Wapi nitapata kazi kama Mtafsiri wa lugha ya kiitaliano/Italian translator

Iyokopokomayoko

JF-Expert Member
Sep 15, 2011
1,785
441
Heshima kwenu wakuu,
Tafadhari naombeni kwa anayejuwa ni wapi au kampuni ipi wanahitaji mtafsiri wa lugha ya kiitaliano, mimi ni mzungumzaji na mwandishi mzuri katika lugha hiyo.

naomba kuwasilisha
 
Nenda Zanzibar kaka halafu kuwa free lance tour guide utakuwa unawatembeza kila kukicha. ila yakupasa uifahamu zanzibar vizuri
 
Nenda Zanzibar kaka halafu kuwa free lance tour guide utakuwa unawatembeza kila kukicha. ila yakupasa uifahamu zanzibar vizuri
Nashukuru mkuu kwa ushauri wako, naifahamu vizuri sana znz nimeshafanya kazi huko kama mwaka mmoja nikifanya kazi hotelini, nilitamani kuwa beach boy wakati nikiwa huko lakini nilishindwa maana niliambiwa ni lazima uwe umeaga kwenu na mimi sikuwa nimeaga nikagaili
 
Nenda Ubalozi wa Tanzania Italia au ubalozi wa Italia Tanzania utaweza kuwafafanulia waTanzania wanaohitaji Visa ya Italia au uwafafanulie waItalia wanaohitaji visa ya Tanzania
 
Nenda Ubalozi wa Tanzania Italia au ubalozi wa Italia Tanzania utaweza kuwafafanulia waTanzania wanaohitaji Visa ya Italia au uwafafanulie waItalia wanaohitaji visa ya Tanzania
Nashukuru mkuu, lakini unafikiri katika ofisi kama hiyo wanakosekana watu kama mimi kweli?!!, sijikatishi tamaa lakini naona ofisi kama hiyo hakuwezi kosekana mtu kama mimi ni mawazo yangu tu mkuu bali nitajaribu kama ulivyonishauri
 
Maisha ni kujaribu kaka usikate tamaa, jua kweli wapo lkn wewe ni bora kuliko wao period
 
Kwa nin unakua mtumwa wa fikra mpaka karne hii? Mbona wao hawasomi kiswah huko kwao italia? Kichaga,kiswahi na kingereza vyanitosha kbsa,ctaki UTUMWA MIE.
 
Nashukuru mkuu kwa
ushauri wako, naifahamu vizuri sana znz nimeshafanya kazi huko kama
mwaka mmoja nikifanya kazi hotelini, nilitamani kuwa beach boy wakati
nikiwa huko lakini nilishindwa maana niliambiwa ni lazima uwe umeaga
kwenu na mimi sikuwa nimeaga nikagaili

Jina lako la kitaliano?
 
Kwa nin unakua mtumwa wa fikra mpaka karne hii? Mbona wao hawasomi kiswah huko kwao italia? Kichaga,kiswahi na kingereza vyanitosha kbsa,ctaki UTUMWA MIE.
Mkuu habari, mbona italy kuna vyuo wanafundisha kiswahili, halafu nijuwavyo mimi ni kuwa waitaliano hawajawahi kututawala kitumwa ila najuwa waingereza unaosema wewe wamewahi kufanya TZ koloni lake. Mi mkuu sijakuelewa kabisa, we nisaidie kama nilivyoomba masuala ya utumwa nitajuwaga huko huko we usijali
 
Inategemea upo wapi, ukija Arusha au Moshi hulali njaa. Makampuni ya tour guide operaters yanatafuta watu kama wewe
Kwa hakika mkuu rafiki zangu wengi wameniambia hivyo, mi nipo dar na itaniuma sana kwenda nje ya hapa lakini kama hali ni hii hadi kesho jioni mi keshokutwa nitapanda ngorika, nashukuru sana mkuu
 
Kwa hakika mkuu rafiki zangu wengi wameniambia hivyo, mi nipo dar na itaniuma sana kwenda nje ya hapa lakini kama hali ni hii hadi kesho jioni mi keshokutwa nitapanda ngorika, nashukuru sana mkuu
..Mkuu wahi season sa hivi, kuna dolari na paundi za nje nje za Watalii. Maisha ni popote sa hivi, usichague kambi.
 
Mkuu wewe ni jinsia gan kwanza? Mie npo arusha na kwa sasa ni high season wagen wapo kibaaoo,kama vp ibuka geto hapa then tufanye michakato coz if u able to speak fluent bas kaz zpo kbao.mie mwenyewe ni mdau katika field hii ya tourism ila ndo hvyo mambo bdo hayajawa dangachee!!
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom