Wapigakura wa Muleba, Bukoba (V+M), Missenye, B'mulo, Karagwe, Kyerwa....

Hakuna mkoa ulionisikitisha zaidi ya Kagera katika uchanganuzi wangu wa matokeo ya uraisi katika uchaguzi uliopita.CCM walipata kura nyingi mno,ukiondoa mikoa ya waswahili wenzake kama Tanga,Mtwara kwa haraka haraka ni rahisi ku-conclude kuwa JK alipata asilimia kubwa sana ya kura kwa mkoa wetu wa Kagera...ndio mkoa unaokata kufit in my theory of observation,kwamba mikoa inayopatikana mipakani mwa nchi yetu ndio inayoleta changamoto kwa CCM.What is wrong with Kagera?Is it a case of being neglected for so long that we have lost our voice of resistance?
 
Hakuna mkoa ulionisikitisha zaidi ya Kagera katika uchanganuzi wangu wa matokeo ya uraisi katika uchaguzi uliopita.CCM walipata kura nyingi mno,ukiondoa mikoa ya waswahili wenzake kama Tanga,Mtwara kwa haraka haraka ni rahisi ku-conclude kuwa JK alipata asilimia kubwa sana ya kura kwa mkoa wetu wa Kagera...ndio mkoa unaokata kufit in my theory of observation,kwamba mikoa inayopatikana mipakani mwa nchi yetu ndio inayoleta changamoto kwa CCM.What is wrong with Kagera?Is it a case of being neglected for so long that we have lost our voice of resistance?
Kwa kumbukumbu zangu na takwimu sahihi zilizopo, ni kwamba katika uchaguzi mkuu wa 2010 kwa upande wa idadi ya kura za uraisi CHADEMA iliibuka kidedea zidi ya CCM ukitaka nitakushushia data za kila jimbo.
 
Mbona Ngara imesahaulika,hili jimbo ndo kabisa. Wako usingizi wa saa 9 usiku ambao hata mlango ukivunjwa hushtuki.
Huyu mbunge alikuwa afisa utumishi mkuu wa serikali miaka zaidi ya 10.Anaishi Dar miaka yote na hata nyumba huko Rulenge alijenga kwa ajili ya kugombea ubunge.

Shida za Ngara hazielezeki,umasikini wa kufa mtu hata PM ni shahidi wakati wa ziara yake naye alisikitishwa na hali ilivyo.
Chama cha magamba ndicho cha kubeba dhamana ya tatizo hili na wananchi wa Ngara achaneni na zimwi hili limekuleni sasa mnataka liwamalizeni.
 
Kutangulia si kufika. Wana wa Kagera sasa wameshindwa na wana wa Arusha hata wana wa Mwanza nao wameanza kuona mwanga. Kwa bahati mbaya, wabunge magamba wa Kagera ni MATAPELI ya kutupwa. Basi tu!!!!!
 
Kwa kumbukumbu zangu na takwimu sahihi zilizopo, ni kwamba katika uchaguzi mkuu wa 2010 kwa upande wa idadi ya kura za uraisi CHADEMA iliibuka kidedea zidi ya CCM ukitaka nitakushushia data za kila jimbo.
Shusha data labda utanirejeshea 'furaha' kwa sababu nilicheck pie chart ya matokeo iliyokuwa ikionesha JK akiwa percentage kubwa sana.Ni trend ambayo hata matokeo ya Ubunge yalionesha hali ya CDM kuzidiwa kura.
 
Maruku Vanila umenigusa, Ruberts na Bigaraone nimewapata. Mimi natokea Jimbo la Nkenge na mbunge wa jimbo langu anatokea CCM na anaitwa Mhe. Asumpta Nshunju. Pamoja na wabunge wengine wa mkoa wa Kagera naamini ujumbe wetu kupitia JF ama wanausoma au watapewa na wasaidizi wao. Mimi ninamtumia Waraka Mhe. Asumpta Nshunju nasema hivi; Mhe, wananchi wa jimbo la Nkenge walikuamini wakaweka tumaini lao kwako. Wewe pia uliwaahidi kuwa utashughulikia kero zao zote na utakuwa nao bega kwa bega. Nao wana Nkenge wakakupa jukumu hilo kwa kumnyang'anya kijiti DR Kamala wakaweka tumaini lao kwako. Sasa elewa kero za wananchi wa Nkenge zimezidi na kwa uchache kwa sasa wanakabiliwa na ukosefu wa madawa wewe unafahamu kuwa pale Mugana DDH, Bunazi Hosp, Kashasha HC,Igayaza HC, Bugandika Disp n.k vifaa tiba ni tatizo na sasa limeongelewa Bungeni, tatizo la mnyauko wa migomba linazidi kutamalaki nawe hujashughulikia huku ukijua kuwa ndizi ndo chakula chetu kikuu, ujenzi wa shule za sekondari za kata umedoda majengo yamekuwa mapagala na wewe uko kimya. Matatizo ni mengi na yanazidi kila kukicha. Sasa ni wakati muafaka kwa wewe kudhihirisha kwamba ama wananchi wa Jimbo la Nkenge walikosea kukuchagua kuwa Mbunge wao au basi hawakukosea nawe uko pamoja nao hivyo shiriki kikamilifu kuwawajibisha viongozi wazembe na mafisadi. Vinginevyo, mimi sitasubiri mwaka 2015, nitaanza sasa hivi, nitaongea na ndugu, marafiki na majirani na wana Nkenge kuwa sasa utufai. Kimsingi tunafuatilia yote yanayoendelea Bungeni na hata utumishi wako tangu uwe Mbunge.
 
Kusema ukweli mnenigusa sana mmenikumbusha sakata la juzi la madiwani wilaya ya Muleba kukataa bajeti nakusababisha mkurugenzi kutoa machozi. Kwa jimbo la Muleba kusini mpaka sasa wananchi tunajuta kwanini tulimchagua Mama prof.nadhani hili ni jimbo lenye mkosi kwenye uchaguzi wa viongozi hasa wabunge. Jimbo halina historia ya kuwa na mbunge makini na mpiganaji. Ukianza na mzee KIKEITO niwe (Zimbihile) huyu ilikuwa ni full kusinzia kama Wassira wa sasa. Tukaweka Masilingi kwamba labda nikijana atatusaidia lakini hakuna kitu alichofanya zaidi ya kupayukapayuka majukwaani. Sasa tumemleta prof mjengoni mama huyu amekuwa bure kabisa sasa sijui ni sababu ya uwaziri au tatizo nini. Niliwahi kusema mama huyu alikuwa anataka tu kuwa mbunge coz alishaahidiwa uwaziri lakini hakujua majukumu ya mbunge ni yapi kwa wananchi.
Mwisho wa siku kazi za uwaziri hawezi na ubunge kaferi. Aliahidi umeme kutoka Kishoju kwenda Runazi kupitia vijiji vya Karutanga, Gwanseli, Ilemera, Lulanda mpaka Runazi na aliahaidi kwamba b4 end of 2011 mpaka sasa kimya. Mama amekuwa muoga sana hata wa kutembelea wananchi wake. Hii ni aibu kwa Mkoa wetu wa Kagera na majimbo yake nadhani kwa umoja wetu kuna ulazima wa kutoa elimu kwa ndugu zetu walioko vijijini ili waweze kufungua macho maana tunazidi kudidimia.
Nimependa kamasemo "OBUNAKU MPARI ONYATA OINAYO".
 
7 Reactions
Reply
Back
Top Bottom