Waraka wa Joshua Nassari kwa Wanaarumeru - "Uadilifu Utashinda"!

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Mar 10, 2006
33,476
39,995
baruayajoshua.png

Na. Joshua Nassari

MATATIZO YOTE YA KIUTAWALA na kiutendaji ndani ya serikali na taasisi zake mbalimbali ambayo tunayaona katika jimbo letu la Arumeru Mashariki yanatokana na Chama cha Mapinduzi. Hakuna jambo lolote linalohusiana na matatizo ya ardhi, maji, afya, elimu, barabara, usalama, na mazingira ambalo halihusiani na utendaji mbovu wa serikali iliyoundwa na CCM. Chama cha Mapinduzi kinachounda serikali nchini ndicho chanzo, sababu na kisa cha yale yote tunayoyalalamikia kila siku katika jimbo letu.

Uchaguzi wa Ubunge siku ya Aprili Mosi ni nafasi kwa wana Arumeru kuzungumza kuonesha kuchoshwa kwao na mwendelezo huu wa mlolongo wa maamuzi mabovu na utendaji mbaya ambao umedumu kwa miaka zaidi ya hamsini sasa. Kwa wana Arumeru kura hii inayokuja ni nafasi ya kusahihisha makosa ambayo wamekuwa wakiyafanya miaka nenda rudi; ni nafasi ya kusema kuwa “tumefunguka” na sasa tunataka kuanza upya. Ni nafasi ya kuchagua mweleko na mtazamo mpya wa mabadiliko.

Kama wazee wetu walivyokuwa watangulizi wa harakati za uhuru miaka sitini iliyopita; harakati ambazo zilikuja kuthibitishwa na wazee wa Dar-es-Salaam, wazee wa Mwanza , Wazee wa Tabora na Wazee wa maeneo mengine nchini vivyo hivyo sisi wajukuu na vitukuu vyao tunaitwa na historia kuwa watangulizi wa mabadiliko yajayo. Wazee wetu walitambua kuwa mfumo wa utawala ambao ulichukua raslimali zao na kuwaacha wakiwa katika nchi yao ulikuwa ni mfumo wa kupingwa. Wazee wetu walikataa kunyanyaswa; siyo hapa Arumeru tu bali katika ardhi nzima ya Tanganyika ya zamani. Kuanzia Upareni hadi Ungonini, kuanzia Usukumani hadi Uhayani wazee wetu walikataa kuwa wageni katika ardhi yao.

Lakini hawakufikia hatua hiyo hivi hivi tu; walifikia hatua hiyo baada ya muda wa kujitambua wao ni nani hasa. Wakati Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere alipounganisha nguvu za wazee hawa na kuharakisha kupatikana kwa uhuru wazee wetu walijijua kuwa wao ndio warithi halali wa raslimali, utajiri, na nafasi ya utawala katika nchi yao. Wazee wetu walijitambua kwanza kwamba wao siyo watumwa au wageni ambao wanahitaji kuwabembeleza watawala. Hoja ya Mwalimu ilikuwa ni kwamba haki yetu wenyewe kama wana na mabinti wa ardhi hii kujitawala wenyewe. Ilichukua muda hoja hiyo kueleweka lakini ilieleweka.

Leo hii miaka sitini baadaye hoja ya kuwa Watanzania si watumwa, wageni, au wahamiaji katika nchi yao inazidi kueleweka taratibu. Hoja ya zamani kwamba CCM inatakiwa kutawala kwa vile ni CCM bila kujali inatawala vipi imekataliwa kila watu walipopewa nafasi ya kufanya hivyo. Kuanzia Mbeya Mjini hadi Mwanza Mjini, kuanzia Hai hadi Kigoma Kaskazini, kuanzia Karatu hadi Maswa, kutoka Mbozi hadi Musoma Mjini Watanzania wameendelea kukikataa Chama cha Mapinduzi; wameendelea kukataa viongozi wake, wameendelea kukataa siasa zake, naam wameendelea kukata sera zake zilizoshindwa! Wana na mabinti wa Arumeru wanapewa nafasi ya kufanya hivyo pia!

Ni uchaguzi wa kuamua kuanza safari mpya ya kuleta mabadiliko Arumeru Mashariki. Binafsi siwaletei ahadi za mabadiliko bali nawahakikishia kuwa pamoja nami tutajiletea mabadiliko tunayoyataka. Iwe kwenye elimu, iwe kwenye maji, iwe kwenye ardhi na umeme! Tunataka kulirudisha jimbo hili kwa wananchi wa Arumeru Mashariki. Msilirudishe Jimbo kwa CCM kwani hawana hati miliki nalo! Kulirudisha jimbo kwa CCM ni sawasawa na kuamua kumrudishia mwizi ng’ombe aliyekuibia ati kwa sababu atakamua vizuri maziwa! Ati ni sawa na kumrudishia mwizi huyo ng’ombe kwa sababu ameahidi kuwa akipatikana ndama jike atakupa wewe! Kura hii ni kura dhidi ya CCM, ni kura ya kuikatalia CCM uhalali wa jimbo la Arumeru Mashariki; ni kura ya kulirudisha jimbo hili mikononi mwa wananchi wa Arumeru.

Wapiga kura wa Arumeru ambao ni walipa kodi wa Arumeru na Tanzania kwa ujumla mmesikia uongozi wa CCM ulivyo; jinsi ambavyo uko tayari kusema lolote ili wazidi kutawala. Wamejaribu kila aina hoja na maneno ya kejeli. Wamejaribu kutusingizia mengi lakini wameshindwa kwa sababu watu wa Arumeru hawajaanza siasa leo! Siasa za kuwapinga watawala zimekomaa hapa; tunaona fahari hiyo na kwa hili CCM wanahitaji kupewa somo gumu.
Haijalishi nguvu za polisi, haijalishi kubebwa na vyombo vya habari vya umma, na haijalishi kutumia raslimali za serikali – kwa kutuma mawaziri – kuja kufanya kampeni. Mwisho wa siku sauti ya mpiga kura wa Arumeru itasikika tena itasikika vizuri kabisa siku ya Jumapili. Uadilifu utashinda, ukweli utashinda, kuwajibika kutashinda naam wana wa Arumeru watashinda kwa kutuma ujumbe usio na utata kuwa sera za CCM zimeshindwa na kukataliwa sasa na daima! Vitisho vya watawala vimefikia mwisho kuanzia sasa na daima! Maneno ya matusi na kufuru yamekataliwa sasa na daima! Ushindi ni wa watu wa Arumeru!

Ndugu zangu, tukianza hapa kama mababu walivyoanza hapa miaka sitini iliyopita tunaipa nchi yetu nafasi; tunatoa mfano kwa wananchi wengine ambao watapatiwa nafasi ya kusahihisha makosa yao miezi inayokuja. Kwamba CCM inaweza kuangushwa hata ikimleta shetani na bakora yake! CCM itakataliwa hata kama itakuja na mavuvuzela yaliyao ufisadi na yaliyoshika matarambuta yenye kuongopa “tunawependa tunawapenda”.

Ninawaalika kwa siku hizi mbili zilizobakia pamoja na kuvaa nguo za rangi ya chama kuvaa mashati meupe au nguo nyeupe, kubeba vitambaa vyeupe vyenye kuonesha ushindi wa uadilifu! Tuvipepee bila haya, tuje navyo kwenye mikutano kwani ushindi wetu ni dhahiri. Tuweke vitambaa hivi vyeupe na vile vyenye rangi ya chama kwenye magari yetu, kwenye nyumba zetu, kwenye miti, kila tunapoweza ili CCM wajue kuwa tayari Jimbo la Arumeru limeshachukuliwa!

NI ushindi wa kishindo utakaoacha mwangwi kwenye ofisi za CCM kuanzia Arumeru hadi Dodoma! Ndugu zangu, tayari tumeshashinda katika mioyo ya watu wetu, tunachoenda kukifanya Jumapili ni kuupeleka benki ushindi wetu! Kila mmoja wetu aliyejiandikisha kupiga kura aje na kitambulisho chake, piga kura yako kwa furaha, fuata sheria zilivyo na uwe tayari kulinda kura yako! Ukishapiga kura kaa umbali wa mita 103 kutoka kituoni kuhakikisha kuwa kura yako inahesabiwa. Haina maana kupiga kura kama haitahesabiwa!

Tupige kura kwa amani, kwa kujiamini, na kwa kuthubutu! Ushindi ni wetu! Waambieni CCM, asante kwa matusi na kejeli lakini kwaheri! “Tunaiambia CCM bai bai, baibai tunachagua CHADEMA!” Nipigieni kura mimi mgombea wenu, mtoto wenu, rafiki yenu na mwenzenu ili kwa kutumia kila uwezo na kipaji nilichojaliwa na Mwenyezi Mungu niwaongoze mahali penye nyasi nzuri kuliko kwenye ukame ambao CCM imewaacha kwa miaka hamsini ya maumivu.

NB: Unaombwa kuusambaza waraka huu kwa wapiga kura wengi kwa kadiri unavyoweza. Kati siku hizi tatu tunaweza tusiwafikie watu wote kwa mikutano lakini ukurasa huu mmoja unaweza kuwafikia watu wengi. Tunawaomba watu wa Arusha watusaidie kutoa nakala chache ambazo zinaweza kugawiwa kwa wananchi wa Arumeru. Fanya uwezalo wakati sisi tunafanya tuwezalo!

My Take: Natumaini katika mtanange huu wa demokrasia ni fikra tu ndio zinazogombaniwa; nani na chama gani kinawakilisha fikra mpya hilo ndilo swali litakalojibiwa Jumapili.
 
Attachments

  • joshuabarua.pdf
    85.9 KB · Views: 173
Siwapendi CCM lakini Siwaamini Chadema..

Chadema ni masifa yao ni chuki zao wakishindwa itakuwa vema wapunguze ngebe
 
''The hardest thing about any political campaign is how to win without proving that you are unworthy of winning''
 
View attachment 50402

My Take: Natumaini katika mtanange huu wa demokrasia ni fikra tu ndio zinazogombaniwa; nani na chama gani kinawakilisha fikra mpya hilo ndilo swali litakalojibiwa Jumapili.
Tatizo kubwa MKJJ ni uelewa. Sasa hivi siasa za Tanzania zimefikia pahala watu wanagombania wapiga kura kama Mungu na Shetani! Huwezi amini watu wazima na akiri zao wanaweza kupanda jukwaani na kutetea upuuzi badala ya kujenga hoja.
 
Yeah, mara nyingi ni kwa sababu hakuna hoja. Bahati mbaya kwa upande wa CDM wangeweza kabisa kwenda na hoja za kuikataa CCM; CCM wangebakia na hoja za matusi..
 
View attachment 50402

My Take: Natumaini katika mtanange huu wa demokrasia ni fikra tu ndio zinazogombaniwa; nani na chama gani kinawakilisha fikra mpya hilo ndilo swali litakalojibiwa Jumapili.
Mzee Mwanakijiji, asante kutuletea waraka huu wa "joshuabarua", nimeikumbuka "Cheche za fikra" mpaka ile closing yake "Unaombwa kuusambaza waraka huu kwa wapiga kura wengi kwa kadiri unavyoweza. Kati siku hizi tatu tunaweza tusiwafikie watu wote kwa mikutano lakini ukurasa huu mmoja unaweza kuwafikia watu wengi. Tunawaomba watu wa Arusha watusaidie kutoa nakala chache ambazo zinaweza kugawiwa kwa wananchi wa Arumeru. Fanya uwezalo wakati sisi tunafanya tuwezalo!".

Asante kwa kutoka kwenye kuandika tuu na kuingia kwenye kutenda!. Huu sasa ndio usaidizi wa kweli kwenye ground zero!. Sasa nimeamini na nimekubali, you don't necessarily have to be there, to play active role on ground zero!.

Asante ya mwisho ni ya utendaji kama wa "Masiha", tenda wema "credits" kwa wengine!.

Ubarikiwe sana!.

Pasco.
 
kwa kweli leo CDM walikaa kijeshi sana; wamenitia moyo sana. More united, more focused and ready to shake the powers that be! Nimewaonea huruma wameenda kulala watu saa kumi alfajiri
 
kwa kweli leo CDM walikaa kijeshi sana; wamenitia moyo sana. More united, more focused and ready to shake the powers that be! Nimewaonea huruma wameenda kulala watu saa kumi alfajiri

Na yakitokea matokeo tofauti na matarajio yangu, then its something to do na waraka huu!.

Tunaweza kufanya quick donee ili kuwajengea uwezo, walio ground zero kuprint as many copies as they can!.

God Bless You!.
 
Sijui bana sisi wengineyetu ni machotu..
 
Nadhani njia pekee ya kuweza kushnda chaguz ndgo ama chaguz zte ni kuhakikisha vjana wote wanapata elimu ya uraia ya kutosha namna ya kuleta mabadiliko ktk nch kwa namna ya kiutawala na kiutendaji, na watafanyaje ni kwa kupga kura zao, uwing wa watu ktk mikutano ci kigzo cha watu hao kwamba watapga kura wote, kwn vjna wa leo weng hawna vitambulisho vya kupga kura, la hasha bas mfumo wa kuendsha zoez la upgj kura ubadilishwe.
 
Back
Top Bottom