jogi
JF-Expert Member
- Sep 25, 2010
- 25,558
- 25,322
Hoja ya msingi :
1:kwanini chadema ilishidwa vibaya kwa kupata viti 23 kati ya 239 kwenye uchaguzi uliopita?
2:Je kulikuwa na ulazima kwa CHADEMA kukaidi amri ya polisi ya kusubiri sensa ipite?
3:Je, ukaidi wa CHADEMA siyo chanzo cha maafa yaliyotokea na yanayotokea mara kwa mara nchini?
4:Je, ingekuwa sawa kwa jeshi la polisi kuwaachia CHADEMA kufanya shughuli ambayo walikwisha wazuia wasiifanye?
5:Je, polisi ingewaachia kufanya jambo ambalo walikwishawazuia wangekuwa wanatimiza sheria na wajibu wao?
6:Je walichukua hatua yoyote ya kisheria dhidi ya polisi au hawana imani na vyombo vya kisheria kama ambavyo Tundu Lissu anavyoziponda mahakama zetu bila kuheshimu kwamba zilimpa ushindi yeye binafsi katika kesi yake ya uchaguzi aliyofunguliwa na mgombea wa CCM, na zile zilizokipa ushindi chama chake zilizowavua ubunge wana CCM huko Sumbawanga na Igunga.
Hizi ni hoja za msingi sana ambazo hazijajibiwa so far zaidi zaidi naona watau wanatapa tapa tu na kumshambulia mtoa hoja binafsi badala ya hoja zake,ondokeni kwenye denial and anger jibuni hoja
hizo ndio hoja za kitoto,
Labda utueleze kikosi cha kutuliza ghasia kilienda kutuliza ghasia gani, zilizoripotiwa kufanywa na nani.
kwa mafunzo waliyoyapata ccp, polisi walishindwaje kuwakamata wafanya ghasia pamoja na kuwa na zana za kisasa kutuliza ghasia.
Hatukuonyeshwa watu wakifanya ghasia, lakini inakuwaje lengo kuu la kutuliza ghasia linakuwa kuua.
Kanuni ya kijeshi inaelekeza kuwa "ukimkamata mateka unawajibika kumlinda" kwa maneno mengine huruhusiwi kumuua, huyu Mwangosi RIP
alikuwa ameshikiliwa na polisi wasiopungua sita, wamemuuaje tena mbele ya makamanda wawili, kamuhanda na kamanda wa kikosi cha kutuliza ghasia.
Cha kujadili hapa ni;
Amri ya kuua ilitolewa na nani kati ya hao makamanda wawili.
Ikiwa muuaji alitekeleza mauaji bila amri ya senior polisi officers, ni vipi hao senior polisi officers hawakulaani mauaji hayo with immediate effect, na kumshitaki kwenye mahakama ya kijeshi immediately.
Kwa kuwa mazingira yanatuelekeza kuwa makamanda walitoa amri ya kuua, ndiyo maana wakachukua hatua ya kumtetea na kumkingia kifua muuaji,
kwa mwendelezo huo huo na nchimbi katumbukia kwenye kosa la kuwatetea wauaji sawasawa na kamuhanda,
Na ccm inamtetea nchimbi, anayewatetea kamuhanda & kamanda wa kikosi cha kutuliza ghasia, wanaomtetea askari muuaji.
Hatudanganywi kwa waraka wa MTU ALALAYE NA MAMA YAKE KAMA ALAVYO NA MKEWE, kama alivyouhakikishia umma kwa ahadi ya kurudi ccm.