Wapo wapi wanaojiita maprofesa?

hittler

Member
Jul 18, 2011
55
10
Tanzania ya leo imevamiwa, wasomi wetu wamesahau role yao katika jamii, wameamua kufumbia macho matatizo ya jamii, wameamua kugoma kuwa wa kweli, wameamua kukaa kimya nakusahau kuwa wana kazi yakutoa ushauri kwa serikali, wameamua kuwa vibaraka wa serikali, wameamua kuwa waongo ili kulinda nafasi zao, wameamua kuwa mafisadi na kujilundikia mali wameamua Tanzania iangamie kwa kujikita kwenye siasa za nchi.
Wasomi siku zote ni taa ya jamii, hutegemewa sana kushauri na kutoa njia mbadala ya kutatua matatizo mbalimbali, hili limeanza kuwa ndoto asa pale ninapoona wasomi wakijikita kwenye siasa na kukimbia kazi zao za ualimu. Unamkuta mtu anajiita Profesa wa uchumi wakati inflation rate imefikia double digit, au profesa wa sheria wakati kina Chenge wamegonga watu na kuwaua wanapewa adhabu ya faini laki saba, unamkuta mtu anajiita profesa wa makompyuta wakati Most of the IT managers in different companies are Foreigners. Eti profesa unashindwa kusimama na kusema ukweli kisa unaogopa utavuliwa u dean wa faculty au school, huo ni ujinga,inaonyesha jinsi usivyojiamini. Wasomi wamekuwa hovyo, ni kheri yule asiyejua akadanganywa kuliko wewe unayejiita VC au DVC ukadanganywa na ukadanganyika na kusifia uongo. Mnakuwa wanafiki mnamsifia Rais kwa mapungufu yake ili kulinda matumbo yenu, mwambieni ukweli na mpeni njia mbadala za kutatua matatizo ya nchi.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom