Elections 2010 Wapinzani Mbeya waazimia kumuunga mkono Dk. Slaa

Njowepo

JF-Expert Member
Feb 26, 2008
9,710
2,226
Na Thobias Mwanakatwe

Mgombea ubunge wa Jimbo la Kyela, Dk. Harrison Mwakyembe (CCM).
Umoja wa vyama 10 vya upinzani katika Jimbo la Mbeya Mjini ambavyo vimemsimamisha mgombea ubunge mmoja, Prince Mwaihojo (CUF), umetangaza kumuunga mkono mgombea urais kupitia Chadema, Dk. Willibrod Slaa.
Hatua hiyo imefuatia kitendo cha Dk. Slaa kumpigia kampeni mgombea ubunge wa Jimbo la Kyela, Dk. Harrison Mwakyembe (CCM).
Mwenyekiti wa shirikisho hilo, Godfrey Davis, aliwaambia waandishi wa habari jana kuwa kitendo kilichofanywa Dk. Slaa kinaungana na kauli mbiu ya shirikisho hilo ya “Mbeya kwanza vyama baadaye” ambayo inalenga kuweka kipaumbele katika maendeleo ya Mbeya na si vyama.
Davis alisema kufuatia kitendo cha Dk. Slaa kumnadi mgombea wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Dk. Harrison Mwakyembe ilihali chama chake kimesimamisha mgombea wake katika jimbo hilo la Kyela ni cha kishujaa kinacholenga kuwaelekeza Watanzania katika mabadiliko ya kuwaletea maendeleo bila kujali itikadi za vyama
Alisema ujasiri wa Dk. Slaa kuamua kumnadi Dk. Mwakyembe hadharani huku chama hicho kikiwa kimesimamisha mgombea kilionyesha wazi kuwa ni kiongozi mwenye dhamira ya kweli ya kuwatumikia wananchi.
Wakati wa kuundwa kwa umoja huo, vyama hivyo vilitoa tamko la kutowapinga wagombea wanne wa CCM, Dk. Harrison Mwakyembe, Prof. Mark Mwandosya (Rungwe) Mashariki, Prof. David Mwakyusa (Rungwe) Magharib na Godfrey Zambi (Mbozi Mashariki) kwa imani kuwa viongozi hao hawajaweka mbele maslahi ya chama chao bali ya wananchi katika utumishi wao.
Umoja huo unaundwa na APPT-Maendeleo, CUF, NCCR-Mageuzi, TLP, UDP, Tadea, Jahazi Asilia, Demokrasia Makini na AFP.
Akiwa kwenye kampeni katika jimbo la Kyela, Dk. Slaa, alilazimika kumnadi Dk. Mwakyembe, badala ya mgombea wa Chadema, Eddo Makata, kufuatia wananchi kumweleza kuwa chaguo lao kwa nafasi ya ubunge ni Dk. Mwakyembe.
CHANZO: NIPASHE
MYTAKE
Wamesoma alama za nyakati
 
tunasubiri lipumba nae atangaze hivyo wiki moja kabla ya uchaguzi, na awaambie wafuasi na wanachama wake kuwa kura zote walizotaka kumpa yeye wampe Dr. Slaa.
 
Chonde chonde Lipumba si usome alama za nyakati basi Uwazili wa fedha na uchumi utakuwa wako
 
tunasubiri lipumba nae atangaze hivyo wiki moja kabla ya uchaguzi, na awaambie wafuasi na wanachama wake kuwa kura zote walizotaka kumpa yeye wampe Dr. Slaa.

Akifanya hivyo atakuwa amefanya la maana sana japo uwezekano wa kufanya hivyo ni mdogo kwani yeye inasemekana ni moja wa watu wanaochukua bahasha kutka kwa Rostam Aziz ambaye matakwa yake ni Kikwete ashinde ili aendelee na ujangili wake wa kuhujumu uchumi wa nchi yetu.
 
Ila naamini ule usemi kuwa Lipumba nae yuko kwa ajili ya kuvuruga upinzani tuu
 
Back
Top Bottom