collezione
JF-Expert Member
- Oct 22, 2010
- 352
- 178
- Thread starter
- #21
mengine yote ni safi sana Naunga mkono hoja
Lakini baba hapo kwenye red! Yaani hakuna statement mbovu na iliyoniudhi kama hiyo, na hasa inapotoka kwenye kinywa cha Willy.
Yaani anasikiliza kero?Kusikiliza! Kutoka kwa nani. Yaani hajui? Kutoka US siyo kuwa umetoka sayari nyingine kiasi cha kusahau ulikotoka. Au anataka kusema kuwa hajui mpaka aambiwe? Angekuwa anafanya utafiti namna bora ya kutatua matatizo ya wananchi ningemwona wa maana. Kusikiliza? I have a very low esteem on people with such statements.
Pili collezione usidanganyike na hawa watu wanaotoka ughaibuni, mara nyingi hakuna lolote kabisa. Ni sawa na mtu wa kijijini kama mimi na bibi yangu tunavyodanganywa na watu walioko mijini. Wanakuja na nguo nzuri, perfume na hata dawa ya meno inatuzengua, tunawachinjia kuku, mbuzi na tunaamini hawali vitu dhaifu kama vya kwetu kijijini. Fika uone anakoishi, utalia na kuona aibu. hali ni hiyo hiyo kwa wanaotoka ughaibuni. Nafuu sana wanaosoma, lakini kwa wengine! Mh! Fahamu kuwa hawa wenzetu ni wabaguzi na wanasystem imara ya kupeana kazi, mgeni anaishia kwenye kazi za kibarua kama kusafisha madanguro nk.
Ujenzi wa taifa au hata kusidia wananchi kila mmoja anaweza bora atimize wajibu wake.
kaka nakubaliana na wewe moja kwa moja.. kila mtu inabidi atimize wajibu wake kujenga nchi yetu.
ila hapa kuna kitu kimoja, TZ yetu hii ukianzisha biashara au mradi wowote ule. kama usipotimiza matakwa yao ya 10%. lazima wakubwa wenye uroho na pesa wakudhulumu au wahujumu mtaji wako wote.. Hapo wanasahau kuwa unatoa huduma kwa jamii, na vile vile unatengeneza ajira.
sasa sisi wananchi wa kawaida ni vigumu sana kupenyeza na kufikia malengo, kuliko hawa jamaa. Hata kama una malengo ya kusaidia jamii yako, serikali itakunyanyasa. mwishowe utakata tamaa.
My challenge kwa hawa watu, ni kwamba watumie kutambulika kama si kuogopwa kwao,. ili walete huduma kwa jamii. na sio kukimbilia posho za mjengoni.
asante