Waraka wa jamii

Kamuzu

JF-Expert Member
Oct 14, 2008
993
298
Naam wana JF, kuelekea uchaguzi mkuu ujao, tumeanza kuona na kusikia mengi, mojawapo ni hili la nyaraka za madhehebu ya dini kuelekeza wananchi juu ya nini cha kuzingatia/kifanyike wakati wa uchaguzi.

Tulianza na waraka wa wakatoliki na sasa wa waislamu na pengine kuna wataofuata.

Ni wazo langu basi kwamba sisi kama wana JF ambao tumeweza kujipambanua na kujiweka mbele katika mijadala mbalimbali inayohusu siasa ya nchi yetu, haki, wajibu na matarajio ya wananchi wa tz, nasi tuna wajibu wa kutimiza katika hili.

Natoa wito kwenu yeyote anayeweza kuifanya kazi ya kuandaa waraka wa Jamii kwa ushirikiano na wengine humu, na kurejea mabandiko mbalimbali yaliyowahi kuwekwa humu jamnvini na kufanya walau kazi isiwe ngumu sana. Waraka uandikwe kwa lugha ya kiswahili na uguse maeneo muhimu ili kuziba pengo lililopo kwenye nyaraka zilizotangulia.

Kabla sijafika mbali sana naomba kuwasisha, nikiamini Mods watajdili hili na mkiona kuna umuhimu, waandishi na wachangiji ni wengi -Mzee mwanakijiji usichoke.

Mwisho ni kwamba WARAKA huo usitolewe Bure, uuzwe kwa gharama nafuu ili kuwafikia wengi na fedha yote itakayopatikana itunishe mfuko wa JF ili kuendeleza mapambano ya HAKI.

...................................................

Amani yetu inatumika vibaya!
 
Back
Top Bottom