Elections 2010 Wapinzani walipitishiwa hoja zipi bunge la Samwel Sitta?

Kieleweke

Member
Jun 23, 2009
79
8
Inawezekana wengine hatukumbuki na msinicheke.

Najua hoja ya ufisadi wa EPA ililetwa bungeni na Dr. Slaa lakini Samwel Sitta akaikemea kwamba bunge haliwezi kujadili hoja zenye ushahidi wa kwenye internet.

Hivyo Dr.SLaa akaiondoa hoja ile bungeni, akaihamishia Mwembeyanga alipowatangaza mafisadi.

Kumbe, pamoja na hoja ile kutetemesha nchi, bado huwezi kulisifia bunge lililopita na spika wake (Sitta) kwa sababu haikuwahi haikujadiliwa bungeni, na kwa hakika ilizuiwa.

Hoja ya Mkataba wa Buzwagi aliileta Zitto Kabwe lakini badala ya kujadiliwa ikageuzwa kumtaka Zitto athibitishe uongo wa Karamagi. Zitto akatimuliwa bungeni kwa miezi kadhaa.

Hizi ni hoja mbili ninazozikumbuka, na katika hizi huwezi kusema wapinzani bungeni walisaidiwa kivyovyote.

Nakiri sikumbuki vizuri uanzilishi wa hoja ya RICHMOND. Ninachokumbuka Kamati Teule (ya Mwakyembe) ilipoundwa na iliposomwa Lowasa akajiuzulu. Hapa naomba mnikumbushe kwamba ni mbunge gani wa kwanza kuileta bungeni ijadiliwe kama hoja ya bunge.

Na kama kuna hoja zingine ambazo zilianzishwa na wabunge wa upinzani naomba tuzi-list hapa kwa kuweka majina ya wabunge waleta hoja na jinsi zilivyofaulu kupita bungeni.

Nataka kujiridhisha kama ni kweli bunge lililopita liliwa-favor wapinzani kama inavyodhaniwa kwa baadhi yetu, hasa kipindi hiki ambapo kuna mabishano hadi kudhani kuna spika anayeweza kuwa favourable kwa wapinzani.
 
tunashangaa Sitta alikuwa na Matusi nakumbuka aliwahi kumtukana mzee mapesa Dr Slaa na kuwakalisha chini ,wote yeye na chenge hawafai
 
Kieleweke,

Nakushukuru kwa kuleta hoja hii, binafsi nawashangaa wote wanaomsifia Sitta kuwa anafaa kuwa spika wa bunge letu, watetezi wa sitta wanasema Sitta aliongoza vizuri bunge lililopita. Samwel sitta alikwamisha sana hoja nyingi toka upinzani.

Chenge na Sitta hakuna nafuu, wote hawafai
 
Back
Top Bottom