Kwanza, heshima yako na pole kwa majukumu ya kila ya ujenzi wa taifa hili.\
Pili, Uniwie radhi kama nitakayosema yatakuwa mambo ya kawaida sana kiasi chakutostahili waraka huu. Hata hivyo nimeona yaweza kuwa ni ya muhimu kwangu/kwetu wahanga wa tatizo hili.
Mheshimiwa Rais mimi na wenzangu wafanyakazi wa UDOM tulikuwa promoted November 2010 na November 2011 kutoka ngazi moja ya utumishi kwenda nyingine. Kwa wale wa November 2010 tulikaa pasipo kulipwa mshahara wa ngazi mpya ya mshahara kwa miezi 13 pasipo kulipwa mshahara huo mpya hadi hapo December 2011 tulipolipwa.
Baada ya kulipwa tulijaza salary arrears claim forms mwezi February 2012 lakini hadi leo hatujalipwa malimbikizo hayo. Cha kusikitisha zaidi ni pale tulipokuwa tunajaza form hizo tuliambiwa tujaze mshahara wa chini ya stahili yetu kwa maelezo kuwa Hazina wangetulipa pasipo kujali kile tulichojaza (stahili yetu).
Naandika waraka huu kukuomba mawili;
i) Kuomba utusaidie tulipwe mapunjo (arrears) yetu kwakuwa imechukua muda mrefu sasa.
ii) Kuomba ofisi yako kupitia utumishi utupeleke kwenye ngazi stahili ya mshahara yaani PUTS 2/3 badala ya PUTS 2/1 ambayo tumekuwa tukilipwa tangu November, 2010
Tuna imani ofisi yako itatusadia kupata haki yetu hii cheleweshwa ama tuliyopunjwa kwa muda mrefu sasa.
Ndimi katika ujenzi wa taifa
Mtumishi katika nchi hii.