Wapinzani Tanzania ni Wanafiki - SAMWEL SITTA

Kutoa hoja ya msingi wakati wewe mwenyewe huchukui jukumu la kuishi maisha hayo ni Unafiki! tumewaona kina Seif Sharrif hhamad hapa wakipiga vita wagonjwa kupelekwa India kwa matibabu lakini siku aloumwa yeye aligeuka na kudai ni haki yake kama kiongozi na akaitumia sheria alokuwa akiipiga vita kama ushahidi wa haki yake. Huu ni Unafiki!.

Tazama wabunge wa CUF Zanzibar wanapiga vita Muungano lakini wanapokea misaada yote toka bara na bado wanajiandikisha kuchaguliwa kuwa wabunge ktk bunge la Jamhuri na wamefikia hadi kurekebisha katiba kukidhi matakwa yao wao wenyewe ya kiuongozi hali wakiwa bungeni kila siku ugonvi ni muungano. Unapinga Muungano wakati huo huo unasaini muafaka wa kiutawala unaotuunganisha! huu ni Unafiki!..

Kwa hiyo Sitta anapozungumzia kambi ya Upinzani ni wanafiki hajakosea kabisa na imefanywa makusudi kabisa kuwanyima Chadema mamlaka ya kuchagua viongozi wake. Ndio maana tumeona wenyeviti wa kamati tofauti wakichaguliwa na CCM toka kina Mrema, Cheyo, Zitto na wengineo wakipewa dhamana ili Unafiki wao ujitokezee!


Inawezekana unalosema ni sahihi. Sasa solution ni nini? Mapendekezo/ where do we go from here? Je name calling itamaliza tatizo? Argument ni nzuri kama ikiwa constructive ili tufikie goal yetu (kuwaondolea kero wananchi).

Lakini hii imeishia kwenye jazba na miongozo tu. As I see it, unapotaka soln ya kitu unaanza kwanza na neutral discussion bila kufanya character assassination, then ukishapata jibu au mkisha exhaust all options wakati wakufunga mjadala ndio unaweza ukatoa yaliyoko moyoni. Lakini ukianza na character assassination hamuezi kuwa na substance kwenye mazungumzo.

Na hii sio kwa CCM tu bali na Upinzani pia. I should also say; Sitta pamoja na mapungufu yake nilikua namuona mkomavu flani hivi kwenye haya mambo, lakini kaniangusha sana. Huwa anamisimamo yake peke yake hata kama hayuko sahihi. Lakini anaanza kunistua sasa. Labda amejikwaa sijui ngoja tuone.
 
Sita ni NDUMILAKUWILI NA MBINAFSI wa ajabu. Kelele zote zilikuwa ni kutafuta nafasi za juu sasa kapata anapumua na kucheua nyama choma.Ni Mnafiki toka alipoanzisha CCJ kutafuta Urais. Ni ndumilakuwili anauma pande zote kama joka la mdimu.
Na mijitu ya namna hii ni mibaya sana,kazi yake kubwa ni kung'ata na kupuliza,MACHUMIA TUMBO.
 
Sita ni NDUMILAKUWILI NA MBINAFSI wa ajabu. Kelele zote zilikuwa ni kutafuta nafasi za juu sasa kapata anapumua na kucheua nyama choma.Ni Mnafiki toka alipoanzisha CCJ kutafuta Urais. Ni ndumilakuwili anauma pande zote kama joka la mdimu.
amekera watanzania kiongozi kama ndivio basi !
 
Inawezekana unalosema ni sahihi. Sasa solution ni nini? Mapendekezo/ where do we go from here? Je name calling itamaliza tatizo? Argument ni nzuri kama ikiwa constructive ili tufikie goal yetu (kuwaondolea kero wananchi).

Lakini hii imeishia kwenye jazba na miongozo tu. As I see it, unapotaka soln ya kitu unaanza kwanza na neutral discussion bila kufanya character assassination, then ukishapata jibu au mkisha exhaust all options wakati wakufunga mjadala ndio unaweza ukatoa yaliyoko moyoni. Lakini ukianza na character assassination hamuezi kuwa na substance kwenye mazungumzo.

Na hii sio kwa CCM tu bali na Upinzani pia. I should also say; Sitta pamoja na mapungufu yake nilikua namuona mkomavu flani hivi kwenye haya mambo, lakini kaniangusha sana. Huwa anamisimamo yake peke yake hata kama hayuko sahihi. Lakini anaanza kunistua sasa. Labda amejikwaa sijui ngoja tuone.
Nakuelewa sana mkuu wangu lakini bado hujapata jibu la UNAFIKI. Mtu mnafiki, hakuna sababu ya ku discuss kitu hali ukijua rohoni anataka kitu tofauti yaani hajali matokeo ya upande wowote..Kwa mtu kama huyu hakuna mahala pazuri pa kuanzia kama kumwambia wazi usoni mwake kabla hajaanza! Hapa tunazungumzia wanafiki na jinsi ya kukabiliana nao.


Na labda nichukulia maelezo yako yote kwa kufupisha kwamba chukulia huyo Kafulila, hadi leo sielewi sababu ilomfanya akahama Chadema! sielewi zaidi ya kupigwa chini ktk uongozi wa Vijana akahamia NCCR na sii kwa sababu ya kiitikadi bali kutokubaliana na viongozi wa CDM ambao yeye mwenyewe anawaona wanafiki na upande wa pili wanamwona yeye mnafiki - hivyo ktk unafiki character assassination ni njia mojawapo ya kujikosha upande wa pili ambao pia ni wanafiki (nyani haoni kundule)..

Kifupi hatuna watu wengi bungeni wanatuwakilisha hatuna majuzi tu Lipumba naye alikuwa India, na ati kwa kuokoa nauli na malazi wameamua kuwaleta Apollo wawekeze nchini wakati uwezo wa kugharamia ya ujenzi wa Hospital kama hiyo nchini tunao.. Na wala sii kwamba hatuna fedha lakini ndio hayo ya posho na malupulupu hawataki kuachia. Pia nakuhakikishia kwamba hata madaktari mabingwa wa kufanya upasuaji tunao wengi wanafanya kazi Brazil na Marekani isipokuwa wanashindwa kuja kwa sababu hakuna matayarisho ya maana kwa ajili yao.

Na nikisema matayarisho utawasikia Wabongo wakilalamika matayarisho gani? kama wanataka kurudi warudi lakini wakati huo huoi wanapinga due citizenship. Wanapinga duo citizenship lakini wanakubali wahindi waje kuinvest hiyo Apollo nchini kwa gharama kubwa za kuwalipa madaktari wao na bila shaka kubwa kuliko hata fedha ambazo wazawa wangelipwa wakiwa wamerudi nyumbani.

Kwa hiyo ktk kila kipengele Mbongo lazima apinge na atapinga hilo pasipo kuwa na solution ili mradi tu anapinga kufurahisha baraza. Na akitoka hapo utamsikia akijisifia kamzima mdomo fulani.. tunayaona Bungeni na mitaani yaani sifa ya Mbongo ni kusema sana na ktk kusema sana ndiko sifa zake zinapatikana hali ufanisi ktk matendo yake ni zero!

Utanisamehe mkuu lakini waulize wabunge woote hao, wamewafanyia nini wananchi wao waliowachagua - Hakuna, isipokuwa sifa zoote wanazitafuta bungeni mahala ambapo CV zao za kuuchonga mdomo ndiko zinapatikana.
 
..he is finally revealing his true colors.

..Sitta hana matatizo na ufisadi, ana matatizo na Lowassa.

..hawa walizidiana mahesabu ktk nafasi ya uwaziri mkuu.

..kama Sitta angekuwa anachukia ufisadi, na ufujaji mali za umma, basi asingetumia mabilioni ya fedha kujijengea ofisi ya Spika wa Bunge jimboni kwake Urambo.
 
Alipoanza kumjibu Kafulila nilidhani atasimamia ule usemi wake wa wanasiasa wanatakiwa kuwa na ngozi ngumu!Lakini akarudi kulekule kwenye kuteteana badala ya kujibu hoja.Sitta next time usifurahishe chama tetea watanzania kama unavyojiita mpambanaji sijui na ufisadi na kutetea watz.Neno legelege linawafanya mzalilike?Mmelewa na nyimbo za kina Komba na wasanii njaa kipindi cha uchaguzi?
 
Kuna kipindi nilisema Mhe.samwel sitta ni mtu aliyekaa kimaslahi maslahi tu.Amekaimishwa uongozi wa shughuli za serikali bungeni na ameonyesha rangi yake halisi.Kumbe fikra zake juu ya vyama mbadala ndiyo hizo?Mtu ambaye amekuwa spika wa bunge?Huyu vita yake ni ya kimaslahi zaidi,i dont take hime serious!
 
nimekuwa nikiandika humu kuwa samweli sitta ni kiongozi mnafiki na wanaomfagilia ni wajinga, nimechagua neno zuri wajinga.

Tangu aliposimamaia vita ya kumkomoa lowasa kwa mgomgo wa vita vya ufisadi nimemdharau huyu mzee!

Kwa bahati mbaya sana wengi humshangilia ......tiafa la waliochoka kufikiri. Leo tena ametukana watanzania wanaokosa huduma za afya kuwa yale malalamiko ni unafiki!

Hongera kafulila kwa unafiki wa kuwatetea wanyonge!

Hivi kama wizara ya afya inapewa fedha kidogo halafu mwisho wa mwaka fedha hizo kidogo zinatolewa nusu hivi wanaoitetea serkali kuwa ni legelege wana akili za za wapi!

Tulishasoma humu kuwa wizara yenyewe inanunua suti 2000 toka uingereza kwa ajili y 77 na 88 ,watazania tunachekea tu,
afu kina mama wanakufa tunasema hakuna fedha!

Kwa ujinga huu hata shetani anaweza kutukana kuwa si wake kwa sababu akili zetu ni ndogo na hazina msaada kwake!

Eeh mungu mlaani samweli sitta na wale wote wanaotuona kuwa watanzania ni wajinga!

Kuna siku mungu atatupa nguvu kuushinda upumbavu huu!
kwa tukio la leo nimejifunza sitta ni mtu
 
Chachu kidogo huchachua donge nzima. Sifa na umahiri wote wa samwel umechachuka kwa maneno yake dhidi ya upinzani. Eti hoja za upinzani bungeni hazina mantiki ni unafiki! Hata sakata la rada nalo ni unafki? Kama anadhani kuwa kauli yake ni sahihi, basi juhudi zake dhidi ya dowans ni unafiki mtupu, bila shaka alilenga kulipiza kisasi. Ktk hili la hoja za upinzani kudai maslahi ya wanyonge yanayonyonywa na viongozi wa serikali "sikivu" kuitwa unafki halikubaliki ng'oo. Hoja nyingi za upinzani ni sahihi, watanzania wengi wanajua na dunia nzima inajua.
 
Kama maneno ya Sitta ndio haya mimi sioni makosa yake. Mnafiki ni mtu ambaye kauli zake zinakwenda tofauti na matendo yake. Sasa kama wabunge wa kambi ya Upinzani kina Kafulila wanapinga posho hali zikitolewa wanachukua ndio unafiki wenyewe huo.Ni bora hao kina Sitta wanaopendekeza Posho wazi na kuendelea kuchukua kuliko wabunge wanaopinga posho lakini nyuma ya pazia wanapokea posho hizo na kujipanga ktk misafara ya kupokea posho...Kifupi hili neno Mnafiki itabidi tulizoee kwa sababu ni utamaduni mpya tulojifunza baada ya kuingia Ubepari. Asilimia kubwa ya viongozi wetu ni wanafiki na hakika wengi wao wameingia ktk SIASA ili kujinufaisha wao, ni wachache sana waloingia kwa manufaa ya umma na hao wachache wanapigwa vita kila siku.
Magamba Camp. Umepigwa upofu wala huelewi mema na mabaya. Sita na alaaniwe maana anapinga watetezi wa wanyonge, Mungu ni wetu sote lakini kama unafanya dhambi kwa kukusumdia na ukategemea msamaha, u are finished kabisa. Mungu sikia kilio chetu wanyonge. Na mimi nawahakikishia ni mpiga kura wake SITA, ila kwa hili nimegundua kuwa huyu si mbunge wangu na mtetezi wetu, yuko upaode mwingine wa shiringi. I Hate u Sitta.
 
6 Siku zote yuko strategic sana na mambo yake. chunguza kauli zake, utagundua kila anachosema kina maana fulani nyuma ya pazia.
Nina wasiwasi kama anajaribu kujikomba kwa mwenye kaya vile....? kuna jambo labda kali target vile so kulipata inamlazimu kujikomba kwa mwenye kaya. Na kujikomba ni kutamkatamka vile apendavyo.
 
Kaimu Waziri Mkuu Samwel Sitta amesema Wapinzani ni Wanafiki kwani kuna Wabunge wamekuwepo Bungeni miaka mitano Bunge lilillopita na Kuchukua posho leo wanasema hawazitaki posho! Amesema warudishe posho walizo chukua miaka mitano iliyopita!
Source TBC1 kutoka Bungeni
 
Sasa nimeamini kua ule uhuru wa wa wapinzani kuleta hoja pale bungeni tena hoja yenye tija na ni kwa manufaa ya wananchi wote bila kujali ni wa chama gani, lakini kitendo cha spika pamoja na wale manaibu wake akiwepo Ndungai kweli kwenye kile kikao cha jumanne jioni kwa wabunge wa chama pinzani akiwepo muheshimiwa mchungaji Msigwa pamoja na mamaa Mdee kuwasilisha hoja japokua muda haukua unatosha, kweli sio kitendo cha kiungwana kuwakatisha wabunge tena wa chama pinzani kuleta hoja ya msingi halafu naibu spika unawakatisha wabunge wa upinzani waziwazi na sisi watanzania wavuja jasho tunaona hii si halali!

Kweli nasema na ninatabiri vizazi vinavyokuja vitakuja kuwahukumu kama sio wewe Ndungai pamoja na bosi wako Anne Makinda kwa vitendo mnavyovifanya hapo bungeni, hii inasikitisha tena mno! Sina mengi ya haya bali watanzania wenye kuishi kwa matumaini ya maisha bora kwa kila mtanzania! japokua imeshageuka na kua sijui kwanini watanzania ni masikini! hii haitasaulika kamwe TIME WILL TELL! Bunge linaloendelea hapo Dodoma haliko fair kwa wapinzani wenye uchungu kwa kutoa hoja yenye manufaa kwa wananchi wenye maisha duni, tunakwenda wapi Anne Makinda/Ndungai na manaibu akiwepo mwenyekiti kama kweli mnauchungu na nnchi hii? Nawasalisha!
 
CDM ukweli huwa unakusumbueni sana! Je hakuna wabunge ambao miaka mitano illiyopita waliramba posho? Wazee wa Magwanda kubalini hili kweli kuna Unafiki hapa! Mlitaka Sitta asemeje? Tanzania tuna Wapinzani Wanafiki hasa wavaa magwanda! ambao kwao wakiambiwa ukweli hugeuka kuwa maadui wa aliye wasema kwa uovu wao!
 
Amefulia, anajutia kufanya maumuzi magumu enzi zilee za dowans!! Sasa ameukwa ugonjwa wa kuogopa kufanya maamuzi magumu. Ni heri kuwa na kiongozi anayeonja rushwa kdogo ila mchapa kazi, anawaokoa wa tz na dimbwi la umaskini, kuliko ajifanyaye mwadilifu ila mshabiki wa maisha duni kwa wa tz!
 
Kwa kauli hiyo na kwa nafasi yake kumkaimu waziri mkuu,Sitta amedhihirisha kuwa hata IQ yake ni ndogo sana maana kuwa bungeni hata ingekwa kwa miaka 20 bado uamuzi wa kuona suala la posho sasa basi lilikuwa la kishujaa sana.haijalishi unaanzia wapi but CCM imekuwa madarakani miaka 40 sasa mbona hawakuwahi kufikiri kupunguza gharama kwa ustawi na maendeleo ya nchi!!Kwa mantiki hii pamoja na idadi ndogo ya wabunge wa upinzani bado quality yao ni kubwa sana ndio maana CCM wamechanganyikiwa kiasi hiki!!Hii ni sawa na jeshi dogo lenye ndege na vifaa vichache vya kisasa linavyoweza kusambaratisha jeshi kubwa lenye vifaru kibao lisilo na techniques.Bravo Kafulila na wapiganaji wengine,long live CDM.
 
Back
Top Bottom