Wapo wengi

sawabho

JF-Expert Member
Feb 25, 2011
5,286
3,107
Ndugu wana JF ni matumaini yangu kuwa aina zote za maisha au tabia zinaweza kujaribiwa na kuchwa kama hazifai lakini sio ndoa. Ndoa haijaribiwi. Ni vizuri mtu anapotaka kuingia katika kundi hili atafakari kwa kina kama anayeingia naye anamfaa kweli. Kuna rafiki yangu mwaka 2009 kachumbia Mdada, huko mikoani (nyumbani) yeye anaishi na kufanya kazi mjini. Watu wa karibu wakamwambia kuwa huyo Mdada hafai kuwa mke wa mtu labda kwa starehe tu. Walifikia hata kunipigia simu na kuniomba nimshauri. Jamaa kang’ang’ania, mpaka kaoa. Kibaya zaidi, kamwambia mkewe kuhusu wale waliomtahadharisha. Mrs kawapiga marufuku nyumbani kwake nikiwemo mimi. Sasa baada ya kumleta mjini mambo yamekuwa magumu, bahati mbaya ndoa imechewa kujibu, jamaa yangu akirudi kutoka kazini Mrs hayupo na simu haipatitikani. Jamaa kamrudisha nyumbani kwao (Kwa wazazi wa mwanaume), huko tunasikia Mdada amefungulia mbwa. Sasa Jamaa yangu anasema hataki kumwona huyo shem wangu, wanawake ni wengi ataoa mwingine. Tatizo ninaloliona hapa ni hili: i) Unapoa/olewa tayari umepiga hatua katika maisha, kuacha /kuachwa ni kurudi nyuma kimaisha; ii) Umelipa mahari ambayo ungeyatumia kwa shughuli za maendeleo na inakuwa vigumu kurudishwa; iii) Ukiacha/kuachwa unaweka doa katika familia yako kwa maana watu watakapotaka kuoa au kuolewa kwenu wataangalia historia ya familia yako. Je, Wana JF huu msemo wa ….Wanawake/ Wanaume wako wengi ni msemo sahihi au unapotosha?
 
ni sahihi kabisa, wanawake /wanaume wapo wengi saaaana, lakini wanawake/wanaume wa kufunga na kuishi kwenye ndoa ni wachache, tena sana.
 
Maisha ya ndoa yanahitaji ushauri na km mtu anashauriwa hakubali itakula kwake km huyo jamaa
 
Back
Top Bottom