Waraka wa Pascal Mayalla - Asanteni Sana!

pole sana kaka hiyo yote mipango ya mungu,iliyobaki kumshukuru yeye kwa yote na kutoa sadaka imeniuma sana kwani nami babayangu alikufa kwenye ajali ya pikipiki on the spot.na nimesikia ni ajali yako ya pili ushauri wangu sasa kaa nayo mbali kabsa maana ya tatu haikopeshi na ndivyo ilivyotokea kwa baba yangu mpendwa miaka 21 iliyopita MUNGU AMREHEMU na akusaidie kujipanga upya ndo maisha kaka.
 
Bila shaka wewe ndiye mgeni hapa jamvini maana inaonesha umejiunga jan - feb 2009 na Pasco amekuwa hapa kitambo.
Sawa mkuu, lakini kama Pasco unayemzumgumzia hapa ndiye huyu Pascal Mayalla, basi alikuwa hapa kitambo, mimi namzumgumzia huyu aliyejiunga hapa Sun, Aug 2009!
 
Pole sana kaka,warwa wak umenigusa sana,atuendelee kumuomba Mwenyezi Mungu akurehemu upate nafuu mapema,pole sana ndugu yangu
 
pascal pole saaana kwa ajali iliyokupata. Swali la kujiuliza hapo nije kwa nini wewe mungu akupendelee kuishi tena? Jibu litakuwa gumu ila cha msingi endelea kumshukuru na kumuabudu kuliko ilivyokuwa mwanzo sababu ana makusudi mema na wewe.

bwana apewe sifa!
 
Pole sana Pascal na kweli hili la kutembelea wagonjwa kuna kiongozi mmoja wa dini aliniambia kwamba week end kuliko kuwapleka watoto sinema,wet 'n' wild mara sijui mlimani city ni bora ukawazoesha watoto kubeba zawadi ndogo ndogo mkawatembelea wagonjwa hospitali.Makes a lot of sense hasa ukisoma maneno ya mpiganaji Pascal 'mzee wa kipindi cha kitimoto' enzi hizo wakati waandishi bado wakiogopa kuikosoa serikali.Kwa kweli kina Pascal ndo pioneers wa talk show nchi hii hata kama ilikuwa inakuwa recorded.Kaka nakuombea uwe buheri wa afya,inshallah.
 
.....mpiganaji Pascal 'mzee wa kipindi cha kitimoto' enzi hizo wakati waandishi bado wakiogopa kuikosoa serikali.Kwa kweli kina Pascal ndo pioneers wa talk show nchi hii hata kama ilikuwa inakuwa recorded.Kaka nakuombea uwe buheri wa afya,inshallah.

Daah mkuu Bishanga umenikumbusha mbali....enzi zile za KITIMOTO huyu jamaa alikuwa mdadisi sana, he was very daring kuchallenge politicians enzi zile!

Nilitaka nimuulize ile project kwani iliishia wapi ati...was very good!
 
Pole sana Mwamini Mungu kama ulivommwamini alivokuinua kutoka kilindini...atakufikisha mahali usipoapatarajia...yeye ni mweza wa vyote, alfa na omega. hakuna linalomshinda.

Nakutakia nafuu zaidi na mafanikio katika kazi mpya!
 
Bw. Mayalla pole sana kwa yale yaliyokukuta, lakini Mungu ni mkuu wa yote kwani ni jambo la kumsifia kuwa hadi sasa kakuweka hai. Najua ilikuwa big challenge kwako pamoja na familia yako lakini kwa Mungu yote yawezekana na umeweza kurudi hapo ulipo.

Vilevile nilikuwa napenda kuchukuwa nafasi hii kukukaribisha hapa jamvini maana naamini ni Pascal Mayalla halisi ndiye aliyejiunga na hili jamvi.
Hapa JF tunatofautiana kiitikadi na mitazamo lakini linapokuja suala la matatizo JF members do great. Kwa misingi hiyo JF kwa njia moja au nyingine itakuwa inafuatilia kwa nia nzuri maendeleo yako kama JF member ukiwa unaendelea na matibabu yako.
POLE na KARIBU......
 
Pascal pole sana kaka. Wengine tunaisikia hii tragedy yako kwa mara ya kwanza na kweli tunaona uwepo na uwezo wa Mungu. Mungu anakazi na wewe na anataka uifanye kabla hajakuita. Nadhani mojawapo ni hii ya kutufundisha kuwaona na kuwatembelea wagonjwa. Tumejifunza sana toka kwenye maandishi yako. Mungu aendelee kukupa neema yake na kukubariki na kukuponyesha. Mungu wetu ni Mwaminifu na anatupenda.
 
Kwenye maandishi ya rangi nyekundu:pascal umeni sikitisha sana kwa kitendo chako cha kurudi eneo la tukio,umeenda kufanya nini hapo? ujui kuwa unatengeneza Agano na imani ya vitu usivyo vijua? wewe ni mkristo nadhani RC! ulipaswa jana uende kanisani utoe sadaka ya kumshukuru Mungu kukuepusha na kifo na kukupa uponyaji wake.Unajua watu ni kwamba tuna fanya vitu ambavyo atuvijui na kumtumikia shetani tukidhani tuna mtumikia Mungu.
Hope he understands. Mungu anakupenda sana hivyo sifa na utukufu na hata hiyo kumbukumbu pia ni ya kukumbuka jinsi Mungu alivyoonyesha Ukuu wake katika maisha yako.

Barikiwa.
 
kila mtu yupo duniani kwa sababu na kila kitu kinachomtokea mtu kina sababu, Mungu kwa kukupa kamuda kengine ka kuishi ni kwamba kazi yako bado ujaimaliza na pia kupata kwako ajali mbaya yenye kukatisha tamaa, pia ni somo kwako na tunaokuzunguka, hapo pana somo kubwa sana na kwa mujibu wa maelezo yako ya shukrani wa wote waliokusaidia, umeongea mambo mengi mazito na inaonekana mengi umejifunza kutokana na hiyo ajali,
cha muhimu ni kushukuru kwa kila jambo na mungu hawezi kukupa kilema ambacho hautakimudu
pole sana kaka Mayalla
 
Pole sana, Mungu akuongezee imani.

Hongera kwa biidi ya kuendelea na shughuli zako ktk wakati huu mgumu hasa masomo yako.

Ni wachache wakumbuka kusema ASANTE!, japo neno hili sasa linapotea.
 
Pole Pascal kwa mitihani mikubwa ya maisha uliyopitia.Mchango wako kwa jamii na Taifa bado unahitajika. Nakutakia kila la kheri katika kuzikabili changamoto zilizopo mbele yako
 
Back
Top Bottom