Waraka: Kanisa Katoliki laandaa waumini uchaguzi 2010

Status
Not open for further replies.
You tell lies Tk. The Roman Catholic Church does not hold that it is the only true Church. It teaches that it has the fullness of the truth, but it recognizes the existence of varying amounts of truth in other Churches as well. In fact, it teaches that the Orthodox Church is a true Church.

If you have a bone to pick with the Catholic Church, then you should at least inform yourself about its essence first. It is devious of you to simply throw mud at it and hope that some of it will stick.

The Church has remained unscathed by hordes of strong persecutors throughout the centuries. She carries within her a promise, from her founder, that He will be with Her always; unto the consummation of the world!

Huyu ni MUUMINI wa kweli haswa....

Tatizo issue ni Tanzania na mwingiliano wa jamii za kiimani na siasa za nchi...

Hekima kubwa inahitajika hapa ndugu zangu

Omarilyas
 
Si Tanzania tu ambako Mabaraza ya Maaskofu huhimiza umuhimu wa kuchagua viongozi bora. Uchaguzi wa mara ya kwanza wa Tonny Blair ulisaidiwa sana na jarida la "The Common Good" ambalo lilitolewa na maaskofu katoliki wa huko.

Kaka mazingira tofauti,

Uingereza malkia ni kiongozi wa dini hata kama sio mfuasi wa kanisa la katoliki. Lakini pia Uwiano wa kidini ni tofauti sana na sisi hapa. Na vilevile wenzetu wamekomaa kidemokrasia na asasi zenye jukumu za kupunguza athari za mambo haya zipo na zimekomaa....

Sio kwenye demokrasia hovyohovyo kama tulionayo sisi...sio kwenye jamii inayofundisha waumini ubaya wa imani za wengine zaidi kuliko uzuri wa imani zao....

Kuna mtu anasema CHANGE IS COMING...

Ni kweli inakuja lakini ni change ya aina gani? Ni kwa manufaa ya nani?

Kila wakati nimekuwa nikionya kuhusu kushabikia hii inayodaiwa vita ya Ufisadi na zaidi hatari ya UMASIHA FEKI....tusipokuwa makini, uchungu na chuki zetu kuhusiana na hali mbaya tuliyonayo (UFISADI NA MAOVU MENGINE), tutajikuta tunashabikia kina HITLER wa enzi hizi...Wanaweza wasiwe wabaya kama tunavyoambiwa HITLER alivyokuwa, lakini wakawa wenye kutupeleka kama kule HITLER alipowapeleka WAJERUMANI....

Katika nyakati kama hizi ambazo serikali na wanasiasa walio wengi wamepoteza UHALALI (LEGITIMACY) ni wazi akili na busara za wananchi ndio zaweza kutulinda. Busara za viongozi wa kijamii nazo zina umuhimu wake mkubwa sasa.

Hata kama ni kweli serikali za CCM zimetuharibia nchi, hata kama mfumo wa siasa tulionao unalinda na kuneemesha ufisadi, hata kama ni kweli dini na siasa haziwezi kutenganishwa, lakini ukweli unabaki palepale....

Kwa Tanzania ni hatari sana kuchanganya mambo haya mawili haswa waziwazi kama inavyoendelea sasa....

Haihitaji kuwa genious kujua kuwa zaidi ya wakati wowote ule, huu sio wakati wa viongozi ama asasi za kikristo kuonekana wanamobilize wafuasi wao dhidi ya serikali inayoongozwa na MUISLAM.....Its wrong moraly but also strategically.

Ni wazi kuwa kanisa la Katoliki wakati wote limekuwa mstari wa mbele katika kufanya haya lakini kulikuwa na umakini mkubwa na sio kama sasa. Naamini hii ni dalili ya kuwa hali sio nzuri kimaadili, kiasasi na kiuongozi katika kanisa hili.

Na unapoingiza na makanisa ya kilokole ambayo ukweli ni kuwa katika enzi hizi yako more established, well networked and well financed kuliko THE MIGHTY CATHOLIC CHURCH, na ambayo upatikanaje wake wa viongozi hauko thorughly kama wenzao (CATHOLIC CHURCH) ndio kabisa tunawasha sigara katikati ya bwawa la petroli.....

Ndugu zangu tujihadhari kushabikia hizi njia za mkato katika kutafuta suluhu ya majanga yanayotukumba.....pale tu tutakapokuwa tayari kufuata njia iliyonyooka ndio tutakapojihakikishia tunapata mafanikio yaliyonyooka...

omarilyas
 
Nillikuwa nakuona tu huko kuoote huko ulikuwa unarahirahi, kuuma na kupuliza ila hapa ndo umeonesha yaliyopo moyoni mwako . Ni ajabu kusema kanisa katoliki linaonekana kumobilize wafuasi wake dhidi ya uislamu au sijui rais msilamu..lakini unashindwa pia kuona michango ya wezio walopita walodai eti kanisa lilimweka JK madarakani. Sijaelewa hizi hoja mnazitoa wapi na kwa nini. Hivi nataka nijulishwe, serikali iliyopo sasa hivi madarakani ni ya kiislamu?

Lete sababu za kuamini huu sio wakati wa kufanya haya. Kama zamani walikuwa wakiyafanya haya, why not now? Ni lipi limeongezeka au limepungua mpaka waache kufanya walichokuwa wakikifanya?

Hiyo sigara unayoizungumzia ni sigara gani mazee. Jadili hoja tafadhali..msiingize mambo ya madhehebu mengine kwenye hili wakati hakuna mafungamano.

Nadhani wewe ndiye hasa unataka kuturejesha nyuma. Raia kupata mwamko wa kujua haki na wajibu wao ndipo haswa kutakapopelekea kuchagua viongozi based on valid merits badala ya kuanza ku-resist changes ambako wewe unakuhubiri. Kutoa elimu kwa walengwa katu si njia ya mkato. njia ya mkato ni kukimbia kutatua tatizo au kuliahirisha.
 
Last edited:
Nillikuwa nakuona tu huko kuoote huko ulikuwa unarahirahi, kuuma na kupuliza ila hapa ndo umeonesha yaliyopo moyoni mwako . Ni ajabu kusema kanisa katoliki linaonekana kumobilize wafuasi wake dhidi ya uislamu au sijui rais msilamu..lakini unashindwa pia kuona michango ya wezio walopita walodai eti kanisa lilimweka JK madarakani. Sijaelewa hizi hoja mnazitoa wapi na kwa nini. Hivi nataka nijulishwe, serikali iliyopo sasa hivi madarakani ni ya kiislamu?

Lete sababu za kuamini huu sio wakati wa kufanya haya. Kama zamani walikuwa wakiyafanya haya, why not now? Ni lipi limeongezeka au limepungua mpaka waache kufanya walichokuwa wakikifanya?

Hiyo sigara unayoizungumzia ni sigara gani mazee. Jadili hoja tafadhali..msiingize mambo ya madhehebu mengine kwenye hili wakati hakuna mafungamano.

Nadhani wewe ndiye hasa unataka kuturejesha nyuma. Raia kupata mwamko wa kujua haki na wajibu wao ndipo haswa kutakapopelekea kuchagua viongozi based on valid merits badala ya kuanza ku-resist changes ambako wewe unakuhubiri. Kutoa kwa walengwa katu si njia ya mkato. njia ya mkato ni kukimbia kutatua tatizo au kuliahirisha.

Kwa ushabiki na munkari kama ulio nao sidhani kama nahitaji kupoteza muda wangu kubishana nawe...

Tulia...soma maoni yangu kwa umakini....elewa kama upo hapa kuelewa na sio kuendesha malumbano...

omarilyas
 
You said it all. Pamoja na dhamiri na mipango inayo sound gud but still gud to them not to the majority of Tanzanians. It is a gud program to the wrong institution Tanzania being a circular government it should be neutal to all issues related to governance/executives; legislation/Bunge and Judiciary/Mahakama. I take it as double standard kwa watu kukataa mahakama ya kadhi na kukubali kanisa katoliki kama institution ya kidini ku peleka elimu ya uraia kwa raia wa Tanzania ambao mbele ya katiba wote ni sawa. kama itapeleka elimu hiyo kwa baadhi ya raia ambao ndo wanahusika nao ki sheria vipi hao ambao hawapo under custodianship yao? Siyo kuwa watakua wamebaguliwa? Wao wahubiri dini/imani ndiyo haki yao kikatiba maswala ya elimu ya uraia waache institutions zenye legitimacy zifanye hivyo. Otherwise its out of selfishness na being a christian thats not Jesus kind of doing things its a selfish motive to attain whatever they dont want us to know which is against christian faith of loving your neighbour well as u do to ur self for this case people of other believes are the so called neighbours. Wasitugawe we still need to enjoy our unit and love. Kama ufisadi waukemee ndani ya makanisa na kuonya waumini wao mbona inapofika hapo wana shy away? Most of the condemed are their members if they can deal with them tutakuwa na better system kuliko kupanda mbegu ya udini na chuki kwa selfishness ya in the name of elimu kwa mpiga kura.

Ok to start with..tanzania is a secular country sio circular..

Secondly unasema eti hii plan nzima ya kutoa elimu kwa waumini wake kuhusu elimu ya uraia ni kulinufaisha tu kanisa badala ya taifa zima...this is a fallacy unless unambie elimu watakayoitoa itawalenga wao kama waumini na si kama waTz. Tukumbuke kuwa watz ni sote, ila ndani yake kuna subsets za kidini, kikabila, kijinsia n.k. Kutoa elimu wa kikundi flani kama watz is ok, ila kutoa elimu kwa kikundi flani kama kikundi ni ok tu provided amani haihatarishwi wala kuvunja umoja na mshikamano wa watz. hili ndilo la msingi.

tatu,kuhusu mahakama ya kadhi, sielewi unawezaje lifananisha hili suala la kutoa elimu ya uraia na mahakama ya kadhi. ni kama kutaka kufananisha mchana na usiku.

Nne, baada ya kupinga suala la kanisa kujihusisha kutoa elimu ya uraia, eti tena unahoji kwa nini hawaitoi kwa wengine wasio ktk kanisa. hii inashangaza. Kama hiyo elimu wanayoitoa haina faida iweje uulize wengine hawatoipata? na kama unaona umuhimu wa hiyo elimu kwanini usiunge mkono juhudi hata hizi ndogo wanazozionesha?

Tano, kuhusu huo unaudai kuwa ni u-selfish inashangaza sana kuona wewe usiyejiona uselfish wako unaanza kuwanyooshea vidole wengine kabla hujatazama hata hayo maandishi yako vizuri. Hii elimu haitolewi kwa kuangalia vyeti vya ubatizo au ulibatizwa parokia gani..hii process imelengwa kwa wote hasa waumini ambao nadhani ni folks ideal kwa sasa, siamini kama mtu wa imani nyinghine unakatazwa kuingia kupata elimu. Kama unashahidi kuwa lengo ni waumini wakatoliki pekee, then we can talk something on this.

Sita, kuhusu ujirani mwema you got all confused again. Kama niliposema hapo juu, hili zoezi lipo wazi kwa yeyote na ideal folks kwa sasa ni waumini wenyewe..msilete vitu visivyokuwepo kwa kusukumwa na chuki zenu binafsi tafadhali.

Saba, kuhusu ufisadi sioni kama kuna la kuzungumzia hapa. Kama wewe unayejinadi ni mkristu, you should know better kuwa kanisa linasimamia amri za Mungu ikiwemo ya usiibe. Kama una ushahidi kuwa kanisa katoliki linajihusisha systematically na hao mafisadi kwenye vitendo hivyo, hapo tunaweza kukaa chini kujadili..otherwise tusilete sentensi za jumljumla zisizo na tija.
 
Sasa mwenye munkari ni nani kati ya mimi na wewe? Mimi nimesoma na kujibu post yako kipengele kwa kipengele. Kama mkiishiwa hoja mnaanza kuleta visingizio. Nadhani hoja zangu zimekufikia, tulia uzisome uzielewe kama hazijibiki unaweza ukaendelea na thread nyingine hulazimishwi saaana kihivyo.
 
Kanisa linataka kwenda nje ya mstari na hii ni hatari sana mimi kama mkristu ntalipinga kwa nguvu zangu zote. Kama lingefanya kazi yake ya kumwingiza kristo ndani ya mioyo ya waumini kwa uaminifu basi mafisadi wangekuwa wanapatikana kwenye imani nyingine na si kwa wakatoliki na labda wakristu kwa ujumla. Hiyo kazi hawaifanyi kama Yesu anavyoelekeza sasa kama wameshindwa kutoa evil spirits ambayo ndo hasa kiini cha ufisadi wataweza kupeleka elimu sahihi kwa raia? Wafanye kazi ya imani kwa uaminifu na mengine yatafuata, kanisa halina nguvu zaidi ya Yesu kama yeye hakuhitaji mafarisayo wala waandishi kubadili tabia za watu iweje leo wale walio wake wafanye tofauti na yeye aliye mwanzilishi wa hiyo kazi? Kama ni imani basi mwongozo wetu unatuambia vita vyetu si vya damu na nyama bali katika ulimwengu wa roho zidi ya mapepo wabaya hii ni pamoja na roho ya ufisadi haiondolewi kwa elimu ya kuchagua kiongozi bora bali kuuondoa uovu huo ndani ya hao watakao kuwa viongozi ili kuwepo na pool kubwa ya expected viongozi bora. By the way hao bora watatoka wapi wakati kazi ya kuwafanya wawe bora imetelekezwa na haohao wanaojidai wanafundisha watu kuchagua viongozi bora? What a deception? Tufanye research tuone walioko kwenye mihimili yote mitatu wakatoliki ni % ngapi hao tu wangekuwa waaminifu ufisadi ungepitia kona ipi? Shule zote bora ni seminari za katoliki implying wasomi waliobobea wana mkono wa kanisa katoliki wako wapi hao kama kweli wana Yesu huyu tunaemwamini wawasaidie watanzania wanaogelea kwenye wimbi la umaskini? U wapi upendo wa agape? Let us not be deceived if we can not do well in spirit how can we manage canal things? Kanisa fanya kazi yako ya ku-cast out devil inside the people if u do it well viongozi bora ni automatic; Paul said injili ina nguvu ya kujitetea yenyewe haihitaji inticing words from human being. It has power and by that power u r also going to be consumed by the fire of holly spirit if u will continue with your selfish motives. Being a christian I will never let the name of Jesus to be mis-used.

Mosi, unasema kanisa linataka kwenda nje ya mstari, fine enough hayo ni mawazo yako na inaonesha wewe sio muumini wake. Kama kuelimisha watu kufanya maamuzi sahihi ni kwenda nje ya mstari..Inapojenga mahospitali ni kwenda nje ya mstari..inapojenga shule ni kutoka nje ya mstari..and the list goes on and on..Kama huku ndiko kwenda nje ya mstari, then nadhani binafsi napendekeza lizidi zaidi kwenda nje ya mstari.

Pili, uhusu ufisadi kama nilipoeleza hapo juu, ufisadi wa mtu binafsi hauwezi kuhusika na imani au dhehebu lolote la linalomhubiri Kristu. Tatizo lingekuwepo iwapi kama ufisadi ungekuwa unabarikiwa na kanisa, hapo tungekuwa na la kuongea. Lakini kwa sasa tukubali tu kuwa kama mtu ameamua kuwa mwizi vitendo vyake vinamgharimu yeye mwenyewe, kazi ya kanisa ni kuonya, na sidhani kama unao uthibitisho kudhihirisha vinginevyo.

Tatu, unadai kuwa kanisa lisijihusishe na mambo ambayo umeyaita carnal, fine enough huo ni mtazamo wako na ni sahihi provided unakubaliana na watu wengine wenye mawazo tofauti na wewe. Kanisa linao wajibu wa kuwaelekeza wananchi hususan waumini wake ili wapate afya bora ya kiroho na kimwili. Sasa kama wewe unadhani kanisa linahitaji tu kulinda afya za kiroho peke yake, fine enough waavhe watu wanaoamini vinginevyo nao wafurahie uhuru wao wa kuamini na kuchagua wanachoona ni sahihi.
 
Sijawahi kusikia watu wengi hivyo wakiogopa Elimu ya Uraia. Wote tunakubali Kanisa Katoliki linatoa Elimu bomba. Ndio maana tunawakimbizia watoto wetu kusoma huko. Sasa wakiamua kutoa Elimu ya Uraia kwa waumini wote kuna mbaya gani?

Msiogope ELIMU. Hata kama ni ya Uraia. Yaani mnapinga watu kufundishwa umuhimu na namna ya kuchagua viongozi bora? Wasieleweshwe watu namna ya kupambana na hongo na wizi wa kura zao? Nasema hamueleweki!
 
You said it all. Pamoja na dhamiri na mipango inayo sound gud but still gud to them not to the majority of Tanzanians. It is a gud program to the wrong institution Tanzania being a circular government it should be neutal to all issues related to governance/executives; legislation/Bunge and Judiciary/Mahakama. I take it as double standard kwa watu kukataa mahakama ya kadhi na kukubali kanisa katoliki kama institution ya kidini ku peleka elimu ya uraia kwa raia wa Tanzania ambao mbele ya katiba wote ni sawa. kama itapeleka elimu hiyo kwa baadhi ya raia ambao ndo wanahusika nao ki sheria vipi hao ambao hawapo under custodianship yao? Siyo kuwa watakua wamebaguliwa? Wao wahubiri dini/imani ndiyo haki yao kikatiba maswala ya elimu ya uraia waache institutions zenye legitimacy zifanye hivyo. Otherwise its out of selfishness na being a christian thats not Jesus kind of doing things its a selfish motive to attain whatever they dont want us to know which is against christian faith of loving your neighbour well as u do to ur self for this case people of other believes are the so called neighbours. Wasitugawe we still need to enjoy our unit and love. Kama ufisadi waukemee ndani ya makanisa na kuonya waumini wao mbona inapofika hapo wana shy away? Most of the condemed are their members if they can deal with them tutakuwa na better system kuliko kupanda mbegu ya udini na chuki kwa selfishness ya in the name of elimu kwa mpiga kura.

Ni ipi institution yenye legitimacy ya kutoa elimu ya uraia Tanzania?
2005 BAKWATA ilipokea 200M Toka UNDP Tanzania kwa ajili ya kutoa elimu ya uraia. Je ilikuwa na Legitimcy ya kufanya hivyo? Kama haikuwa nayo kwa nini walizipokea. Na je walitoa elimu hiyo au walizifanyia nini mahela hayo?
 
Ok to start with..tanzania is a secular country sio circular..

Secondly unasema eti hii plan nzima ya kutoa elimu kwa waumini wake kuhusu elimu ya uraia ni kulinufaisha tu kanisa badala ya taifa zima...this is a fallacy unless unambie elimu watakayoitoa itawalenga wao kama waumini na si kama waTz. Tukumbuke kuwa watz ni sote, ila ndani yake kuna subsets za kidini, kikabila, kijinsia n.k. Kutoa elimu wa kikundi flani kama watz is ok, ila kutoa elimu kwa kikundi flani kama kikundi ni ok tu provided amani haihatarishwi wala kuvunja umoja na mshikamano wa watz. hili ndilo la msingi.

tatu,kuhusu mahakama ya kadhi, sielewi unawezaje lifananisha hili suala la kutoa elimu ya uraia na mahakama ya kadhi. ni kama kutaka kufananisha mchana na usiku.

Nne, baada ya kupinga suala la kanisa kujihusisha kutoa elimu ya uraia, eti tena unahoji kwa nini hawaitoi kwa wengine wasio ktk kanisa. hii inashangaza. Kama hiyo elimu wanayoitoa haina faida iweje uulize wengine hawatoipata? na kama unaona umuhimu wa hiyo elimu kwanini usiunge mkono juhudi hata hizi ndogo wanazozionesha?

Tano, kuhusu huo unaudai kuwa ni u-selfish inashangaza sana kuona wewe usiyejiona uselfish wako unaanza kuwanyooshea vidole wengine kabla hujatazama hata hayo maandishi yako vizuri. Hii elimu haitolewi kwa kuangalia vyeti vya ubatizo au ulibatizwa parokia gani..hii process imelengwa kwa wote hasa waumini ambao nadhani ni folks ideal kwa sasa, siamini kama mtu wa imani nyinghine unakatazwa kuingia kupata elimu. Kama unashahidi kuwa lengo ni waumini wakatoliki pekee, then we can talk something on this.

Sita, kuhusu ujirani mwema you got all confused again. Kama niliposema hapo juu, hili zoezi lipo wazi kwa yeyote na ideal folks kwa sasa ni waumini wenyewe..msilete vitu visivyokuwepo kwa kusukumwa na chuki zenu binafsi tafadhali.

Saba, kuhusu ufisadi sioni kama kuna la kuzungumzia hapa. Kama wewe unayejinadi ni mkristu, you should know better kuwa kanisa linasimamia amri za Mungu ikiwemo ya usiibe. Kama una ushahidi kuwa kanisa katoliki linajihusisha systematically na hao mafisadi kwenye vitendo hivyo, hapo tunaweza kukaa chini kujadili..otherwise tusilete sentensi za jumljumla zisizo na tija.

Wewe ni mkristo au mwisilamu? Kama jina ndo sawa na imani basi naomba kukwambia kuwa objective ya Kanisa si kujenga ufalme wa dunia bali ufalme wa Mungu; kujenga mwili wa kristo ambalo ndo kanisa na priciple zake ni tofauti na hizi za ufalme wa dunia. Jesus put it simple and clear alipo ulizwa je ni wakati huu ambapo wana waisrael watarudishiwa ufalme wao? They were thinking kwamba Yesu ata mtreplace mfalme wa wakati ule if u r a christian u have the answer if not then ask me or church members. Kwanza strategies wanazotumia ni za kisiasa siyo spiritual kwa uwazi kabisa nikwambie jinsi wanavyo fanya si tofauti sana na PCCB wanavyoishughulikia rushwa kwa kukamata dagaa. Viongozi wakuu wengi ni wakristo kama kanisa lingewainjilisha neno la Mungu lina nguvu kuliko well developed structure ya kanisa. Kwakutokufanya hilo wanaikana nguvu ya Mungu na kuwa wapinga kristo they think they can do better than what the word of God can do. Neno la Mungu lina sema bwana asipo ujenga mji waujengao wafanya kazi bure; utafuteni kwanza ufalme wa Mungu na hayo mengine mtapewa kama ziada. Vipi kanisa lianze kujenga ufalme wa duniani wakati wambinguni ndo unatakiwa uanze kwanza? Wanatumia canal strategies na kuacha spiritual principles by this anguko lao ni kubwa wala haliko mbali. Let me tell them bad news; sons and daughters of Zion are coming up with mighty power to take over they are not known by their dominions but by the name which is above all the names they use the power which they rejected thinking by them being organised then they can do everything. Waangalie historia ya Ulaya na America then they will probably perceive what I am saying.

Fikiria wewe ungekuwa mwisilam alafu unasikia dini fulani inapeleka elimu ya uraia ungeacha kuwa suspicious? What is to do so I already put it "right program to the wrong institution". Una panda mbegu ya udini for kutokana na background yetu ni rahisi mtu mmoja akawa mislead mass kwa ubinafsi wake akishafanya calculations zake nakuona kama atawatumia wakristo au waislam basi nitapata kura kadhaa na hivyo kwa usiri au ujanja atawaambia msimpigie fulani kura kwa sababu atafanya nchi yetu kuwa ya whatsoever he would want to cheat them so as to win election. Ubinafsi hauna dini ni gene iliyoko kwa mwanadam yeyote ambaye hajawa renewed in mind.
 
Sijawahi kusikia watu wengi hivyo wakiogopa Elimu ya Uraia. Wote tunakubali Kanisa Katoliki linatoa Elimu bomba. Ndio maana tunawakimbizia watoto wetu kusoma huko. Sasa wakiamua kutoa Elimu ya Uraia kwa waumini wote kuna mbaya gani?

Msiogope ELIMU. Hata kama ni ya Uraia. Yaani mnapinga watu kufundishwa umuhimu na namna ya kuchagua viongozi bora? Wasieleweshwe watu namna ya kupambana na hongo na wizi wa kura zao? Nasema hamueleweki!

Hakuna anaepinga elimu ya uraia tunapinga elimu hiyo kutolewa kwa jina la kanisa. kama kanisa linataka kutoa mchango basi lingekaa na madhebu na dini nyingine pamoja na serikali kuona jinsi gani watafanya hivyo; kwanini wao waende kama wao na si kama raia wa nchi hii? Watoe human resource au institution zao za Elimu lakini kwa mpango utakao ondoa hisia ya kidini na wawashirikishe watu wote wenye uwezo wakufanya hivyo mbona shule wanasomesha hata waislam na wapagani na madhebu mengine? Vipi kwenye kutoa elimu ya uraia waende kama kanisa na si kama raia? Kwanini kwa waumuni tu na siyo raia wote wa Tanzania?
 
Hivi wewe Abdulhalim inaonekana umejawa na jazba ya chuki sitostaajabu ukiwa si mtanzania, first wote tumeshajua ni dini gani una-represent na view zipi unazozitaka wewe regardless of your alias the thing that perplexes me at the moment we kweli ni mwenzetu? kwa sababu umen'gang'ana na kila mtu umu anaekuja na views ambazo zina respect others beliefs, offer solutions that would include all 'Tanznanians' na sio watz kama unavyotuita hilo ni neno la wakenya wanapo wa describe 'wabongo' another popular term if you dont know.

we ni mtu ambae utaki kusikia la wengine especially amani umen'gan'gana na sera za division tu ambazo wengi humu ndani tunajua azina mwisho mzuri baadae. yaani unakua kama vile mkikuyu ambae anaamini Raila Odinga atakiwi kushika serikalini kisa raila Odinga si mkikuyu. sijui hila nitasema ni mtanznania wa kwanza kama ni mbongo na si mtz kwa faida yako utetei mabadiliko peke yake bali unataka na makundi yawepo yaani kama mkenya vile, au ulikaa sana uko mazee maana maneno yako mengi yana sound like one au labda upo out of date kwa sababu mazee wabongo utumia Mjomba.

Mungu Ibariki Tanznania
 
Ingawa baadhi ya magazeti wamelipotosha hili kwa kusema kwamba kanisa katoliki linataka mgombea "wake" wa urais 2010 sio kweli. Kwetu sisi amabao tayari tumeshiriki katika semina/warsha hizi hakuna kitu kama hicho. Lengo kuu ni kuamsha hali ya waumini kushiriki katika uchaguzi kikamilifu kuanzia ngazi ya chini kabisa hadi juu. Kusema kweli waumini wengi wakatoliki hawashiriki vilivyo katika uchaguzi halafu wanalalamika kwamba kuna uongozi mbaya. Ili kukata mzizi wafitina kanisa linasema basi mshiriki kikamilifu katika kuwania uongozi na kupiga kura. It is simple as that.
 
Naona hoja zimeisha vimebaki vioja. Wakati unaendelea kushangaa shangaa nakusema mimi si mtanzania blah blah anza kabisa kumeza hoja nilizozileta so far..usilete maelezo ya jumlajumla na ad hominem.

we ni mtu ambae utaki kusikia la wengine especially amani umen'gan'gana na sera za division tu ambazo wengi humu ndani tunajua azina mwisho mzuri baadae. yaani unakua kama vile mkikuyu ambae anaamini Raila Odinga atakiwi kushika serikalini kisa raila Odinga si mkikuyu. sijui hila nitasema ni mtanznania wa kwanza kama ni mbongo na si mtz kwa faida yako utetei mabadiliko peke yake bali unataka na makundi yawepo yaani kama mkenya vile, au ulikaa sana uko mazee maana maneno yako mengi yana sound like one au labda upo out of date kwa sababu mazee wabongo utumia Mjomba.

Mungu Ibariki Tanznania

Mazee, naweza kuwa Mkenya au utaifa wowote unaotaka kunipa, lakini hilo halitabadilisha ukweli wa hoja ninazozimwaga hapa jamvini. Ningependa wakati unashangaa maandishi yangu uwe pia unajaribu kufanya tafakari ya ninachokiandika..

Next time jaribu kuleta vitu vyenye sense, badala ya kuishia kufikiri ndani ya contena lako.
 
Ingawa baadhi ya magazeti wamelipotosha hili kwa kusema kwamba kanisa katoliki linataka mgombea "wake" wa urais 2010 sio kweli. Kwetu sisi amabao tayari tumeshiriki katika semina/warsha hizi hakuna kitu kama hicho. Lengo kuu ni kuamsha hali ya waumini kushiriki katika uchaguzi kikamilifu kuanzia ngazi ya chini kabisa hadi juu. Kusema kweli waumini wengi wakatoliki hawashiriki vilivyo katika uchaguzi halafu wanalalamika kwamba kuna uongozi mbaya. Ili kukata mzizi wafitina kanisa linasema basi mshiriki kikamilifu katika kuwania uongozi na kupiga kura. It is simple as that.

Mazee unajua watu wengi humu wapo negative kwa sababu zifautazo, wengine ni chuki walizonazo za muda mrefu kuhusu kanisa katoliki, sasa linapokuja hapa jamvini jambo lolote watarusha kila dongo na kumaliza chuki yote waliyonayo hata kama hakuna mahusiano na hoja iliyopo ukumbini.

Wengine wako negative kwa sababu hawako informed, wanakisia kisia tu na wanajazana ujinga vijiweni na kuamini na hawataki kujishughulisha kujua ni nini hasa kinachoendelea, hawa wapo wengi pia.

Wengine ni wale wasiojiamini au wanaona maslahi yao yapo compromised na mwamko wowote utakaoleta mawazo chanya ktk jamii, hao nao wapo wengi tu. Watafanya kila jambo ku-discredit effort yeyote itakayoleta mabadiliko na kuwafumbua watu macho waone kilichopo mbele yao na kufanya maamuzi sahihi kuhusu mustakabali wa maisha yao.

Ila tuendelee kuelimisha, mwenye kutaka maarifa atapata, na yule mwenye lengo la kuleta mtafaruku tumuweke bayana pia.
 
Hakuna anaepinga elimu ya uraia tunapinga elimu hiyo kutolewa kwa jina la kanisa. kama kanisa linataka kutoa mchango basi lingekaa na madhebu na dini nyingine pamoja na serikali kuona jinsi gani watafanya hivyo; kwanini wao waende kama wao na si kama raia wa nchi hii? Watoe human resource au institution zao za Elimu lakini kwa mpango utakao ondoa hisia ya kidini na wawashirikishe watu wote wenye uwezo wakufanya hivyo mbona shule wanasomesha hata waislam na wapagani na madhebu mengine? Vipi kwenye kutoa elimu ya uraia waende kama kanisa na si kama raia? Kwanini kwa waumuni tu na siyo raia wote wa Tanzania?

Umetoa hoja nzuri kuwa kwa nini watoe elimu ya uraia kwa jina la kanisa. Lakini huwa husomi mawazo ya wengine na hivyo kuishia kuelewa yale unayoyataka tu. Nilikwisha eleza kwenye posts zilizopita kuwa kanisa ni taasisi huru inayo-operate ktk jamii yetu. Kitu cha msingi ni je, wanafuata sheria za nchi au la? Jibu nadhani unalo. Pia nilieleza kuwa hiyo elimu wanayoitoa wanaitoa kwa sababu wao watz na sio ni kwa sababu ni waumini. Tatizo lingekuwapo iwapo kama elimu ya uraia ingewalenga wao kama waumini badala ya kama raia wa tz.

Pili je wanapofanya hayo mafunzo ni siri? jibu ni hapana? Je kuna ajenda ya siri ktk mafunzo yao? Jibu ni hapana. Sasa kama jibu ni hapana hofu yao ni unfounded na haina mantiki. Kwa msingi uleule wa kanisa kufungua mashule na kutoa huduma nyingine za kijamii, ndio msingi huohuo unaotumika kutoa elimu ya uraia kwa waumini wake na yeyote mwenye kutaka.
 
Wakati mwingine huwa nawashangaa sana watu wanao jiona kuwa matawi ya juu!? Na hali ni makabwela wa akili tu, kama si kudumaa kwa mawazo yao kutokana na uhafidhina ulio komaa na kuoteana tabaka za ukasuku na kujiona kuwa wao ni mamba kumbe ni mijusi kafiri...!
 
Kwa miaka mingi serikali imekuwa ikiheshimu sana madhehebu yote ya dini kiasi kwamba ilikuwa tayari kupoteza hata mapato ya taifa kwa ajili ya ku support shughuli za madhehebu hata zile amabzo zilikuwa si za kidini mradi tu zinafanywa na mashirika ya dini. Serikali ilikuwa ikifanya hivyo ili kutoa fursa kwa madhehebu ya dini yasaidie kuwaelimisha waumini wao kiroho na hivyo kuwafanya wawe raia wema kwani mtu akiishi kwa kufuata maadili ya dini yeyote ile (ispokuwa ile dini ya shetani) basi atakuwa mtu mwema anayeishi kwa kufuata sheria na hivyo kuipunguzia matatizo serikali.

Kilichotokea ni kama hali ilivyo sasa, baadhi ya makanisa, hasa kanisa katoliki, na pia baadhi ya dini nyingine, zimejisahau kutimiza wajibu wao huo na kuanza kuingilia utendaji wa serikali. Mara nyingi viongozi wa vyama vya siasa na serikali, wamewashauri viongozi wa dini kuwa kama wanataka kuingia katika siasa basi wavue majoho yao na waingie katika ulingo wa siasa na waache kuleta uchochezi na waendelee kutoa huduma za kiroho.

Baadhi ya viongozi wa dini wameendelea kukaidi ushauri huo na matokeo yake ni kuwa heshima ya pekee ambayo serikali ilikuwa ikitowa kwa mashirika ya dini sasa wameanza kuiondoa. Miaka yote mashirika ya dini yalikuwa yakipewa misamaha ya kodi kwa ajili ya shughuli zao bila kujali kuwa ni za kidini au la. Katika Bajeti hii, kwa mara ya kwanza serikali imefuta misamaha yote ya kodi kwa mashirika ya kidini maana inaona kuwa muelekeo wao si wa kiroho tena bali ni washindani katika harakati za kushika dola. Infact yanakuwa kama ni vyama vya upinzani kutokana na ukweli kuwa program zao zianenda sambamba na program za vyama vya upinzani. Kwa hiyo serikali imeona ni kwa nini iwasaidie kama wako pale kuipiga vita?

Tayari makanisa yameanza kupigia kelele hili la kufutwa kwa misamaha ya kodi, lakini ni wao wenyewe ndio wamepoteza ile heshima waliokuwa nayo mbele ya serikali. La kusikitisha zaidi ni kuwa utukutu huu wa madhehebu machache umeathiri pia yale madhehebu ambayo yanafanya wajibu wao kwa mujibu wa kumtumikia Mungu.

Hebu viongozi wetu wa dini wajirekebishe na watende wajibu wa kazi yao kwa kwanza kuwahubiria waunmini wao ndani ya sehemu zao za ibada mambo yanayo wakera viongozi hao, kama vileufisadi n.k. badala ya kuwafuata maofisini mwao kuwaondoa katika nafasi zao. Hii inaleta hali ya confrotation na matokeo yake yameanza kujitokeza. Litalofuata sasa ni serikali kupuuza kabisa ushauri wa viongozi wa dini ambao hapo awali ulikuwa ukipata nafasi kubwa ya kusikilizwa.
 
Hakuna anaepinga elimu ya uraia tunapinga elimu hiyo kutolewa kwa jina la kanisa.

Elimu hiyo itatolewa na Kanisa, sio kwa jina la Kanisa. Na angalau ungesema kuitoa kwa jina la Kanisa kuna ubaya gani!

kama kanisa linataka kutoa mchango basi lingekaa na madhebu na dini nyingine pamoja na serikali kuona jinsi gani watafanya hivyo; kwanini wao waende kama wao na si kama raia wa nchi hii?

Mbona hulalamiki wanapojenga shule kama wao? Wanapojenga Hospitali au shule lazima wakae kwanza na Makanisa mengine wajadiliane cha kufanya? Kwa kisa gani?

Vipi kwenye kutoa elimu ya uraia waende kama kanisa na si kama raia? Kwanini kwa waumuni tu na siyo raia wote wa Tanzania?

Nani kakwambia "hawaendi" kama raia wa Tanzania? Usiogope. Kanisa linataka tu kuwaelimisha wananchi namna ya kuchagua viongozi bora. Kwa nini kitu kama hicho kikusumbue?
 
Wewe ni mkristo au mwisilamu? Kama jina ndo sawa na imani basi naomba kukwambia kuwa objective ya Kanisa si kujenga ufalme wa dunia bali ufalme wa Mungu; kujenga mwili wa kristo ambalo ndo kanisa na priciple zake ni tofauti na hizi za ufalme wa dunia. Jesus put it simple and clear alipo ulizwa je ni wakati huu ambapo wana waisrael watarudishiwa ufalme wao? They were thinking kwamba Yesu ata mtreplace mfalme wa wakati ule if u r a christian u have the answer if not then ask me or church members. Kwanza strategies wanazotumia ni za kisiasa siyo spiritual kwa uwazi kabisa nikwambie jinsi wanavyo fanya si tofauti sana na PCCB wanavyoishughulikia rushwa kwa kukamata dagaa. Viongozi wakuu wengi ni wakristo kama kanisa lingewainjilisha neno la Mungu lina nguvu kuliko well developed structure ya kanisa. Kwakutokufanya hilo wanaikana nguvu ya Mungu na kuwa wapinga kristo they think they can do better than what the word of God can do. Neno la Mungu lina sema bwana asipo ujenga mji waujengao wafanya kazi bure; utafuteni kwanza ufalme wa Mungu na hayo mengine mtapewa kama ziada. Vipi kanisa lianze kujenga ufalme wa duniani wakati wambinguni ndo unatakiwa uanze kwanza? Wanatumia canal strategies na kuacha spiritual principles by this anguko lao ni kubwa wala haliko mbali. Let me tell them bad news; sons and daughters of Zion are coming up with mighty power to take over they are not known by their dominions but by the name which is above all the names they use the power which they rejected thinking by them being organised then they can do everything. Waangalie historia ya Ulaya na America then they will probably perceive what I am saying.

Kuhusu jina langu ..inashangaza kidogo umeishiwa na hoja kiasi cha kutaka kuyaingiza hata majina ya mtoa hoja ktk mada. Ok, nasikitika kuwa hapa si mahala pake kuanza kuongelea majina.

Ama kuhusu kanisa kujenga au kutokujenga ufalme wa dunia hiyo ni tafsiri yako potofu kuhusiana na maandiko uliyoitengeneza wewe mwenyewe kichwani mwako. Nitapenda kuliongelea hili siku nyingine na mahali muafaka hapa sio mahala pake.

Pili naona unaongea tu kwa hisia bila ya kuwa na vitu tangibles. Unadai neno la lina nguvu, sasa sijui ulitaka watu waache kufanya kazi wakae chini wafanye maombi tu bila kujishughulisha na kila kitu kitatelemka kutoka mbinguni kama mana? Kuna usemi unaosema sala na kazi. Kukaa tu madhabahuni na kuhubiri huku hujali kinachoendelea mitaani ni kutokuwa mchungaji mwema. Uchungaji wa kweli wa kondoo walikabidhiwa wawatunze ni lazima uangalie maendeleo ya mwili na roho kwa pamoja. Huo ndo uchungaji wa kweli na hata Yesu aliwaponya watu shida zao za mwili na kuwaponya na roho zao pia, hakufanya kimoja tu na kuwaacha watu njia panda.

Hayo mengine niliyoya-bold ni yako na sijui yanakoanzia wala yanakoishia na yanakusudia nini na yanalenga kufanya nini.

Fikiria wewe ungekuwa mwisilam alafu unasikia dini fulani inapeleka elimu ya uraia ungeacha kuwa suspicious? What is to do so I already put it "right program to the wrong institution". Una panda mbegu ya udini for kutokana na background yetu ni rahisi mtu mmoja akawa mislead mass kwa ubinafsi wake akishafanya calculations zake nakuona kama atawatumia wakristo au waislam basi nitapata kura kadhaa na hivyo kwa usiri au ujanja atawaambia msimpigie fulani kura kwa sababu atafanya nchi yetu kuwa ya whatsoever he would want to cheat them so as to win election. Ubinafsi hauna dini ni gene iliyoko kwa mwanadam yeyote ambaye hajawa renewed in mind.

Unaongelea kuwa suspicious..Kuwa suspicious ni one thing na kukishutumu kitu au kukipinga baada ya kujua undani wake ni suala jingine. Unaruhusiwa kuwa suspicious provided unaonesha some kind of efforts kuutafuta undani wa unachokitilia mashaka. Kukitilia tu kitu mashaka na kutoendelea kutafuta undfani wa jambo lenyewe ndio hasa wengi wenu mnachokifanya hapa.

Unauliza kama ningesikia watu wa imani nyingine wanafanya utaratibu wa kuelimisha watu wao, jibu langu ni kuwa chochote kilicho chema kwao ni chema kwangu provided hakina lengo baya.

Mwishoni naona una-recycle hoja zilezile. Inaonekana hauna taarifa ya ukweli wa mambo ulivyo. Wengi wetu tunayo mazoea ya kutupia tu shutuma na lawama bila ya kuchukua muda kuona tunachokilaumu ni nini na iwapo tuna sababu za msingi kulaumu. Kwa taarifa tu, kwa nyakati tofauti kanisa limekuwa likishirikiana na serikali kwenye mambo ya afya, elimu na kampeni mbalimbali, na wakati mwingine wataalamu wa serikali huja mpaka madhabahuni kuhamasisha kampeni mbalimbali za kijamii. Hili hulijui au hutaki kuliona, inashangaza.

Nakushauri uangalie thread nyingine kama mbili hivi, nadhani kuna moja ipo attachment kuhusiana na hii plan. Unaweza kusoma na mawazo ya wenzio kuona wanachoongea na kukipima badala tu ya kushikilia cha kwako.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom