EasyFit
JF-Expert Member
- Jul 4, 2011
- 1,269
- 1,082
Waraka wasambazwa
Watu wasiojulikana jana walisambazwa waraka ambao unadaiwa kuandikwa na wabunge wa CCM ambao wanapiga vita ufisadi wakitaka mgombea wa CCM, Sioi Sumari asichaguliwe kwani atawaongezea nguvu mafisadi kuelekea Uchaguzi Mkuu mwaka 2015.
Waraka huo ambao jana ulikuwa ukisambazwa katika mitaa mbalimbali ya Usa River na kwenye mikutano ya kampeni ya Chadema na CCM, una kichwa cha habari kisemacho "Chama cha Mapinduzi na Kamati maalum dhidi ya ufisadi."
Katika waraka huo ambao haujasainiwa na mtu yeyote unadaiwa kutumwa kwa wananchi wa Meru na wabunge wa CCM ambao picha zao zimeambatanishwa.
"Tunawaandikia waraka huu kwa kuwa tunaamini kabisa kwa kufanya hivyo tunamfurahisha Mungu na kuwanusuru na kiu ya damu ya baadhi ya viongozi wa nchi hii. Mafisadi hawa wameshindwa kabisa kuacha ufisadi na sasa wanatumia fedha walizowaibia Watanzania…" inasomeka sehemu ya barua hiyo.
Kadhalika waraka huo unamtaja mmoja wa makada wakongwe wa CCM (jina tunalihifadhi) kwamba ameamua kutunisha misuli yake na kuhakikisha Sioi anashinda ubunge Arumeru, lengo likiwa ni kuonyesha kwamba ana nguvu zaidi kwa kutumia fedha zake.
Chadema jana walikana kuufahamu waraka huo na kusema kuwa wenye uzoefu wa kuandika nyaraka za aina hiyo ni CCM.
Mkuu wa operesheni wa uchaguzi huo wa Chadema, John Mrema alisema: "Sisi hatuwezi kuandaa waraka kama huu, haya ni mambo ya CCM wenyewe."
Meneja Kampeni wa CCM, Mwigulu Nchemba hakupatikana jana kuzungumzia waraka huo.
Source: Mwananchi.