Waraka wa Shigongo kwa Ze Original Komedi

"Ametoa kwenye gazeti na kasema pia wiki ijao atatoa waraka kwa Seki. Kama kweli ana nia nzuri si ange watafuta privately awape ujumbe?"


Lakini ujumbe si umefika? kama wao wanavyotumia TBC1 kuwarushia watu makombora basi kwa style hiyo nao watajibiwa....

Maneno ya Busara Eric..Big up!!!!
 
Ila kiukwelii ni kwamba bila Shigongo kutumia mbinu zake chafu, leo Mashaka asingekuwa wa kubangaiza. Shigongo ndiye aliyehakikisha jamaa anakuwa bankrupt na kumfilisi kabisa.

Ndo maana ktk post yangu ya wali mwanzo wa thread hii nilisema tope limechafua vumbi...
mwenye akili afahamu
 
Sasa kama sekioni ni yatima tatizo ni nini ? Sekioni alikuwa anaishi kimara baruti na hakuwahi kulelewa na reginald mengi kama shigongo anavyotaka tuamini

Ili kumsaidia mtu sio lazima uishi nae; kuna yatima wengi duniani wanasaidiwa na watu wanaoishi Ulaya na Marekani kwa wafadhili wao kuwatumia pesa za karo pamoja na matumizi. Seki alifadhiliwa na Mengi na kwa utamaduni wa kiafrika mtu anayemtukana mfadhili wake hupatwa na laana; nadhani vijana hawa hawayajui haya! Shigongo amewapa darasa zuri sana hasa ule mfano wa kondomu kwani ni ukweli usiopingika kuwa Manji [kama walivyo wahindi wote] atawathamini hawa vijana pale tu watakapokidhi mahitaji yake baada ya hapo atawatupilia mbali. Ukweli ndio huo.
 
Last edited:
Wakasema Eddie Lunyamila wa Yanga eti choka mbaya, akiwashtaki watasemaje, eti alikuwa anamtegemea mkewe na alipokufa naye kwisha kazi, unaweza kumsimangia mtu kweli kifo cha mkewe?

Waraka wa Shigongo unatoa baraka kwa Orijino Komedi kuwakaanga ambao hawajawasaidia ila wasifanye hivyo kwa ambao hawajawasaidia. Ushauri ambao ni very unfair
 
Wekezeni, acheni kiburi cha umaarufu na fedha

Kwenu wadogo zangu.

Masanja, Joti, Mpoki, Wakuvwanga, McRegan, Seki na Vengu.

Nianze kwa kuwakumbusha msemo wa Kiingereza usemao “You can not be a champ for life, one day you will go off and some else will come” sikumbuki vizuri msemo huu kwa mara ya kwanza ulisemwa na nani lakini ni wa zamani hapa duniani na maana yake haichuji kila siku ni mpya, kwamba huwezi kuwa bingwa milele lazima uondoke bingwa mwingine aje!

Najua mlitarajia kwa jambo mlilonifanyia ningeibuka na kisasi, mimi si mtu wa aina hiyo, mwenzenu Dudubaya aliwahi kupewa saa nzima kwenye kipindi cha Nani ni Nani Channel Ten, akanitukana matusi yote aliyoyafahamu lakini sikulipa kisasi, baadaye alipowekwa ndani akikaribia kufungwa ni mimi niliyemtoa mahabusu! Sikufanya hivyo kwa kutafuta sifa bali kutimiza kile kisemacho Wasamehe waliokukosea, leo hii Godfrey Tumaini ni rafiki yangu mkubwa...

Uamuzi niliouchukua si kupigana nanyi, maana ugomvi wa sisi kwa sisi hautasaidia chochote, bali nimeamua kuwapeni ushauri ili mfahamu kwamba kila enzi ina mabingwa wake, leo hii ninyi ni mabingwa lakini mfahamu kwamba wengine watakuja ninyi mtaondoka hivyo badala ya kuwacheka na kuwatukana watu, ni vizuri mkawekeza.

Enzi zile za Hitler aliyeua Wayahudi milioni sita duniani kote hakuna binadamu aliyewahi kuwaza eti siku moja angekuja kutokea mtu aitwaye Osama Bin Laden autingishe ulimwengu kwa mauaji na kusakwa bila mafanikio! Enzi zile za tajiri John D. Rockerfeller hakuna mwanadamu aliyewahi kufikiri atakuja mtu aitwaye Bill Gates au Warren Buffet na kuwa tajiri namba moja.

Enzi zile za Pele hakuna binadamu aliyewahi kufikiri atakuja kutokea mtu aitwaye Christiano Ronaldo au Messi, enzi zile za Mohamed Ali akiwa bingwa wa Ndondi wa dunia hakuna mtu aliyewahi kufikiri atakuja kutokea mtu aitwaye Mike Tyson na katika enzi za King Majuto, Mzee Small au Jangala aliyetuweka kila siku usiku tumezunguka redio kusikiliza michezo ya kuigiza, hakuna Mtanzania aliyewahi kufikiri kwamba ipo siku mngekuja kutokea ninyi. Kweli kila enzi na watu wake.

Mmekuja na mtapita kama walivyopita wengine wengi waliotangulia kabla yenu, ambao leo hii ukiwatafuta utashangazwa na maisha wanayoishi ingawa waliwahi kutingisha Taifa letu na wengine Dunia, baadhi wanateseka wakisubiri kusaidiwa! Kwenu hivi sasa jua linawaka lakini giza linakuja.

Mifano niliyoitoa ya watu niliowaongelea hapo juu inaonesha kwamba hakuna binadamu anayeweza kubaki bingwa siku zote, lazima aondoke ili kutoa nafasi kwa mabingwa wengine, tutake tusitake ni lazima tuondoke hivyo ni lazima kufanya mambo sahihi wakati huu tukiwa katika ubingwa wetu. Huu ndiyo ujumbe wangu kwenu leo.

Swali linalowasumbua watu wengi duniani na ambalo kila mtu mwenye akili timamu ni lazima ajiulize ni hivi siku nitakayotupwa nje nitafanya nini? Itakuwaje siku nitakayokuwa siwezi kucheza soka? Nitafanya kitu gani siku nitakayokuwa siwezi kuchekesha luningani na watu kunishangilia kila ninakopita? Kama binadamu mwenye akili timamu ambaye umaarufu haukupagawishi ni vizuri kujiuliza maswali haya kwani kila mmoja wetu siku moja atajikuta yupo nje ya mchezo.

Wadogo zangu,
Ilikuwa niwaandikie Waraka huu tangu wiki mbili zilizopita baada ya kunitoa kwenye kipindi chenu cha Orijino Comedi na rafiki yangu mpendwa aliyewahi kuwa mshindani wangu wa Biashara huko nyuma Mashaka Matongo au Abiola! Ingawa hamkututaja majina yetu lakini kila mtu aliyekiona kipindi hicho alielewa mliwalenga nani na nani na nina uhakika aliyetoa wazo hilo ni Sekioni David kwa sababu yeye ndiye aliwahi kuwa rafiki wa karibu sana na Mashaka Matongo enzi hizo wakiigiza pamoja katika kikundi cha MAMBO HAYO, pia akiwa mfadhili wake mkubwa.

Kwa wale ambao hawakubahatika kukiona kipindi hicho nitawasimulia kidogo; kilichotangazwa na vijana hao maarufu hivi sasa nchini Tanzania wakitembelea magari ya kifahari na kufanya kila aina ya starehe wanayoona inafaa ni kumwonyesha Bw. Mashaka Matongo ambaye huko nyuma aliwahi kumiliki magazeti kadhaa Pendwa akiwa amefilisika vibaya! Kazi yake hivi sasa eti ni kunyoa nywele huko Sinza na kuomba misaada kwa watu! Wakanionesha mimi kama mtu aliyefanikiwa ‘sana’ kuliko Mashaka Matongo katika kazi hiyo na kumcheka wakimfanya mjinga.

Inawezekana kwa kunionesha mimi niko juu na mwenzangu akiwa amefilisika mlifikiri ningefurahishwa na kitendo hicho, naomba niwaeleze wazi kwamba mimi si mtu wa aina hiyo, wanaonifahamu wanaelewa na kitendo hicho hakikunifurahisha hata kidogo, sipendi umaarufu wa bei nafuu (Cheap popularity) napenda ninapopewa sifa iwe ni halali na ya kutolea jasho. Mpaka leo ninapowaandikia makala hii binafsi sielewi mwenzangu alijisikiaje baada ya dhihaka hiyo kurushwa na TBC 1 ambayo Mkurugenzi wake ni mtu ninayemheshimu sana katika fani hii, Tido Mhando.

Kilichonituma niandike makala hii ni kuwakumbusha wadogo zangu wa Orijino Komedi kwamba, maisha ni safari ndefu. Kwa kuonekana kwenye luninga kila Alhamisi na Jumapili, kupita huku na kule wakishangiliwa, wasijione wamefika kwenye kilele cha mafanikio na kuanza kucheka wenzao, ninachofahamu mimi na uelewa wangu mdogo juu ya mafanikio ni kwamba safari kwao ndiyo kwanza imeanza.

Safari ya maisha ni ndefu wadogo zangu, hakuna sababu ya mtu kumcheka mwenzake. Mzee mmoja aliwahi kuniambia ni kama safari ya kwenda umbali wa kilometa elfu moja kwa miguu, kila mtu ataondoka kwa staili yake. Mwingine atakimbia mwingine atatembea au kutambaa zote hizo ni safari lakini hakuna mwenye uhakika kwamba atafika mwisho wa safari yake salama kiasi cha kuwacheka wenzake, hiki ndicho ninachotaka kuwaeleza wadogo zangu wa Orijino Komedi.

Ninachojua mimi hakuna anayeweza kukimbia umbali wa kilometa elfu moja bila kupumzika, lazima mahali fulani mbele ya safari atachoka na kuketi chini ya mti ili kuwapisha wengine wapite na pengine huo ndiyo ukawa mwisho wa safari yake huku uliowaacha nyuma wakitembea taratibu wakipita na kukuambia “Mzee tunatangulia” huu ni ukweli.

Inavyoonekana kwa hivi sasa wadogo zangu wa Orijino Komedi mmeanza safari yenu kwa kukimbia kiasi cha kujiona ni wajanja kuliko wanaotembea hata kufikia hatua ya kuwacheka kama mlivyofanya kwa Mashaka Matongo ambaye huko nyuma alimlisha na kumtunza Sekioni! Mmesahau kwamba mbele ya safari ni lazima mahali fulani mtapumzika na waliokuwa wakitambaa na kutembea wakaja na kuwapita mkiwa chini ya mti, nimekwishawaeleza hapo juu kwamba binadamu huwezi kuwa bingwa milele lazima siku moja utoke na wengine waingie, kumbukeni walikuwepo mzee Majuto na Small kabla ninyi hamjaja.

Kibaya zaidi na kinachositikisha ni kwamba mmeanza hata kuwatukana watu waliowasaidia kufika mlipo leo! Hiki ni kitendo cha ukosefu wa shukrani cha kiwango cha juu kabisa ambacho nimewahi kukiona chini ya jua. Kila Mtanzania anafahamu mlipotokea, namna ambavyo mtu kama Reginald Mengi na vyombo vyake vya habari amesaidia kuwafikisha ninyi kwenye mwanga, ambaye hakika hamuwezi kusimama mahali popote duniani kutoa historia yenu mkaacha kutaja jina lake, lakini huyu ndiye amekuwa mtu wa kutukanwa kila siku katika vipindi mnavyofanya! Hili ni jambo la kusikitisha sana.

Najua mnatiwa kiburi na utajiri wa fedha na umaarufu ambao hivi sasa mnao! Mmethibitisha ile kauli kwamba hakuna kitu kigumu duniani kwa mwanadamu kuwa na fedha au mafanikio halafu akabaki yule yule! Fedha na umaarufu ni shetani, huwabadilisha watu na kuwapa tabia ambazo huko nyuma hazikuwahi kuonekana, sitaki kuwahukumu wadogo zangu lakini jambo hili limethibitika kwa matendo mnayoyafanya hivi sasa.

Najua mnatumiwa na watu kutimiza malengo yao, mambo mnayoyafanya si yenu yote, baadhi ni ya kuwafurahisha watu wanaowaweka mjini! Lakini kumbukeni mfano wa Mzee Kijiti aliyesafiri kwenda miji ya mbali akimwacha mke wake nyumbani, akiwa huko ashki ya tendo la ndoa ilimshika na kujikuta akitafuta mwanamke wa kuondoa haja yake.

Akifahamu kuna gonjwa la Ukimwi mzee huyo alilazimika kutafuta mpira wa kujikinga na gonjwa hilo. Kwa mahali alipokuwa ilikuwa kazi kidogo kupata mpira huo, akazunguka huku na kule kwenye vibanda bila mafanikio, mwili wake ukiwaka tamaa ya ngono. Mwisho mhudumu wa nyumba ya wageni aliyofikia alimpa mpira mmoja, akafurahi na kuingia chumbani ambako alifanya shughuli yake mpaka kufikia tamati akauvua mpira na kuutupa sakafuni tena akasikia kinyaa na kujilaumu kwa kitendo alichokifanya kusaliti ndoa yake.
“Ichukue” Akamwambia mwanamke aliyekuwa naye.

“Ichukue wewe” Mwanamke akakataa.
Baadaye wote wawili waliondoka na kuuacha mpira huo sakafuni, sasa wakiwa na akili timamu kondomu haikuwa na umuhimu tena, ilishawasaidia kuwaepusha na Ukimwi basi ilikuwa inatosha, kazi yake ilishakwisha.
Wadogo zangu,

Kwa mfano huu wa Mzee Kijiti naamini mtakuwa mmenielewa vizuri, jiepusheni sana na kutumiwa na watu wenye malengo yao ambao mwisho wa siku yakitimia watawatupa kule kama Kondomu na hawatawajali tena. Mkilijua hili mtafanya mambo mawili, la kwanza ni kuwekeza na la pili ni kujiepusha na matusi kwa watu waliowasaidia kufika mlipo kwani kesho ni lazima mtarudi kwao kuwashika mikono, hivyo ndivyo Mungu anavyofanya kazi.

Jiepusheni na starehe na kulewa umaarufu, jua haliwaki siku zote, kuna mchana na usiku. Muda huu mkiwa juu, ni vizuri kujiuliza giza litakapoingia na mwanga kupotea, au siku tutakapotupwa tutaishi vipi? Anasa hazina mwisho, zipo tu, mlizikuta, mtaziacha na wengine watazikuta na kuziacha hivyo ni vizuri kuwa makini katika kipindi hicho ambacho neema bado ipo, maana mchekaji huwa mchekwaji kesho na mchekeshaji huwa mchekeshwaji kesho kutwa.

Mmekwishanitukana mimi mara nyingi lakini mimi sijali, nimekwishazoea, katika miaka kumi na moja niliyofanya kazi hii ngumu ninao maadui wanaoweza kufanya chochote ili wanichafue, kinachoniuma sana ni kitendo mnachokifanya kwa mzee Mengi ambaye bila yeye TBC1 wasingewaona, kwa umri wake mzee huyu ni sawa na mzazi wenu na mnachokifanya ni utovu wa nidhamu wa hali ya juu sababu tu mmelipwa!

Inawezekana mkawa hamfahamu kwamba umaarufu wenu unapotezwa na kitendo hiki, Watanzania hawapendi watu wenye maringo na kujisifu tabia ambayo hivi sasa imewagubika ninyi mkiwa mwanzo tu mwa safari ya maisha! Mnakumbuka kilichowapata uwanja wa Taifa siku ile mlipopigwa kwa chupa na makopo ya soda? Hilo linapaswa liwe fundisho ili mjiangalie upya, mimi naamini mnaweza kurejesha hali mliyokuwa nayo zamani kwa kujiepusha na matusi kwa watu waliowasaidia.

Mkiendelea na tabia hii si tu mtachukiwa bali mtailetea TBC1 matatizo makubwa sana ya kulipa watu mabilioni ya fedha jambo ambalo najua kabisa TBC1 hawatakuwa tayari kulifanya, hivyo kuamua kujiepusha nanyi! Hata kama TBC1 ni chombo cha serikali, inaelewa kabisa kuna mahakama na hakuna aliye juu ya sheria, kitendo cha wao kuwaruhusu ninyi kuendelea kutukana watu kwa maneno ya uongo, kitakuja kuwaingiza kwenye matatizo makubwa ambayo hatimaye yatavunja ndoa yenu.

Najua maneno yangu yatawaumiza lakini naomba msikasirike kwani tiba ya ugonjwa siku zote inauma lakini mwisho wa siku inaponyesha! Naomba mnivumilie na myafanyie kazi yale mtakayoona yanafaa, binadamu hatujatimia, tunayo mapungufu mengi na kila siku tunafanya kazi kurekebisha sehemu mbalimbali maishani mwetu, nanyi nawasihi mchukue hatua hiyo. Mtu hahitaji kuwa na elimu kubwa sana kuelewa kitakachowapata kama mkiendelea na mtiririko huu mnaokwenda nao.

Sisi sote ni Watanzania tuacheni kuchekana bali tuwatie moyo waliovunjika na tuwasaidie kusimama walioanguka! Matendo hayo ndiyo yatakuwa akiba yetu mara giza litakapoingia hawa mnaowacheka na kuwatukana leo si ajabu ndiyo watakaowasaidia ikitokea siku moja kigogo anayewafadhili sasa akawa hafanyi kazi na ninyi tena jambo ambalo si ajabu kutokea.

Naomba niseme neno moja natumaini sitamuudhi mtu. Watanzania tuna tatizo ambalo ni lazima tulishughulikie kama kweli tunataka kupata mafanikio ya kweli maishani mwetu, tuna tabia ya kuridhika mapema hata kwa mafanikio kidogo. Hapo mlipo wadogo zangu wa Orijino Komedi tayari mmesharidhika, lakini kumbukeni kufika Uingereza au kuendesha ‘Haria’ peke yake haitoshi, kuna mambo mengi sana ya kufanya, kama kufika nje na kuendesha gari ingekuwa kila kitu basi watu wangekwisha acha kufanya kazi.

Hili ni kosa kubwa sana ambalo sisi Watanzania tunalifanya, mafanikio kidogo tu yanatulewesha na kuanza kutukana watu bila kujua kwamba kuna kesho, hata Orijino Komedi mtakubaliana nami katika hili! Wadogo zangu mmelewa sifa mapema, kila mahali mnapoingia mnataka huduma ya VIP? Kumbukeni wanaojikweza hushuswa bali wanaojishusha hukwezwa! Chapeni kazi wadogo zangu, bado hamjafika popote, mafanikio ni safari ndefu mnahitaji sana watu kuliko mnavyohitaji fedha.

Nimeongea mengi sana wadogo zangu, lakini huu ndiyo Waraka wangu kwenu sisi ni ndugu lazima tuelekezane kwa maneno ya ukweli na si visasi, ni vizuri mkakumbuka mlikotoka badala ya kujisikia mmefika mwisho na kuanza kuwatukana watu waliowasaidia kufika juu! Ni vizuri kuelewa hamtakuwa mabingwa siku zote, pengine mtakapokuwa mnaporomoka hawa mnaowatukana leo watakuwa bado wako juu na mtahitaji msaada wao.

Naomba niishie hapo.

Jipu limepasuka siwezi kuwa adui kwa kusema kile ninachoamini ni ukweli. POLE SANA MASHAKA MATONGO, MANENO YA ORIJINO KOMEDI YASIKUVUNJE MOYO, PAMBANA TU HATIMAYE UTAFIKA JUU, YOTE YAWEZEKANA, IF THEY CAN, YOU CAN!

Wiki ijayo nitamwongelea Sekioni David, yatima aliyesaidiwa na Reginald Mengi ambaye hivi sasa kila kukicha anamtukana mzee huyo sababu leo hii anafadhiliwa na Yusuph Manji.

nakubaliana na waraka huu kabisa, ni watu wachache sana wataelewa umuhimu wa waraka huu, na si kwa ze commedy wenyewe bali hata kwa maisha yetu ya kila siku, tunachanganyikiwa na mafanikio kidogo sana tunayopata tukumbuke ....if u dont raise your eyes eneough and see far you will think you are in the highest peak.....
 
Nafikikiri Shigongo ametoa ushauri mzuri tu kwa hao madogo, kwa sababu sio vizuri hata kidogo kufanyie mizaha kwenye TV hali za maisha za watu. This is a very sensitive issue which leaves other people embarrased and feeling down. Mtu kama mambo yake hayamwendei vizuri sio wa kumdhihaki hata kido, because that is just a destiny and anyone can be in that position. I think this guys need to find some other issues to make fun on rather than making a joke a other people's situations.

The other thing is, a good advice is a good advice and it does'nt matter where its coming from. The fact of the matter is that Shigongo has given these guys a very good advice, and whether Shigongo is not clean or not cannot trivialise the advice. Kama some of you wana JF mnataka kusuggest that mtu asitoe advive mpaka nae awe msafi, nani anaweza akaprove kweli kama yeye ni msafi sana. Kila mtu ana mapungufu yake, and thats why we are human beings, but that does not stop us from giving advice from our relatives, friends etc.

We need to create the habit of taking the advice as it is and trying to digest and see if its good advice rather than weighing it based on where it is coming from.
 
nakubaliana na waraka huu kabisa, ni watu wachache sana wataelewa umuhimu wa waraka huu, na si kwa ze commedy wenyewe bali hata kwa maisha yetu ya kila siku, tunachanganyikiwa na mafanikio kidogo sana tunayopata tukumbuke ....if u dont raise your eyes eneough and see far you will think you are in the highest peak.....

True Nguli ni sisi tu wachache! Finally I can see.
 
alichokifanya Shigongo ni hoja dhaifu, anaanza kumjadili mtu na si hoja.

Tukianza kumjadili na yeye humu kweli atabaki?mbona tunamwangalia namna alivyoandika makala zake za Napasua jipu pwaaa juu ya amina chifupa tena katika critical situation tukauchuna? anatafuta issue ya kuuzia gazeti i think..na ni mtu wa maslahi zaidi ya kitu anachokiamini.

Tuache kila mtu afane kazi yake, nakubali kukosoa uendeshaji wa kazi upo katika kuboresha lakini si kama shigongo alivyofanya.
 
alichokifanya Shigongo ni hoja dhaifu, anaanza kumjadili mtu na si hoja.

Tukianza kumjadili na yeye humu kweli atabaki?mbona tunamwangalia namna alivyoandika makala zake za Napasua jipu pwaaa juu ya amina chifupa tena katika critical situation tukauchuna? anatafuta issue ya kuuzia gazeti i think..na ni mtu wa maslahi zaidi ya kitu anachokiamini.

Tuache kila mtu afane kazi yake, nakubali kukosoa uendeshaji wa kazi upo katika kuboresha lakini si kama shigongo alivyofanya.

Umesema ukweli mkuu. Tatizo huku kuna watu wana bisha bila kuangalia pande zote. Nadhani wengine ili mradi tu wawe wamebisha ndiyo wana ridhika.
 
Sijui kama nipo sahihi, but nilichomsoma mwandishi wa waraka ni kuwa "Abiola ndo kamlea Seki" Mengi kawapa kuonekana kama wachekeshaji wazuri via matukio.

Ila pia kama kuzidisha wanazidisha basi wanaweza kupunguza, ila kama hawazidishi sidhani kama hiyo nayo kuwa ni P.

Pia sisi ndani jamvini si tunatakiwa kuchukua mazuri kadri ya lengo????? N akama maneno yana uzuri basi tuyapimie hapo hata kam aliyesema kawa naye ni walewale.
 
Nakubaliana na shigongo katika mtizamo mmoja tu....ushauri wake ni muhimu kwa macelebrity wa bongo. Hiyo ya orijin komedi mmh wanajuana wenyewe...waswahili husema nyani haoni kundule. Nani asiyejua shigongo ni bingwa wa kuwachafua watu tena hasa wakina dada wanaomnyima uroda...mi ningemshauri abadilishe kichwa cha habari na aseme....Waraka maalum kwa vijana wenye umaarufu Tanzania.

Kama kufulia ndio kafulia watu wengine wakumbushwe the hard way. Hiyo inakubalika kabisa bwana, hata wenyewe komedi wanajua watakuja kusemwa na yeye huyo huyo wakifulia. Aende zake kule, mbona kadhamini the utamu watu hatumgusa au amesahau alimia 60 ya habari zake alikuwa akizotoa the utamu, si yeye aliyeitangaza ile blog kwa nguvu ili asiishiwe na story. Nashangaa kwanini hajaguswa na watu wa usalama. Hii nchi bwana.
 
Alichosema Shigongo ni sahihi kabisa, ametoa ushauri kwa hawa vijana ambao ni mzuri sasa haya mengine yanayomhusu yeye sio issue yaje kwa wakati wake, kama naye ana matatizo ina maana haruhusiwi kumshauri mtu? Tuwe wakweli jamani sio sahihi hata kidogo kumcheka mtu aliyeanguka kimaisha kwani hakuna apendaye; jana tena nimeone wakimcheka Saida Karoli kwamba amekuwa muuza chipsi, jamani wasaidieni hawa vijana kwa ushauri.
 
I find a lot of hyprocracy in this 'waraka'......his udaku newspapers are full of gossip and dirty pictures....then who is clean btn Eric and the orog..co...ur udaki newspapers are spoiling so many Tanzanians..
Shigongo please try to practice what u preach!!!
 
Mwe!!
huyu nae kafulia kweli.
Sasa kama walimsema Mashaka yeye imeuma nini?
"Iso kuwasha hujailamba"-Mjomba Mpoto.
 
Fasihi ilivyo ina tafsiri nyingi na mara nyingi tafsiri yoyote inaweza kukubalika kulingana na inavyojengewa hoja. kwa upande wa mwandika waraka naona ile sehemu ya aliyee....... imemboa sana na kwa mtazamo wake anaona jamaa kama vile wanajiona wao sasa ndo wako matawi ya juu na kwasababu hiyo wanawapuuza waliojichokea (waliofulia)- (Vema kabisa ndo mawazo yake hayo). Lakini angeweza kufikiria kwamba jamaa wanataka kila mtu akaze buti mahali alipo ili asije fulia. Kimsingi kila mtu hapendi kuporomoka kimafanikio lakini wakati fulani baadhi ya watu wanalewa mafanikio na kujisahau kuweka misingi imara ya kuendelea kuwa katika hali hiyo ya mafanikio na mwisho wake ni kufulia.
 
Huyo Mengi kama katukanwa si aende mahakamani?

Seki $ ITV na EATV walikuwa wanategemeana, sio kweli kwamba Seki alikuwa anamtegemea Mengi bali ktk vipindi vyake na Mengi alikuwa anaweka matangazo yake anapata pesa.
 
Huyu asitupoteze muda mjinga wa kwimba hana mpya angelijuwa ni kiasi gani mamia kwa mamia ya watanzania wamejipiga vitanzi na kuimia vibaya nafsi zao kwa ajili ya magazeti yake ya udaku wala asingefikia hatua ya kutaka kujikosha kwa mashaka huyu ni mjinga na mpenda sifa kuliko anavyojaribu ku-pretend kasha jaribu kushindana na clouds na primie time akajiona hana uwezo yote ilikuwa ni kutafuta umaarufu na sifa za kijinga leo anasema hatafuti umaarufu isipokuwa uanatafuta nini? mdanganye rafiki yako tippoh athumani si wajanja wa mjini uliowakuta hapa mjini
Sasa huyo Dudu baya unaweza kumuelezea nani akakuelewa status yake hata mwendawazimu anamjuwa kuwa ni mwendawazimu ndio maana anaimba kisukuma mpaka leo zaidi ya hapo jina lake DUDU BAYA
 

Similar Discussions

0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom