Waraka wa Kibanda kabla ya kufikishwa mahakamani

Status
Not open for further replies.
NDUGU ZANGU WATANZANIA, KATIBA SI MILIKI YA MTU AU TAASISI MOJA HATA KUKASHAWISHIKA KUHODHI UUNDWAJI WAKE: DALILI ZOTE HIZI ZA HAPA MWISHONI NI DHAHIRI IKULU KUNA TATIZO TENA ZITO SANA!!!

Watanzania enzangu,

tangu hii timua timua kiholela holela katika vyuo vikuu vyetu kote nchini, kamata kamata ya sauti pinzani kila mkoa na hivi sasa bambika bambika ya hizi kesi za kuchonga kuminya zaidi sauti huru kusikika na wananchi kudai uhuru wa kujitungia katiba, wazee wote tunatahadharisha hapa kwamba pale Magogoni kuna tatizo tena lisiloweza kupatiwa ufumbuzi kivile.

Kila mmoja anayeweza leo hii tunaamkia Mahakama ya Kisutu na ni huko huko ndiko kutakakokua huko! Kama Kisutu ndio karamuni wavujajasho tunakoshereheshwa kila tunapolilia HAKI nchini, hebu sasa twendeni karamuni tukasheherekee tangu asubuhi ya saa tatu vile.

Ndugu zetu Kibada na Mwigamba waonekana ni wahalifu hata kabla ya kesi kufunguliwa shauri tu ya kulilia katiba mpya; sote kote twendeni karamuni sasa!!
Alikwambia anataka kujaribu udikteta kidogo kwa hii miaka mitatu aliyobakiza akinogewa anaongeza mingine mitano kama alivyofanya Museven lets get prepared.
 
Inaonyesha ni jinsi gani usivokuwa makini. Bila shaka utakuwa mbwa mmoja wa TISS waliogeuzwa sasa mbwa wa viongozi na kuchumia tumbo. Sasa kama hujui kama habari iliandikwa kwenye gazeti la Absalom unajuaje habari yenyewe na kuiandikia maneno marefu yasiyokuwa na chembe ya umakini?
Ukweli ni kuwa huo ni ukandamizaji wa uhuru wa habari. Mwandishi mwigamba aliwaandikia maaskari kwa kuwarudisha kwenye mstari walipo wananchi badala kuwa kama mbwa anayetupiwa nyama na viongozi na kusahau kuwa wanapaswa kuwatumikia wananchi si kutumikia amri za kukandamiza haki zinazotolewa na viongozi walioshindwa wajibu wao. Kama wewe ni mmoja wa viongozi hao unafaidika na ufirauni wa viongozi wetu ujue sisi wananchi tuko nyuma ya watu kama Absalom na Mwigamba. Mnachokifanya ni kuwa mnatumia dola kukandamiza sauti ya wanyonge inayopazwa na kina Absalom ila amini usiamini ipo cku kama sio sisi basi watoto wetu watashindwa kuvumilia na kuwatia bunduki matakoni kama Ghadafi. Salama yenu ni pale tu mtakapo acha kubughudhi sauti ya umma na kuvitungia kesi sizo na kichwa kama hizo za kina Absalom na kuacha wananchi waamue hatima yao.
I guess the same kwa huyu jamaa, post ndefu bila kitu ndani anamwambia Kibanda aache woga wakati yeye amekurupuka Kijitonyama alikojificha tangu 2006. MREKEBISHARIKA acha woga siku yao ikifika imefika hakuna wa kuizuia Gaddafi alikuwa na guard tena kali zaidi yetu akaishia kusomezwa kijiti makalioni.
 
Tunapoendelea na comments zetu hebu tujikumbushe na huu walaka wenyewe wa Samson Mwigamba.




MAKALA hii ilikuwa itoke Jumatano ya wiki iliyopita lakini kwa sababu za kiufundi ikashindikana. Imekuwa ni bahati nzuri kwamba inapotoka leo, ijibu swali la askari polisi dereva wa gari la maji ya kuwasha.

Askari huyo alimweleza Mwalimu Mkuu wa watu jinsi roho inavyomuuma pale anapowamwagia Watanzania wenzake maji hayo ya kuwasha wakati wakidai haki yao. Askari uliyeuliza na wenzako wote someni makala hii kwa utulivu. Huu ni waraka maalumu kwa askari wote wa majeshi yote vikosi vyote Tanzania Bara na Visiwani.
Kwa lugha ya wazi zaidi nazungumza na askari wa Jeshi la Polisi Tanzania, Askari wa Jeshi la Kujenga Taifa, askari wa Kikosi Maalumu cha Kuzuia Magendo (KMKM), askari wa Jeshi la Magereza na wale wa Jeshi la Wananchi (JWTZ).
Kuwa mwanajeshi lolote kati ya hayo niliyoyataja si dhambi na si kweli kwamba kuwa mwanajeshi kunakuondolea uwezo wa kufikiri na badala yake ukawa unafikiriwa na watu wengine.
Wala haimaanishi kuwa askari kuwa kama robot ndio nidhamu bora kuliko zote duniani. La hasha! Mimi nilikataa utumwa huo!
Mwaka 1999 nilihitimu elimu ya cheti cha ufundi mchundo, yaani Full Technician Certificate (FTC) katika uhandisi wa Elektroniki na Mawasiliano ya Anga, yaani Electronics & Telecommunications Engineering kutoka Taasisi ya Teknolojia ya Dar es Salaam (DIT).
Nikiwa bado sijapata kazi ya maana, mwezi Aprili mwaka 2000 niliona tangazo la kazi ya Radio Technician katika Jeshi la Magereza. Nikatuma maombi na kuitwa kwenye usaili uliofanyika Chuo cha Maofisa wa Jeshi la Magereza Ukonga, Dar es Salaam mwezi Juni 2000.
Wote tuliofaulu usaili tulipangiwa siku ya kuripoti Chuo cha Magereza Kiwira kule Tukuyu, Mbeya.
Kufika kule nilishuhudia mambo ya ajabu. Ingawa wao hufurahia na kusema eti wanakutoa uraiani na kuwa mwanajeshi lakini baadhi ya matendo yanayofanyika wakati wa mafunzo ya jeshi ni ya kuwapumbaza askari wetu ili baadaye wakiwa kazini, watawala wawatumie watakavyo.
Nilishindwa kuvumilia kaulimbiu ya wakufunzi wa jeshi pale walipoelekeza kwamba chochote kruta (askari mpya mafunzoni) unachoambiwa lazima uitikie "ndiyo afande". Nilishindwa kuitikia kwa mfano pale mkufunzi mmoja mwenye cheo cha koplo alipotutamkia mfululizo wa sentensi zifuatazo:
Mkufunzi: Nyinyi makruta mbona wote hamkuja na majembe?

Makruta: Ndiyo afande!
Mkufunzi: Hamkuambiwa makao makuu ya jeshi kwamba lazima mje na majembe?
Makruta: Ndiyo afande!
Mkufunzi: Kwa hiyo kwa kuwa hamkuambiwa na nyinyi hamkuyabeba?
Makruta: Ndiyo afande!
Mkufunzi: Wote ni wapumbavu pamoja na mama zenu waliowazaa.
Makruta: Ndiyo afande!
Ni hayo pamoja na mambo mengine ya kulazimishwa kwenda kwenye kile kinachoitwa disko, ambapo pamoja na uchovu wa kutwa nzima wa kazi ngumu na nyingi bado ni lazima ukae hapo mpaka saa 4 usiku tena ukinyooshewa kidole tu na mwenzako lazima usimame na kuimbisha wimbo tena kwa tabasamu, wimbo mmoja wapo ukisema "Magereza ninavyokupenda nitakunywa sumu juu yako", ndiyo yaliyonifanya nikakataa kazi ya jeshi baada ya wiki moja tu ya mafunzo.
Siku niliyokataa jeshi ilikuwa ni Jumatano asubuhi ambapo sikwenda mchakamchaka na wakati wenzako wanatawanyika kufanya usafi wa nje maeneo mbalimbali, mimi nilibeba begi langu na kuanza kuondoka chuoni majira ya saa moja na nusu hivi asubuhi.
Nilikamatwa na mkufunzi mmoja wa jeshi na kupelekwa pamoja na begi langu kwa Ofisa Mafunzo wa chuo. Aliponiuliza sababu nilimtajia mbili, kwanza kwamba sifurahii mambo ya jeshi na kubwa zaidi kwamba mimi ni Msabato na nimeambiwa na wenzangu kwamba hapa hakuna kwenda kusali, siku zote za juma ni kazi.
Kitu ambacho sitaweza maana Sabato takatifu lazima nipumzike! Bila kuuliza zaidi aliconclude kwa kuniambia kwamba, "Sijawahi kuona mtu anaacha kazi kwa ajili ya mambo ya dini.
"Ni dhahiri wewe ulikuja kutupeleleza na hivyo kazi yako imeisha sasa unataka kurudi. Tutakuweka rumande, tena ile ya polisi kwa wiki mbili wakati tunafanya upelelezi juu yako."
Askari aliyenileta alianza kunivuta ili kunipeleka rumande lakini nilikataa huku nikiendelea kujieleza kwa ofisa mafunzo ili ajue kwamba sikuwa na mpango huo aliousema.
Baada ya kuelemewa na hoja zangu alinipeleka kwa makamu mkuu wa chuo ambaye yeye alitumia zaidi Biblia kunihubiri kwamba nakaidi amri ya mamlaka wakati hakuna mamlaka isiyotoka kwa Mungu.
Jibu langu lilikuwa fupi na lenye msimamo mzito kwamba ikiwa mamlaka ya wanadamu inafika mahali inanena tofauti na Mungu, Mtume Petro ametuandikia kwamba katika hali ya namna hiyo, "Imetupasa kumtii Mungu kuliko mwanadamu".
Na yeye alinishindwa akanipeleka kwa mkuu wa chuo na wao wote wakiwapo. Ushauri waliokuwa wakimpa mkuu wa chuo ni kwamba mimi niwekwe rumande kwanza ili wafanye upelelezi. Lakini sikuyumba katika msimamo wangu.
Nilimweleza mkuu wa chuo kwamba mimi ni raia na si mpelelezi. Nilizirudia rudia sababu zangu za kuacha jeshi tena kwa ujasiri mkubwa na kumhakikishia mkuu wa chuo kwamba akinipa hayo ninayoyataka niko tayari kubaki jeshini.
Hatimaye kauli ya mwisho ya mkuu wa chuo ilikuwa ni hii: "Jeshi ni wito. Tunaweza kumlazimisha huyu kijana kuwa mwanajeshi lakini baadaye ikatuletea madhara makubwa sana." Akamalizia kwa kusema, "chukueni maelezo yake kwa maandishi kisha arudishe vifaa vya jeshi."
Wakati naondoka nilimsikia ofisa mafunzo akitoa maelekezo kwa walio chini yake kwamba mwanafunzi mwingine wa jeshi akija kuripoti na kwenye daftari akajaza kwamba ni Msabato, msimsajili kwanza mpaka aje kwangu! Sijui kama Wasabato wameendelea kupokewa kwenye hicho chuo cha magereza lakini ninachotaka askari wote wa majeshi yetu yote na vikosi vyote, ni kwamba askari unaweza kusimama kwa miguu yako na kufikiri kwa akili yako mwenyewe!
Ndugu zangu askari, nchi imefika mahali ambapo Waingereza hupenda kupaita ‘critical point'. Ni mahali ambapo wananchi wako tayari kwa mabadiliko na watawala wako tayari kwa mapambano ili kubaki madarakani.
Katika point hii askari wetu wanakuwa na nafasi kubwa ya aidha kuwezesha mabadiliko hayo kutokea kwa wakati wanaoutaka wananchi, tena kwa amani ama kuyachelewesha (si kuyazuia) na kusababisha yatokee baadaye kidogo kuliko wananchi walivyotaka, tena baada ya kumwaga damu nyingi ya Watanzania wasio na hatia!
Napenda kurudia kwamba hakuna jeshi lolote duniani hata kama tungekusanya majeshi yote ya dunia hii na kuyaleta Tanzania hawataweza kuizuia nguvu ya umma pale inapokuwa imeamua kufanya mabadiliko.
Napenda tena kurudia kwamba si lazima askari mfanye kile ambacho wakubwa wenu wanataka na kuwaamuru kufanya. Tunaweza kusimama imara na kutetea haki za Watanzania tukiwamo na sisi askari. Niliwahi kugoma kutii amri ya kukamatwa na kuwekwa rumande.
Lakini pia mifano ni mingi na nisingependa kuchukua mifano kutoka nchi za Ulaya kama Uingereza ambako tulishuhudia wananchi wakiandamana mitaani na askari wao hawakuwahi hata kumpiga kofi tu mwandamanaji hata mmoja.
Walipohojiwa na vyombo vya habari walisema dhahiri kwamba waandamanaji ni raia halali wenye haki ya kufanya kile wanachokifanya kwa mujibu wa katiba na sheria za nchi yao. Katiba ya Tanzania na sheria za nchi hii zinatoa haki kama zile za Uingereza. Tofauti ni utekelezaji wa matakwa hayo ya kikatiba na kisheria. Watawala wa Uingereza wako tayari hata kung'oka madarakani ili kutekeleza matakwa ya nguvu ya umma.
Lakini wale wa Tanzania wako tayari kung'oa uhai wa raia wengi ili mradi kuzuia nguvu ya umma inayodai haki na wananya hivyo kwa sababu ya hofu ya kung'oka madarakani, jambo ambalo hawataki kabisa kulisikia. Na ndugu zangu askari napenda kuwaambia kwamba yote yanafanywa na watawala wetu kwa kuwategemea nyinyi.
Wanaminya haki zenu nyinyi wenyewe, haki za wazazi wenu, dada na ndugu zenu, marafiki zenu, jamaa zenu na majirani zenu. Chukulia mfano rafiki zangu Mtaki na Edwin. Tumesoma wote shule ya msingi pale Magu.
Nilichaguliwa kujiunga na Mazengo Sekondari, shule kubwa na ya muda mrefu ambayo sasa imegeuzwa kuwa chuo kikuu bila mabadiliko ya majengo.
Shule iliyokuwa na maabara nne kwa maana ya maabara ya baiolojia, kemia, fizikia na jiografia. Ilikuwa ni sekondari ya ufundi na hakuna karakana ambayo haikuwapo.
Shule iliyokuwa na walimu wa kutosha, vyumba vya kutosha vya madarasa na vya kulala mabwenini.
Katika bweni la Ujamaa kwa mfano, nilikokuwa naishi mimi, kuna vyumba kadhaa havikuwa na watu. Darasa la Form IVA ambalo nilikuwamo lilikuwa na wanafunzi 21 tu darasani.
Na mazingira mengine mengi ambayo sitaweza kuyataja hapa ambayo yanafanya wanafunzi wa leo wa Chuo Kikuu cha Mt. John wajiulize kama kweli ile ilikuwa ni shule ambayo haina maktaba wala vitabu vya kutosha, na mengineyo mengi mnayoyafahmu.
Nikafaulu kwa kiwango cha daraja la juu lililoniwezesha kuendelea mpaka chuo kikuu na kupata kazi nzuri kwenye Umoja wa Mataiifa.
Rafiki zangu nakumbuka mlivyoamua kujiunga na Jeshi la Polisi si kwa sababu mlipenda kazi hiyo ama kwamba mlikuwa na wito wa kuwa polisi kama mnavyodanganywa kwamba jeshi ni wito.
Nakumbuka mlijiunga huku mkilalamika kwamba mnalazimika kujiunga huko kwa sababu kiwango chenu cha ufaulu hakiwapi fursa ya kazi bora zaidi ya hiyo. Lakini mimi nawafahamu vizuri. Najua uwezo wenu wa darasani. Mliathiriwa na mazingira ya hovyo ya shule mlizosoma.
Rafiki zangu nyinyi wote leo ni wakuu wa vituo vikuu vya polisi vya wilaya katika wilaya za Mbozi na Igunga.
Leo hii mimi nimeacha kazi ya Umoja wa Mataifa kwa ajili ya kushiriki vema katika mapambano ya kutafuta ukombozi wa taifa hili.
Wadogo zenu na wadogo zangu mnawajua wako katika juhudi za kutafuta maisha lakini ni magumu. Wengine walikosa kabisa nafasi ya kujiunga hata na hiyo Magu Day.
Wakaishia Bulima na Kinango, ambako hali ilikuwa mbaya zaidi. Wakafeli kabisa na leo wanahangaika hapa na pale lakini watawala wanawawekea mazingira magumu mno ya kuendesha maisha.
Na sasa chukulia nao wametambua hali yao duni inasababishwa na watawala walafi na walaghai. Wamejaribu kutumia njia za kidiplomasia kudai haki zao wanakutana na watu wanaitwa wakuu wa wilaya na mikoa.
Wanaamua kuandamana, mnashiriki kuamrisha askari walio chini yenu kuwapiga na kuwaweka rumande na hatimaye kuwafungulia kesi za kubumba!
Askari wetu igeni mfano wa askari wa Misri! Pale wananchi walipoamua kuandamana kukomesha utawala wa kidhalimu wa miaka 30 chini ya Hosni Mubarak, askari waliwalinda badala ya kuwapiga.
Walikataa kwa sababu hata wao walikuwa wakiumizwa na Mubarak lakini zaidi ya hayo, waliokuwa wakiandamana walikuwa ni dada zao na ndugu zao na marafiki zao.
Hivi sasa nchi iko njia panda. Ugumu wa maisha umeongezeka mara nne na zaidi. Watawala hawalioni hilo wala hawajishughulishi kurekebisha hali ya mambo hususan hali ya uchumi.
Wako busy na kujiandaa kwa uchaguzi wa 2015. Mawaziri wako busy na kampeni za kuteuliwa kuwa wagombea wa urais kupitia chama tawala hapo 2015 na rais naye yuko busy kuandaa mtu wake ambaye anadhani akimrithisha jumba jeupe la pale Magogoni atasema mwacheni Ndugu Kikwete apumzike kwa amani.
Taifa limeamua kuandika katiba mpya, rais na serikali yake na chama chake wameamua kuuteka mchakato ingawa haikuwemo kwenye ilani yao ya uchaguzi ili tu waturudishie katiba ya mwaka 1977 na kuipa jina juu ya jalada KATIBA YA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA YA MWAKA 2014.
Natambua juhudi zinazoendelea hasa zikiongozwa na CHADEMA kujaribu kumkumbusha rais kwamba katiba iko juu yake na katiba ni mali ya wananchi na yeye anaajiriwa kwa katiba hiyo na si yeye kujiandalia katiba ili atawale kwa ulaini.

Lakini juhudi za kidiplomasia zikishindikana hapo ndipo itabidi haki ya watu idaiwe kwa maandamano na hapo askari wote tuungane na kuwa kama Misri, kwa kuwa Katiba mpya ni kwa masilahi yenu pia! Jaribuni kutafakari!
 
mapinduzi halisi ndo yanakuja, magamba mtabana sana lakin mwisho nguvu ya umma itachukua nafasi yake. kila la kheri Kamanda
 
WATANZANIA HIZI BUSARA ZA KUKATAA KUWEKEZA KWA WANANCHI KUJIANDIKIA KATIBA MPYA KWA AMANI NA BADALA YAKE KUJICHAGULIA KUWEKEZA KWA UZITO WOTE KWENYE VYOMBO VYA FFU NA KARATASI ZA KURA GHILIBA KWA AJILI YA 'CCM KUTOBOA 2015' KWELI TUTAFIKA?

Kuna maneno mazito sana yametumika na Mjumbe Feedback hapo chini. Haya maeno yake au nukuu wala si ya kuchukulia mzaha hata kidogo.

Nasema hayo maneno wala si masimulizi au maneno tu ya kubuni bali ni kwamba yalitaamkwa mchana kweupe pale uwanja wa Sabasaba. Lakini ikachukua tu takriban wiki tatu tangia hapo na haya yote kuanza.

Licha ya ukweli kwamba nchi yetu tumekubali kwamba sera yetu ya mambo ya nje ni diplomasia ya uchumi, uteuzi wa mablozi wapya hivi majuzi ni dhahiri umekiuka misingi hii kwa kuwa watu tuliowapeleka huko ni lazima kusamehewa kila wakati kukija kwenye mazungumzo ya afya njema ya uchumi wetu.

Mfano mdogo tu, hivi majuzi tumempeleka Babu Marmo Uchina
( huyu mkuu si mwana-Uchumi wala hajawahi kumiliki hata banda la kuuzia maziwa nchini kiasi cha kutukuna na kuamua kumpeleka akatuwakilishe kwenye uchumi mkubwa kama ule duniani) kuchukua nafasi ya Mzee Mapuri, hadi hapo tunajiuliza tunachotaka kukipata toka Uchina kwa kumtumia Babu yetu huyu mbaye miaka yote varanda zake za kuchezea ni ofisi nyeti za serikali ni nini?

Watu watasamehewa endapo watajiuliz kwamba pengine tunampeleka huko kwa ajili ya kazi hizi mbili kuu zikiwa ni pamoja na kutununulia vyombo vya FFU pamoja na au safari yake lina lengo kuu la kutununulia zile Karatasi-KARATA-TATU zilizotumika 2005 ili zije zikatumike kwa pamoja kutekeleza lile azimio la Uwanja wa Sabasaba pamoja na kutekeleza pia NDOTO ZA MWISHO ZILIZOSALIO kukivusha tena CCM 2015, WaTanzania tupende tusipende?

Hivi sasa ni dhahiri kwamba kuna mchakato unatekelezwa na wazuia mabadiliko ili kujiongezea siku zaidi serikalini.

Ndio, ni ukweli usiopingika kwamba tangu pale Azimio la Udikteta utangazwe pale uwanja wa Sabasaba hadi matukio yote yanayojitokeza tangia hapo ni kweli ukurasa mpya wa Udikteta ulifunuliwa na kutekelezwa kwa kasi na nguvu ajabu.

Kada wa kwanza kuonjeshwa machungu ya azimio hilo ni wanafunzi wapenda mabadiliko wa vyuo vikuu kote nchini. Majuzi ilikua ni MaKamanda Lema Dr Slaa, Mbowe na Lema kwenda lupango na hivi sasa mvua hizi za damu zaonekana kuwageukia wanaharakati nchini.

Hata hivyo dawa yake ni ndogo sana; KUSIMAMA PAMOJA NA SOTE KUSEMA KWA KINYWA KIPANA KWAMBA Tanzania bila Udikteta inawezekana - kwa swala la Katiba mpya kamwe hakuna kurudi nyuma hata hatua moja!

Kama kuna kitu kinanitia wasiwasi zaidi hadi sasa ni swali tu la kwamba je katika haya yote mwenye programu yake anategemea WaTanzania tukamrudishie nini kwa kipindi hicho cha utekelezji wa mchakato wake huo??


Alikwambia anataka kujaribu udikteta kidogo kwa hii miaka mitatu aliyobakiza akinogewa anaongeza mingine mitano kama alivyofanya Museven lets get prepared.
 
NN, its not too much to ask, ili la kuwataja majina ili muwaone ni heroes, kunaweza kupelekea watu wenye chuki zao, kuwachafua!.

Ili kukidhi haja maridhawa, nakubaliana na wewe, waandisho wote Tanzania, ni wachumia tumbo!, hakuna msafi hata mmoja!.
Nimekubali yaishe, turudi kwenye mada ya Kibanda.

Hakuna mahali niliposema waandishi wote Tanzania ni wachumia tumbo na hakuna msafi hata mmoja. Unanitwisha maneno ambayo sijayaandika popote pale.
 
Lets hope you are not among of them.
90cart01102006oo6.jpg
Feedback, I hope you mean him!, let name calling alone, I bet He is not one of them!. Waandishi wachumia tumbo, itawajua sio kwa kiingiacho mifukoni mwao, bali kile kitokacho vinywani mwao/kwenye kalamu zao!.
 
1.Jenerali Ulimwengu 2.Lula mwananzela 3.Padri kalugendo 4.Masoudi Kipanya 5.Larry King
Kinachonishangaza ni kwanini hawa waandishi wanaliacha bunge litunge sheria ambazo baadae zitawakandamiza?.... Hao weote uliowataja nashindwa kuelewa kama walikuwa hawajui kuwa hizi sheria zimepitishwa na bunge. Walikaa kimya!.... why?

Kama wako serious, huu ni wakati wa kuonyesha unconstitutionality of cap.500 especially sec.8 of 1966. Itakuwa kazi sana kwani hao kina Ulimwengu wamekuwa wandishi chini ya sheria hizo, walijifunza kuziheshimu sasa siju watasemaje..... It's a tough case, almost a slam dunk for the State!
 
Waandishi wote mnaolipwa na Lowassa, very soon mtaelewa ni nani aliyemtoa Uwaziri Mkuu huyo bosi wenu. Maneno mengi ya kishujaa kumbe ni wachumia tumbo tu! Now what watu wote humu tunatakiwa kuamini kwamba Kibanda ni Mandela? Ha! Ha! Lowassa please go away tuachie taifa letu!
 
Kwani ni siri?wao c wanawaandikia watu?
NN, its not too much to ask, ili la kuwataja majina ili muwaone ni heroes, kunaweza kupelekea watu wenye chuki zao, kuwachafua!.

Ili kukidhi haja maridhawa, nakubaliana na wewe, waandisho wote Tanzania, ni wachumia tumbo!, hakuna msafi hata mmoja!.
Nimekubali yaishe, turudi kwenye mada ya Kibanda.
 
nilijua watu kama ndugu yangu Pasco,kina mzee mtashabikia tu jambo hili,lakini nisema tu kwamba afadhali Pasco nakujua sisemi sana kwa huyo anaejiita mzee,nakuuliza hivi msukuma mwenzangu:
Jigoku,
Kwa kawaida wanaodandia 'ya abiria', hudandia kwa nyuma kichwa kikishapita, mbona wewe unataka kudandia kwa mbele!. Mbona Wasukuma hatuko hivi?!.

Ulijua watu kama mimi tutashabikia?, hivyo mimi ndio nimeshabikia?.

Maadam umesema unanifahamu, kabla sijajibu hayo maswali yako, naomba unikumbushe posti yangu niliyoshabikia kiasi cha kuniweka kundi moja na 'Mzee'!.

Ila Jigoku pamoja na kunisingizia kuwa ninashabikia, lakini bado nakushukuru kwa hoja zako za msingi na utetezi wa Mwigamba na Kibanda. Kwa vile hatujuani proffesional zetu humu, ila kusema ukweli wewe kama ni mwanasheria, basi u wakili mahiri, kwa vile hizi points ni final submission tena kwa kuisight part I Order ya geshi ambayo hutumika kwa mageshi yote, umemaliza kila kitu na Mwingamba na Kibanda wameshinda kesi!.
 
Waandishi wote mnaolipwa na Lowassa, very soon mtaelewa ni nani aliyemtoa Uwaziri Mkuu huyo bosi wenu. Maneno mengi ya kishujaa kumbe ni wachumia tumbo tu! Now what watu wote humu tunatakiwa kuamini kwamba Kibanda ni Mandela? Ha! Ha! Lowassa please go away tuachie taifa letu!
WJM, sio kila mtetezi wa EL yuko kwenye payroll yake, najipambanua wazi hata mimi binafsi kama Pasco wa jf (leave name calling alone), namkubali sana EL kwa facts za ukweli as the axisis ya mafanikio ya mwanzo ya JK na baada ya kuondoka matokeo ndio haya tunayoyaona, naamini kama angelikuwepo, tusingelifika hapa tulipofika!. Kama kwa utetezi huu ndicho kipimo cha wachumia tumbo, basi nakubaliana na hoja kuwa waandishi woote wa Tanzania ni wachumia tumbo, with no exceptional!.
 
Mkuu WJM, sijasema Tanzania hamna waandishi wachumia tumbo, nimesema waandishi wachumia tumbo wapo mpaka makanjanja wapo, ila sio waandishi wote wa Tanzania, ni wachumia tumbo, tunao baadhi ya waandishi wazuri, wasafi, wenye wito ambao sio wachumia tumbo!.

Hili la kuwaona members wa jf mazezeta limetokea wapi?.

Mwisho mimi ni Pasco wa jf, hapa jf tukisha jitambulisha kwa pen names tunaishia hapa, zaidi ya hapa ni name calling!.

Pasco si uwataje basi?? mbona na wewe unaonekana kama hujiamini??

Mie naanza na Kamanda Jenerali (sina hakika kama ni msafi vilevile).......... labda tutaje na waliokufa
 
Masirahi ya wakubwa yakiguswa mara nyingi huwa ni vita na mara nyingi anayeumia ni yule aliyeshika kwenye makali. Na mihimili yote haiko huru kutoa maamuzi ya haki kwa sababu viongozi wote wa hiyo mihimili ni wa kuteuliwa na hao hao wakubwa, hivyo chochote watakachoamuliwa kukifanya wanafanya bila kuangalia haki ni yanani? Ndio hasa maana ya UTAWALA.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom