kilimanjaro pekee hili pia linathibitisha kwamba Watanzania wamekikubali CDM na hivyo kutoona kama kuna matatizo yoyote ya kuwapigia kura wagombea wake wa nafasi ya Ubunge. Mpaka sasa hivi katika sera zote za CDM sijaona sera yoyote ile ambayo imekaa kikabila au kidini. Hivyo

Ndani ya CDM pia kuna wanachama wengi na wafuasi wa CDM ambao ni Waislamu na wamekikubali chama hicho pamoja na propaganda za nguvu zinazofanywa nchini ili kukionyesha chama cha CHADEMA kama ni cha Wakristo.

Hivi karibuni hapa jamvini nimesoma bandiko la mwenzetu mmoja aitwaye mohamed Mtoi kwa kweli lilinifariji sana na kunithibitishia tena kwamba CDM si chama cha kidini kama ambavyo magamba wanatama tuamini.

Bandiko la Mohamed ni hili hapa:

Mimi huwa namshangaa sana Ritz! Hata kama ni muislamu wa siasa kali uislamu wetu hauna chuki na upande wa pili namna hiyo! Kwanza muislamu yoyote uislamu wake hauwezi kukamilika kama hakiri kutambua uwepo wa ukristo kama jinsi ukristo unavyotambua uwepo wa uislamu! Uelewa mdogo ndio unamfanya Ritz anakuwa mbumbumbu wa mambo ya dini kiasi hiki!

Hapa leo anawatetea ccm na kusahau kuwa ccm ndio waliichafua cuf kuwa ni chama cha udini na kigaidi, baadae haohao wakasema chadema ni chama cha wakristo lakini wao hawasemi kuwa ni chama cha dini gani! Sasa ukija hapa ukimuona jinsi ritz anavyotoa povu la udini unajua kabisa aidha uelewa wake ni mdogo au yuko hapa kwa kazi maalum ya kipato kutoka Lumumba.

Mimi ni muislamu lakini napingana sana na misimamo ya Ritz! Alisha diriki kuniambia Mohamedi na chadema wapi na wapi?! Huu ni upovu iliopiitiliza na tangu siku ile niliamua kumsamehe bure na kumkabidhi Mungu maana nimeona ni mtu ambae ana uabisha hata uislamu wenyewe.

Hapa chini sijakuelewa. Pale ulipoandika kuwakwaza wananchi kuabudu na kupingana na mawazo ya kiimani. Je, una maana CDM inawakwaza wananchi kuabudu na pia inapingana na mawazo ya kiimani? Naomba ufafanue tafadhali kama muda wako unakuruhusu kufanya hivyo.

"Nchi yetu halina dini kwa maana kwamba milihili ya utawala wa nchi yetu haitakiwi kuundwa ama kujenga policies zinazotokana na imani ya dini moja isipokuwa serikali inawawezesha wananchi wenye ibada zao. Kuwakwaza wananchi kuabudu kama walivyofanya China na Urusi. Kupingana na mawazo ya kiimani kwa kutunga sheria moja kwa wote itatafsirika tu kama exclusive ama sheria ya kuwatenga wao hivyo kuzaa underground movement kupingana na sheria hiyo. Imetokea sana nchi zilizowakwaza waumini wa dini au kuwayenga makabila kama Wayahudi nchi za Ulaya."

Natanguliza shukrani

Kama mumenisoma vizuri utagundua kwamba nachozungumzia mimi ni Chadema kutokuwa na defensive strategy inayohusiana na maswala haya. Tuna silaha nyingi sana za kuishambulia CCM na Mchambuzi katupa hints ni ngao zipi CCM inajivunia leo. lakini hapo hapo hakutazama kama Chadema nayo ipo uchi sana haina ngao zake isipokuwa silaha tupu za mashambulizi. Tukishambuliwa ktk Ukanda, Udini au Ukabila mara zote huja na mifano ya Zitto.. Yaani kweli Zitto pekee ndio sababu ya kutulinda ktk Ukanda, Ukabila na Udini. Nini ngao zetu? sisi tunaweza vipi kujivunia kutoshiriki ktk hizi tuhuma za KUJUANA tofauti na CCM ambao hadi kesho tunaunga mkono baadhi ya ushirika wao wenyewe. Hatuna majibu mkuu wangu tunaulizwa kila siku hapa JF mara zote majibu hutolewa na kina Mkandara au Mohammed Mtoi.. Mimi na Mohammed Mtoi tunaweza vipi kuwa na majibu ya uongozi wa Chadema inapokabiriwa na tuhuma nzito kama hizi hata kama najua sii kweli.. sema kweli maana janvi hili ni mawazo ya mtu mmoja mmoja sio janvi la chama.

Uvumi siku zote ndio hujenga imani za watu, wanasema Chadema ni chama cha Ukanda au udini, wewe huzioni, mimi zisioni na vile vile kumbuka hata mtu wa CUF anaamini hivyo hivyo. Na sidhani kama tunaweza kuonyesha Udini wa CUF lakini Je ni watanzania wangapi wanaamini CUF sio chama cha Waislaam au Wazanibar?..wamepewa majibu gani?.. maana ukweli ni kwamba CUF wenyewe hawana ngao, hawana majibu wala defence mechanism inayo onekana isipokuwa wao wenyewe wanajiingiza zaidi ktk ukimya.. Je ktk hali hiyo unafuu na credit zinakwenda wapi - CCM, uongo! I have done my study mkuu wangu na nakuhakikishia najua nilichokiandika..
 
Mkuu Mkandara kwanza nikupongeze kwa kazi yako nzuri na ngumu.

Mimi nasema nzuri kwamujibu wa mapitio yangu katika waraka huu unaotoa msukumu wa kujitazama hata kama kinacholengwa hakipo. Hiyo ndio maana ya HONGERA mkuu.

Simaanishi hiki ulichokisema HAKIPO ndani ya Chadema na wala SIKUBALI moja kwa moja kuwa KIPO.

Mimi nasimama kwenye uchambuzi wako murua tu, Uchambuzi wako unasura moja tu ya kisiasa na ndio maana nausifu na kuheshimu sana andiko hili.

Kwanza umesimamia na kuisujudu kura ya TURUFU, hili ndilo linalompasa mwanasiasa wa leo na mwangalizi wa siasa makini kama Mkandara,

Mimi niseme tu ujumbe umefika bila makunyanzi, hauna madhara kwa kura ya turufu bali una mafaa, Ieleweke kuwa kura ya TURUFU ndio kura muhimu waitafutayo Watanzania wa leo. lakini waraka huu unamadhara kwa waliojipa uhafidhina wa nchi hii.
 
mimi sija soma waraka wa Mkandara wote, lakini kwa kiasi nimeona matatizo ya cdm , kikubwa tatizo lake ni structure yake ina mapungufu mengi, sasa kuna watu wameshikilia nafasi na wanajua waki karibisha watu fulani basi ni wazi structure itabadilika, na pili kutumia taarifa za watu , ku-black mail, sasa hili halitawezesha mtu yoyote serious kijiunga nacho, rejea utaratibu wao mtu kujiunga na kuzitoa taarifa hizo, mitandaoni au kwenye magazeti nk., matokeo yake kwa mtu serious kama huwezani na ccm, na cdm ndio wana urasimu wao basi ni wazi kutaanza kwa utitiri wa vyama vingine, matokeo yake come 2015, watakosa kura sehemu zingine, kwani watu walio powerful sehemu zingine ambao hawawezi kuishi structure yao watakwenda adc, au chama kingine tu kinaweza kutokea.
 
L

mkandara umenielewa vema! Wala hoja yangu haijifichi kwenye mistari kama unavyojitahidi kuuficha uislamu kwenye riwaya yako.

Kama unataka kujua utanzania ni nini, msubiri kuna mtu toka malawi anaitwa Chiume anakuja dar. bado kitambo kidogo.
Waislamu safi wanajua kuwa uislamu ni harakati za kuwapeleka peponi ama kuwakutanisha na muumba wao, hakuna kipengele cha urais wala u-mizengo pinda kwenye kuruani, ndio maana kupitia utanzania wao ikulu inakuwa wazi kabisa.

Huendi ikulu na mashuka yako ya kimasai eti wewe nadumisha mila, kama unataka umasai wako nenda kwa laigwanani na morani huko kwenye himaya ya nyumbu.

Una matheory yasiyotekelezeka achana nayo. Usijidanganye kuwa watanzania ni wavivu wa kufikiri, mara useme ni wajinga, jifunze kuwaheshimu ndipo uwape huo ujumbe unaotaka kuwapa, na ujumbe uwe na viwango, sio paragraph nzima huna ulichosema. Tunashindwa kukutoautisha na porojo za nape.
Hujanisoma . hunielewi na wala hutanielewa waislaam wanasema - Summun bukmun umyun fahum layarji..

Nani kazungumzia Pinda au kkiti cha Ikulu au nazumgumzia Utawala unaowapa uhuru haki na usawa waumini wake. Mbna Uingereza na Marekani ni nchi ya wazungu na Kikristu, lakini wanatoa Uhuru, haki na usawa kwa wananchi wake waumini wa dini zote wafanye ibada zao pasipo kupingwa?..
 
Kwa matukio yanayotokea siku za karibuni issue udini imekaa vibaya sana kwa CCM zaidi ikifuatiwa na CUF zaidi ya CDM.CDM watabanwa katik ukanda ila tayari stonghold yake imeshift sana Mbeya, Iringa, Mwanza, Kigoma itategemea na Jinsi ZItto atajiweka ,Songea,Morogoro na Kwingine Tayariwameshajiona kuwa wamechelewa wamechelewa jiunga na CDM. CDM ni brand ambayo kila siku kuna watu wanaharakisha kujiunga kama wanavyotaka account ya facebook.

CUF wana shida kwani bado hawajaweza jipamabanua vizuri umbali wao na CCM huku ikiwabidi kugawana wafuasi na Hamad rashid kaatik chama kipya. Wakati CCM itabanwa na waislam kuhusu mahakama ya kadhi, na wakiitoa nusunusu waislam watagawanyika.Kwa kuweka mahakama ya kadhi kamili kutaamsha hasira za wasio waislam na hivyo kuiadhibu CCM.CCM watakuwa na mgogoro na waislam sana tofauti na wanavyodhani kwani bado waislam wataihitaji kadhi wao asiwe kama ilivyokuwa Bakwata.Kwani bado waislam hawana imani na hilo baraza.

Suala la ukanda ktik CDM wamejipanga kuliweka sawa ndio maana kila mara CCM wakijaribu lichomekea mbele za watu response wanayopata inawatia adabu.CUF wakifanya makosa kulitumia litawatafuna sana kwani, tayari wao nguvu zao kubwa zinaonekana ni kutoka wapi.Hata kama ni matokeo tuu ya uchaguzi ila si haba kupata mzanzibar atakayejisahau na kusema neno la kibaguzi kwa mgongo wa CUF.

Pia ikumbukwe kuwa CDM hawajachoka kufanya suprises, CDM nao watakuwa offensive kwa CCM tofauti na wanavyodhani, kwani by the time CCM wanadhani wamepanga timu ya mashambulizi watakuta tayari hiyo timu in mamluki wa CDM.Hii si geni kwani katik ya hao 55 + Mh Sitta, nani anawajua hao wengine waliopatikana katik dili nyingine.Tayari UVCCM wameshaanza bomolewa makazi na CCM inahofu kuwa ni CDM. CDm wamewaambia CCM nchi haitotawalika hadi leo haitawaliki na mziki unaendelea.

Matumaini yangu ni kwamba tayari CDM wana kila sabau ya kushinda.Tena wakiamua sasa hivi ama kwa maandamano ama kwa kuifanya CCM ku implode kam Soviet.
 
Unavyofikiria wewe.. tatizo ni kwamba hamtaki kuelimika isipokuwa kwa yale mnayoyapenda wenyewe. Ebu nambie vyama vyote nchini vina wanachama wangapi, na nini jumla ya hesabu ya wapiga kura nchini wanaotarajiwa mwaka 2015. Ushindi hupatikana vipi?..Itakula kwenu na mtakuja shtuka its too late..
 
Nadhani ni kama usivyopenda wewe zaidi ya kinyume chake.Wanachama wanaongezeka na wapiga kura watakuwa mara dufu.This time tume itarekebisha daftari na watu watapewa vitambulisho kwa wingi.

Tatizo lipo kwa CCM kwani wamejiweka katik mazingira magumu sana na problems zinazidi kuongezeka as time goes by.Every problem wanayo create ili ijeruhi wengine ina bounce back more strongly .

Ni wewe tuu na wana CCM si wasikivu na mnakimbia ukweli, na wala sioni faida yake.Ni bora wakajipanga na kuminize domain ya problems.Ili baadaye wakijaanza pigana vikumbo watabaki na resources kidogo sana za kuziba nyufa na kupata mgombea, achilia mbali makovu mapya ya uchaguzi.kama haya tuu ya uchaguzi uliopita hayajaisha ni vipi wataweza simama na chama machachari kama CDM?

Itategemea CUF watajipanga vipi wanaweza kuwa na crucial role ktk chama tawala na chama kikuu cha upinzani.Pia kutokea ushindi tofauti wa sehemu mbili za nchi.Yaani chama tofauti bara na tofauti visiwani.nadhani ahpa ndipo pa kuumiza vichwa na si hivi brainwashing articles.

By the way..Mkuu kwanini umetumia lugha km hii?ina utofauti sana na waraka hapo juu..waraka unaonekana kama ulikuwa uanbrainwash.Ila hi response kama unatongoza.Namkumbuka mwalimu wangu mmoja alikuwa mzuri sana katik kufundisha, alikuwa akifundisha kwa ustadi mkubwa sana .Na alicontrol sauti vizuri sana,kiasi ch akuwafanya wanafunzi waweze flow na maneno yake.Kuna siku aliniacha.Kuna vitu havikuwa viki add up na previous knowledge.Nikatulia ku-digest.bahati mbaya siku hiyo nilikaa mbele, aakanipiga jicho akakuta kama nipo deep kufikiri alichosema siku hiyo.Rohoni alijua kuwa alichofundisha siku hiyo hakuwa akikijua vizuri..basi akaanza insist sana kwa maneno kama fulani kuwa hiyo "ndio kweli" na "kila mtu ajue hivyo" ila" maswali hayatoki sana huko" ndipo niliposhtuka na kuangalia posibility kuwa inawezekana si mimi ni kilaza ila mwalimu anaweza kuwa hakuwahi soma wala fundihs hiyo topic kwani mtaala ni mpya.Na baadaye kweli nikawa right.Nilipojisomea vizuri kesho yake tulipokutana class naye akawa amesoma ili kuondoa embarasment, basi tukawa tunaelewana vizuri na mwalimu akawa ana amani sana.
 
Bila shaka lakini huu ni waraka wangu na nimeulekeza kwa watu wangu. Wewe soma kiasi chako, ukirudi kesho endelea halafu utafikia mahala utamaliza kisha jenga hoja. Ni mtazamo wangu tu...

Hiki ndo nachokikataa mimi na ninapogundua kuwa we ni mtu wa namna gani katika kunena lakini ukashindwa kuonesha unachokinena kwa matendo ni ushahidi tosha kuwa ni mtu mnafiki.
Ngoja nikwambie kwa nini nimesema hivyo; waraka wako uko wazi kwa kusisitiza umuhimu wa kuwa mtu wa watu wote kama kiongozi. Na tafsiri ya uongozi hapa ni kuwa kila binadamu mwenye akili timamu ana sifa za uongozi. Umetuo ushauri wa kiuongozi lakini umeshindwa kuonesha tabia za kiungozi.

Katika jibu lako hilo umebagua, umesema una watu wako kwamba uliyemjibu sio sehemu ya kusudio lako maana kuna watu umewalenga. Sasa utawezaje kuhubiri kitu kuhusu kuthaminiana wakati wewe hujathamini?!
Teh teh teh Tanzania bhana.

Kwa ufupi, waraka wako una madhaifu mengi. Nayafanyia kazi halafu nitakujibu.
 
Back
Top Bottom