Wapinzani wanaohamia CCM hufaidi kwa muda na kutupwa, kwa nini Mh. Wasira kafaidi muda mfefu?

DT125

JF-Expert Member
Oct 19, 2011
380
573
Nimekuwa nafuatilia wanasiasa wengi kutoka upinzani wanaohamia au kurudi CCM hunufaika kwa kupewa post mbalimbali na baadaye hutupwa kapuni, kama nitakavyowataja baadhi ya waliotupwa baada ya kula matunda ndani ya chama hicho, nani anajua siri ya Waziri Steven Wassira kudumu katika nafasi mbalimbali ndani ya serikali ya CCM?

Hawa wafuatao walikuwa hawawazi kesho wanakula nini leo wanawaza leo wanakula nini achilia ya kesho;
1. Tambwe Hiza- kazunguka nchi na propaganda za Mh. Makamba alivyotoka CUF leo historia.
2. Dr. W Kaburu- alipewa ubunge wa Afrika Mashariki alivyotoka CHADEMA leo anasota
3. Dr. Masumbuko Lamwai - Wakiri maarufu alivyotoka NCCR leo hasikiki.
4. Mh. Nsazungwako mbunge wa Kasulu Mashariki kwisha kabisa baada ya kukosa ubunge hata ukuu wa mkoa kakosa.
5. Mh. Mgesi alijitoa kugombea ubunge Morogoro Kusini akiwa M/Kiti mkoa CHADEMA akajiunga CCM leo choka mbaya.
6. Mh.Shitambala alijitoa CHADEMA akiwa M/kiti wa mkoa Mbeya ahadi aliyopewa iliyeyuka kama theruji ya Mt. Rungwe.
Kuna wengine waongeze ili wenye wazo kama hilo watafakari mara mbili kabla ya kufanya maamuzi.
 
nasikia ana kabinti karembo hivi, na yuko karibu sana na mkulu
 
Labda yeye alienda upinzani bila kuwa mpinzani wa kweli. Alienda kufanya ushushushu baada ya kumaliza kazi aliyotumwa akarejea CCM ndiyo maana bado anatesa.
 
CCM -- NCCR-Mageuzi -- CCM
Wassira aliwahi kuanzisha chama chake. Lakini sababu kubwa ya kurudi CCM ni kwamba aliwekewa vizingiti katika biashara zake za samaki na akaona heri arudi CCM. Kitu kingine ambacho kimemsaidia Wassira ni kwamba ni hasimu mkubwa wa Warioba na Kikwete hampendi Warioba. So the enemy of my enemy is my friend.
 
vigeu-geu flip- floppers that is what they have to havest Tyson is to strong like his name that is why he survived all storms

Ila kuna mambo yaliyobadilika au sijui ni kitu gani. Wakati wa awamu ya tatu yalikuwa ni mambo ya kawaida kumuona Mkapa leo kamkumbatia huyu kesho yule...sasa sijui ni strategy za M/kiti aliyepo na yule ni tofauti?
 
Wassira aliwahi kuanzisha chama chake. Lakini sababu kubwa ya kurudi CCM ni kwamba aliwekewa vizingiti katika biashara zake za samaki na akaona heri arudi CCM. Kitu kingine ambacho kimemsaidia Wassira ni kwamba ni hasimu mkubwa wa Warioba na Kikwete hampendi Warioba. So the enemy of my enemy is my friend.
Hata mimi ningekuwa Wassira nisingerudi nilikokuwa. Jamaa alikuwa Gombe kimaisha sio utani. Ubabe wake kwa hoja za wapinzani wa JMK ndani na nje ya CCM umemfanya akubalike sana kwa bosi wake huyu.
 
Back
Top Bottom