Waraka wa Prof. Mark Mwandosya, kuhusu Demokrasia

Ngambo Ngali

JF-Expert Member
Apr 17, 2009
3,517
1,359
Prof Mark Mwandosya, waziri wa Maji na Umwagiliaji, Mbunge wa Rungwe Mashariki na Mjumbe wa Halmashauri kuu ya Taifa CCM, amefunguka na kutoa waraka murua na wa ukweli kuhusu demokrasia. kitabu hicho kinaitwa Sauti ya Umma ni sauti ya Demokrasia.

Katika waraka huo Professa anatuelezea kuhusu mchakato wa uchaguzi wa CCM mkoa wa Mbeya 2007.

Katika kitabu hicho anatufundisha:

1. Makundi yaliyojitokeza katika uchaguzi wa CCM Mbeya 2007 yalitokana na utupu wa kiitikadi,uliozaa makundi ambayo hayana msingi.

2. Kuna hatari kubwa ya wafanyabiashara kubadili umiliki wa chama, kutoka chama cha wakulima na wafanyakazi, kuwa chama cha wakulima, wafanyakazi na wafanyabiashara,wafanyabiashara ambao sasa inajitokeza kuwa watataka au watafanikiwa kukiongoza chama kutokana na uwezo mdogo wa wa vyama vya siasa.

3. chama kirudi katika misingi ya uongozi bora inayokataza matumizi ya fedha katika kuwashawishi wajumbe wa kikao cha uchaguzi kumchagua mgombea au anayewania kugombea nafasi katika chama.... Matumizi ya fedha kwa namna hiyo ni ishara tosha kwamba mgombea hafai kuwa Kiongozi.

4. Kitendo cha wasimamizi wa uchaguzi ( wa chama) kusahau, kuacha au kupuuza jukumu la usimamizi wa uchaguzi ni kielelzo cha kutokuwepo au uhafifu wa mafunzo ya uongozi na utawala kwa viongozi wetu.

Publisher: not disclosed
ISBN: not disclosed
 
Mbona unajichanganya kitabu au waraka :nono::nono::nono::nono:
 
Huu ni mwaka 2012! Tunataka tathmini ya sasa na siyo historia. Mabadiliko ya kisiasa yanakwenda kwa kasi ya ajabu hivyo ni budi kwenda na wakati.
 
Mwandishi anasema ukurasa wa Sita nimeona niandike uzoefu nilioupata ili nimwachie kumbukumbu msomamaji na mwanachama wa CCM au yoyote Yule ambaye angependa kufuatilia siasa za vyama, kwa sababu zifiatazo:

1. Chama kikisimamia vizuri Katiba na taratibu zake, wanachama wakiishi katika misingi na wakiongozwa na Imani ya chama chao basi hata serikali inayoongozwa na chama hicho huwa imara na makini.

2. Chama kisipoheshimu Katiba yake na miongozi yake, basi si rahisi kusimamia vilivyo serikali ambayo Kimepewa Imani na wananchi kuiongoza.
 
Matumizi ya pesa za ndani ya chaguzi Hasa chama Tawala ni Historia? serikali legelege ni historia? Utupu wa kiitikadi ndani ya chama chetu cha CCM ni histori? Tumia vizuri Ubongo wako acha uvivu wa kufikiri!
 
2. Kuna hatari kubwa ya wafanyabiashara kubadili umiliki wa chama,

Kama kimetoka 2007 na bado Prof. alikuwa anadhani "kuna hatari.." napata mashaka fulani alimaanisha nini? au aliogopa kusema tayari wameshakuwa wamiliki?...manake tayari muda huo kwa weledi wake alikuwa ashaona umiliki ulivyokwisha hamia upande mwingine..
 
Amekosea kusema hivyo au amechelewa?

Hajaogopa kusema alisema na anarudia tena kwa faida ya wananchi.

Soma kwanza kitabu.
 
Je ukweli ndo wanaujua leo au ndo kusema wameishiwa kwanini hakusema mashamba ya ndugu zake yalipokuwa yakiuzwa Mbarali, kwanini ilipokuwa inauzwa Kiwira hakusema?, kwanini leo baada ya kupewa kinachoitwa sumu ndo anakumbuka wanyonge na alale, atamka na hatakuta mtu hata aking'aka mchana wananchi wanaendelea kuamka siku hadi siku yeye na alale tu.
 
Akojoe akalale!
Je ukweli ndo wanaujua leo au ndo kusema wameishiwa kwanini hakusema mashamba ya ndugu zake yalipokuwa yakiuzwa Mbarali, kwanini ilipokuwa inauzwa Kiwira hakusema?, kwanini leo baada ya kupewa kinachoitwa sumu ndo anakumbuka wanyonge na alale, atamka na hatakuta mtu hata aking'aka mchana wananchi wanaendelea kuamka siku hadi siku yeye na alale tu.
 
Mwandishi anasema ukurasa wa Sita nimeona niandike uzoefu nilioupata ili nimwachie kumbukumbu msomamaji na mwanachama wa CCM au yoyote Yule ambaye angependa kufuatilia siasa za vyama, kwa sababu zifiatazo:

1. Chama kikisimamia vizuri Katiba na taratibu zake, wanachama wakiishi katika misingi na wakiongozwa na Imani ya chama chao basi hata serikali inayoongozwa na chama hicho huwa imara na makini.

2. Chama kisipoheshimu Katiba yake na miongozi yake, basi si rahisi kusimamia vilivyo serikali ambayo Kimepewa Imani na wananchi kuiongoza.

Mkuu hii kitu kwa CCM itabaki kuwa ndoto, kwa mfano utamshawishi vipi Lowasa, Rostam, Mulla (mwenyekit Mbeya), Chenge au wengine wa aina hiyo kutotumia fedha kama silaha yao wanapotafuta nyadhifa katika Chama? Je yeye hajahonga kufika hapo alipo??
 
Je ukweli ndo wanaujua leo au ndo kusema wameishiwa kwanini hakusema mashamba ya ndugu zake yalipokuwa yakiuzwa Mbarali, kwanini ilipokuwa inauzwa Kiwira hakusema?, kwanini leo baada ya kupewa kinachoitwa sumu ndo anakumbuka wanyonge na alale, atamka na hatakuta mtu hata aking'aka mchana wananchi wanaendelea kuamka siku hadi siku yeye na alale tu.
Mtu Kama Huyu AKIUKALIA mwiba hataelewa kitu mpaka aambiwe na nesi wakati pingili inanig'inia!
 
Mkuu hii kitu kwa CCM itabaki kuwa ndoto, kwa mfano utamshawishi vipi Lowasa, Rostam, Mulla (mwenyekit Mbeya), Chenge au wengine wa aina hiyo kutotumia fedha kama silaha yao wanapotafuta nyadhifa katika Chama? Je yeye hajahonga kufika hapo alipo??

Kazwile, issue hapa Ndio hiyo viongozi wengi wa CCM Wana ushawishi wa hela kuliko uwezo wao wa kuongoza amegusia kwenye kitabu chake anasema

" binafsi, naamini kwamba matumizi ya fedha kwa namna hiyo ni ishara tosha kwamba mgombea hafai kabisa kuwa Kiongozi. Kwani anaficha udhaifu wa kutokuwa na uwezo kwa kuwanunua wajumbe wa kikao huduma"
 
duh, bora kupata kopi yake.

Uchambuzi wake unaanzia 2007? How?
Nilidhani ungeanzia machakato wa kumpata aliyepo madarakani way back to 2000 na kuendelea.
 
Nafikiri dhana ya kuwanona wafanyabiashara kama maadui wa demokrasia inamapungufu makubwa. Nchi nyingi zilizoendelea ikiwepo Marekani wamewategemea sana wafanyabiashara ili kukuza uchumi wao na wengi wao wameombwa kufanya kazi serikalini ili kuboresha utendaji kazi wa serikali. Dhana ya wakulima na wafanyakazi ilianzishwa na nyerere kwa sababu alipenda kelemea upande wa kikomunisti na hivyo hakuwapenda wafanyabiashara. Kama vile ambavyo kuna wafanyabiashara wasiokuwa na utu na maadili mazuri, pia wapo wafanyakazi na wakulima wenye hulka hizo hizo. Kwa sababu tuu mtu ni mfanyakazi au mkulima haimuondoloi hulka ya wizi, ufisadi au ubinafsi. Hivyo wafanyabiashara wasionekani ni maadui wa maendeleo au uongozi bora. Kama tuna miiko ya uongozi tunayoiheshimu na kusimamia kwa dhati hatupaswi kuwa waoga au kubagua mtu eti kwa sababu yeye ni mfanyabiashara na siyo mkulima au mfanyakazi. Kwani hao wafanyakazi walioko serikali utendaji kazi wao uko vipi, ni kweli kwamba wao ndiyo waliotukuka? Kama ndivyo mbona nyumba za serikali na magari pamoja na samani nyingine wameendelea kujiuzia wao kwa bei ya kutupa? Wao wanalipa kodi zaidi ya watanzanaia wengine? Let's be more careful in our analysis na tusifuate tu falsafa kwa bila kujiuliza chanzo chake ni nini!!! There are a lot of very good honest businessmen and women out there and we ought to give them a chance just like we should give to all workers and farmers... hizi falsafa za ki-maxist za "workers unite you have nothing to loose except your chains," siyo za kweli siku zote!!
 
Back
Top Bottom