Wapinzani Tanzania ni Wanafiki - SAMWEL SITTA

'HATA AKITUA MALAIKA NDANI YA CCM HAWEZI KUPAMBANA NA UFISADI' Maneno hayo aliyatoa Dr. Slaa kwenye mkutano wa kwanza wa kampeni pale Jangwani.Ni muda mfupi sana tangu alipoitoa kauli hii na tayari imejidhihirisha watu wengi waliokuwa wanajifanya makamanda wa UFISADI wameota magamba makubwa zaidi ya kobe.But we know that time will tell.
 
Mizee inayozeeka bila kuwa na adabu,ni mnafki tu hana lolote huyoo anadhani atakuja kuwa waziri mkuu,shame on hiiiiimmmm.
 
Sita kama kuna mtu wa kuogopwa yule ni mnafiki kuliko wote bungeni huwa anacheza na popularity
Mkuu thats how politics games played, au umesahau CMD wanachezaje huu mchezo.
Sita kuanzisha CCJ kunadhambi gani? mnataka kuniambia maneno anayo zungumza Slaa leo ndio alizungumza akiwa CCM?
Siku zote sita atazungumza kama sita na mwana CCM, lakini huwezi kupuuzia utendaji wake kwa kuwa hafikirii unavyofikiria wewe
 
Kwani kasema uongo? Ni kweli wabunge wa CDM ni wanafiki.

Binadamu ndivyo tulivyo! mtu akisema ukweli tunamkatisha tamaa kwa kumwita mnafiki!labda unafiki hatujuhi maana yake halisi! hwbu sikililiza michango yote ya wabunge wa CCM,ni kuilalamika juu ya huduma,bajeti mbaya na mengine!!!!!baadae tena mtu anasema anaunga mkono hoja,wakati kaponda na malalamiko kibao....sasa unaunga mkono hoja ipi?wakati unalalamika.

Kafulila amesema ukweli mtupu! sasa unafiki wake uko wapi?kwani ni haki kutegemea 98%ya pesa ya maendeleo ya afya yatoke kwa wafadhili? wakati wabunge wanajilipa posho kwa kodi za wananchi?
 
Kwani kasema uongo? Ni kweli wabunge wa CDM ni wanafiki.
kwani unafiki ni nini? Kuzungumza uongo au kusema ukweli? Nani muongo kati ya wabunge wa CDM na CCM? Tukiwa na jibu ndio tutajua kweli nani mnafiki na pia kama yeye Sitta anaamini kuwa wahukumu ni wananchi basi atakuwa amekosea kutoa hukumu yeye bila kusubiri hukumu ya wananchi.
 
kujisahihisha kwa mambo unayodhani ulikuwa unafanya ndivyosivyo hauwezi kuwa unafiki. Unafiki ni kutoa hoja nyepesi kama wabunge wa ccm pamoja na huyo samwel sitta kuwa ati wabunge wa upinzani walikuwa wapi??. Hoja ya kujadili ni je, posho za vikao wanazo pewa wabunge zinastahili au la?

sure mkuu!kwa hiyo sitta anasema km mtu umeishakosea usirudi nyuma!hata kwenye dini kuna kutubu!
Hicho kisiwe kisingizio cha kupindisha hoja!waache kula kodi za wananchi vibaya!
 
Kumsikiliza Sitta ni heri nikaangalie sanaa za maonesho kwakua nikielelezo cha viongozi mufilisi
282560_10150244713041193_594661192_7869259_1528593_n.jpg
 
nilipata kusema huko nyuma kuwa kati ya wanasiasa wanafiki sana ni huyu sita na mwakyembe,nawahukumu kwa kuficha ukweli halisi wa ripoti ya kamati ya kuchunguza richmond,hawa wangekuwa wakweli basi hili swala la umeme na mwelekeo wa siasa na kiuchumi ungekuwa umebadilika,kwa unafiki wao leo hali ni mbaya
 
I will have to search for the exact words that Mzee Sitta has used. BUT if what is reported here is correct then Mzee Sitta is becoming another bother himself!

If you discover that you have been doing an incorrect thing it is always good to amend and move in the right way. Opposition MPs have been taking the so called "posho" in the past but they now feel the same has to be scraped. What is wrong with this?! Because they have been taking posho in past they do not have the right to question whether or not posho is right?

Mzee Sitta should look at it in a more critical way and come up with something more reasonable.

Again I will verify what excatly Mzee Sitta said before passing the verdict.
 
Sioni kosa la sita, kwani unafiki ni nini? Ni neno baya? Si ametumia uhuru wa kutoa maoni? Mlitaka mwana ccm aipigue mapambio kambi ya upinzani?
 
Unapoleta mada ya kujadili hapa si wote walioshuhudia matamshi ya Samweli Sitta bungeni. Ujitahidi kuandika paragrafu inayoelezea habari kamili ili tuelewe nini unaongelea, maana hapa naona tu malalamiko na hujaleta habari iliyokamilika tukasoma, tukaielewa na kuanza kuchangia. Tunapoleta mada hapa tutumie utaratibu wa kitaaluma, vinginevyo itakuwa ni kama flag, au sentensi isiyokamilika kwa muundo wa subject and predicate. Sijui nichanangie nini
Pointi ,,,,, maana nimejaribu kufikiria nikashindwa kumuelewa mwenzetu
 
Kwa wale mliofuatilia bunge leo mtagundua kuwa SS mzee ni mnafiki/mpumbavu kuliko maelezo! He lost his bearing......No wonder CCM walimpiga chini nafasi ya Uspika.
 
SITA AMESEMA HIVI

MH SAMWELI SITTA:

Anasema angewasihi Wabunge wa CCM kuwa hawa wapinzani hawa ndio kazi waliyotumwa kuifanya wapinzani ni Wanafiki na mambo yao mengi yamekaa kinafikinafiki, Mfano kuita posho za vikao ni kuibia wananchi na baadhi yao wamekaa humu miaka mitano wakila posho sasa leo wanaziita kuwa si halali, hivi kweli wananchi watawaamini hawa.

wataendelea kuwa hivi hivi na kubaki wapinzani

Miongozo imechachamaa

Mhagama anasitisha shughuli za Bunge huku Mic zote zipo on KAMA SOKONI Aiseee
Kama maneno ya Sitta ndio haya mimi sioni makosa yake. Mnafiki ni mtu ambaye kauli zake zinakwenda tofauti na matendo yake. Sasa kama wabunge wa kambi ya Upinzani kina Kafulila wanapinga posho hali zikitolewa wanachukua ndio unafiki wenyewe huo.

Ni bora hao kina Sitta wanaopendekeza Posho wazi na kuendelea kuchukua kuliko wabunge wanaopinga posho lakini nyuma ya pazia wanapokea posho hizo na kujipanga ktk misafara ya kupokea posho...

Kifupi hili neno Mnafiki itabidi tulizoee kwa sababu ni utamaduni mpya tulojifunza baada ya kuingia Ubepari. Asilimia kubwa ya viongozi wetu ni wanafiki na hakika wengi wao wameingia ktk SIASA ili kujinufaisha wao, ni wachache sana waloingia kwa manufaa ya umma na hao wachache wanapigwa vita kila siku.
 
mara zoote huwa nasema ccm ni kusanyiko na wajinga na walafi watu mnabisha, sasa leo mmejua kuwa hakuna alieimamu ? hao ni genge la walaji na walafi katika sekta ya umma, huyo mbabu Sitta hana huruma hata chembe na WATANZANIA.
 
Kama ishu yenyewe ndo hivyo kwanini unamuita mh sitta mnafiki ni kipi hasa kinakupelekea wewe kumuita yule mzee mnafiki..
 
Sioni kosa la sita, kwani unafiki ni nini? Ni neno baya? Si ametumia uhuru wa kutoa maoni? Mlitaka mwana ccm aipigie mapambio kambi ya upinzani?

Mkuu hili ndilo tatizo kubwa tulilonalo Watanzania.

Sio swala la kupigia mapambio upinzani ni swala la hoja. Kwanini tusiangalie kama hoja ina mantiki au la na siyo aliyeleta hoja? Kama hoja ya Kafulila kwangu mimi ina mantiki kabisa ukiitazama kwa undani; sasa mipasho ya nini?

Sitta kwenye hili ameniangusha kabisa, sikujua anaweza kushabikia vitu bila kuchambua. Hata kama yeye alishatibiwa nje fine; sheria iliopo inamruhusu hivyo. Sasa tufanyeje kuwasaidia majority? (Sitta ana mapendekezo yeyote anaweza kutoa kuiboresha sekta ya afya kwaajili ya majority?)

Kama hana then aachie wengine wachambue; tunataka tujue wapi tunakosea/babaisha then tufanye marekebisho kwa manufaa ya taifa letu. Kwa staili hii kweli unafikiri tunaweza kupata solution ya kitu chochote?
 
Siasa za Tanzania tumezizoea za kuponda au kuunga mkono kutegema wakati huo hupo upande gani.Umakini wa fikra sahihi hufutika tu pale wanapokwaa post za upande wa utawala watafagilia kila kitu ziwe pumba au chochote kilichombele ya high table.Hao wanaotema makapi ukiwabadirisha leo uwatoe upande wa utawala wawe backbencher utasikia makombola ya nguvu yakiilenga serikali kwa usahihi.Kinachotusumbua ni unafiki,majungu,mizengwe,njaa. Na sisi wananachi wa kawaida bila kujua tunapoteza muda kushangilia mipango tasa.
 
Mkuu hili ndilo tatizo kubwa tulilonalo Watanzania. Sio swala la kupigia mapambio upinzani ni swala la hoja. Kwanini tusiangalie kama hoja ina mantiki au la na siyo aliyeleta hoja? Kama hoja ya Kafulila kwangu mimi ina mantiki kabisa ukiitazama kwa undani; sasa mipasho ya nini? Sitta kwenye hili ameniangusha kabisa, sikujua anaweza kushabikia vitu bila kuchambua. Hata kama yeye alishatibiwa nje fine; sheria iliopo inamruhusu hivyo. Sasa tufanyeje kuwasaidia majority? (Sitta ana mapendekezo yeyote anaweza kutoa kuiboresha sekta ya afya kwaajili ya majority?) Kama hana then aachie wengine wachambue; tunataka tujue wapi tunakosea/babaisha then tufanye marekebisho kwa manufaa ya taifa letu. Kwa staili hii kweli unafikiri tunaweza kupata solution ya kitu chochote?
Kutoa hoja ya msingi wakati wewe mwenyewe huchukui jukumu la kuishi maisha hayo ni Unafiki! tumewaona kina Seif Sharrif hhamad hapa wakipiga vita wagonjwa kupelekwa India kwa matibabu lakini siku aloumwa yeye aligeuka na kudai ni haki yake kama kiongozi na akaitumia sheria alokuwa akiipiga vita kama ushahidi wa haki yake. Huu ni Unafiki!.

Tazama wabunge wa CUF Zanzibar wanapiga vita Muungano lakini wanapokea misaada yote toka bara na bado wanajiandikisha kuchaguliwa kuwa wabunge ktk bunge la Jamhuri na wamefikia hadi kurekebisha katiba kukidhi matakwa yao wao wenyewe ya kiuongozi hali wakiwa bungeni kila siku ugonvi ni muungano. Unapinga Muungano wakati huo huo unasaini muafaka wa kiutawala unaotuunganisha! huu ni Unafiki!..

Kwa hiyo Sitta anapozungumzia kambi ya Upinzani ni wanafiki hajakosea kabisa na imefanywa makusudi kabisa kuwanyima Chadema mamlaka ya kuchagua viongozi wake. Ndio maana tumeona wenyeviti wa kamati tofauti wakichaguliwa na CCM toka kina Mrema, Cheyo, Zitto na wengineo wakipewa dhamana ili Unafiki wao ujitokezee!
 
Nimekuwa nikiandika humu kuwa Samweli Sitta ni KIONGOZI mnafiki ,na wanamfagilia ni WAJINGA,nimechagua neno zuri WAJINGA.
Tangu aliposimamaia vita ya kumkomoa LOWASA kwa mgomgo wa vita vya ufisadi nimemdharau huyu mzee!
Kwa bahati mbaya sana wengi humshangilia ......Tiafa la waliochoka kufikiri
Leo tena ametukana Watanzania wanaokosa huduma za afya kuwa yale malalamiko ni UNAFIKI!hoNGERA KAFULILA kwa UNAFIKI WA KUWATETEA WANYONGE!
hivi ;;;kama wizara ya afya inapewa fedha kidogo halafu mwisho wa mwaka fedha hizo kidogo zinatolewa nusu hivi wanaoitetea serkali kuwa ni LEGELEGE WANA AKILI ZA ZA WAPI!
tULISHASOMA humu kuwa wizara yenyewe inannua suti 2000 toka Uingereza kwa ajili y 77 na 88 ,Watazania tunachekea tu,
Afu kina mama wanakufa tunasema hakuna fedha !
Kwa ujinga huu hata shetani anaweza kutukana kuwa si wake kwa sababu akili zetu ni ndogo na hazina msaada kwake!
EEH MUNGU MLAANI SAMWELI SITTA NA WALE WOTE WANAOTUONA KUWA WATANZANIA NI WAJINGA!
KUNA SIKU MUNGU ATATUPA NGUVU KUUSHINDA UPUMBAVU HUU!
Sita ni NDUMILAKUWILI NA MBINAFSI wa ajabu. Kelele zote zilikuwa ni kutafuta nafasi za juu sasa kapata anapumua na kucheua nyama choma.
Ni Mnafiki toka alipoanzisha CCJ kutafuta Urais. Ni ndumilakuwili anauma pande zote kama joka la mdimu.
 
Back
Top Bottom