Mubezi
Member
- Sep 27, 2010
- 71
- 23
MGOMBEA ubunge wa jimbo la Lindi mjini,kwa tiketi ya CCM, Bw, Mohamedi Abdullaziz amewakatisha tamaa wakazi wake, baada ya kuwaeleza bila ya aibu kuwa Serikali haina mpango wa kuboresha bandari yao kwa kile alichokieleza kukosekana kwa bidhaa za kusafirisha kutoka mkoani humo kwenda maeneo mengine.
Abdullaziz ametoa kauli hiyo katika mikutano yake mbalimbali ya kampeni akiomba ridhaa achaguliwe tena kuongoza Jimbo hilo kwa mara ya nne mfululizo, katika viwanaj vya kata ya matopeni na Wailes mjini hapa.
Mgombea akiomba tena ridhaa hiyo, Amesema Serikali kwa sasa haina mpango wakujenga au kuboresha Bandari iliyopo katika mji wa Lindi, kutokana na kukosabidhaa za kutosha za kusafirisha pamoja na abiria.
Abdullaziz ambaye anawania tena nafasi hiyo kwa mara ya nne mfululizo alisema Serikali ingeboresha bandari hiyo iwapo wananchi wangekuwa wanazalisha zaidi mazao mbalimbali, ambayo ingesaidia meli zinapofika katika mji huo kupeleka mizigo na kurejea tena na mizigo ikiwa ni kwa ajili ya kupunguza gharama za meli kurudi bila ya kubeba bidhaa.
Jamani tusidanganyane na mtu yeyote, Serikali haina mpango wa kujenga bandari kutokana kutokuwepo kwa mizigo na abiria wa kusafirisha kwa meli kutoka Lindi kwenda Dar es salaam,,,,,,, Hivi ni nani atapanda meli masaa 24 na kuacha basilinalo safiri kwa masaa sita hadi manane?.
Kama malori ya tani kumi yanaleta mzigo na kurudi bila kubeba mizigo mingine,je meli ikija bandari ya Lindi itabeba kitu gani? Amehoji mgombea huyo
Kwa upande wa viwanda Bw, Abdullaziz ambaye pia ni mkuu wa mkoa wa Iringa alisema kutokana na Serikali kujiondoa katika Shughuli za kibiashara, haina mkakati wowote wa kujenga viwanda kutokana na kile alichokieleza kukosekana kwa mali ghafi za kutosha kwa ajili ya uendeshaji wake.
Mgombea ubunge huyo ameitaja mali ghafi hizo kuwa ni pamoja na kutokuwa na umeme wa uhakika, miundombinu ya barabara, maji,mawasiliano ya ambavyo kwa jimbo la Lindi na Tanzania kwa ujumla ni tatizo kubwa.
Abdullazizi amesema wajibu wa kujenga viwanda uko mikononi mwa wawekezaji ambao uchagua maeneo au mikoa ya kuwekeza katika viwanda wakizingatia upatikanaji wa huduma muhimu za kijamii.
Mgombea huyo amewaomba wananchi wa jimbo hilo la Lindi mjini kumchagua yeye kuwambuge kwa mara ya nne mfululizo, Jakaya mrisho Kikwete kuwa rais wa Jamuhuri ya muungano wa Tanzania pamoja na madiwani wote kupitia Chama cha mapinduzi (CCM).
Wakizungumza na gazeti hili baada ya mkutano huo, baadhi ya watu waliojitokezakumsikiliza wameondoka katika mkutano huo,huku wakisikitishwa na kauli ya mgombea huyo amekiuka ahadi zake alizokuwa akizitoa wakati wa kampeni zake za kuomba ridhaa achaguliwe katika mikutano yake, ikiwemo ile ya mwaka 2000
na 2005 alipokuwa akisema akichaguliwa atahakikisha bandari inajengwa ili watu waendelee kupata ajira.
Huyu mtu anakanusha hata ahadi zake, kwani uchaguzi wa mwaka 2000 na 2005 wakati akiomba tumchague alituambia moja ya kero atakalolishighulikia ni pamojana uboreshaji wa bandari, Leo ametugeuka? Wamesema Martin Michael na Issa Selemani.