Wapigania uhuru wa Zanzibar waungwe mkono!

Kwanza niwashukuru wakuu, leo nimefarijika maana nilishafikia mahali nikadhani nina tatizo la kufikiri.
Kwa muda mrefu nimekuwa napinga sana hili suala la serikali 3 au mkataba.
Nimepinga kwasababu hali ilipofikia muungano wetu utavunjika na naomba hilo litokee.

Muungano unavunjika kwasababu ule uvumilivu waliokuwa nao Watanganyika umefika mwisho. Ile karata ya Wazanzibar kutishia kila jambo ili wapate sasa inafika mwisho.
Na kwa vile Tanganyika isiyonufaika na lolote kutoka Zanzibar imechoka basi ni wazi Zanzibar haina ubavu wa kulinda tena muungano.

Nimekuwa nauliza, je ni kwanini tufkirie jambo lingine ikiwa huu muungano wa kubebana umeshindikana?
Nimewahi kusema kuwa Tanganyika ni lazima tuwe macho kwasababu kundi la Sultan likiongozwa na Maalim Seif, Ahmed Rajab, Jusa na Ali Salehe linataka kutufanya tufikiri wanavyotaka wao.

Wamefanikiwa kuwafanya Wazanzibar zombie kwa kauli ya 'tuache tupumue'. Unaachwaje upumue ikiwa watoto, wake, waume na wajukuu zako wanapumua Tanganyika ili nawe upumue?

Maalimu Seif amekana sera za chama chake ingawa nazo sikubaliani kuhusu serikali 3.Mnafiki huyu anawezaje kukushauri mtu mwenye kutumia kichwa kilicho na ubongo?

Hajwawahi KUTAMAKA VUNJA MUUNGANO hadharani, ingawa kwa unafiki anatamka katika vikao vya vichochoroni.
Mtu mnafikina kama Maalim Seif hawezi kushauri muungano wa mkataba bila kuwa na sababu!

Seif na kundi lake linalopinga mapinduzi wanajua fika kuwa Zanzibar kisosholojia,kiuchumi, kisiasa inategemea sana Tanganyika.
Huu ni ukweli mchungu lakini hilo wanalijua lakini wamewageuza wananchi wao mazombie kwa kutowaambia ukweli

FJM, muungano wa Uswis, Snegambia, EU, Morocco na Botwsana ni katika kutapa tapa.
Maalimu alitoa maelezo kuhusu serikali 3 na zigo la kuziendesha.
Tuliigeza hoja yake kama asusa, in fact mtu wa kiwango chake ilikuwa ni dhalili ya hali ya juu sana. Namshukuru mungu hakuwahi kuwa Rais na hatakuwa kiongozi wa nchi yangu hata siku moja.

Huu mkataba wanaoutaka si mkataba, ni utegemezi!
Niambieni Tanganyika itafaidika na nini katika mkataba wanaoupendekeza (Nitajieni jambo moja tu)

Nimeuliza sana maswali, Mkataba wa jambo gani? Ahmed Rajab, Seif na kundi la Sultan hawajawahi kujibu hata siku moja. Badfo wapo magazetini na mikutanoni wakihubiri huu upuuzi kwa kudhani kuwa sote ni Wazanzibar.Wanadhani kwavile wamewageuza Wazanzibar ma-toy basi wanaweza kutugeuza Tanganyika.Maalim Seif, Ahmed Rajab na Sultan inc wameshindwa kuvitetea kwanini watuuzie upuuzi nasi tuwaangalie tu! Tuwaambie bila kificho huo ni upuuzi! period.

Natoachangamoto , Tanganyika ulizeni kuwa mkataba uhusu nini? Mbona tuna mkataba tayari ?
Tusiingie kichwa kichwa, hili genge la Wahuni wawili au watatu ushauri wao mwisho Chumbe!
Hatutaki chochote zaidi tunawataka tuwasaidie wajitoe katika ukoloni.

Tuwasaidieni, Maalimu Seif akija katika mikutano ni kumwambia UNAFIKI hatutaki arudi akaijenge Zanzibar.

Tuwasaidie waondoke haraka, natamani kama kuna jambo wangeniomba niwasaidie kufikia ndoto yao.
Wazanzibar wajue jambo moja, UPUUZI WA MKATABA mwisho Chumbe! Ushauri wa Sultan & sons co ltd mwisho Chumbe! Unafiki mwisho Chumbe! Muda wa kubebana mwisho rasi kilomoni! Tupasue jahazi
 
narudia tena Wakishaondoka ardhi ni mali ya mtanganyika, katiba itamke kwa herufi kubwa NI MARUFUKU KWA MGENI KUMILIKI ARDHI TANGANYIKA si bure wanataka mkataba ili waendelee kuishi huku kama kwao pia.
 
Zanzibar ni sehemu ya Jamhuri ya Muungano. Hivyo ni huru. Tafuteni lugha nyingine ya kuwaelezea. Ni matusi kusema kuwa Znz si huru. Nani anaikalia kama si huru? Je maana yake ni kwamba hata Tng si huru? Je hii haimaanishi kuwa Tz nzima si huru. Acheni kuzua na kuanzisha hoja ambazo ni ngumu kuzitetea.
Kusema Zanzibar ni huru sijui utaanzia wapi,mwaka 1963 december,mwingereza aliikabidhi kwa Sultani,then mapinduzi yakaja mwaka 1964,mwaka huo huo,ukaja muungano na Tanganyika na Zanzibar,muungano ambao ni kama maruweruwe kwasababu hauonyeshi taifa huru la Zanzibar,kwa maana kwamba wananchi hawakuridhia huo muungano.Nakubali kuwa Zanzibar haijawahi kuwa huru!maybe kwa miezi mitatu tu baada ya mapinduzi.
 
Mwanakijiji fanya unavyojua make sure hii makala unaitupia Mzalendo.net

Wakisoma makala hii akilizitawakaa sawa...fanya hivyo please
 
Hii ni khatari kubwa sana kwa vijana kufikiria vitu kiurahisi rahisi tu.

Mimi nimeshafafanua sana hapa JF kuwa kama utauchukulia muungano wenu KISIASA unaweza kuona njia ulizotoa ni mujarab kabisa kama suluhisho. ILA MUUNGANO WENU UMEPITISHWA KISHARIA na si KISIASA.

Hivyo hata kuuvunja kwake ni lazima upite kisharia na si Kisiasa. Nakusihi sana usitoe suluhisho jepesi kwa mas'hara ya kisharia

Mkuu Mzee Mwanakijiji, with due respect, Muungano umeundwa kisharia na sio kisiasa!.

Sio lazima kila mkataba uwe ni wa maandishi, lakini mkataba wowote wa ardhi, land au pango, lazima uwe wa maandishi!. Wewe unaweza kununua gari na kumzawadia mpenzi/mke/ ndugu au mzazi kwa kauli tuu na ukawa ni mkataba halali!.

Lakini kama una land yako, ukiamua kumzawadia yoyote, hata ukimzawadia kwa kauli, lazima maandishi yafuatie ndio yatakayo halalisha hiyo kauli!.

Mzizi asili haswa wa muungano ni kauli, ya Nyerere na Karume.

Nyerere " Sisi ni ndugu, kwa nini tusiungane?".
Karume " Tuungane, wewe rais. mimi makamo".

Shughuli ilianza na kumalizika in a split of a second!.

Kwa vile hizi ni nchi mbili tofauti zenye uhuru wake na zote ni Jamuhuri huru, kauli pekee haitoshi kuziunganisha, lazima kufuata taratibu, sheria na kanuni ili kuhalalisha nia na kauli hizo, ndipo zikaandaliwa hizo articles of union!.

Articles zile japo zilikosa sifa ya kisheria ya kuutwa mkataba "contract" kutokana na tatizo la kisheria liitwalo "privity of contract", articles zile zilikuwa na sifa zote za kuitwa ' international treaty" kuunganisha nchi mbili, na ili any international treaty kupata uhalali na nguvu ya kisheria, ni lazima treaty hiyo iwe ratified na mabunge ya nchi husika!.

Ratification is a process ambayo hufanywa kwa procedures maalum na kufanywa in writing!.

Bunge la Tanzania lilifuata sheria, taratibu na kanuni zote ku ratify zile articles of union kwa maandishi!.

Zanzibar, walikuwa ndio kwanza wametoka kwenye mapinduzi, hivyo hawakuwa na bunge, Baraza la Mapinduzi ndilo lililokuwa kila kitu!. Lilipaswa kuziridhia zile articles of union kwa ratification ambayo hufanywa kwa maandishi!. Vikao vyote vya BLM vina hansard, lakini hilo halikufanyika na hakuna kumbukumbu yoyote ya maandishi kwamba ratification ilifanyika!.

Kisheria Muungano ni wa bara tuu, ndio maana Dourado alipomtonya Jumbe kuhusu Zanzibar kutouratify muungano na wakataka kuweka mambo sawa, Jumbe alishughulikiwa ipasavyo!.



Hebu tazama harakati mbalimbali za kuundwa kwa Serikali ya tanganyika ima kwa kuimarisha au kuvunja muungano.

Mdahalo wa kwanza juu ya mfumo na muundo wa Muungano ulianza kwa njia ya maoni juu ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano mwaka 1983/84. Hapo, kwa mara ya kwanza ilibainika kuwa viongozi wa juu wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, wakiongozwa na Rais Aboud Jumbe, na wale wa Serikali ya Tanzania, wakiongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano, Mwalimu Julius Nyerere, walikuwa na mitazamo tofauti inayokinzana juu ya Muungano.
Jumbe na timu yake walitaka Muungano uwe na Serikali tatu kwa maana ya Serikali ya Tanganyika, Serikali ya Zanzibar (iliyopo sasa) na Serikali ya Muungano yenye kushughulikia mambo ya Muungano tu, ambayo yameainishwa katika Ibara ya 6(a) ya Katiba ya Muungano (Articles of Union) na kifungu cha 8 cha Sheria ya Muungano (Acts of Union) Namba 22 ya 1964, na hatimaye ibara ya 4 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya 1977.
Jumbe alikwenda mbali zaidi kwa kuandaa Hati ya Maombi ya kuhoji na kutaka ufafanuzi kwenye Mahakama Maalum ya Kikatiba juu ya muundo sahihi wa Muungano kwa kutumia ibara ya 125 ya Katiba.
Tofauti hizi kati yake na Mwalimu hazikwisha salama kwa Jumbe kuthubutu kukanyaga mahali “patakatifu” bila kuvua viatu. Jumbe alilazimishwa kuachia ngazi zote za uongozi wa nchi kuanzia Urais wa Zanzibar, Umakamu wa Rais wa Muungano, na nafasi zote za kichama Januari, 1984.


harakati nyingine
Utata huu uliibuka tena kwa nguvu mpya zaidi wakati Wabunge 55 (maarufu kama G55) wa Bunge la Muungano, walipowasilisha bungeni mwaka 1993, hoja ya kutaka kuundwa/kurejeshwa kwa Serikali ya Tanganyika kwa kukasirishwa na hatua ya Zanzibar kujiunga na OIC kama nchi huru nje ya Muungano, Desemba 1, 1992.
Ukweli, Bunge lilikuwa limekwisha kupitisha kwa kauli moja, Azimio la kuanzishwa kwa Serikali ya Tanganyika Agosti 24, 1993 kwa maana ya kuwa na Serikali ya Muungano inayoundwa na Serikali hai zenye Mamlaka huru, za Tanganyika na Zanzibar, kama vile tu alivyotaka Rais Jumbe mwaka 1983.
Hata hivyo, Azimio hilo lilipigwa rungu zito na Mwalimu Nyerere na likavunjika.. Na kama ilivyokuwa kwa Jumbe, hapa napo mambo hayakuisha salama; safari hii Waziri Mkuu wa wakati ule, John Malecela na Katibu Mkuu wa CCM, Horace Kolimba, walipoteza nyadhifa zao kwa sababu ya ama kunyamazia au kuunga mkono hoja / Azimio la G 55.


 
Mwanakijiji fanya unavyojua make sure hii makala unaitupia Mzalendo.net

Wakisoma makala hii akilizitawakaa sawa...fanya hivyo please

Kwanini aende Mzalendo wakti hapa hapa anapewa vidonge vyake.

Unajuwa ameeleza kisiasa zaidi na sio KITAALAMU. Ni sawa na angesema watu wote kutoka Tanganyika muamua kuwafukuza watu wote mnaojuwa wametoka Znz na kuhakikisha wanarudi kwao na hapo mtaona mumevunja muungano wenu.

Lakin mkumbuke Mvungano wenu umeundwa kisharia hivyo kuuvunja kwake ni lazima sharia zifuatwe.

Poleni sana

 
Hizo unazoita sharia Maalim Seif, Jussa, Duni wanazijua? wanazizingatia katika kutoa matamshi yao kwenye BLW na kwenye majukwaa ya kisiasa? Usiwe mnafiki Barubaru.

Hata wewe unatamani Muungano uvunjike sasa hivi. Rudi Zanzibar mkajadiliane na wenzako mnarudi vipi na uhuru mnaoutaka sasa ni ule wa mwaka 1963 au ni ule wa 12.1.1964
 
Makala hii niliisoma jana kwenye gazeti la Tanzania Daima. Itakuwa imewafikia WATANZANIA wengi tu. Maalim Seif & Co. waitafakari na wachukue hatua stahiki. Bahati nzuri CUF iko kila mahala. CUF wapo ndani ya Bunge la JMT, CUF wako BLW, CUF wapo ndani ya GNU-Z. Waachane na hizi siasa uchwara za majukwaani. Wana kila nyenzo za kufanya kila wanalotaka kufanya ili kufanikisha azma yao hii.

Vinginevyo tumtake Rais Kikwete ailinde KATIBA ya JMT kama alivyoapa.
 

Mimi nimeshafafanua sana hapa JF kuwa kama utauchukulia muungano wenu KISIASA unaweza kuona njia ulizotoa ni mujarab kabisa kama suluhisho. ILA MUUNGANO WENU UMEPITISHWA KISHARIA na si KISIASA.

Hivyo hata kuuvunja kwake ni lazima upite kisharia na si Kisiasa. Nakusihi sana usitoe suluhisho jepesi kwa mas'hara ya kisharia
Mkuu, hapa muungano ni wa kisheria.

Kisheria Muungano ni wa bara tuu, ndio maana Dourado alipomtonya Jumbe kuhusu Zanzibar kutouratify muungano na wakataka kuweka mambo sawa, Jumbe alishughulikiwa ipasavyo!.

Hapa kisheria Muungano ni wa bara tu!

Sielewi unasimamia wapi.

Lakini hoja ya msingi ya Mzee Mwanakijiji ni hii: kuwa mijadala inayoendelea Zanzibar kuhusu muungano ni ya kuonesha kuwa Tanganyika inaionea, inaitawala, inaikalia kimabavu Zanzibar. Wanatuita wakoloni weusi. Tunataka watu wanaosema hivyo wasiwe wepesi kusema kwa maneno tu. Jussa yupo kwenye Bunge la Muungano, na tunategemea kumuona yeye na wabunge wenzake kuanza kuonesha kwa vitendo kukerwa na ukoloni huu mweusi, wagomee na kususia mambo ya kikoloni (ya muungano), wakatae ajira ndani ya serikali ya Muungano. Jussa na wenzake watangulie kuonesha mfano. Vinginevyo ni unafiki.

Wazanzibar wametufanya watu wa ku compromise, kila wakilalamika hili eti tunawabembeleza, na daima wanalalamika zaidi. Tumechoka. Waende zao.

Hatupendi sifa hiyo ya kuwa wakoloni tena weusi.

Zanzibar anzeni kuonesha hatua za kijasiri. Watanganyika tumewachoka, nendeni zenu muwe huru.
 
Mkuu, hapa muungano ni wa kisheria.

Hapa kisheria Muungano ni wa bara tu!

Sielewi unasimamia wapi.

Lakini hoja ya msingi ya Mzee Mwanakijiji ni hii: kuwa mijadala inayoendelea Zanzibar kuhusu muungano ni ya kuonesha kuwa Tanganyika inaionea, inaitawala, inaikalia kimabavu Zanzibar. Wanatuita wakoloni weusi. Tunataka watu wanaosema hivyo wasiwe wepesi kusema kwa maneno tu. Jussa yupo kwenye Bunge la Muungano, na tunategemea kumuona yeye na wabunge wenzake kuanza kuonesha kwa vitendo kukerwa na ukoloni huu mweusi, wagomee na kususia mambo ya kikoloni (ya muungano), wakatae ajira ndani ya serikali ya Muungano. Jussa na wenzake watangulie kuonesha mfano. Vinginevyo ni unafiki.

Wazanzibar wametufanya watu wa ku compromise, kila wakilalamika hili eti tunawabembeleza, na daima wanalalamika zaidi. Tumechoka. Waende zao.

Hatupendi sifa hiyo ya kuwa wakoloni tena weusi.

Zanzibar anzeni kuonesha hatua za kijasiri. Watanganyika tumewachoka, nendeni zenu muwe huru.

Ahali yangu,

Nimebainisha hivyo kwa watu wanaotaka njia nyepesi.

Na mimi naamini wazi kama majeshi na vyombo vikuu vya doula yenu vingekuwa Znz basi saa hizo wabara wote wangekuwa tayari wamefukuzwa Znz kama vile walivyofanya wakti wa mapinduzi ya 1964.

tatizo kubwa ni kuwa nguvu zote za doula kuanzia majeshi na vifaa na zana zote za kivita zipo Tanganyika. Hivyo znz wakilianzisha tu basi nguvu zote za Kijeshi zitaletwa toka Tanganyika.

Ila na nyie watanganyika kwa kuwa katika muungano wenu mmeshika Mpini mna nafasi kubwa kuingia kila nyumba wanazoishi wa Znz na kuwafukuza kama mnafikiri hicho ni kitu rahisi kisharia.Niliobainisha ni mawazo ay fikra za watu duni kiakili.

Kwani hayo kwa sie tulikuwepo enzi hizo huko Tz tulishuhudia ilipovunjia EAC. na baadae mkaona madhara yake baada ya sharia kuanza kushika mkondo wake.

msimamo wangu ni kuwa zitumike njia za kisharia ima kuujenga na kuuimarisha au kuuvunja muungano wenu.

 
Barubaru hujajielekeza kwenye nini Mzee Mwanakijiji anasema au hoja yake ikoje. Iwe ni Muungano wa "kisharia" au "kisiasa" inaonekana kwamba Wazanzibari wamechoka kunyonywa na wakolonni Watanganyika. Hahitaji maelezo mareefu yenye tambo za ujuvi usio na mashiko kuelewa kwamba njia rahisi ya kumsaidia mwenye mzigo uliomuelemea ni kumtua mzigo huo.

Hoja ya Mwanakijiji ni kwamba kama wazanzibar wanataka uhuru wao basi wasiutake nusu nusu au chambilecho kwa "Kisebu sebu na kiroho papo". Wazanzibar waonyeshe kwa matendo kwamba wanataka Uhuru wao na waanze kwa kuwazuia wabunge wao kuhudhuria kikao kijacho cha Bunge na kuwarudisha watumishi wote Wazanzibar wanaofanyakazi kwenye serikali ya Muungano warudi Zanzibar.

Kama ni mgawanyo wa mali au hadhi yoyote ni baada ya wazanzibar kujitenga. Kuna ugumu gani kutoka kwenye Muungano unaowazuia "kupumua". Hamuoni kwamba kuendelea kuvumilia kuishi kwenye muungano wa aina hiyo mwisho wa siku mtakosa kabisa Pumzi na hatimaye kufutika kabisa kwenye Ramani ya dunia?
 
Last edited by a moderator:
Tanganyika haihitaji Zanzibar na haiitegemei Zanzibar kwa chochote.

Huwezi kumpinga mkoloni huku anakulisha, kukulinda na kukupa maisha yako!

Tumeyasema haya zamaniiiii wakati wewe na wenzio, the vast preponderance of Watanganyika, bado mmelewa chang'aa ya "urithi wa Baba wa Taifa." Baadae pombe ilipoanza kuwatoka mkaingia kwenye hangover ya kukubali kwamba Muungano hauna manufaa lakini mnawashambulia Wazanzibar wanaotaka kujitoa. Sasa hangover ya pombe ya Muungano inawaisha ndio mnaanza kuliona tulilokuwa tunalisema baadhi yetu zamaaani kwamba "utasemaje "Let Zanzibar Go" halafu akitokea Mzanzibar anaesema "I want to go" badala ya kum support unamtukana?

Ndo maana kina Jussa hata wakisema the most ignoramus of things, "tumepoteza jimbo Zanzibar kwa sababu wapiga kura walikuwa Wakristo kutoka Bara..." mimi huwa nasema saaawa baba, nakuunga mkono unachopigania, tuvunje Muungano! With all these inanely extremist rhetoric used, I support the penultimate endgame, tuvunje Muungano!

Leo Mwanakijiji unasema Tanganyika haiihitaji Zanzibar? Leo unakubali Bara inaitunza na kuilisha Zanzibar? Kwa hiyo wakati ule ukiitetea legacy ya Nyerere kwa dhati uvumba na udi ulikuwa unatetea nchi moja kuitunza nyingine bure, huna uchungu na nchi yako? Watanzania kwa nini hatuna uchungu na national interests and treasures zetu? Sasa pombe ya Mwalimu imekutoka? You should apologize first!
 
Barubaru hujajielekeza kwenye nini Mzee Mwanakijiji anasema au hoja yake ikoje. Iwe ni Muungano wa "kisharia" au "kisiasa" inaonekana kwamba Wazanzibari wamechoka kunyonywa na wakolonni Watanganyika. Hahitaji maelezo mareefu yenye tambo za ujuvi usio na mashiko kuelewa kwamba njia rahisi ya kumsaidia mwenye mzigo uliomuelemea ni kumtua mzigo huo.

Hoja ya Mwanakijiji ni kwamba kama wazanzibar wanataka uhuru wao basi wasiutake nusu nusu au chambilecho kwa "Kisebu sebu na kiroho papo". Wazanzibar waonyeshe kwa matendo kwamba wanataka Uhuru wao na waanze kwa kuwazuia wabunge wao kuhudhuria kikao kijacho cha Bunge na kuwarudisha watumishi wote Wazanzibar wanaofanyakazi kwenye serikali ya Muungano warudi Zanzibar.

Kama ni mgawanyo wa mali au hadhi yoyote ni baada ya wazanzibar kujitenga. Kuna ugumu gani kutoka kwenye Muungano unaowazuia "kupumua". Hamuoni kwamba kuendelea kuvumilia kuishi kwenye muungano wa aina hiyo mwisho wa siku mtakosa kabisa Pumzi na hatimaye kufutika kabisa kwenye Ramani ya dunia?

Nimebainisha hivi nisome vizuri utanielewa kwani hiyo ni njia rahisi sana. Kwani nguvu zote za Doula zipo Tanganyika na sio Znz. Nisome tena vizuri uelewe nimekusudia nini.
Nimebainisha hivyo kwa watu wanaotaka njia nyepesi.

Na mimi naamini wazi kama majeshi na vyombo vikuu vya doula yenu vingekuwa Znz basi saa hizo wabara wote wangekuwa tayari wamefukuzwa Znz kama vile walivyofanya wakti wa mapinduzi ya 1964.

tatizo kubwa ni kuwa nguvu zote za doula kuanzia majeshi na vifaa na zana zote za kivita zipo Tanganyika. Hivyo znz wakilianzisha tu basi nguvu zote za Kijeshi zitaletwa toka Tanganyika.

Ila na nyie watanganyika kwa kuwa katika muungano wenu mmeshika Mpini mna nafasi kubwa kuingia kila nyumba wanazoishi wa Znz na kuwafukuza kama mnafikiri hicho ni kitu rahisi kisharia.Niliobainisha ni mawazo ay fikra za watu duni kiakili.
 
narudia tena Wakishaondoka ardhi ni mali ya mtanganyika, katiba itamke kwa herufi kubwa NI MARUFUKU KWA MGENI KUMILIKI ARDHI TANGANYIKA si bure wanataka mkataba ili waendelee kuishi huku kama kwao pia.

Pigania hili. https://www.jamiiforums.com/jukwaa-la-siasa/334649-tundu-lissu-na-kiini-macho-cha-muungano-11.html

Ardhi hiyo tunawakodisha wageni (wazungu, waarabu, wahindi ,matapeli "wawekezaji" aka wavuna shamba la bibi kwa miaka 99).
Tunawahamisha wanavijiji kwa ajili ya kupisha matapeli.

Kwa nini tunajenga chuki na watu waliopewa ahadi ya "maisha bora kwa kila mtanzania aka kugawana umaskini" wakati njia za amani za kumaliza mazingaombwe zipo?

Ni wazi kuwa hatulijui tatizo letu. Tumewapa wakimbizi kwamaelfu na malaki uraia na haki za kumiliki ardhi.

Tulifanya makosa,tusitafute mchawi. La kufanya ni kusahihisha makosa.
 
Barubaru, angalia hoja zilizopo kwa sasa Zanzibar:

Seif asema Tunataka Zanzibar yetu
Written by Stonetown (Kiongozi) // 07/10/2012 // Habari // 42 Comments
"Mimi sitafuni maneno kwamba ni muumini wa Zanzibar yenye mamlaka kamili kitaifa na kimataifa itakayofuatiwa na mashirikiano kati yake na Tanganyika kupitia Muungano wa Mkataba. Namshangaa leo anakuja kiongozi wa Zanzibar anasema tuna bendera na muhuri na wimbo wa taifa, hayo yanatosha. Hivi huyu anajua anachokisema au anatumikia maslahi ya waliomtuma? Una bendera gani hii ambayo mwisho wake Chumbe? Mimi nataka niione bendera ya Dola ya Zanzibar inapepea Umoja wa Mataifa, New York pale. Nataka tuwe na Paspoti ya Zanzibar, nikisafiri nitoe Paspoti ya nchi yangu. Nataka tuwe na Ofisi za Kibalozi za Zanzibar katika nchi za nje.


Leo hata mamlaka ya kiuchumi hatuna. Tumeamua rasilimali yetu ya mafuta na gesi asilia yasiwe mambo ya Muungano, mpaka leo Tanganyika wamekwamisha, wanatuzuia tusinufaike na rasilimali zetu tukajenga uchumi wetu. Wanasema tuna viwango na mfumo mmoja wa kodi lakini bidhaa zikitoka Zanzibar wanazitoza ushuru tena. Lengo ni kuua uchumi wetu ili hatimaye tudhoofike na tusalimu amri kwao. Yaguju! Wasahau hilo. Leo hata katika mikutano ya kimataifa, viongozi wetu wa Zanzibar hawapewi heshima ya uwakilishi wa nchi yetu.

Inafika mahala hata Naibu Waziri tu wa Bara anaongoza ujumbe wa Tanzania wakati kuna Waziri kamili kutoka Zanzibar lakini haheshimiwi. Tutarejesha mamlaka yetu kamili. Tuwe na Benki Kuu, tuwe na sarafu yetu ya Zanzibar, tupange uchumi wetu kwa maslahi ya watu wetu. Tunataka tuwe na uanachama katika jumuiya na mashirika yote ya kimataifa. Tuwe na Waziri wa Mambo ya Nje wa Zanzibar. Tuwe na uwezo wa kuingia mikataba na nchi za kigeni. Hayo ndiyo tunayoyataka. Tukisema hivi hatuna maana tunataka ugomvi na Tanganyika. Hapana! Tunataka tuwe majirani wema na Tanganyika kama tutakavyokuwa na ujirani mwema na Kenya. Hayo yatafikiwa kupitia Muungano wa Mkataba wa Madola mawili huru kamili."

Source: Seif asema Tunataka Zanzibar yetu | Mzalendo.netSeif asema Tunataka Zanzibar yetu | Mzalendo.net

my take:
Ndio maana tunasema: Tuwasaidie Wazanzibar 'wajikomboe' toka huyo mkoloni mweusi. Tuwahimize waondoke.

Lakini tuwahimize kwa kuwaomba wachukue hatua za dhati: na si "kisebusebu na kiroho papo". Jussa na wabunge wenzako tunataka tuone hatua
 
Kweli Zanzibar kuna vugu vugu la kudai zanzibar huru, lakini najiuliza hii zanzibar huru wanaidai kwa nani? w
1. wana nchi yao
2. wana raisi wao
3. wana makamo wawili wa raisi
4 wana baraza la wawakilishi ( bunge) lao
5. wanabendera yao
5. wanavikosi vyao vya ulinzi na usalama
6. wanakatiba yao
7. wana wimbo wao wa taifa

SWALI: uhuru wanaudai kwa nani?

1. ni nani toka Tanganyika anatawala Zanziba?
2. Raisi Kikwete kasafiri kuja Zanzibar mara ngapi (kama koloni) lake?
4. kwa nini wasikae na kuamua jinsi wanavyotaka kuishi?
5. Fikra za kutawaliwa wamezitoa wapi?
6. Je wakishajitenga na Tanganyika fikra za kutawaliwa zitakua zimeisha?
7. Tuachwe tupumue,.. wanataka wapumue kwa kutumia nini?
8. nani anawachagulia wabunge wa kwenda kwenye bunge la Tanzania?
9. Ni lini wataitisha mjadala wa kitaifa wajadili mustakabali wa nchi yao?
10. ni liniwalipeleka muswada bungeni wa kutaka kujadili mustakabali wa nchi yao ukatupwa?

NOTE: Niliwazalo au nilionalo, MAPINDUZI MENGINE YANAKUJA.
 
Ninasubiri kwa hamu bunge la muungano mwezi November. Kama wabunge wa CUF toka Zanzibar watahudhuria basi unafiki wa Maalim Seif utakuwa wazi.

Maalim Seif ni katibu mkuu wa CUF, tena katibu mkuu mwenye nguvu za kipekee kwa chama chake. Anatakiwa aamue moja, ama asimamie kauli zake za kutaka Zanzibar huru kwa vitendo na hivyo kuwakataza wabunge wa chama chake kuingia kwenye bunge la mkoloni, au kuthibitisha kuwa ni mnafiki na kauli zake za kutaka uhuru ni hadaa.

November iko karibu.

" ya nini yote hayo, wabunge wa CUF watoke wende wapi? kwani bunge la Tanganyika hilo? bunge bado ni la Tanzania subiri hadi hapo mtakapokuwa na Tanganyika yenu ndo unaweza kuleta hoja yako hiyo. ......

Sisi hatuna haraka, kwani tume ya kukusanya maoni si inaendelea na kazi yake iliyopewa? huko sisi ndio tunatoa madai yetu, tusubiri yakusanywe na ripoti itolewe ... kama kutatokea "kuchakachua" plan B itatumika ...

Sisi hatuendi tu kama wanyama ati ... tunadai chetu kwa ustaarabu na maarifa bila mikwaruzano kama ambavyo wewe, mwanakijiji na baadhi ya wengine wanavyotaka
"

 
" ya nini yote hayo, wabunge wa CUF watoke wende wapi? kwani bunge la Tanganyika hilo? bunge bado ni la Tanzania subiri hadi hapo mtakapokuwa na Tanganyika yenu ndo unaweza kuleta hoja yako hiyo. ...... Sisi hatuna haraka, kwani tume ya kukusanya maoni si inaendelea na kazi yake iliyopewa? huko sisi ndio tunatoa madai yetu, tusubiri yakusanywe na ripoti itolewe ... kama kutatokea "kuchakachua" plan B itatumika ... sisi hatuendi tu kama wanyama ati ... tunadai chetu kwa ustaarabu na maarifa bila mikwaruzano kama ambavyo wewe, mwanakijiji na baadhi ya wengine wanavyotaka
"


Sahamani kutumia huu mfano, unachosema ni sawa na mwanamke anayepiga kelele kuwa anabakwa lakini wakitokeza watu kumuokoa anaseme 'mwacheni amalizie!

Mnasema mnataka kupumua, mnataka mamlaka kamili, ,mara uhuru, lakini hapo hapo mnasema mnasubiri hadi bunge la Tanganyika liwepo ndipo wabunge wa zanzibar wataacha kuhudhuria (mwacheni amalizie)!
 
Back
Top Bottom