Wapigania uhuru wa Zanzibar waungwe mkono!

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Mar 10, 2006
33,474
39,987
UMEFIKA wakati watu wa bara (Tanganyika) waanze kuwaunga mkono wapigania uhuru wa Zanzibar wakiongozwa na Seif Sharrif Hamad na Ismail Jussa. Viongozi hawa wawili kutoka chama cha CUF wamejitambulisha kuwa wanataka Zanzibar iwe “Dola Kamili” kwanza na baadaye kuwepo Muungano wa Mkataba.


Kwa muda mrefu viongozi hawa na wengine walio nyuma yao wanaamini kuwa Zanzibar imebanwa na Tanganyika na wapo ambao kati yao wanaona Tanganyika imegeuza Zanzibar kuwa koloni lake.


Makala yangu hii basi ni ya kuwaunga mkono wapigania uhuru hawa ili hatimaye kabla ya mwisho wa mwaka huu Zanzibar iwe taifa huru lenye mamlaka kamili ya mambo yake ya ndani na nje na ikipeperusha bendera yake kwenye Umoja wa Mataifa na ikiwa ni nchi kamili.


Kwa vile sasa hivi Zanzibar imemezwa na Tanganyika na kwamba wananchi wanaamini nchi yao inatawaliwa kimabavu na utawala wa Rais Jakaya Kikwete wakati wao wanahitaji kuwa huru kutoka katika ukoloni huu ili hatimaye na wao waweze “kupumua” kama vile mtu anayevua koti lililokuwa likimbana.


Sababu zao zina nguvu
Kundi hili la Wazanzibari ambalo wanataka uhuru wao linaamini kuwa Muungano wa Tanganyika na Zanzibar uliozaa Tanzania siyo halali na kuwa una kasoro nyingi ambazo haziwezekani tena kutatuliwa isipokuwa kwa kuvunja Muungano huu. Wanaamini kuwa mfumo wa sasa unaneemesha zaidi Tanganyika na kuwa Zanzibar inakuwa na kutendewa kama sehemu ya Mkoa wa Tanganyika.


Lakini sababu kubwa ambayo ina nguvu sana ni kuwa Zanzibar tayari ilishawahi kuwa dola kamili na hivyo kudai dola kamili ni kudai kurudishwa kwa kilichopotezwa. Haijalishi kwa kweli kinachotakiwa kurudishwa ni Zanzibar ipi; kama ni ile kabla ya uhuru wa 1963 au ile ya kati ya uhuru na mapinduzi ya Zanzibar (chini ya Waziri Mkuu Shamte) au ni ile ya mara tu baada ya mapinduzi na kabla ya Muungano (chini ya mzee Karume). Vyovyote vile ilivyo wapigania uhuru wanachotaka ni kile kinachoimbwa sana siku hizi kuwa “Zanzibar Kwanza” halafu mengine baadaye.


Njia ya haraka ya Zanzibar kupata uhuru wake
Nimeshaandika huko nyuma lakini leo nimeona nirudie kwa sababu kwa namna fulani wapigania uhuru hawa wa Zanzibar wanatumia njia ndefu sana ya kulalamika majukwaani – badala ya kutumia njia rahisi zaidi. Kuna msemo kuwa umbali mfupi zaidi kati ya sehemu A na B ni kwa kuchora mstari ulionyoka. Hii ni kweli kwa sehemu ambayo ni tambarare kwani mahali ambapo kuna mabonde, milima na makorongo sehemu mbili zinaweza kuwa karibu sana lakini haziwezi kufikiwa kwa mstari ulionyoka isipokuwa kwa kuzunguka.


Binafsi naamini suala la Zanzibar kuwa huru siyo suala la kuzunguka kivile kwani linaweza kumalizwa kwa mstari ulionyoka endapo tu wapigania uhuru hawa watakuwa tayari kufuata ushauri wangu ambao tayari nimeutoa mara kwa mara mwaka huu hasa baada ya kutambua kuwa hatuna viongozi wa Muungano (ukiondoa wachache sana) ambao wameweza kuutetea Muungano. Hakuna cha viongozi vijana wala wazee ambao wameweza kuwa watetezi wa Muungano huu. Na kwa vile Muungano huu sasa hauteteeki ni muhimu kufanya kila jitihada ili uvunjwe mapema na kila mtu achukue zake.


Njia rahisi ya Zanzibar kupata uhuru inaotamani ni kwa viongozi wa Zanzibar kwanza kabisa kukataa kutambua Muungano uliopo sasa. Hili ni jambo la muhimu sana kwani mara moja litatangaza mgogoro kati ya pande hizi mbili. Haiwezekani upande mmoja waone kuwa Zanzibar inakaliwa kimabavu na Tanganyika na kudai “uhuru” lakini wakati huo huo wanaishi kama wanautambua Muungano wa sasa.


Fikiria jinsi ambavyo viongozi hawa hawajajaribu kutaka wabunge wa CUF wanaotoka Zanzibar wajiondoe kwenye bunge la Muungano ili kupinga ukoloni. Maana mkoloni anayekubali kuwa na wabunge na kuwapa heshima zote kama wabunge wengine ni mkoloni gani? Lakini tukikubali kuwa Tanganyika ni mkoloni wao basi jambo la kwanza ni kukataa kutambua taasisi za Kimuungano. Hivyo, tunawatia shime kuwa kikao kijacho cha Bunge la Muungano CUF na kina Maalim Seif na wenzao wawakataze wabunge wao kuja kwenye Bunge la Muungano.


Kama watakuja wabunge kutoka Zanzibar kwenye kikao kijacho na kama miongoni mwao wamo wa CUF tutatambua kuwa wapigania uhuru hawa hawataki Zanzibar iwe huru bali wanasema maneno ya kufurahisha hadhara.
Pamoja na hilo wapigania uhuru wa Zanzibar wanahitaji kuwahamasisha Wazanzibar wao kuachilia nafasi wanazoshikilia kwenye taasisi za “Muungano”. Kama Muungano wa sasa siyo sahihi na kuwa ulilazimishwa na kuwa siyo wa mkataba ni wazi kuwa hakuna njia nyingine isipokuwa kuwahamasisha Wazanzibar wanaotumika kwenye Muungano huo kuachia nafasi zao.


Binafsi nitapenda kuwasikia kina Jussa na Seif na wenzao wenye kuwaunga mkono wakitoa tamko la kuwatia shime watumishi wa Zanzibar kwenye Serikali ya Muungano wajiondoe. Hii itakuwa ni kuanzia na Makamu wa Rais, Dk. Gharib Bilal na watumishi wengine wote – kuanzia jeshini, hadi kwenye taasisi nyingine nyingi ambazo si za Muungano.
Ili tujue kweli wanataka wawe na nchi yao cha kwanza ni kukataa kula cha mkoloni! Warudi ‘kwao’ Zanzibar kama ambavyo wapigania uhuru wengine walivyowahi kufanya. Huwezi kumpinga mkoloni huku anakulisha, kukulinda na kukupa maisha yako!


Hatutaki muungano mwingine
Sasa mojawapo ya vitu ambavyo vimenishangaza sana wakati umefika kuviita ni vya kipuuzi ni kuwa wanaotaka kutoka kwenye Muungano huu wa sasa hawachelewi kusema ati wanataka Muungano wa “Mkataba”. Hivi nani kawaambia kuwa wakijitoa kwenye Muungano huu sisi Watanganyika tunataka Muungano wowote tena? Yaani wao waamue kutoka halafu wao hao hao waamue wanataka Muungano wa aina gani? Kwa kitu gani walichonacho?


Naomba niwekwe kwenye rekodi kuwa Muungano huu ukitushinda hatutaki Muungano mwingine wowote; uwe wa mahaba au wa mkataba! Kama huu wa sasa tumeshindwa kuutetea nani anafikiri ujao wa mkataba utalindwa? Kama huu wa sasa umeshafikia kuitana wakoloni hivi huo ujao utakuwaje? Na kama wa sasa umejaa kero nyingi hivi ni kwa nini tuamini kuwa huo ujao utakuwa salama?


Wanatuambia ati utakuwa ni wa “mkataba” kwa maana ya Muungano kama ule wa Jumuiya ya Ulaya! Hivi wameona yanayoendelea huko? Leo hii katika Muungano wa Ulaya nchi ndogo ndogo ambazo zimekuwa tegemezi kwa nchi kubwa zimejikuta kwenye matatizo mengi sana kiasi kwamba imebidi zichukue hatua kali za kujifunga mikanda. Ugiriki, Ureno na Uhispania nikitaja nchi chache zimejikuta kwenye hali ngumu sana ya kiuchumi. Cha kushangazani kuwa nchi ambayo imejikuta ikitumia utajiri wake na nafasi yake kubwa ya kiuchumi yaani Ujerumani ndio imebebeshwa mzigo wa kusaidia nchi hizi nyingine.


Haya ndiyo malipo ya muungano wao. Ujerumani imejikuta kuwa kama kaka mlezi wa kuwasaidia hawa. Kama ambavyo unaweza kuwa umesikia au kusoma Chansela Angela Merkel amejikuta analindwa na askari zaidi ya 6000 katika ziara yake ya kutembelea Ugiriki nchi ambayo iko kwenye hali ngumu zaidi ya kiuchumi. Badala ya Wagiriki kumshukuru Merkel kwa kutumia utajiri wan chi yake kuokoa nchi yao Wagiriki hawa (ambao baadhi walishambulia ofisi za Jumuiya ya Watanzania huko) wamekuwa wa kwanza kumuona Merkel kama mtu anayewakandamiza. Sasa Tanganyika ikiingia mkataba kama huu na Zanzibar si ndio tutajikuta tunabebeshwa mzigo mkubwa kuliko tunavyotaka?


Wazanzibari wakitoka kwenye Muungano huu wa sasa Watanganyika hatutaki Muungano mwingine maalumu nao. Tutakutana nao kwenye taasisi nyingine za kimataifa kama ni SADC, EAC, UN au kwingine. Lakini sijui mkataba mwingine maalumu ni kujitakia matatizo na hivyo Watanganyika wanapoenda kutoa maoni yao kwenye Tume ya Katiba wawe wazi kabisa kuwa wanachotaka ni Muungano kamili wa nchi moja na serikali moja nje ya hapo ni Utengano. Utengano ambao kwa kweli siyo uadui bali ni kutambua kuwa hatuwezi kuwa na Muungano wowote kwani huu wa sasa umetosha kuumiza watu vichwa.


Tanganyika haihitaji Zanzibar na haiitegemei Zanzibar kwa chochote. Ni kwa sababu hiyo naamini ili kuharakisha Zanzibar kujitoa na viongozi hawa wapigania uhuru kuweza kupata nafasi ya kuongoza taifa la Zanzibar natoa pendekezo kuwa kwa ukarimu wetu kutoka Tanganyika tutenge shilingi bilioni 400 hizi ili kuwasaidia Zanzibar kuanza maisha mapya wao wenyewe. Tuchukue madeni yao ya nje na kuwa tayari kuwalipia mshahara wa vyombo vile vilivyokuwa vya Muungano ili Zanzibar wasije wakasema kuwa wameonewa. Nina uhakika bilioni 400 ni fedha nyingi sana ambazo Wazanzibari watashukuru.


Hivyo, nawasihi wale wote ambao wanataka kina Jussa na Seif waharakishe kuondoa Zanzibar kwenye Muungano tuwaandikie na kuwaambia “Let Zanzibar Go” yaani “Tuiache Zanzibar Iende”! Iende na kuwa taifa huru na lenye mamlaka kamili. Na itakuwa vizuri kama kina Jussa na Seif wanaamini kuwa wana mashabiki wengi basi wajue uamuzi wao wa kujitoa kwenye Muungnao utaungwa mkono Zanzibar kwani hadi hivi sasa inaonekana kuungwa mkono huku kupo.


Ni serikali ya Dk. Mohammed Shein ambayo inaonekana kubariki jambo hili na wakati umefika kuwaunga mkono na wao. Tuwaunge mkono kwani wakiamua kujitoa tu tayari mfumo wao wa serikali uko kamili na ambao hauitaji mambo mengi mapya.


Binafsi nitawapuuzia wapigania uhuru hawa kama wataendelea kung’ang’ania watu watoe maoni na kuwa wanataka Zanzibar huru lakini hawachukui hatua zozote za kutaka uhuru huo utimie. Ikumbukwe kuwa serikali ya Muungano haitatumia nguvu kuwalazimisha Zanzibar.
Kila la heri Wazanzibari, tukutane UN.
 
Zanzibar ni sehemu ya Jamhuri ya Muungano. Hivyo ni huru. Tafuteni lugha nyingine ya kuwaelezea. Ni matusi kusema kuwa Znz si huru. Nani anaikalia kama si huru? Je maana yake ni kwamba hata Tng si huru? Je hii haimaanishi kuwa Tz nzima si huru. Acheni kuzua na kuanzisha hoja ambazo ni ngumu kuzitetea.
 
Tehe tehe tehe. Hay basi mkuu, kwa mtaji wa huo ushauri ninawaunga mkono hao wapigania uhuru wa Zanzibar lakini si kwa zaidi ya sekunde 5 tangu sasa.
 
Ninasubiri kwa hamu bunge la muungano mwezi November. Kama wabunge wa CUF toka Zanzibar watahudhuria basi unafiki wa Maalim Seif utakuwa wazi.

Maalim Seif ni katibu mkuu wa CUF, tena katibu mkuu mwenye nguvu za kipekee kwa chama chake. Anatakiwa aamue moja, ama asimamie kauli zake za kutaka Zanzibar huru kwa vitendo na hivyo kuwakataza wabunge wa chama chake kuingia kwenye bunge la mkoloni, au kuthibitisha kuwa ni mnafiki na kauli zake za kutaka uhuru ni hadaa.

November iko karibu.
 
Pia tumuunge mkono Mtikila+Mchambuzi kuidai TANGANYIKA yetu.
 
Mzee Mwanakijiji,

Kwanza kabisa napenda kukushukuru kwa hoja hii ambayo inaibua mjadala mpya wa Muungano wetu japokuwa wengi wenu mnatumia hisia zetu za Utaifa wenu kufikia maamuzi ambayo9 kusema kweli yanazidi kutoposha zaidi ktk kiza cha Udanganyika..

Sina budi kusema ya kwamba Maalim Sief na Jussa ni vibaraka wa serikali liyoondolewa ktk utawala mwaka 1964 ktk Mapinduzi ambayo yameunda serikali hii. pamoja na kwamba walikuwa wapinzani wakubwa wa Mapinduzi wamepewa haki zote za Uraia na kuishi pamoja na Wazanzibar wengineo kutokana na ukweli kwamba Mapinduzi yale yalikuwa kuuondoa Utawala wa Sultan hivyo wanachama wa chama hicho hawawezi kupoteza Uraia wao kutokana tu kujiunga na chama au mtazamo tofauti ktk lindi la siasa na utawala.

Ifahamike ya kwamba UMOJA wa nchi za Kiafrika uliasisiwa kabla kabisa ya UHURU wa nchi zetu, ni mpango ulikusudia kuziunganisha nchi za Kiafrika na hakika ilikuwa NCHI MOJA kwa bara zima la Afrika, ndipo waasisi wetu walipobuni mbinu ya kuanza na majimbo huru kwanza mbele ya muungano ambao usingeweza kudumu wakati kuna nchi ambazo bado hazikuwa huru. Hii ndio AFRIKA ilokusudiwa.

Sasa yawezekana kabisa wananchi wakabadilisha mtazamo na fikra zilizotuletea UHURU wa nchi za Kiafrika lakini pamoja na yote haya mabadiliko haya yatafanywa na wananchi wenyewe kwa kushinikiza kisheria Ujio wa taifa jipya. Kama kuna Madai ya Zanzibar huru ni lazima Wazanzibar wenyewe waamue kwa kupitia kura za maoni ili isije tokea tukawakabidhi nchi hii watu wenye tamaa ya kutawala wengine, watu wenye visasi kwa wale ambao wanapingana na Utawala uliopo ama mapinduzi yenyewe.

Tumeyaona haya yakifanyika huko Libya na hata Sudan ambapo kundi la watu wameweza kuurubuni Umma kufanya Mapinduzi au mageuzi ilihali ndani yao wenyewe wana chuki kubwa juu ya wale wanaoungana na Utawala uliopo. Tumeona Libya watu wote walokuwa wakimpenda Ghadaffi na Mlibya mwenzao wakiuawa hovyo, watu weusi wakiuawa kwa sababu tu ya rangi zao. Hadi leo pamoja na Mapinduzi yale kuna sehemu serikali hawana mamlaka kabisa, bado watu wana Mapenzi na Ghadaffi, wengine hawataki serikali mpya na hawakubali kabisa kuingiliwa.. Matokeo kama haya hayawezi kupendekezwa kwa njia yoyote ile.

Tunaijua fika Historia ya Zanzibar na yalotokea enzi za Mkoloni na Usultani hayawezi kurudishwa kwa mihadhara na mikutano ya baadhi ya watu wachache ambao wameunda serikali ya mseto kwa kuwahusisha tu wanachama wa vyama viwili vya CCM na CUF wakati wapo viongozi WAZANZIBAR wa vyama vingine hawakuhusishwa wakiwadanganya wananchi kwamba serikali hii ina lengo la kujenga Umoja wa Wazanzibar. Lakini maajabu yanakuja leo hawa hawa walojenga Umoja huo wanakuja na sura mpya ya kuitaka Zanzibar HURU wakati wao ndio viongozi ktk serikali ya Zanzibar inayotawala.

I mean, jamani tuweni wakweli ktk haya. Hivi kweli Mkoloni wakati wa EAC iloungana wangeweza kumpa Mtanzania (Mtanganyika) kuwa rais wa Tanganyika, Mwingine rais wa Uganda na Kenya, sijui wachague mawaziri wao wenyewe halafu viongozi hao hao waende kudai hawako HURU?.. Haya ni maajabu ya Firaun hakika..

Kama kuna swala lolote kuhusu Zanzibar huru basi inatakiwa kwanza kuwaondoa hawa waliopo madarakani maana wao ndio watawala. Kuitafuta Zanzibar isiyokuwa na Muungano na Tanganyika, maamuzi yake yatapokelewa tu ikiwa WAZANZIBAR wote kupitia vyama vyote vya siasa vilivyosajiliwa zanzibar watahusishwa ktk maamuzi haya na sio kundi la watawala ambao wanakula fedha ya wananchi isiwatoshe kuja na hoja za UHURU wa Zanzibar wakipeperusha bendera ya Sultan Jamheed.. Tena pasipo hekima wamekuja na bendera ya Sultan hadi Mnazi Mmoja, Dar - Es - Salaam na kujisifia U Hizbu wao. Hata Tanganyika kabla ya Uhuru tulikuwa na bendera yetu ikiwa na alama ya Mkoloni pembeni (union Jark) lakini itakuwa maajabu sana kwa mtu mwenye akili timamu kuja dai Tanganyika Huru akipeperusha bendera ya Mkoloni..Hawa watu hawaheshimu Mapinduzi hata kidogo..

Nasema tena JK ameshindwa Uongozi wa nchi hii na anawaendekeza sana watu hawa. Hiyo Haki na UHURU wa wananchi wa Zanzibar hauwezi kupitia mahubiri yenye kashfa na matusi mazito ilihali hawa watu hawakuwepo wala kuhusika ktk Mapinduzi ya nchi hiyo. Hawa ni vibaraka wanaopenda sana kutumia Uzanzibar kama turufu ya Uhalali ktk madai yao lakini deep down hawana mapenzi na nchi yao isipokuwa bendera ya Sultan na nyimbo za kumsifia Sultan. Mapinduzi yaligharimu roho za watu na tunajaribu sana kusahau na kuijenga Zanzibar Mpya. Urogho wa madaraka wa watu wachache usitulaghai akili zetu tukasahau nini malengo yao..Wazanzibar, wazanzibara na wabara wote ni ndugu wenye kuheshimiana japokuwa kuna tofauti zetu ambazo ni muhimu na lazima tuzikubali na kupeana uhuru wa kuenzi tamaduni na mila za watu wake..

Zanzibar ni ya Wazanzibar sio Maalim Seif na Jussa - Hapana mkuu wangu tusijidanganye kabisa, kama itatokea kuvunjika kwa muungano ni lazima tuhakikishe tunaikabidhi Zanzibar kwa Wazanzibar wenyewe na sio kundi la watu waliojipanga kutafuta umaarufu.
 
Last edited by a moderator:
Waende zao huko! WaZanzibari wanatikisa kiberiti kwakua wameshaona sisi waTanganyika ndo tunawabembeleza kwahiyo wanaitumia hiyo kama 'leverage' wakitaka chochote tuwape eti kwakuwa tu watajiondoa kwenye muungano, yani watu milion 3 watuendeshe sisi zaid ya 35 milion?
 
Mkandara ni lini mara ya mwisho kuwa bongo and more specifically ni lini ulitia mguu Zanzibar? Post yako haiendani kabisa na hali halisi iliyoendelea Zanzibar. Almost kila nyumba Zanzibar wamebandika matangazo - 'waachwe wapumue'.

Kwanini tusiwaunge mkono watu wanaotafuta 'neema'. Tunawapenda sana Zanzibar na ndio maana hata bill za umeme tunawalipia, na hata Maalim Seif akijisikia kuja kusalimia tunamtumia ndege imlete kwa raha na starehe zake. Sasa wanataka 'kupumua' wamekuwa watu wazima hawa (48yrs), kwanini tusiwaunge mkono ndugu zetu hawa?

Na wapo watu wengi, tena wazito hawasemi hadharani kama Maalim Seif lakini ukiongea nao pembeni wanasema hayo hayo anayosema Seif. Midahalo ya kudai Zanzibar 'huru' kwa sasa inaongozwa na mwanasheria mkuu wao! Na mimi nasema ni haki yao kabisa. Waachwe waende (including no show Dodoma next month).

Hapa tulipofika ni ama tugawane mbao yaishe, au nchi moja yenye mikoa kadhaa. Hata serikali mbili haiwezekani tena, ni mzigo. Time to move on. LET ZANZIBAR GO.
 
Last edited by a moderator:
Zanzibar ni sehemu ya Jamhuri ya Muungano. Hivyo ni huru. Tafuteni lugha nyingine ya kuwaelezea. Ni matusi kusema kuwa Znz si huru. Nani anaikalia kama si huru? Je maana yake ni kwamba hata Tng si huru? Je hii haimaanishi kuwa Tz nzima si huru. Acheni kuzua na kuanzisha hoja ambazo ni ngumu kuzitetea.

Kwani ni sisi tunaodai kuwa Zanzibar inakaliwa kimabavu na kuwa haina uhuru; au hujawasikia wapigania uhuru wa Zanzibar wanavyoona Tanganyika ikiitawala - by proxy- Zanzibar na kufanya koloni lake?
 
Mungu amrehemu sana Julius Nyerere!
Tungekuwa nae huyu Jusa na Maalim Seif nadhani tungekuwa hatuko nao tena! Kwa sababu hawa wanataka kutuletea waarabu waliowatesa mababu zetu, tena sisi tunapaswa tuwalipizie visasi hawa wanaorudi kwenye nchi yetu. Ni wajukuu zao hawa!
 
Hapa issue siyo wanadai wao ni nani. Hatuwezi kukubali kuangukia kwenye mtego wao. Lazima nasi tutumie akili zetu hata ikiwezekana kuwashauri maana Muungano si mali ya upande mmoja wala kundi moja. Hivyo ni wajibu wetu kama wadau kuepuka kupelekwa na mkondo wa mawazo chakavu yanayolipa taifa letu jina baya la mkoloni. Tulipigana na ukoloni si nchini mwetu tu bali hata kwenye nchi jirani. Hivyo ni kashfa kutuita wakoloni. Ni uhaini na kukosa aibu na shukrani. Walituomba wao tuungane nao ili wasinduliwe na waarabu waliowapindua. Kuna haja ya kurejea na kuisoma historia vizuri badala ya kufuata mkumbo na kuangukia kwenye mtego wa kujidhalilisha na kujiona kama wakoloni. Nadhani hadi hapa tunaelewana.
 
Mzee Mwanakijiji mnaotaka serikali moja mnamaanisha "unitary Government"?

Tuna maana tu kuwa hakuna "nchi mbili, mataifa mawili"; tunaamini tukisolve hilo tunaweza kuwa na serikali za mahali katika mfumo wa "duality" badala ya "serikali mbili". Yaani kuwe na "Serikali kuu ya kitaifa" na serikali za Mikoa (regional government). Serikali za mikoa zinajitegemea na kujiendesha kwenye mambo mengi tu ambayo serikali ya kitaifa haigusi au inagusa kwa mipaka fulani. So Zanzibar kwa mfano katika mfumo ambao utakuwepo haiwi na "serikali yake" bali inakuwa ni sehemu ya serikali za mikoa (Unguja ya kwake na Pemba ya kwake) na hivyo hivyo kwa mikoa mingine! Inafuta kabisa huu mfumo wa sasa wa nchi mbili, marais wawili, serikali mbili n.k!!
 
Mkandara ni lini mara ya mwisho kuwa bongo and more specifically ni lini ulitia mguu Zanzibar? Post yako haiendani kabisa na hali halisi iliyoendelea Zanzibar. Almost kila nyumba Zanzibar wamebandika matangazo - 'waachwe wapumue'.

Kwanini tusiwaunge mkono watu wanaotafuta 'neema'. Tunawapenda sana Zanzibar na ndio maana hata bill za umeme tunawalipia, na hata Maalim Seif akijisikia kuja kusalimia tunamtumia ndege imlete kwa raha na starehe zake. Sasa wanataka 'kupumua' wamekuwa watu wazima hawa (48yrs), kwanini tusiwaunge mkono ndugu zetu hawa?

Na wapo watu wengi, tena wazito hawasemi hadharani kama Maalim Seif lakini ukiongea nao pembeni wanasema hayo hayo anayosema Seif. Midahalo ya kudai Zanzibar 'huru' kwa sasa inaongozwa na mwanasheria mkuu wao! Na mimi nasema ni haki yao kabisa. Waachwe waende (including no show Dodoma next month).

Hapa tulipofika ni ama tugawane mbao yaishe, au nchi moja yenye mikoa kadhaa. Hata serikali mbili haiwezekani tena, ni mzigo. Time to move on. LET ZANZIBAR GO.
Maadam unataka kujua nitamwambia, ilikuwa mwaka jana 2011 mwezi wa tatu, niliondoka Bongo mwezi wa nne hivyo sidhani kama nimechelewa sana. Na sielewi kumetokea maajabu gani zaidi kwa sababu tayari serikali hii ilikuwepo na matatizo ya Wazanzibar yalikuwepo palepale, mateja na madangulo yazidi kuongezeka siku baada ya siku. Imechukua nguvu ya watu binafsi kufanya hata madogo ambayo serikali hiyo ilitakiwa kuyafanya na hakika naipenda Zanzibar ile ya Marehemu Karume kuliko hii ya leo. Na kibaya zaidi Aloyafanya Marehemu Karume (The worse President u can imagine) huwezi kuyalinganisha na mjumuisho wa marais wote waliopita ktk kuujenga Uzanzibar. Kwa hiyo ukweli siku zote ndio unanisukuma kuyasema haya.

Kila nyumba kubandika tangazo haina maana hawa watu wanaelewa, ni washabiki kaa wale wanaoweka yasini milangoni kwa kuamini tu lakini hawajui ujumbe mzima wa Yasini na kufuata yale wanayopaswa. Hivyo sipingi kabisa Zanzibar ijitenge na nadhani miye ni mmoja wa watu wanaotaka sana Let's zanzbar go lakini tutawapa wananchi wenyewe sio kundi la hawa watu..Kuna wakati sisi wenyewe tunatakiwa kuwa wakweli na kuisimamia haki maanake hili bara letu ni UMASKINI na UJINGA pekee ndio unaoendesha siasa za nchi..
 
ASSALAAMU 'ALAYKUM NI KATIKA
KUSHIRIKIANA KWA KUPEANA HABARI KWA
PICHA NA MATUKIO, KUKUMBUSHANA
YALIYOJIRI HUKU NA KULE NA KUWEKA
KUMBUKUMBU AMBAYO WEWE UNAETEMBELEA
ITAWEZA KUKUHABARISHA AU KUKUMBUSHA KITU, JAMBO AU TUKIO ZanziNews ‹ › Home View web version Wednesday, October 10, 2012 MAPARA at 9:20 PM Dk Shein azindua kazi ya kulaza
waya wa umeme Rais wa zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la
Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,(kulia)
akipata maelezo kutoka kwa Naibu
Mkurugenzi wa Mradi wa ESBI,pia Mshauri
Mwelekezi wa Mradi wa MCC Johan Swan,wa
Ireland(kushoto) alipofika kuuzindua Ulazaji wa Waya wa Umeme katika ufukwe wa bahari
ya Fumba hadi Ras -Kiromoni Tanzania Bara,
(wa pili kulia) Balozi wa Marekani Nchini
Tanzania Alfonso Lenhardt. Rais wa zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la
Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,(kulia)
akipata maelezo kutoka kwa Naibu
Mkurugenzi wa Mradi wa ESBI,pia Mshauri
Mwelekezi wa Mradi wa MCC Johan Swan,wa
Ireland(kushoto) alipofika kuuzindua Ulazaji wa Waya wa Umeme katika ufukwe wa bahari
ya Fumba hadi Ras -Kiromoni Tanzania Bara Pichani Mafundi wakiwa tayari kuanza kazi kwa kutumia Kijiko aina ya Hyundai kikiwa kimezuia Waya wa Umeme kutoka katika fukwe za Fumba,utakaolazwa katikati ya Bahari hadi Ras-Kiromoni
Tanzania bara,kazi hiyo itachukua siku kumi na
moja,mpaka kumalizika kazi hiyo inayofanywa
na Kampuni ya Viscas kutoka nchini Japan.
[Picha na Ramadhan Othman,Ikulu.] Na Rajab Mkasaba, Ikulu RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein amezindua ulazaji wa waya wa pili wa umeme kutoka Ras Fumba Zanzibar hadi Ras Kiromoni Dar-es-Salaam na kusema kuwa sasa mwelekeo wa kuwa na umeme wa uhakika hapa Unguja umetia sura. Hafla hiyo iliyofanyika huko Fumba, Wilaya ya Magharibi, Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja, ilihudhuriwa na viongozi mbali mbali wa vyama
na serikali pamoja na wananchi kutoka maeneo mbali mbali ya Zanzibar ambapo pia, katika hafla hiyo Makamu wa Kwanza wa Rais Maalim Seif Sharif Hamad na Makamu wa Pili wa Rais Balozi Seif Ali Idd walihudhuria. Dk. Shein alisema kuwa Serikali inathamini sana na kupongeza ustahamilivu wa wananchi katika kipindi chote cha tatizo la umeme na kutoa nasaha zake kwa wananchi kuendelea kuwa wastahamilivu kwa kipindi kifupi kilichobaki. Aliwaeleza wananchi kuwa wakati Serikali ilipofanya maamuzi ya kuchukua hatua za dharura za kuwa na umeme wa mgao, ilifikia maamuzi ya kuzidisha jitihada zake ilizokuwa imezianzisha za kutafuta ufumbuzi wa kudumu wa tatizo hilo kwa lengo la kuimarisha uchumi na ustawi wa wananchi. Dk. Shein alieleza kuwa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar kupitia Shirika lake la umeme, kwa kushirikiana na washirika wa maendeleo ilifikia
maamuzi ya kutekeleza kwa haraka miradi mbali mbali ukiwemo waya mpya wa umeme. Alieleza kuwa waya huu mpya uliolazwa hivi leo una uwezo mkubwa zaidi ya ule mkongwe unaotumika hivi sasa, na kueleza kuwa kwa mujibu wa wataalamu waya huo mpya utakuwa na uwezo wa kusafirisha umeme wa Megawati 100. Dk. Shein alieleza kuwa kiwango hicho ni zaidi ya mara mbili ya uwezo wa waya wa zamani, na bila shaka ni mara mbili zaidi ya mahitaji ya umeme wa hivi sasa, na kusisitiza kuwa waya unaotumika hivi sasa bado utaendelea kutumika pindi ukihitajika hivyo ipo haja ya kuutunza na kuishughulikia miundombinu yake. Pia, Dk. Shein alitoa pongezi na shukurani kwa Serikali ya Marekani kupitia Shirika la Changamoto la Milenia la Marekani (MCC) na MCAT kwa ushirikiano mkubwa katika kufanikisha mradi huu. Dk. Shein alitumia fursa hiyo kuipongeza Serikali ya Japan kwa juhudi zao mbali mbali katika kuiendeleza sekta ya nishati hapa Zanzibar kupitia Shirika lake la JICA pamoja na kutoa shukurani kwa watendaji wa Kampuni ya VISCAS CORPORATION ya Japan, KALPATARU Power Transmission Ltd ya India na SYMBION- ARENA ya Marekani na Ufaransa kwa juhudi zao katika kufanikisha mradi huo Aidha, Dk. Shein alisema kuwa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar siku zote inahakikisha kuwa Zanzibar inaenda sambamba na mabadiliko ya teknolojia yanayotokea duniani katika sekta ya habari na mawasiliano. Dk. Shein alisema kuwa ndani ya bomba linalobeba waya wa umeme, utapitishwa waya wa mawasiliano ambapo ni muhimu sana katika kuimarisha mawasiliano kwa ajili ya mitandao, simu na pia katika kuimarisha huduma za redio na televisheni na kueleza kuwa mradi huo pia utasaidia kuimarisha Shirika la ZBC hapa nchini. Aidha, Dk. Shein alisema kuwa utekelezaji wa mradi huo ni miongoni mwa jitihada za Serikali katika kutekeleza Mpango Mkuu wa Kukuza Uchumi na Kupunguza Umasikini Zanzibar (MKUZA) ambao sasa upo kwenye awamu ya pili. Pamoja na hayo, Dk. Shein aliwataka wananchi kujiepusha na vitendo vya uharibifu na vya hatari kwa maisha ikiwa ni pamoja na kujenga karibu na miundombinu ya miradi hiyo na uchimbaji wa michanga karibu na nguzo za umeme. Kadhalika, aliwataka wananchi kujiepusha na tabia ya kujenga karibu na maeneo yaliopita umeme au nyaya za mawasiliano na wawe wepesi wa kutoa taarifa kwa wahusika mara tu wanapobaini tukio linaloashiria uharibifu wa miundombinu hiyo. Dk. Shein alitoa pongezi kwa Rais mstaafu wa awamu ya tatu Mhe. Bejamin Wilium Mkapa, kwani wakati wa uongozi wake ndipo mazungumzo ya mradi huo yalipoanza pamoja na kutoa shukurani kwa Rais Kikwete kwa kuendeleza mchakato huo na hatimae kutia saini msaada wa fedha za mradi huo na mengineyo, Rais George Bush na Rais Obama wa Marekani kwa msaada wao huo kwa Zanzibar Waziri wa Wizara ya Ardhi, Makaazi, Maji na Nishati Mhe. Ramadhan Abdalla Shaaban katika hotuba yake fupi alieleza kuwa ukamilishaji wa mradi huo utasaidia sana kutimiza azma ya Serikali ya Mapinduzi Zanzibar ya kuwapatia wananchi wake huduma bora ya umeme ili kuimarisha ustawi wa jamii, kuimarisha uchumi na kuwavutia wawekezaji. Nae Balozi wa Marekani nchini Tanzania Mhe. Alfonso Lenhardt alieleza kuwa Marekani itaendelea kuiunga mkono Zanzibar katika kuimarisha sekta za maendeleo na kusisitiza kuwa mradi huo ni hatua kubwa ya kukuza uchumi hapa nchini. Mapema Katibu Mkuu wa Wizara ya Ardhi, Makaazi, Maji na Nishati Mwalimu Ali Mwalimu alisema kuwa ni dhahiri kwamba Mradi huo utawanufaisha moja kwa moja Wazanzibari wote nchini na utahuisha mfumo wa mawasiliano ya kimtandao wakati huu ambapo
Zanzibar inaingia katika mfumo wa Serikali Kimtandao (e-Government). Katibu Mwalimu alisema kuwa kama ulivyo ule waya wa umeme wa Pemba- Tanga, waya huu hautumii teknolojia ya mafuta kama huo uliopo hivi sasa, na kwa hivyuo changamoto zake za matengenezo ni ndogo mno kwa kulinganisha ambapo matarajio yake ni kuishi kwa muda wa miaka 40. Alisema kuwa kwa mujibu wa ongezeko la matumizi ya umeme ya asilimia 7 kwa mwaka inategemewa kuwa waya huu utaweza kuhimili matumizi hadi mwaka 2024. Kampuni ya VISCAS ilianza rasmi kazi ya utengenezaji waya tarehe 19 Novemba mwaka 2010 na kukamilika tarehe 5 Aprili mwaka huu. Mradi huo wa uwekaji wa njia ya pili ya umeme kutoka Ubungo Tanzania Bara hadi Mtoni Zanzibar umegharimu dola za Marekani 72,193,750.00 kati ya dola 206.5 milioni kwa sekta ya nishati Tanzania nzima, ambapo SMZ imechangia dola 1,465,625.00 kufidia mali za wananchi. Zoezi hilo litachukua siku 11 ambapo waya huo una urefu wa km 37.
 
Tuna maana tu kuwa hakuna "nchi mbili, mataifa mawili"; tunaamini tukisolve hilo tunaweza kuwa na serikali za mahali katika mfumo wa "duality" badala ya "serikali mbili". Yaani kuwe na "Serikali kuu ya kitaifa" na serikali za Mikoa (regional government). Serikali za mikoa zinajitegemea na kujiendesha kwenye mambo mengi tu ambayo serikali ya kitaifa haigusi au inagusa kwa mipaka fulani. So Zanzibar kwa mfano katika mfumo ambao utakuwepo haiwi na "serikali yake" bali inakuwa ni sehemu ya serikali za mikoa (Unguja ya kwake na Pemba ya kwake) na hivyo hivyo kwa mikoa mingine! Inafuta kabisa huu mfumo wa sasa wa nchi mbili, marais wawili, serikali mbili n.k!!
Unafikiri wazanzibar wako tayari kwa aina hiyo ya "duality" ambapo kunakuwa na Pemba na Unguja kama mikoa si taifa moja. Unataka kusema Wanzibar si wamoja na jina lao la sasa la nchi yao walipeleke wapi? HIvi kwenye muungano wetu ni lazima kuwasikiliza Wazanzibar au hata Watanzania (Tanganyika?) wanaweza kuwaambia wazanzibar "nendeni zenu" kama wewe unavyowahimiza "watoke" kwenye muungano?
 
Tuna maana tu kuwa hakuna "nchi mbili, mataifa mawili"; tunaamini tukisolve hilo tunaweza kuwa na serikali za mahali katika mfumo wa "duality" badala ya "serikali mbili". Yaani kuwe na "Serikali kuu ya kitaifa" na serikali za Mikoa (regional government). Serikali za mikoa zinajitegemea na kujiendesha kwenye mambo mengi tu ambayo serikali ya kitaifa haigusi au inagusa kwa mipaka fulani. So Zanzibar kwa mfano katika mfumo ambao utakuwepo haiwi na "serikali yake" bali inakuwa ni sehemu ya serikali za mikoa (Unguja ya kwake na Pemba ya kwake) na hivyo hivyo kwa mikoa mingine! Inafuta kabisa huu mfumo wa sasa wa nchi mbili, marais wawili, serikali mbili n.k!!
Mkuu wangu mawazo ya serikali moja DULITY ni kupuuza Muungano wa nchi mbili.. Zanzibar ni nchi ina soveign yake na muhimu sana ktk majadiliano kama haya tuheshimu kuwepo kwa Zanzibar na kuenzi Muungano uliopo..Hivyo kuifananisha Zanzibar na Mikoa ya Mwanza, Arusha na kadhalika ni wazo linalopotosha zaidi..

Kuna njia mbili tu zinazoweza kukubalika 1. Kuunda serikali tatu,(Ya UMoja wa Taifa, na zile za Tanganyika na Visiwani) ama 2. Kuuvunja Muungano kutokana na kura za maoni za Wazanzibar ambao wataambiwa ukweli na wawakilishi wa makundi mawili majukwaani. Ikiwa ni pamoja na kundi la wale wanaoutaka Muungano wakiwaeleza wananchi kwa nini muungano ni muhimu kwao, halafu wale wanaopinga Muungano na kwa nini hautakiwi.. Kisha wananchi wakisha elimishwa hilo Wazanzibar wote watapiga kura za maoni yao na yataheshimika. Kura za Hapana zikiwa nyingi tutaendelea na mfumo uliopo wa serikali mbili na pengine kurekebisha tu kero zilizopo..
 
Maadam unataka kujua nitamwambia, ilikuwa mwaka jana 2011 mwezi wa tatu, niliondoka Bongo mwezi wa nne hivyo sidhani kama nimechelewa sana. Na sielewi kumetokea maajabu gani zaidi kwa sababu tayari serikali hii ilikuwepo na matatizo ya Wazanzibar yalikuwepo palepale, mateja na madangulo yazidi kuongezeka siku baada ya siku. Imechukua nguvu ya watu binafsi kufanya hata madogo ambayo serikali hiyo ilitakiwa kuyafanya na hakika naipenda Zanzibar ile ya Marehemu Karume kuliko hii ya leo. Na kibaya zaidi Aloyafanya Marehemu Karume (The worse President u can imagine) huwezi kuyalinganisha na mjumuisho wa marais wote waliopita ktk kuujenga Uzanzibar. Kwa hiyo ukweli siku zote ndio unanisukuma kuyasema haya.

Kila nyumba kubandika tangazo haina maana hawa watu wanaelewa, ni washabiki kaa wale wanaoweka yasini milangoni kwa kuamini tu lakini hawajui ujumbe mzima wa Yasini na kufuata yale wanayopaswa. Hivyo sipingi kabisa Zanzibar ijitenge na nadhani miye ni mmoja wa watu wanaotaka sana Let's zanzbar go lakini tutawapa wananchi wenyewe sio kundi la hawa watu..Kuna wakati sisi wenyewe tunatakiwa kuwa wakweli na kuisimamia haki maanake hili bara letu ni UMASKINI na UJINGA pekee ndio unaoendesha siasa za nchi..

24 hrs ni muda mrefu sana kwa siasa za Tanzania let alone Zanzibar! Hivyo April 2011 ni sawa na mwaka 1947. Mambo yanakwenda kwa speed kubwa.

Na kama niliandika, wapo wakubwa wengi sana wanaokubaliana na hoja za Maalim Seif (Tofauti na huko awali). Ndio maana sikubalini na hoja yako kwamba "tuwape watu wenyewe na sio kundi la watu". For better for worse, wanzanzibari waachwe wafanye wanavyotaka. LET ZANZIBAR GO.
 
Back
Top Bottom