Wapiga Kura ndio Wahanga wa Mabomu: WanaJF nk wanamtetea nani?

Albert Msando

JF-Expert Member
Nov 2, 2010
1,019
171
Wandugu,

Inapotokea janga kama Gongo la Mboto lawama zote kwa CCM na viongozi wake. Waliodhurika wanahurumiwa, wanaonekana wanyonge na wanaostahili kutetewa. Michango inakusanywa na misaada inapelekwa. Dr Slaa anaenda kuwatembelea. sisi wengine tunaendelea kuwaombea.

Lakini, baada ya kusoma post ya Waberoya, nimelazimika kujiuliza, mpiga kura ni nani? Mhanga wa Mabomu ni nani? Je kuna uwezekano wakawa ni walewale? Kwa haraka haraka ni swali la kijinga, lakini ukijiuliza zaidi unashawishika kutaka kulijibu. Je mhanga ndie aliyemchagua aliyezembea hatimaye maisha yake yamekatishwa?

Swali hili linakuwa chungu na lenye kukera pale unapotaka kumjua Mbunge wa Gongo la Mboto ni nani. Diwani wa eneo lile ni nani? Mwenyekiti wa Mtaa ule ni nani?

Unajiuliza, hawa walichaguliwa ili nini? Mbona wao hawajaambiwa wajiuzulu? Waziri na Mkuu wa Jeshi wajiuzulu, na mwenyekiti wa mtaa? na Diwani? na Mbunge?

Katika hali ambayo ni ya kawaida kabisa hakuna anayeangaika nao. Na mimi nawaacha.

Nitarudi kwa wapiga kura wao. Mbona na wao wako kimya? Kwani hawaoni kama waliowachagua pia ni wa kulaumiwa? Walikuwa wapi mpaka janga hili likatokea? Kwa nini wanatokea baada ya tatizo na si kabla ya tatizo.

Sisi wengine tunaopaza sauti na kuwatetea wahanga, tunawatetea dhidi ya nani?

Sina lengo wala nia ya kuwalaumu wahanga kwa kuwachagua viongozi wao. Lakini nina haki na wajibu wa kuwakumbusha kuhusu viongozi wao ni kina nani. Wao ndio waliowachagua. Walimchagua Mwenyekiti wa Mtaa wa Chama wanachokipenda na kukiamini, hivyo hivyo kwa Diwani na Mbunge!!

Nitawalaumu CDM na wengine kwa sababu moja tu, kwa nini tuliowaweka kugombea hawakushinda? Ni uzembe wetu au ni maamuzi ya wananchi?

Bado nasumbuka na mawazo. Hii nchi nani anachagua viongozi? Wanokosa ajira, wanaokosa elimu, wanofiwa na watoto na wake zao wakati wa kujifungua, wanaonunua sukari kwa bei ya juu, wanolipa nauli kubwa, wanaokosa umeme, wanaokufa kwa kipindupindu, waotozwa kodi kubwa, wanaolipwa mshahara kiduchu wanaoibiwa na majambazi, wanaohamishwa kwa nguvu ili wawekezaji wafaidi, wanaocheleweshewa malipo yao ya uzeeni na wengine wengi huwa wanamchagua nani kuwaongoza???? Ina maana ni watu Milioni Mbili (2Million) tu ambao ndio hawana ajira, hawana umeme, hawana elimu, wanafiwa na watoto na wake zao wakati wa kujifunua n.k??? Katika watu Mil 35 ni watu Mil 2 ndio wanaona sababu ya kubadili uongozi? Au wengine wanaona kuna sababu lakini hawamuoni kiongozi mbadala? Au watu Mil 5 waliomchagua kiongozi yule yule hwana shida hizo nilizotaja?

Hayo yote hayajaanza 2010. Yameanza na yamekuwepo siku nyingi. Mbona wanachaguliwa wale wale? Au wanaoathirika na uzembe na shida ndani ya nchi hii hawapigi kura? Wakati wa kupiga kura huwa shida zao hazipo tena?? Kwani aliyezembea mabomu ya Mbagala ni nani? Je ambaye hajalipa fidia kwa wahanga wa Mbagala ni nani???


Wapiga kura ndio wahanga wa mabomu. Ndio wahanga wa shida katika nchi hii. WanaJF wanamtetea nani?? Wanaharakati na vyama vya siasa vinamzungumzia nani?? Mbona WanaJF, viongozi wa vyama vya siasa na wanaharakati hawaonekani kama watu wenye shida saana!! Au ni upendo wao kwa wengine??

Ni mawazo tele.
 
Ni kweli JK! Nipo arusha nawatetea washtakiwa ambao ni wanachama wa CDM. As you are aware CDM sio mshtakiwa.
 
Na hili la hii picha uliyoweka ni vipi tena JK? Ni symbol ya urafiki au uhasama wa hao wawili?
 
Back
Top Bottom