Mkuu WJM, sijasema Tanzania hamna waandishi wachumia tumbo, nimesema waandishi wachumia tumbo wapo mpaka makanjanja wapo, ila sio waandishi wote wa Tanzania, ni wachumia tumbo, tunao baadhi ya waandishi wazuri, wasafi, wenye wito ambao sio wachumia tumbo!.Pasco unasema Tanzania hamna waandishi wachumia tumbo? I mean are you serious au unaona members wa JF ni mazezeta? Ukiona mwandishi yoyote bongo yuko introuble ujue tayari amechanganya interest za tumbo lake, au tutajie waandishi wasafi bongo ni nani?
- Halafu wewe si muandishi pia je msafi?
Huyo anatumiwa na Chadema hana lolote. Hatupo tayari kuvumilia uchochezi wa aina yoyote ile.
Huyo anatumiwa na Chadema hana lolote. Hatupo tayari kuvumilia uchochezi wa aina yoyote ile.
Amina amina amina! Oh! Aminakweli ww ni mzee na hakika umejizeekea, hvyo ninachoona ni kwamba unasubiri kulala pema peponi amina.
Mhariri mtendaji wa Tanzania daima bw.Absalom Kibanda ataripoti tena polisi keshn na ikiwezekana ataburuzwa mahakamani.Huu ni muendelezo wa kesi inayoitwa ya"Uchochezi" kufuatia ile makala ya Samsoni Mwigamba kwa jeshi la polisi.Ikiwa imebaki masaa machache kabla ya kuripoti polisi Kibanda ameandika yafuatayo kwenye ukurasa wake wa facebook:
"Kesho saa 3:00 asubuhi natarajia kuripoti Makao Makuu ya Jeshi la Polisi jijini Dar es Salaam tayari kwa lolote, kubwa likiwa ni kuburuzwa kortini Kisutu kusomewa shitaka la uchochezi. Hatua hii inakuja siku tatu tangu niliposhikiliwa , nikahojiwa, nikatoa maelezo yangu na kisha nikawekewa dhamana na rafiki na mdogo wangu, Saed Kubenea.
Taarifa tulizozipata kutoka kwa viongozi waandamizi serikalini ambao wanatutakia mema zinaeleza kwamba limekuwapo shinikizo kubwa kutoka kwa wakuu wa dola la kutaka mimi ambaye ni Mhariri Mtendaji wa Tanzania Daima nifunguliwe mashitaka ya Jinai kama njia ya kujibu hasira za wakubwa dhidiyangu binafsi na dhidi ya gazeti la Tanzania Daima ninaloliongoza.
Habari kwamba nilikuwa miongoni mwa wahariri waliokuwa wamewekwa katika orodha ya kufikishwa mahakamani kwa makosa ya jinai na siyo ya madai kama ilivyo ada tulielezwa miezi kati ya mitatu na minne iliyopita. Taarifa hizi zilitolewa na mmoja wa mawaziri kwa mmoja wa wahariri ambaye ni rafiki yake mkubwa.
Baya katika uamuzi huu si kwamba anayeshitakiwa ni Absalom Kibanda, ambaye ni Mhariri wa Tanzania Daima na Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri la hasha, bali ni uamuziwa hatari wa baadhi ya viongozi wa serikali ambao wameamua kuminya uhuru wa kikatiba wa watu kutoa maoni yao.
Uamuzi huu wa sasa wa kuanzakuwashitaki wahariri kwa makosa ya jinai yanatukumbusha maneno ya Waziri Mkuu mstaafu Frederick Sumaye aliyetabiri kwamba kiongozi anayesaka umaarufu na ikulu kwa njia ya vyombo vyahabari akiingia madarakani atalinda himaya yake kwa risasi.Ni wazi kwamba dhamira ya kupambana na watu wanaokukosoa wewe binafsi au serikali yako kwa njia ya kuwakomoa au kuwaumiza si tu ni udikteta unaofanana kimantiki na wa zama za Adolf Hitler bali unadhihirisha namna tulivyo na madikteta wanaofichwa na uhuru wa kidemokrasia waliokuta ungalipo hata kabla hawajaingia madarakani.
Hatua ya kulitumia Jeshi la Polisi kukandamizi uhuru wa habari kwa kuwakamata waandishi wamaoni kama walivyofanya kwa Samson Mwigamba wiki iliyopita na wahariri wa magazeti kama inavbyofanyika kwangu haina budi kupingwa kwa matamko na kwa njia nyingine za kudai haki iliyowekwa rehani.
Hakika kama taifa tupo njia panda. Nimeamua kwa dhati kulitumia tukio hili kama somo kwa madikteta wa Tanzania na wengine wa Bara la Afrika. Nimehamasishwa kujitoa mhanga kuleta mabadiliko ya kweli ya uhuru wa habari na wawatu kutoa maoni yao pasipo kuvunja sheria. Ukisoma makalaambayo imewapotezea polisi, mahakama, magereza na wapendwa wetu muda adhimu huwezi ukaamini kwamba tuna viongozi wanaofikiri sawasawa.
Ni hatari kuwa na kiongozi mkuu aliye tayari kuumiza watu wadogo kama sehemu ya kupumua au kupunguza hasira na machungu yake moyoni ambayo yamesababishwa na kupwaya kwake au kushindwa kwake mwenyewe. Ni aibu kuwa na viongozi dhaifu ambaokwao kuumiza wengine ndiyo kipimo cha nguvu za kikatiba walizopata tena kwa njia ya sanduku la kura. Kama kweli tunalitakia mema taifa hili hatuna budi kuanzisha mapambano makali ya kupigania uhuru ambao sasa umewekwa rehani. Wanahabari na wanahabari tunapaswa kujitoa mhanga kuyaongoza mapambano haya mapya".
Nimekumbuka ile katuni ya kenya ikionyesha waandishi wa kibongo wakilamba viatu vya JK.
Waandishi wa kibongo wakawa mbogo not knowing that was 'honey moon' and honey moons never last long
Lets hope you are not among of them.Mkuu WJM, sijasema Tanzania hamna waandishi wachumia tumbo, nimesema waandishi wachumia tumbo wapo mpaka makanjanja wapo, ila sio waandishi wote wa Tanzania, ni wachumia tumbo, tunao baadhi ya waandishi wazuri, wasafi, wenye wito ambao sio wachumia tumbo!.
Hili la kuwaona members wa jf mazezeta limetokea wapi?.
Mwisho mimi ni Pasco wa jf, hapa jf tukisha jitambulisha kwa pen names tunaishia hapa, zaidi ya hapa ni name calling!.
Ukisoma alichoandika kibanda napata shida na Shaka kuamini Kama Mtu mzima kweli anaweza andika haya aliyoyaandika. Nilivyoelewa mimi ni kwamba kama amepatwa na uwoga vile au alikuwa hajuinkuwa muandishi kuandika,wananchi kusoma na vyombo vya usalama,kuuliza kama wanaona yaliyoandikwa yanahatarisha usalama wa nchi au yanachochea mambo fulani.
Kwanza kibanda angetuambia Ndani ya baraza hili Kama ni kweli kuwa ni yeye na gazeti lake ndiyo Walioandika haya. Maaana sina hakika Kama Jakaya na wenzake walimtuma akayaandike haya na baadae walimkataa katika Yale anayoyaita kuwa Watu wanatumia wamemfix. Au a nataka kutumia kuwa ndiyo mkuki umerudi kwa binaadamu.
Sidhani pia Kama kuna uhuru usio na mipaka.nifikiriavyo huu uhuru wa vyombo vya ulinzi na usalama kumuuliza Mtu yeyote na mahakamani ndiyo haki itakako patikana ndugu yangu na si katika mtazamo we kukandamiza uhuru wa vyombo via habari Kama ambavyo ndugu yangu Huyu anajaribu kuiambia dunia.nazungumza hili kwa kuwa umekuwa ni utamaduni sasa kwa vyombo vya habari kuzusha na kuandika mambo ya ajabu au habari za uzushi kwenye magazeti bila hata ya kuwa na uhakika wa habari hizo ,eti yote hayo ni katika yale wanayoyaita uhuru wa kutoa habari au maoni.maoni ya Namna gani haya ambavyo Ndani yake hayana hata chembe ya uzalendo,utu na uhalisia.nijuavyo mie ni kwamba kwa waandishi makini lazima ingefanyika research ya maana Sana kabl hamjaandika jambo au haya maoni Kama ambavyo anatuambia kibanda.haiwezi ikawa ndiyo jamii hii ambapo kila Mtu atandika tafsiri yake katika tukio Fulani ambavyo yeye kwa upande wake au kwa upande wake kisiasa au kihisia anaconda ndivyo ilivyo.
Tatizo ni kwamba wamezoea kuona mambo yakiharibika kwa upande mmoja na raha ikija kwa upande mwengine na sasa anatafuta sababu katika mwamvuli wa kukandamizwa kwa demokrasia wakijidai kuwa Watu wanatafuta umaarufu. Ahahah kaka kibanda toa wasi na yoga,ni utaratibu wa kawaida Sana kwa jeshi la polish au chombo cha usalama kumuuliza Mtu na pale linapoona kuwa kuna nia ya kufanya kesi basi watapeleka katika vyombo husika. Kama hivi ndiyo utaratibu, wapi ukandamizwaje wa uhuru.kama polisi hawakukuita na kumuuliza maws ali Yao hiyo Hali itapatikana vp Kamanda au umesahau Kazi za mahakama au umesahau zipo wapi? Billicanas.
Pamoja na hili Mbona mwenzake alipoitwa kuhojiwa na polish ali toa ushirikiano na hakulalamika.hebu angalia alivyo pews Chumba hotelini na Kesha yake asubuhi baada ya mahonia no akapelekwa mahakamani Kama haya kosa mdhamini na outings jela.nini wasi wasi wako kwani inamaana haujui kuwa hapo polish ni kuandika maelezo na kushirkiana naomkujua au kupelekwa sababu za Msingi zilipelekea wewe kuandika article.Huu umekuwa ni utaratibu we kawaida. Haya Sasa SWAZI langu, bwana kibanda alitaka polisi wafanye nini na huyu anayemsema kuwa alitafutanumaarufu kwa magazeti na sasa anatumia dola kulinda mamlaka yake alitaka afanyaje?
Nionavyo Mimi, vyombo vinatimiza wajibu wake. Iwe wewe Mimi au Yule, nifikiriavyo ukikosea jambo au pale vyombo vinapoona kuwa hili lililotendeka si jambo la kawaida ni wajibu wao kutumia na kumuuliza Mtu yeyote na Kama adhabu itatolewa na mahakama. kwa kufanya hivi muandishi mkongwe kibanda unataka nini Kama sio Kuwa unajitoa akili Angaki unajua kuwa polisi agungwi Mtu kwa upande mmoja na pili kwamba kazi yako ilikwisha baada ya makala kutoa na watu kununua kwa wingi na baadae kuingia mtaani na kuona kwamba ulichoandika ni taarifa sahihi,huku vyombo vikisoma na kuangalia uzuri aw maneno yako ambayo Leo katika maandishi yako,unasema yalikuwa maoni.
Pole brother, umetimiza wajibu wako kama muandishi,umeweza.
Polisi wamekuita ili watimize wajibu wao,toa ushirikiano hakuna ugomvi
Wananchi tutaliongea na matarajio yetu Kama utajibu Maswali ya wahusika vizuri na sio kutumia forum zenu kulalamika.
Pole Sana MPIGANAJI, kaza moyo mapambano
yanaendeleaje,waache wafanyaje kasi Yao Acha uwoga. Fanya kama upo chumba cha habari billicanas pale.[/QUIOTE]
Inaonyesha ni jinsi gani usivokuwa makini. Bila shaka utakuwa mbwa mmoja wa TISS waliogeuzwa sasa mbwa wa viongozi na kuchumia tumbo. Sasa kama hujui kama habari iliandikwa kwenye gazeti la Absalom unajuaje habari yenyewe na kuiandikia maneno marefu yasiyokuwa na chembe ya umakini?
Ukweli ni kuwa huo ni ukandamizaji wa uhuru wa habari. Mwandishi mwigamba aliwaandikia maaskari kwa kuwarudisha kwenye mstari walipo wananchi badala kuwa kama mbwa anayetupiwa nyama na viongozi na kusahau kuwa wanapaswa kuwatumikia wananchi si kutumikia amri za kukandamiza haki zinazotolewa na viongozi walioshindwa wajibu wao. Kama wewe ni mmoja wa viongozi hao unafaidika na ufirauni wa viongozi wetu ujue sisi wananchi tuko nyuma ya watu kama Absalom na Mwigamba. Mnachokifanya ni kuwa mnatumia dola kukandamiza sauti ya wanyonge inayopazwa na kina Absalom ila amini usiamini ipo cku kama sio sisi basi watoto wetu watashindwa kuvumilia na kuwatia bunduki matakoni kama Ghadafi. Salama yenu ni pale tu mtakapo acha kubughudhi sauti ya umma na kuvitungia kesi sizo na kichwa kama hizo za kina Absalom na kuacha wananchi waamue hatima
yao.
Hiyo mipaka ya uhuru ni wapi? Kutogusa maovu ya viongozi? Kutowaambia maaskari wasiwapige wananchi wanaoandamana kwa amani badake wawaunge mkono? Kaandika kitu kinachoaribu amani ya nchi au kuhatarisha usalama? La hasha! Kaandika makala inayotishia usalama wa viongozi wabovu. Ni ujumbe mahsusi wa kizalendo. Vipi Pinda na bibi Kiroboto wa Bungeni walioandikiwa posho ya laki2.8 na Jairo kuwahonga? Nani alistahili kuwa wa kwanza mahakamani? Vipi kuhusu Ngeleja na Naibu wake wanaojilipa posho ya Mil4 kwa siku? Hawakustahili kuitwa polisi na kuhojiwa? Uovu wa nchi ulikofika ni hatua ya mwisho kwa tawala dhalimu iliyopo kuachia ngazi. INA MISUKOSUKO KAMA ILIVOANZA SASA, waandamanaji kupigwa risasi, wanafunzi kufukuzwa chuo kwasabu ya siasa, kuwafungilia watu kesi za kichochezi na uhaini ila uzuri hapo ndipo inapoishilia. Mola akurehemu uyashuhudie hayo machungu kwa wezi na waharibu nchi CCM.