BAK
JF-Expert Member
- Feb 11, 2007
- 124,790
- 288,006
Wananchi watoa masharti kwa wagombea ubunge
Merali Chawe, Mbeya
Daily News; Saturday,January 10, 2009 @20:06
Merali Chawe, Mbeya
Daily News; Saturday,January 10, 2009 @20:06
Baadhi ya wakazi wa Mbeya Vijijini, wamesema Mbunge atakayechaguliwa kuongoza jimbo hilo, anatakiwa kuhakikisha anatatua kero za msingi za wananchi zikiwamo za umeme, maji, barabara na madaraja kabla ya mwaka 2010.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti na HabariLeo wakati wa mikutano ya wagombea ubunge wa CCM, CUF na SAU, walisema mgombea atakayeshindwa kutekeleza ahadi zake asijitokeze katika Uchaguzi Mkuu mwaka 2010.
William Nyomezi alisema kwa muda mrefu sasa wagombea wamekuwa wakitoa ahadi zisizotimizwa na mara baada ya uchaguzi hakuna kiongozi anayeonekana hadi uchaguzi mwingine unapokaribia, hali ambayo inakatisha tamaa wananchi.
Alisema aliyekuwa Mbunge wa Jimbo hilo, Richard Nyaulawa, alijitahidi kutekeleza ahadi zake na kwamba wanaamini kuwa mbunge atakayechaguliwa safari hii, atakuwa na kipimo cha kutekeleza ahadi zake kabla ya mwaka 2010, ili wananchi waweze kumwamini na kumchagua tena.
Eliah Dafwile alisema kwa muda mrefu wamekuwa wakipewa ahadi za kupewa umeme, maji, barabara na madaraja bila kutekelezwa."Ukizunguka hapa kuna nguzo za umeme zilizowekwa tangu mwaka 1999, lakini hadi sasa ikiwa ni miaka takribani tisa, hakuna umeme," alisema.
Alisema kipimo cha wagombea wa sasa ni jinsi watakavyoweza kutekeleza ahadi zao kabla ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2010 na kwamba atakayeshindwa kutekeleza ahadi zake, asitarajie kuchaguliwa tena katika Uchaguzi Mkuu ujao.
Wakati huo huo, Mbunge wa Kuteuliwa, Tom Mwang'onda, amewataka wananchi kuchagua mgombea wa CCM, Mchungaji Luckson Mwanjale, kwa kuwa chama hicho ni imara na kwamba ndoa ya ASP na TANU iliyounda chama hicho haijavurugika hadi leo.Alisema vyama vya upinzani vimekosa msimamo ambapo ushirikiano wao unaelekea kuvunjika katika kipindi kifupi na kwamba wakipewa ridhaa ya kuongoza nchi hawataweza.