Waraka wa Tambwe Hizza kwa watanzania

Waraka umetolewa kisiasa zaidi!

Acheni ushabiki wa kitoto tambwe pamoja na mapungufu yake mengi tu kwa hili namuunga mkono,ameongea mambo ya msingi sana ambayo yanahitaji tafakuri pana sana kabla ya kuleta ushabiki,kwanini chadema walikiuka amri ya jeshi la polisi wakati mara zote jeshi hilo hilo walipokwenda kuliomba ruhusu limekua likiwapa?
 
Tambwe anatia aibu sana,siku hizi ni mzururaji pale lumumba,ingekuwa enzi za Mwalimu huyu angekamatwa kwa uzembe na uzururaji!! Jmosi ameshinda na kipensi chake pale Lumumba tena kwenye benchi akipiga soga tu! Huyu mdomo ndio unamuweka mjini!!!
 
Ngoja tupunguze wingi wa propaganda. The bottom line is Polisi walivunja sheria katika ishu nzima ya Mwangosi. Kama Chadema walifanya makosa bado sio justification ya polisi kufanya makosa.
 
hivi kwanini chadema hampendi kuambiwa ukweli kama viongozi wenu,juzi sitta kuwaeleza ukweli kwamba mna safu nyembamba ya uongozi mkakasirika na kumwita majina mbalimbali kama mnafiki,anatia aibu,anazeeka vibaya n.k.leo tambwe mwenye uzoefu na upinzani hapa nchini kwa kuwa ndio uliomkuza kisiasa anawapa facts hamna hoja za kumjibu mnatumia wingi wenu tu humu kumtusi na kuleta hoja nyembamba kama ilivyo kwa safu yenu nyembamba ya uongozi iliyomezwa na slaa na mdogo wake mbowe na watu wa kaskazini mwa nchi hii tu(kina zitto hawatakiwi kwa kuwa hawatoki kaskazini)
 
Ngoja tupunguze wingi wa propaganda. The bottom line is Polisi walivunja sheria katika ishu nzima ya Mwangosi. Kama Chadema walifanya makosa bado sio justification ya polisi kufanya makosa.

mbona unakwepa kutumia maneno chadema walivunja sheria kama ulivvyofanya kwa polisi?au ndio ule usemi mkubwa hakombi mboga akikomba tunaondoa ukali wa maneno kwa kusema kaipenda?tuwe wakweli tuache unafiki na ushabiki kupita kiasi
 
NA RICHARD TAMBWE HIZA-PICHANI
WIKI hii waandishi wa habari kutoka katika vyombo mbalimbali nchini waliandamana kulaani kuuawa kwa mwandishi wa habari wa Kituo cha Chanel 10 huko Iringa, kifo cha mwandishi huyu kwa bahati mbaya na kwa mara nyingine tena kimewagawa wananchi katika makundi yanayotofautiana kifikra kuhusu chanzo na hatimaye kufariki kwake.

Wapo wanaoona na kuamini polisi wametumia nguvu kubwa katika kukabiliana na tatizo lililokuwepo, wapo wanaoamini kwamba jeshi la polisi lilikuwa linatimiza wajibu wake na madhara haya makubwa yaliyotokea yanatokana na CHADEMA kuendeleza ghasia katika nchi na kujaribu kuifanya isitawalike kama walivyoahidi baada ya kushindwa vibaya katika uchaguzi mkuu uliopita (walishinda viti 23 kati ya majimbo 239).

Hata hivyo, kabla ya kuingia katika tafakuri pana zaidi zinazotokana na msiba huu sina budi kutoa pole kwa familia ya Mwangosi, waandishi waliokuwa karibu naye katika kufanikisha majukumu yake ya uandishi wa habari, Kituo cha Channel 10 na Watanzania wote kwa ujumla, kwa kuondokewa na mwananchi mwenzetu katika mazingira ambayo wote hatukuyategemea.

Tumeshuhudia wakati taifa likiwa katika simanzi nzito kutokana na msiba huu, wapo wenzetu walioamua kuutumia kama turufu ya kuleta chuki baina ya jeshi la polisi na waandishi na zaidi umma wa Watanzania ambao usalama wao na mali zao unategemea sana uwepo wa jeshi hilo. Kuna mambo mengi ambayo nimekuwa najiuliza na ningependa Watanzania wote tujiulize, hivi ghasia zilizosababisha msiba huu zilisababishwa na nini/nani?

Je kulikuwa na ulazima kwa CHADEMA kukaidi amri ya polisi ya kusubiri sensa ipite? Je, ukaidi wa CHADEMA siyo chanzo cha maafa yaliyotokea na yanayotokea mara kwa mara nchini? Je, ingekuwa sawa kwa jeshi la polisi kuwaachia CHADEMA kufanya shughuli ambayo walikwisha wazuia wasiifanye? Je, polisi ingewaachia kufanya jambo ambalo walikwishawazuia wangekuwa wanatimiza sheria na wajibu wao? Na je, uhalali wa uwepo wa jeshi hilo ungeendelea kuwepo?

Wananchi wote tunapaswa kuheshimu sheria na polisi wana jukumu la kutulazimisha kufuata sheria tunapozikiuka vikiwemo vyama vya siasa, najua sheria ya vyama vya siasa inavipa fursa vyama kufanya maandamano na mikutano baada ya kutoa taarifa polisi, lakini sheria hiyo hiyo inasema vitafanya hivyo endapo tu kama havitapata amri pingamizi kutoka polisi (sheria ya vyama vya siasa 1992 kifungu cha 11).

Tujiulize kulikuwa na ulazima gani kwa CHADEMA ambao mwaka mzima wamekuwa wakiruhusiwa kufanya mikutano na maandamano kulazimisha kufanya mkutano uliosababisha kifo baada ya kupata amri pingamizi? Kama waliona polisi hawakuwafanyia haki je ilikuwa vyema kuandaa mapambano dhidi ya polisi? Jje walichukua hatua yoyote ya kisheria dhidi ya polisi au hawana imani na vyombo vya kisheria kama ambavyo Tundu Lissu anavyoziponda mahakama zetu bila kuheshimu kwamba zilimpa ushindi yeye binafsi katika kesi yake ya uchaguzi aliyofunguliwa na mgombea wa CCM, na zile zilizokipa ushindi chama chake zilizowavua ubunge wana CCM huko Sumbawanga na Igunga.

Naamini ili jeshi la polisi liweze kuendelea kulinda amani ndani ya nchi ni lazima tuliamini na lazima tujue kwamba lipo, likizuia jambo kwa mujibu wa sheria wote tuheshimu vinginevyo litakuwa halina sababu ya kuwepo. Si mara moja au mbili mamlaka za umma na vyombo vya sheria viliamua mambo muhimu katika maendeleo ya taifa, lakini yalipata upinzani hadi pale polisi ilipotumia nguvu kuhakikisha sheria inafuatwa na utekelezaji wake unatimia.

Je, kumfukuza waziri katika hafla ya kulaani mauaji na kumkaribisha mwana-CHADEMA Dk. Lweitama kuhutubia na kuilaani serikali ni sawa? Je, ni sawa kulilaumu jeshi zima la polisi kwa tatizo lililojitokeza sehemu moja ya nchi tena katika kutimiza wajibu wao? Kitendo cha kutowalaani walioanzisha uvunjaji wa sheria uliosababisha ndugu yetu Mwangosi kupoteza maisha katika umri mdogo kinaashiria nini kutoka katika taasisi zetu za habari?

Hapa ndiyo maswali mengine yasiyo na majibu yanapoanza, kwa nini tamko lililotolewa na CHADEMA na lile la wanahabari yanashabihiana. Kwa nini wanahabari hawakuilaumu CHADEMA hata mara moja kwa kutokutii sheria na kuanzisha ghasia zilizosababisha maafa ya ndugu yetu. Nadhani tunahitaji tafakuri pana zaidi. Je wametumwa? Wana hasira? au nao wameanza kushirikishwa katika ajenda za siri dhidi ya serikali na vyombo vyake?

Wote tumesikitishwa na msiba huu sidhani kama ni vyema kuendelea kushambulia jeshi la polisi bali kuangalia nani ameanzisha sokomoko ili awajibishwe kisheria, kama ikibainika aliyeua ni raia wa kawaida sheria ichukue mkondo wake, pia ikibainika muuaji ni askari akiwa katika kutimiza majukumu yake ni vyema taratibu za kijeshi na mahakama zitumike badala ya kuendeleza chuki zisizo na msingi.

Tusijisahau wote tunawahitaji polisi kama ambavyo tulikuwa tunamhitaji ndugu yetu Mwangosi nikiwemo mimi niliyeshirikiana naye katika shughuli mbalimbali. Tusiwe na hasira maana wahenga walisema hasira hasara. Tutafute suluhisho la yanayotokea yasijirudie.

Huyu jamaa ana akili fupi sana,inawezekana ana matatizo ya akili. Ushabiki ni jambo baya sana kwenye ukweli,haiingii akilini suala la kuuwawa kwa mwandishi uhusishe na malumbano ya kisiasa kati ya CDM na CCM.Kama ndivyo na mwandishi amekiri ,kutakuwa na agenda ya siri kati ya jeshi la polisi kushikiana na CCM kuhujumu peace movement za CDM.
 
laana inamtafuna huyo, kunguru mkubwa

jamani mbona hamna anaejibu hoja zake,kila anaekuja anasema ana laana tu tunataka hoja sio mambo mepesi mepesi kama ya slaa kudai sitta hafai kuwa katibu kata bila kujibu hoja zake za msingi
 
Huyu jamaa ana akili fupi sana,inawezekana ana matatizo ya akili. Ushabiki ni jambo baya sana kwenye ukweli,haiingii akilini suala la kuuwawa kwa mwandishi uhusishe na malumbano ya kisiasa kati ya CDM na CCM.Kama ndivyo na mwandishi amekiri ,kutakuwa na agenda ya siri kati ya jeshi la polisi kushikiana na CCM kuhujumu peace movement za CDM.

ok sawa tukubali hiyo,haya tuje upande wa pili kwa nini chadema ilikiuka amri ya jeshi la polisi ambalo walikwenda kuliomba kibali likawakatalia ili kupisha shughuli ya kitaifa?mbona waislam walipogomea shughuli hiyo tuliwazomea humu,kwanini chadema walilazimisha kufanya yale yale ya waislam lakini katika style tofauti???na mbona polisi hiyo hiyo ndio imekua ikiwakubalia kila walipoomba kwanini nao wasionyeshe fair play kwa kuikubalia polisi kwa angalau hiyo mara moja?tena chadema ina bahati kila wakati ikiomba kibali inapewa cuf enzi za mahita nadhani mnakumbuka ilivyokua ngumu mpaka wakawa wanaforce na nganagari yao ndio wanapewa
 
jamani mbona hamna anaejibu hoja zake,kila anaekuja anasema ana laana tu tunataka hoja sio mambo mepesi mepesi kama ya slaa kudai sitta hafai kuwa katibu kata bila kujibu hoja zake za msingi

ujauzito umeshika??
 
jamani mbona hamna anaejibu hoja zake,kila anaekuja anasema ana laana tu tunataka hoja sio mambo mepesi mepesi kama ya slaa kudai sitta hafai kuwa katibu kata bila kujibu hoja zake za msingi

hoja zimejibiwa tayari ila ukiwa ccm lazima uwe kipofu, kama wewe ulivyo huoni
 
ok sawa tukubali hiyo,haya tuje upande wa pili kwa nini chadema ilikiuka amri ya jeshi la polisi ambalo walikwenda kuliomba kibali likawakatalia ili kupisha shughuli ya kitaifa?mbona waislam walipogomea shughuli hiyo tuliwazomea humu,kwanini chadema walilazimisha kufanya yale yale ya waislam lakini katika style tofauti???na mbona polisi hiyo hiyo ndio imekua ikiwakubalia kila walipoomba kwanini nao wasionyeshe fair play kwa kuikubalia polisi kwa angalau hiyo mara moja?tena chadema ina bahati kila wakati ikiomba kibali inapewa cuf enzi za mahita nadhani mnakumbuka ilivyokua ngumu mpaka wakawa wanaforce na nganagari yao ndio wanapewa

hayo maswali ungeanzia kuuliza kwenye mkutano wa sheh.bilali uliofanyika Tanzania visiwani the same date, month and year? Au wao maagizo ya sensa yalikua hayawausu? Au polisi waliambiwa mwisho wao wa kuzuia maandamano siku ya sensa, ni Tanzania bara tu?
Kujisaidia ajisaidie kuku tu, akijisaidia bata kahara!?
PUNGUZENI CAR bon DIO xi DE kwenye bongo zenu.
 
Tambwe mimi huwa namuona Mbumbu kweli hata siwezi kumsikiliza kabaisa na wala siwezi kusoma walaka wake,namjua sana kichwa hakina kitu!
 
Back
Top Bottom