Elections 2010 Wapinzani wajifunze siasa la sivo...

Mbunge wa CCM

JF-Expert Member
Nov 13, 2009
475
22
Kwenye jimbo langu, vyama vingine pia vina wagombea, lakini baada ya kikao cha NEC nilisafiri kidogo nje ya nchi nimerudi sasa na kukuta wansambaza habari kuwa nahojiwa na TAKUKURU!! uongo kabisa

Ni kweli niliingiza nchini vifaa vya kampeni kama pikipiki na magari kadhaa chakavu na hili suala nilisha-clear na TAKUKURU wakati wa kura za maoni.

Juzijuzi nilitoa vifaa vya michezo kwa vijana jimboni baada ya kuombwa kwa maandishi na nikasaida, nayo nimeisha-clear na TAKUKURU, kuna mambo mengi tu nimefanya, ila linalonikera ni hili suala la vifaa vilivyo njiani, vingine ni vya chama, navyo wanasemasema kuhusu TAKUKURU, TAKUKURU wenyewe walishachoka na uzushi.

Nawaambia, kuwa Jumatano vinatoka bandarini na wiki ijayo nasambaza jimbo zima na wajiandae kwa kampeni ya nguvu

Anayetaka kujua kuwa upinzani si kufanya ujinga, ajaribu kuhusisha haya mamabo na rushwa, nitamfunza adabu na atakapopata akili wenzie tulishakuwa wabunge...
 
Hivi ninyi wagombea wa CCM mnaweza kutuambia kwa ukweli hizi hela za kuingiza vifaa mmezipata wapi? Ni kutoka kwa mishahara yenu?
Nasikia madiwani wamepewa shilingi milioni tano kila mmoja. Zimetoka wapi?
 
ndugu yangu, kila kitu ni maandalizi, tumejiandaa kwa muda mrefu, tunafanya savings na tunakusanya nguvu za wafadhili na mengineyo. sasa usitulinganishe na wanaodandia siasa baada ya kuona baadhi wanajaribu na kupata, wengine hatujaribu, tunafanya tena kwa kujiamini, ndio maana tunashinda siku zote na kwa kishindo kikubwa

angalia sasa, kila kitu takukuru, takukuru, hawajui kuwa takukuru wanazingatia sheria hawazingatii tetesi.

ushindi ni lazima
KIDUMU CHAMA CHA MAPINDUZI
 
Wizi mtupu! Hamna hata aibu jamani!
 
Sijakuelewa vizuri Mgombea Ubunge nia yako hasa ya kuandika kwenye JF ni nini?

  1. Una uhakika gani kuwa wapinzani kwenye jimbo lako ni wana JF hata ukapiga mkwara humu?
  2. Nina wasiwasi kuwa wewe si mgombea una lako jambo humu jamvini
  3. Kama wewe ni mgombea wa kwelikweli tafuta the right audience kwenye jimbo.
 
Kweli best huoni mbali, mwenyewe unajua wazi kuwa wapiga kura zako wengi internet ni msamiati na ukuja kuwachimba mkwala hapa jamvini? Si uwatumie vipeperushi wasikusumbue kwa simu na kubwa zaidi kama umezoea kuwapa chochote wakikupigia simu kwanini wasikutafute?
 
jamani mi nilivyomuelewa huyu jamaa ni kuwa hao anaowachimba mkwara wana access na JF, na tena huyu jamaa sio mara ya kwanza kupost humu jamvini mamabo yake ya ubunge na namna alivyojiandaa, nahisi anagombea jimbo moja la mjini amabako watu wana mwamko na internet.... ni mtazamo tu
 
ndugu yangu, kila kitu ni maandalizi, tumejiandaa kwa muda mrefu, tunafanya savings na tunakusanya nguvu za wafadhili na mengineyo. Sasa usitulinganishe na wanaodandia siasa baada ya kuona baadhi wanajaribu na kupata, wengine hatujaribu, tunafanya tena kwa kujiamini, ndio maana tunashinda siku zote na kwa kishindo kikubwa

angalia sasa, kila kitu takukuru, takukuru, hawajui kuwa takukuru wanazingatia sheria hawazingatii tetesi.

Ushindi ni lazima
kidumu chama cha mapinduzi

kigumu chama cha mapinduzi kwa sababu ya kutumia umaskini wetu kama unavyokiri. Ebu ona aibu sema mawili tu umetufanyia nini hadi sasa kwa jinsi maisha yanavyokuwa magumu kila siku. Pili kweli umefanya maandalizi hayo ili urudisheje gharama zako? Kwa kweli ndugu mgombea unaleta kichefu chefu kwenye serious discussion.
 
Back
Top Bottom