Waraka toka Ikulu: Hebu tuujadili...

NI sahihi!

Ikulu ni mahala pakubwa na panatawaliwa na sheria. kama kosa limeonekana hakuna haja ya kutoa taarifa bali ni kukamata na kumfungulia mashitaka. ikulu inahangaika nini kutoa taarifa kwa jambo kama Hili? tunatataka taarifa kama zihusuzo kushuka kwa thamani ya shilingi mfumuko wa bei n.k
 
Huu waraka haupo kama umetoka Ikulu, una makosa makosa karibu kila aya. Bila shaka First Lady alishaonyesha nia ya kuwa na hilo jukumu, sasa kutokana na mambo ya WAMA yanavyowaendea, wanaamua kuikacha hii. Kama hajawahi jihusisha, basi tutaona hatua za ikulu kwa huyu bwana!!
 
KUNA MZEE MMOJA MIAKA YA 70 BUSH KWETU ALIKUWA TAJIRI WA KUTOSHA AKAWA NA UBARIKIO WA MTOTO WAKE AKATUTANGAZIA MGENI RASMI ATAKUWA MWL NYERERE WAKATI TUNASUBIRI SIKU YA SHEREHE SI YEYE WALA MWL TULIYEMWONA MPAKA MIAKA YA 80 NDIPO TULIPOMWONA KACHOKA MBAYA.

ikulu ni mahala patakatifu.
 
Yaani hii kurugenzi ya mawasiliano ya ikulu ni bora ibadilishiwe jina na kuwa kurugenzi ya mawasiliano ya familia ya baba nanihii
 
THEUNITED REPUBLIC OF TANZANIA

DIRECTORATEOF PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS
Telephone: 255-22-2114512, 2116898
E-mail: ikulumawasiliano@yahoo.com
press@ikulu.go.tz
Fax: 255-22-2113425

PRESIDENT’S OFFICE,

THE STATE HOUSE,

P.O. BOX 9120,

DAR ES SALAAM.

Tanzania.
TAARIFAKWA VYOMBO VYA HABARI
Katika siku chachezilizopita, Mkurugenzi wa Shule ya Chekechea ya Moses Nursery ya Yombo Vituka,Dar es Salaam, Bwana Moses Kabambara amekuwa anasambaza kadi kwa watu binafsi,makampuni, mashirika na ofisi za ubalozi zilizoko nchini akisaka michango kwaajili ya ununuzi wa madawati na ujenzi wa madarasa na uzio wa shule yake.

Katika kadi yake yakuomba michango na kwenye taarifa anazozisambaza kwenye vyombo vya habari,Bwana Kabambara anatumia jina la Mheshimiwa Salma Kikwete, Mke wa Rais waJamhuri ya Muungano wa Tanzania na Nembo ya Taifa kuonyesha kuwa Mheshimiwa Mama Kikwete ndiye mchangishaji na Mgeni Rasmi kwenye matembezi ya shughuli yakuchangia maendeleo ya shule yake.
Aidha, amekuwa anadai kuwa Mama Kikwete ndiye atakuwa Mgeni Rasmi kwenye shughuli hiyo.

Tunapenda kuchukua nafasi hii kuuarifu umma wa Tanzania kama ifuatavyo kuhusu suala hili:
(a) Kwamba Mama Salma Kikwete kamwe hajapata kuridhia kuwa Mgeni Rasmi katika matembelezi hayo
(b) Kwamba Mama Salma Kikwete hajapata kukubali kuwa mchagishaji ama hata mshiriki wa aina yoyote katika uchangishaji fedha kwa ajili ya shule hiyo.
(c) Kwamba Bwana Kabambara anaufanyia udanganyifu umma ili uweze kuamini kuwa Mama Salma Kikwete amekubali kushiriki katika shughuli za uchangiaji fedha shule yake.

Tunapenda kupitia taarifa hii kuutahadharisha umma kuwa macho na vitendo vya baadhi ya watu wanaotumia majina ya Viongozi wa Kitaifa kuchangisha ama kukusanya fedha ama hata kufanya mambo mengine yenye kulenga manufaa au maslahi binafsi. Hili ni kosa la jinaimbali na kwamba vitendo vya namna hii husababisha usumbufu kwa jamii na kwa viongozi husika.

Imetolewa na:
Kurugenziya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu.
Dares Salaam
.

8 Mei, 2012

Je: NI SAHIHI KWA IKULU KUTOA WARAKA WA AINA HII?

Hii kurugenzi imepoteza mvuto.mbona ile ziara ya kwenda kutembelea saloon magomeni hawakutoa tamko.
Mytake:kurugenzi ya habari ikulu imebaki kutoa matamko ya kiswahili kama ilivyo ofisi za balozi zetu nje kuwa na kazi ya kupokea viongozi wa ccm.
 
Mkuuu umeniwai.Pale ikulu kuna tatizo moja kuwa wanakimbilia kujibu hoja za kipuuzi sana kuliko majibu yanaikabili serikali yetu.Mbona awajibu kama serikali imefirisika.Hapa ni kukimbia tatizo na kufunika aibu

kajifunze tofauti ya msemaj wa serikali na msemaj wa Ikulu utaacha kubwabwaja,nendeni mkajifunze kazi za Mnikulu mtajua mama salma anatofauti na kimada wa katibu wenu
 
Ridhwan jk kaingia kwenye record ya kuwa Mtanzania wa kwanza kufanya Part ya harus yake ndan ya viwanja vya Ikulu ya Tanzania
 
hebu muwe waelewa wa mambo kabla ya kuweka thread hivi hujui fist lady katika nchi ni nan!?na anasemewa na nani!?je hata kupewa ulinzi unaona sio haki kwahy,una ulinzi na magari zaid ya matatu ya eskoti,akichafuliwa firslady imechafuliwa ikulu,elewen na mrudi kusoma political science.
 
kajifunze tofauti ya msemaj wa serikali na msemaj wa Ikulu utaacha kubwabwaja,nendeni mkajifunze kazi za Mnikulu mtajua mama salma anatofauti na kimada wa katibu wenu

Ukiona mtu haelewi, jaribu kumuelewesha basi mkuu
 
akichafua first lady, imechafuliwa ikulu yote, akiiendesha ikulu kama kijiwe cha udaku na parties, ni ikulu yote, pakifanyika biashara za wama, ni ikulu yote, pakifanyika sehemu ya washikaji kunywea gahawa na kupikia misheni town za utapeli wa nchi, ni ikulu yote...pakifanyika mahali pa kuteua wahuni kama mkuchika, maghembe, malima nk, ni ikulu yote!
 
Hii ni kudhihirisha kuwa ikulu ni mali ya familia, aliyetoa tamko hili kwa vyovyote aliagizwa na mama mwenyewe kufanya hivyo. "Alisema nawaagiza mara moja mtowe tamko kukanusha taarifa hizi".
 
huu sasa ni upuuzi; kama kweli walichoandika Ikulu ni cha kweli kutoa tamko ni kuthibitisha hofu yetu sisi wengine. Kuna watu hawana kazi isipokuwa kufikiria kila siku watoe tamko gani. Ina maana kweli hakuna mtu huko Ikulu ambaye angewashauri NINI hasa cha kufanya badala ya kutoa tamko?

Hebu toa mfano wa ushauri.
 
Boss wa Boss wenu.
.....
Tanzania,Tanzania,nakupenda kwa moyo wote;
Nchi yangu Tanzania,Jina lako ni tamu sana;
Nilalapo nakuota wewe,niamkapo ni heri mama we;
Tanzania,Tanzania,nakupenda kwa moyo wote;

Tanzania,Tanzania,watu wengi wanakusifu;
Siasa yako na destruri,ilituletea uhuru;
Hatuwezi kusahau sisi,mambo mema ya kwetu hakika
Tanzania,Tanzania,nakupenda kwa moyo wote.

..hivi mbona hii taarifa inaonyesha kama huyu "BOSS wa BOSS wetu" alishaingia "king", and I am convinced huyo jamaa "mwenye shule" hawezi fanya deal kubwa kama hivi (kwenda ubalozi bile knowledge) ya huyu mother (WAMA)..hebu tusubiri labda huu waraka bado Bwana Moses Kabambara hajaupata, au wamemziba mdomo..tusubiri, ila naipenda sana Tanzania
 
Si wamkamate kama ni kosa la jinai? Hapa kuna kitu kimoja nimekigundua. Huenda huyu jamaa alituma maombi ikulu kuomba mama awe mgeni rasmi na akapata go ahead ya mdomo. Kwenye taarifa sijaona wakikanusha kwamba huyo jamaa hajawahi kumuomba mama kuwa mgeni rasmi.
 
Hivi salima kikwete ni kiongozi wa akina nani nchi hii. Alichaguliwa na wananchi ama ameteuliwa cheo gani nchi hii
 
Hii kurugenzi imepoteza mvuto.mbona ile ziara ya kwenda kutembelea saloon magomeni hawakutoa tamko.
Mytake:kurugenzi ya habari ikulu imebaki kutoa matamko ya kiswahili kama ilivyo ofisi za balozi zetu nje kuwa na kazi ya kupokea viongozi wa ccm.

mama salma ni nani tz?nkisema nchi inaongozwa kifalme 2takataa?anyway kwanini m2 asikamatwe waishie kutoa tamko 2,kwa v2 vyakijinga ndo wanatoa tamko kwa ishu za maana wanapiga chni!
 
Hakuna cha kujadili ni upuuzi mtupu, Miezi michache Mtoto wa Mkulima na mama A. Makinda waliviambia vyombo vya habari RAHISI amebariki posho mpya za wabunge, baada ya wadanganyika kuhoji na kulaani hicho kitendo hiyo hiyo kurugenzi inayoongizwa na INFWACT SALVA akasema RAHISI hajabariki, huku yeye rahisi akikaa kimya, hili wameona wananchi wanaanza kuhoji akaanza kukanusha hanajipya NI RWEYEMAMU na Kuaharuki kwa kiupumbavu, kwani yeye ndio mama Salma, kwanini amsemee, kwanini kwenye act mtu akidanganya anafanywa nini ASITULETEE UPOYOYO WAKE KILAZA MKUBWA HUYO
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom