Huwezi kukubaliana na mimim kwa vile kama alivyosema Ibrahim Hussein wewe unapanda ngazi mimi ninashuka ngazi.
Unajuwa hiyo awamu yako ya kwanza ndiyo iliyoleta udini kwa kuleta upendeleo kwa dini moja, kwa kuvunja misingi ya dini nyengina (kwa kuondowa mahakama ya Kadhi) na kudidimiza mikoa iliyokuwa na Wafuasi wa dini fulani( Pwani, Kigoma. Mtwara, Lindi na mengineyo).
Isitoshe Katibu na taratibu zote za kuendesha Serikali zikawekwa kidini fulani (mapunziko Sunday, Friday ni siku ya kazi muhimu) na mambo chungu nzima.
Unachosema kuwa udini unaoletwa kwa awamu zinazoongozwa na watu wa dini nyengine si chengine bali ni harakati za kudai haki tuliyokuwa tukihubiriwa na Ki8ongozi wa awamu ya kwanza aliyekuwa mdini mkubwa wa vitendo huku akilainisha kwa maneno.
Waislamu na Wakirsto ni Watanzania na wote wana haki ya kuabudu kwa mujibu wa Katiba, sasa kwa mmoja iwe wa dini ya pili ndio ampangie kiasi cha kufanya ibada huoni kuwa huwa ni mushkeli. Elewa dini haifanywi nusunusu au kwa matakwa ya binaadamyu bali tunafuata tuliowekewa na imani zetu, sasa iwapo dini mo0ja haina uhuru wa kuabudu kwa mujibu wa imani yao na badala yake waabudu kwa Katiba iliyowekwa kwa shindikizo la dini nyengine, ujue upo mushkeli.
Mwisho babaangu, kama unavyowaona Walimu wanavyoichachafya Serikali kwa kudai haki yao hali hiyo haitakuwa tofauti kwa Waislamu katika kudai haki zao
Mi nakushangaa sana! Kwanza kabisa unaposema waislamu Tanzania hawana uhuru wa kuabudu una maana gani? Maana hii si kweli na hakuna haja ya kubishana kwa hili.
Pili unaposema, mahakama ya kadhi kuondolewa ndio kuleta udini mimi sikuelewi kwa sababu moja ambayo ni kama ifuatavyo: Je unajua kuwa wakatoliki na wao wana "canon law". Canon law ni sheria za kanisa katoliki. Na kanisa katoliki lina mahakama zake ambazo zinatoa hukumu kama vile ilivyo mahakama ya kadhi. Alichofanya serikali ya awamu ya kwanza ni kuiondoa kwa sababu Wakatoliki na wao wangetaka mahakama zao zifanye kazi. Wasabato, Waanglikani, Walutheri, wapagani hata wao wangedai zao. Sasa ili kuwa na mfumo wa haki ulio sawa kwa raia wote, ndio tulisema kuwa tufuate sheria za nchi. Ila kama mahakama hizo zitatumika zitumike tu kwa waumini wake na si kama sehemu ya mfumo wa serikali. Kwa kifupi ndio hivyo. Ukitaka nikupe darasa vizuri, nipo tayari kufanya hivyo. Muda ninao.
Halafu suala la Ijumaa na Jumapili, tulilikuta. Halikuwa la Nyerere wala la Waislamu, wala la Wakristu. Sasa mkisema Nyerere katika hili ni kama tu mnamwonea maana system karibu ya nchi zote za Afrika hiko hivyo ukitoa tu zile za kaskazini mwa Afrika. Fanya utafiti ili ulifahamu hili.
Suala la Waislamu kuonewa, mimi nalipinga mpaka kesho. Rais ni mwislamu, makamu wake ni mwislamu, rais wa zanzibar ni mwislamu, hata katibu wa chama tawala ni mwislamu, mabalozi wetu wengi nje ya nchi ni waislamu, sasa uonezi wa wakristu unatoka wapi? nauliza. Hivi mwislamu anaweza kumwonea mwislamu mwenzake? sasa rais ni mwislamu anaweza vipi kuwaonea waislamu? Nadhani rais amejitahidi kubalance tumwache afanye kazi yake.
Ukitoa mahakama ya kadhi (ambayo vile vile wakristu wana mahakama zao ila hawasemi tu) kuna uonezi gani? Mimi hoja ninazo ukitaka nikupe za kiutaalamu zinakuja.