Waraka kwa mwenyekiti CHADEMA: Sio wapiganaji wote wana hekima!

Muheshimiwa mwenyekiti kamanda wetu Freeman mbowe,
Najua unapita humu ndani na wapambe wako wengi tuko nao
Mimi ni mwanachama wako mtiifu na tuko pamoja kuikomboa nchi hii kutoka kwa hawa mapaka pori yanayotuibia hadi vifaranga vyetu yaani Chama Cha Magamba.
Nimekuandikia waraka huu baada ya kuona kazi kubwa unayoifanya ya kunyoosha maneno. Ajali ya leo ya Nasary kusema Kaskazini itajitenga kama CCM wakiendelea na ubishi ni ajali mbaya sana kisiasa na nina hakika CCM wamepata pa kuanzia. Lakini nakumbuka hii si mara ya kwanza. Mikutano yote niliyohudhuria hapa Chadema Square Arusha mara nyingi umekuwa ukisimama na kukemea maneno makali na ya mzaha yanayoletwa na wapambanaji wako. Ukweli ni kwamba huwa unajipambanua kama Baba sana. Busara zako huwa zinasaidia sana. Lakini matatizo haya hayakomi. Kwanini?
1. Si kweli kwamba kila mkutano wa CDM lazima wote walioko meza kuu waongee. Ninyi mnajuana kiwango cha hekima na ingekuwa busara wale wenye hekima tu ndio wakapewa nafasi. Mfano leo Diwani aliyetoka CCM - Mawazo ameonyesha kabisa kwamba bado ana hulka za kilusinde za CCM. watu wengi hatukupendezwa na maneno yake. Hata Ole millya hakuvutia umati wa watu bado busara ni ndogo sana.
2.Kuna watu wanaweza kuwa na busara ya kutenda lakini sio busara ya kuongea mbele za watu. Mimi naamanini utendaji na uwezo wa kuongea mbele ya hadhara ni vitu viwili tofauti.
3. Kuna watu wanafaa kwa propaganda za wakati na mahali fulani tu mfano Nasary na Lema. Wao ni wazuri sana nyakati za uchaguzi.
Kwa maelezo haya mafupi mwenyekiti ningeomba
A. CCM wanachuo chao cha Magogoni cha siasa - CDM pia tunapaswa kuwa na mahali tunapowapikia watu wetu ili wawe wanasiasa bora zaidi.
B. Kuwe na semina nyingi za ndani ili kuwekana sawa na kukumbushana namna ya kuwasilisha hoja bila mafarakano ya maneno ambayo unapaswa kukemea kila mara.
C. Uongozane na watu wenye uwezo wa kuwasilisha hoja kwa nguvu lakini kwa taratibu bila jazba na busara ikitawala mfano John Mnyika na Hallima Mdee ili vijana wanaoinukia wapate mfano (role models) wa kujenga hoja.
AHSANTE KWA KUNISIKILIZA


Very, very valid points. Nina uhakika wanachama wengi wa hiki chama chenu makini wataafikiana nawe.
 
Siasa ni mchezo mgumu, ukinukuu kila kitamkwacho yaweza kukusumbua, wamachinga mbeya wanamwita Joseph Mbilinyi a.k.a sugu kuwa ni rais wa mbeya! Je, ndivyo ilivyo?? Ccm imetamka mengi sana mabaya kwa wapinzani, waache watu wapumue juu yao, watu wa hovyo sana hao. Ila cdm isipite viwango, rais Jk ni rais wa Tz na Arumeru mashariki pia! Dogo janja, acha upuuzi wa kitoto.

Nadhani hata matendo ya jk ndo yanafanya wamwonyeshe dharau kubwa hivi tena mbele ya hadhara
 
Nassari kwa niaba ya sociologist wote, wenye kuamini umoja ni nguvu utengano ni dhaifu, omba radhi kwa wananchi na wapenzi wako wote walioko tanzania nzima. kumbuka, ushindi wako si juhudi zako, bali ni juhudi za wadau na wanaharakati tanzania nzima. michango iliyotolewa, haikuitoka arusha pekee, ilitoka tanzania nzima hadi zanzibar walikuchangia. hivyo tanguliza busara zaidi kuliko jazba. Karl Marx, Spencer, A. Gidens, A. Frank, Durkeim, Weber Max, Hobert, na scholars wengine, hawajakufundisha uliyoyatamka.

Pili ni kwa Dr. Slaa. Maneno yako uliyoongea Mwanza, yanawaweka askari hadi wapenzi wa CHADEMA wanapopita mitaani, baadhi ya vijana, tena wengi walevi wanatishia, tutavamia kituo, na tutaanza na nyie.

Sakata la ILEMELA, wanafahamika waliolisimamia, kwa nini hao wasishughulikiwe na badala yake kutangaza kuvamia kituo cha polisi ambacho kwa wakati mwingine unakitaka kikusaidie mambo yako?

hapa slaaa naye aliteleza kama nasari

Ujue uhamuzi kama huu unasabishwa na police wenyewe wapokuwa hawafuati haki bali matakwa ya ccm ama shinikizo la wenye hela!
 
Asante mkuu,. Msamehe nassari aliteleza,. Hata mi nilikuwepo nikastuka,. Nassari atakwelewa
 
Nasari funfuka na jitokeza hadharani uombe msamaha maana umewaangusha na kuwavunjamoyo wengi kumbuka mtu mwenye busara hutambua makosa yake na kuomba radhi na mpumbavu hubaki na kiburi chake pia kuomba radhi huongeza heshima na asiyesikia la mkuu huvunjika guu
 
muheshimiwa mwenyekiti kamanda wetu freeman mbowe,
najua unapita humu ndani na wapambe wako wengi tuko nao
mimi ni mwanachama wako mtiifu na tuko pamoja kuikomboa nchi hii kutoka kwa hawa mapaka pori yanayotuibia hadi vifaranga vyetu yaani chama cha magamba.
Nimekuandikia waraka huu baada ya kuona kazi kubwa unayoifanya ya kunyoosha maneno. Ajali ya leo ya nasary kusema kaskazini itajitenga kama ccm wakiendelea na ubishi ni ajali mbaya sana kisiasa na nina hakika ccm wamepata pa kuanzia. Lakini nakumbuka hii si mara ya kwanza. Mikutano yote niliyohudhuria hapa chadema square arusha mara nyingi umekuwa ukisimama na kukemea maneno makali na ya mzaha yanayoletwa na wapambanaji wako. Ukweli ni kwamba huwa unajipambanua kama baba sana. Busara zako huwa zinasaidia sana. Lakini matatizo haya hayakomi. Kwanini?
1. Si kweli kwamba kila mkutano wa cdm lazima wote walioko meza kuu waongee. Ninyi mnajuana kiwango cha hekima na ingekuwa busara wale wenye hekima tu ndio wakapewa nafasi. Mfano leo diwani aliyetoka ccm - mawazo ameonyesha kabisa kwamba bado ana hulka za kilusinde za ccm. Watu wengi hatukupendezwa na maneno yake. Hata ole millya hakuvutia umati wa watu bado busara ni ndogo sana.
2.kuna watu wanaweza kuwa na busara ya kutenda lakini sio busara ya kuongea mbele za watu. Mimi naamanini utendaji na uwezo wa kuongea mbele ya hadhara ni vitu viwili tofauti.
3. Kuna watu wanafaa kwa propaganda za wakati na mahali fulani tu mfano nasary na lema. Wao ni wazuri sana nyakati za uchaguzi.
Kwa maelezo haya mafupi mwenyekiti ningeomba
a. Ccm wanachuo chao cha magogoni cha siasa - cdm pia tunapaswa kuwa na mahali tunapowapikia watu wetu ili wawe wanasiasa bora zaidi.
B. Kuwe na semina nyingi za ndani ili kuwekana sawa na kukumbushana namna ya kuwasilisha hoja bila mafarakano ya maneno ambayo unapaswa kukemea kila mara.
C. Uongozane na watu wenye uwezo wa kuwasilisha hoja kwa nguvu lakini kwa taratibu bila jazba na busara ikitawala mfano john mnyika na hallima mdee ili vijana wanaoinukia wapate mfano (role models) wa kujenga hoja.
Ahsante kwa kunisikiliza

umenena vema
 
Dogo hata mwezi hana toka kuwa mbunge kaishaanza kutoa kauli za kuligawa taifa.
 
Hiki chama kimegeuzwa kuwa chama cha MATEJA, Walevi walioshindikana, Wahuni wote, pia na Vijana wadogowadogo ambao hata ulingo wa siasa hawaujui hasa kwa hawa makamanda wa huku mitaani (Kwa wale wakazi wa Dar hebu angalia wanachama wake maeneo ya Tandale, Tandika, kinondoni Duh inauma, na si huko tu hadi mikoani),sasa kisipoangalia kitapoteza umaarufu. Maana hata mimi ni mwanachama, lkn pindi kunapokuwa na mikutano ya hiki chama chetu cha CDM, matukio ya ajabu yamekuwa yakitokea mtaani hasa baada ya mikutano kuisha. Kweli najisikia vibaya sana unapoona mtu fulani mwenye heshima zake anatukanwa na kamanda mlevi. Ni aibuuuuuuu!!natamani kurudi kwa wazee wa magamba maana naanza kuona wana afadhali.
 
Napenda kumpongeza Mbowe kwa kauli zake za hivi karibuni.....amekuwa akitumia busara kubwa na utulivu wa juu wakati wa kuongea!
Hata mimi naungana na mapendekezo ya uwepo wa malezi na mafunzo ya vijana hata wanachama wa CDM kuhusu mwenendo na tabia za ki-chama.
Tujifunze kuongea kwa kuchagua kama Mnyika na Zitto kabwe!
 
Nasari nadhani unajua psychology ya mtu ambaye ni Extraverts na ambaye ni Introverts, sasa wewe ukiwa jukwaani jaribu kuwa Sensor (show details, facts and examples) Mimi hapa mtaani nimenywea maana ni ngome ya ccm, na yote hii ni wewe badala ya kupanga mambo mawili tu ya msingi ukaze nayo ni unaweweseka redbuls zimekuzidi, narudia kwamba mambo ya JK waachie Mbowe na Dr. Slaa, mambo yako na vijimaneno tunakereka, last week kwenye mechi ya Yanga na AFC umesumbua ukawa kituko mara ujichanganye katikati ya visichana then unatuambia tusikuonee wivu hujaoa, so silly, naijutia kura yangu wewe ni Lusinde wa cdm, halafu tunataka ardhi u have to pay the prize, na hao wanaokutetea we mtoto kilichokupeleka kuomba kura will not only cost u bt cdm as well.
 
Kitu ambacho nakiona, Nassary bado anafuraha ya kuwa Mbunge na hiyo inamfanya ajisahau. Anatakiwa a-control emotions zake. Napia anatakiwa kutambua kwamba baada ya Lema kuvuliwa ubunge na mahakama alipewa kazi ya kuangalia jimbo la Arusha mjini na chama kwa maana ya kuwatia moyo watu wa A-town lakini uangalizi wake haupo kisheria kwahiyo asitake pia kuhalalisha jambo hilo na kuanza kutoa maamuzi ya mambo yanayohusu A-town
 
Kwa macho ya "rohoni" naliona dubwana fulani hivi kuuuuuuuuuuuubwa lenye bonge la tumbo likiwa limevalia rangi ya majani ya mgomba likichungulia uzi huu kwa furaha ya ajabu yenye nia ovu ndani yake! Ni li nani hilo?
 
Tuwe wakweli tuuche ushabiki Chadema kuweni makini na kauli za wabunge wenu naona Dogo kaishaanza kujisahu hata mwezi bado.

Watu mnatetea eti bado mtoto ndio maana kasema hivyo kama anajiona bado mtoto kwa nini aligombea ubunge.

Kama suala utoto mbona yule mbunge wa NCCR Mageuzi ni mtoto lakini yupo makini na kauli zake.
 
ni funzo kwake na kwa wote wanaotamka maneno bila kufikiri unaweza ukatamani sana kitu fulani lakini upime upo katika wakati gani na unaongea na watu gani, unajua nasari anaweza kuongea hivo ili awafurahishe wananchi ila anashindwa kufikiri kuwa yupo wapi na akina nani wanamsikiliza na nashindwa kujua kuwa kuna mizani inapima maneno yake na pia kuna watu wanaoitamani nafasi aliyonayo,mimi naona liwe funzo tu kwake na tumsamehe ila akue kifikra hilo tu basi NAWAPONGEZA WANA CDM KWA KUONESHA TUMEKUA NA HATUNA UVUMILIVU KWA UPOTOSHAJI WA AINA YOYOTE SIJAWAHI KUONA CHAMA KITAMU KAMA CDM SAAAFI ALUTA KONTINUA MAPAMBANO YANAENDELEA ni mimi mbunge mtarajiwa wa MONDULI
 
kiongozi anapopanda jukwaani ni lazima ajue ni kipi cha kuwaambia wafuasi wake na ipi ni miiko anayopaswa kuizingatia awapo jukwaani licha ya hamasa kubwa na muitikio chanya anaoupata toka kwa wasikilizaji wake. inawezekana kabisa Mhe. Nassary ametamka maneno hayo kuwafurahisha wasikilizaji ambao walikuwa na hamu kuambiwa hivyo na kiongozi wao.

amefanya kosa kubwa sana na anapaswa kuamba radhi kama alivyowahi kufanya Marehemu Regia Mtema (RIP) kutokana na kauli aliyoitoa bungeni.!!

kwa muono mwingine: ni kiashiria kuwa CDM ni mkusanyiko wa makundi ya wanaharakati yenye malengo tofauti tofauti...!!
 
Tuwe wakweli tuuche ushabiki Chadema kuweni makini na kauli za wabunge wenu naona Dogo kaishaanza kujisahu hata mwezi bado.

Watu mnatetea eti bado mtoto ndio maana kasema hivyo kama anajiona bado mtoto kwa nini aligombea ubunge.

Kama suala utoto mbona yule mbunge wa NCCR Mageuzi ni mtoto lakini yupo makini na kauli zake.

Mkuu sidhani kama kuna asiye mkweli katika hili tukianza na Mwenyeki Mbowe jinsi alivyokosoa na kukemea jana on-the-spot. Hata michango mingi katika uzi huu imetolewa kwa namna ya kuonya, kukosoa, na hata kurekebisha. Sijui ni ukweli gani zaidi unaoutaka?

Kweli, mimi binafsi nakubali kabisa dogo kachemsha lakini uzuri naamini atajirekebisha na ikibidi atatafuta jukwaa mahsusi la kuombea msamaha. Na huo ndio uungwana tofauti na magamba ambao kukubali kukosolewa na kukosoana kwao ni ndoto.

Kumbuka kauli za Mkapa na Lusinde na jinsi zilivyopigiliwa chapa na Mukama. Kumbuka kauli za vijana kushikishwa ukuta zilizowahi kutolewa na watu wazito huko magambani; nani aliwahi kuzikemea?

At least kwa hili la dogo na jinsi Chadema na mashabiki wao walivyo-react inaonesha umakini wa hali ya juu. Hata hivyo nakupa big up kwa kuongea point kwenye post hii.
 
naungana na wapiganaji wenzangu wote kwamba CHADEMA sasa ni chama kinachokaribia kuchukua dola, ni lazima tuoneshe ukomavu wa kisiasa, busara na hekima. lah sivyo tutapoteza uaminifu kwa wananchi ambao tayari wameshajitoa kukisuport chama! tuwafunde wanasiasa wetu, tushiriki katika shughuli nyingi za kijamii haswa vijijini, tufungue matawi mengi zaidi mijini na vijijini kueneza elimu ya uraia na kukipeleka chama kwa wananchi kwani M4C yenye mafanikio inatakiwa kuanzia vijijini.
 
umenena vema

Mi ni mpenda mageuzi na mpenzi mkubwa cdm lakini kinachonikera Kila ninapohudhuria mikutano ya chadema hapa arusha ni hizi wimbo zinazopigwa za kidini utadhani upo kwenye mikutano ya upako au kakobe tukumbuke mikutano ya siasa sio ya kidini na wafuasi wa Chama wana dini zao na Chama hakina dini hii inawapa shida Sana wafuasi wasio wakristo. na kuanza kujiuliza Kama cdm ni Chama cha wananchi wote pls tunaomba hili lishulikiwe napa Arusha Tunajua mbunge wetu mheshimiwa lema ni mlokole lakini nataka nimkumbushe mbunge wangu lema kua wote unaowaongoza sio wakristo cdm isifanye makosa ya cuf ya kuamini madhehebu moja inaweza kukupa kura za kutosha kuchukua dola!
 
Back
Top Bottom