Radio Producer
JF-Expert Member
- Feb 4, 2011
- 724
- 295
Ndugu Waheshimiwa,
Nawapa pole kwa majukumu hasa vikao vya Bunge vinavyoendelea hapo Dodoma. Nimeandika HATARI kwa sababu ni mambo ya muhimu sana nataka kuwaambieni kupitia jukwaa hili:-
1. Amani- Neno hili sasa limeanza kutokomea mbali sana hapa Tanzania. Tanzania haina amani tena kama ilivyokuwa hapo zamani. Matukio kadhaa yanayoweza kutowesha amani hii ni haya hapa: Mauaji yanayofanywa na Polisi, Waandamanaji wanavyokamatwa na kuwekwa Lumande, Maisha magumu kwa Watanzania, Migomo na migogoro isiyoisha katika vyuo, Ukosefu wa ajira kwa zaidi ya vijana milioni 2.5.
Kiimani machafuko haya yanatimiza maandiko matakatifu katika kitabu cha Mungu, lakini kwanini nyinyi wanasiasa ndio mnakuwa chanzo kikubwa? Mmesahau kuwa maandamano ni haki ya raia? Na yanapotokea haya mbona mmefumba macho? Katika vikao vyenu hapo Dodoma mmejaribu kukemea hata siku moja mauaji haya yanayofanywa na Polisi? Amani mnaitokomeza wenyewe, gharama yake ni kubwa ambayo inaweza kuwaumiza hadi nyinyi. Ikitokea vita nyinyi mtakimbilia wapi? na mkikimbia mtakimbia na nyuma zenu? Tuacheni kusema Chama fulani kinasababisha uvunjifu wa amani, ni chama kipi kimefanya fujo na kuwapiga wanachi hadi wakafa? Mbona mnajificha peupe jamani?
DAIMA MTAILIPA DAMU YA WATU WASIO NA HATIA.
Leo yatafanyika haya na mtapongeza sana mauaji hayo tena mkiwa bungeni? Angekuwa ndugu yako kapigwa na Polisi mngefurahi na kupongeza? sisi raia tunayasikiliza sana hayo mnayoyaongea bungeni, nashangaa wengine wanaongea hadi unajiuliza kweli huyu ni Mbunge katumwa na wananchi? Damu ya watu wasio na hatia mtailipa tu hata mnaoshabikia adhabu yenu ipo.
2. Suala la Katiba- Nazidi kusikitika sana maana muda mwingi mnatumia malumbano tu hakuna mnachojadili kuhusu katiba. Wengine hatuelewi hata maana ya katiba, mngetuelewesha kwanza. Ila kwanini mara ya kwanza mliahidi kuifanyia mabadiliko na leo mmeirudisha vile vile? Mbona mnatufanya wajinga jaman sisi wananchi tuliowapa kura zetu mkatusemee na kutuletea haki zetu. Wabunge wa CCM wasikilizeni wenzenu, nadhani hao wote sio vichaa wanakitu cha maana, mkilazimisha tu yatakuja kuwatokea puani kumbukeni mna watoto, wajukuu, na hata ndugu zenu, mnadhani wao watasalimika na katiba yenye masilahi ya mafisadi?
Nimeshindwa kuendelea kuandika maumivu moyoni yamezidi, Yaani kweli wanasiasa mmeamua kutufanyia hivi? Mali zetu mnatupora halafu mnatuua tena mnataka mtugandamize katika suala la katiba?? Damu ikimwagika itakuwa juu yenu, Kumbukeni na nyinyi ni watu tu, ipo siku mtakufa, Je, Mnaweza kuingia mbinguni (Imani)? Huu ni ujumbe wenu wabunge, ikibidi usomeni bungeni ila kumbukeni sana nyinyi pia ni wanadamu, namaliza maneno machozi yananitoka Mungu ndiye hakimu wa Kweli, ipo siku mtakumbuka!!!!
Radio Producer.