Wapinzani Tanzania ni Wanafiki - SAMWEL SITTA

Baada ya hapo wabuge waliendelea kubishana bila utaratibu, mpaka muda wa kikao ulipokaribia kwisha alitumia madaraka yake kuahirisha kikao hicho akisema: "Sasa muda umekwisha Nanahairisha shughuli za Bunge hadi jioni."Baada ya hapo wabunge walikaa kimya hadi alipotoka ukumbini na baadhi ya wabunge wakalipuka na kuanza kuimba wakisema: "CCJ! CCJ! CCJ!…."

Hiyo ilikuwa ni zomea ya wabunge dhidi ya Samweli Sitta alipoonekana mwiba bungeni kutetea maslahi ya posho

Mwananchi
 
Kafulila alisema inawezekana serikali kuwekeza katika sekta ya afya vijijini, kwani nchi hii ni tajiri.
"Tanzania ni nchi tajiri, lakini ni taifa la saba kwa kupatiwa misaada duniani, tunaongozana na nchi zenye machafuko. Haiwekezani," alisema huku akionyesha jarida la Ecomomist.
Akizungumzia bima ya afya, Kafulila alisema kitendo cha kutopatikana dawa ni utapeli kwa wananchi.

Tanzania Daima
 
Ni baada ya kuambiwa watoto wake na yeye kama waziri wanatibiwa nje hawawezi kutibiwa hospitali za Mwandiga pamoja na kina Kalumanzila.

Licha ya muda kwisha, baadhi ya wabunge wa upinzani waliwasha vipaza sauti na kuanza kumzomea kwa kumwita msaliti kwa vile alikuwa mmoja wa waasisi wa CCJ. Katika zomeazomea hiyo, wabunge hao walikuwa wakiimba CCJ, CCJ...

Pamoja na juhudi za mwenyekiti Jeniffa Mhagama kutetea kutotaja majina kwa kuwa ndani ya bunge kuna Sitta waziri na Sitta asiye waziri sauti zilisikka zikisema 'vyovyote vile utachagua ni yupi anayetibiwa nje'

Source: Tanzania Daima
 
Sita sasa na yeye imefika wakati wa kumtosa alijifanya mpiganaji kumbe ni ndumilakuwili tuu!
 
Yeye anawaita wapinzani wanafiki wakati yeye mwanzilishi wa CCJ huku akijifanya mstari wa mbele CCM?
 
Huyoo ndiye Sitta kamanda wa vita dhidi ya ufisadi huku akijenga Ofisi ya Spika kwenye jimbo lake utadhani Jimbo la Urambo ndilo lingekuwa linatoa spika wa kudumu!!! Sijui kama Anne Makinfa naye atajenga Ofisi ya Spika huko kwao Njombe!
 
Kwani Sitta ni nani jamani,si amekuwa historia ,haitajiwi hata kujadiliwa humu,Sitta ni sawa na Maalimu Seifu kelele zote ni kutaka cheo,na JK kamvika kilemba cha ukoka,sasa anabweka hovyo kama vile mbwa aliyesikia miluzi mingi,hajui afanye nini,miluzi imempoteza kabsa sasa naye ni NDIOOOOOOOO,papapa kwenye meza pale mjengoni
ha haaaaaaaaaaaaanimeipenda sana hiii aiseee!!
 
nanukuu kama pastor wa iriinga alivyo sema mnafiki ni yulea nayeanzisha chama ndani ya chama na c mtu ane pinga posho
 
Pro-CDM-JF, bana kwa kukurupuka walikuwa wanajidanga eti Sitta mwenzetu kamanda wa kupinga ufisadi, leo kawageuka kawaita wanafika
 
Kwani kasema uongo? Ni kweli wabunge wa CDM ni wanafiki.
unafiki unaousema uko wapi iwapo UCHUMI WA NCHI "UNATAMKWA" KUKUA KWA ASILIMIA KARBU 7 WAKATI MASIKINI WAMEONGEZEKA TOKA MILION 11 HADI MILL 14?? Nani kajivua gamba hadi sasa? we wa hovyo sana!
 
hivi mnafiki ni nani anayetetea maslai ya wananchi au anayeanzisha chama akiwa ndani ya chama ni sawa na mtu yuko ndani ya kanisa anaanzisha kanisa tena
 
Kwa hali iliyofikia Chama Cha Magamba sasa hivi ni kama kuangalia ajali ya gari kwenye slow motion. Wanatia huruma na kujipotezea heshima.
 
Back
Top Bottom