Wapi Nape?

Nadhani inatia aibu kusema jambo ambalo huna hakika nalo....nimejaribu kusoma kejeli hapa nyingi sana lakini nasema mambo yatakapo kuwa kama nilivyosema( na bila shaka mnajua wameshaanza) ....msisite kuja hapa kupongeza pia.......

Pengine uko sahihi, lakini wanacho-doubt watu ni ile kasi uliyoanza nayo imeishia wapi?
 
Pole sana Edson, kazi yenu sasa ni kujaribu kuzusha hata ambayo hayaingii akilini, kama nyi wengine ndoa zimewashinda bahati mbaya poleni... Kama mnaweza kuzusha mpaka ya kifamilia, basi sitashangaa kesho mkisema Nape mchina... Maana kama mnaweza kumzushia mtu kutembea hata na mama yake, basi huu ni uzushi wa kutisha...pole sana maana mmetafuta ufisadi wa Nape mpaka miguu imeota vigimbi... Dawa ya uchafu kuoga si kujaribu kuchafua wengine kwa kudhani utakua msafi

Nakubaliana na wewe japo kwa hili, tujadili hoja na si mambo binafsi yasiyosaidia nchi...
 
Ila si alikuwa anawaleza wanachama wao nchi nzima na kujitambulisha kwao kuwa yeye ndo MWenezi? sasa kazi amemaliza anafuatilia utendaji!! tunamuona sana kwenye news akitembelea vyombo vya habari... mie napenda V8 yake tu sio siasa ya mkodo wake
 
Kwa hili unapaswa uone aibu. Mambo yapi yaliyoanza! Rostamu kaondoka kwa sababu ya siasa Uchwara na si kwa kulazimishwa na mtu. Usiongee kwa mafumbo kama Mwimba taarabu. Yataje mambo yaliyokwishaanza ni yapi! Tunachoweza kukushauri ni kwamba Usifanye shingo ngumu, rudi kwa akina Mzee Lowasa ukawaangukie, wale ni watu wazima wanaoelewa kwamba ulikuwa unaganga njaa tu watakusamehe, lakini ukiendelea kufanya shingo ngumu, itavunjika. Mzee wako Msekwa ndio huyo tena ni aibu nyingine. Kumbe nalo ni jizi tu la mali ya Watanzania. Sasa atawezaje kumnyooshea kidole Mzee wa Vijisenti! Halafu kuwa makini sana, kwani imeshaonekana kwamba CCM hakuna mtu msafi kuanzia waliopo sasa na wengi waliopita. Angalia wasije kuanza kufichua na Madudu yaliyofanywa na Waliotangulia, Wengine ni Wazazi wetu! Akina Lowasa wanajua mengi!

Asante sana SB, umesema yote! Hata wale tuliowaona wanaafadhali leo yanaibuka madudu kibao!
 
Nadhani inatia aibu kusema jambo ambalo huna hakika nalo....nimejaribu kusoma kejeli hapa nyingi sana lakini nasema mambo yatakapo kuwa kama nilivyosema( na bila shaka mnajua wameshaanza) ....msisite kuja hapa kupongeza pia.......

Pole kwa swaum shehe..
 
Nadhani inatia aibu kusema jambo ambalo huna hakika nalo....nimejaribu kusoma kejeli hapa nyingi sana lakini nasema mambo yatakapo kuwa kama nilivyosema( na bila shaka mnajua wameshaanza) ....msisite kuja hapa kupongeza pia.......

Swali hapa ni kwamba ni nani msafi ndani ya chama cha magamba mpaka nape aendelee na kengele zake???? dua la lowasa limefanya kazi maana waliokuwa wanamnyooshea kidole na wenyewe wanaanza kuumbuliwa mmoja mmoja. chama cha magamba hakina msafi hata mmoja. Nasema nikiona mtu anashabikia hiki chama natamani kum.........................
 
Zamani facts na arguments vilikuwa ni mapambo hapa jamvini, sikuhizi hisia na kejeli zinajitahidi kupamba jukwaa.....

Siku nikiingia Igunga mtajua tu, hakuna sababu ya kuandikia mate wakati winno upo......
Nakushauri Igunga nenda kwa step usije kuondoka kwa aibu kuna mbegu inapandwa kule kuwa wewe ndiye chanzo cha kipenzi chao kuondoka hawataki kukuona wanajiandaa kama si kukupopoa kukuzomea popote utakapopita, habari ndio hiyo.
 
Nape anajiandaa kwani yuko na watu makini wasiojua ni vigumu kunielewa.Nyie subirini mtaona tu kimya cha Nape, hiyo yote inayosemwa ni njama za mafisadi ila watashindwa tu.Watu mnaowataja walishachafuka hawasafishiki hata kwa gunia la sabuni ya unga.



Unajua Watanzania tatizo letu ni kutofanya utafiti kumjua mtu au kitu. Nape alipambwa na magazeti kwa kile kilichoelezwa kuibua uozo kwenye project ya UVCCM.Alichokuwa anatafuta ni cheap popularity tu maana huyu jamaa ni mnafiki.Hakukuwa na uchungu wa aina yoyote.UVCCM ilishachafuka kabla ya project hiyo ila yeye alichofanya ni kupandia mgongoni mwa Lowasa baada ya kuukosa uwaziri mkuu wakati alipokuwa waziri mkuu Nape alikuwa ndiye mpeleka habari kwa Lowasa. Ukitaka kujua hilo waulize waliosoma naye India. Wakati akiwa India maisha ya wanafunzi yalikuwa magumu maana walikuwa hawatumiwi pesa kwa wakati au zilikuwa hazitoshi. Wakati wanabrainstorm on the wayforward basi yeye alizoea kuwahamasisha wagomee masomo. Siku moja akiwaamemaliza kuwahamasisha na wao wamekubali kwenda mpaka kwa balozi ndio akasikika akipiga simu akiwa chooni anaongea na mtu ambaye intelligence ilionyesha alikwa ni Lowasa maana walizoea kuongea naye maramara kwa mara. Alikuwa anampa update ya kile ambacho wanafunzi walikuwa wamepanga kukifanya.

Hivyo tunatakiwa kumfahamu huyu bwana ni nani.Ni mnafki wa kutupwa na kichwani ni mweupe. Hamna kitu kabisa ndio maana ni rahisi kutumiwa.Sasa ameshidwa kusoma alama za nyakati.Anafikiri CCM ilishafuka na mapacha watatu. Ilianza na Azimio la Zanzibar, Ikauza mbuga zetu za wanyama, ikabinafsisha mashirika mithili ya muuza njugu, ikaleta ubaguzi mbaya kuliko hata ukaburu kwa kili kinachojulikana kama mtandao wa kumwingiza kikwete ikulu.Mtandao ni kundi la kimafya ambalo linakula bila kunawa. Sasa mtu uliyekwenda shule utashindwaje kufanya critical cum critic analysis? Kama aliyemteua wote hawana taaluma except profession of lies and manipulations
 
Nnauye mbona umekimbia???
Nimemuona sasa hivi nje ya makao makuu ya ccm ofisi ndogo ya Lumumba yuko na mzee Kingunge Ngombale Mwiru wanapiga story, huku Land cruiser v 80 limepaki linamsubili Boss Nape, na anachonikosha huyu bwana hajavaa kinafki kama kingunge, Nape amepiga shati safi na Jeans na simple shoes na mkononi ana bahasha ya kaki nadhani ina posho ya lunch kwa ajili ya akina Muhadhili, Ritz & co.
kudos Nape huu ndio muda na wewe kula hadi uvimbiwe.
 
*`-0 Jamani Mbwa Jamani Mbwa... Ah! Kumbe Jibwa lenyewe Koko!
 
Alikuwa anaona urefu wa pua yake.Pole Nape.
Alianza kwa Mkwara. Wapimaji wa mambo wakasema ni Mkwara wa Nanasi ambao Nje ni Miba wakati Ndani ni utamu mtupu.

Baada ya kelele nyingiiii, baadae amejigundua kumbe amezungukwa na kundi la Wanafiki, akavunjika nguvu. Wapi Operesheni Vua gamba? Wapi Mapacha Watatu aliotuambia wamewapa siku tisini na kuwaandikia barua?

Zile kelele zooote ngumbe ni ndege mnana tu! We unacheza na Mkweree wewe! Full Unafiki!!

Rudi ukawaombe radhi akina Mzee Lowasa uliojifanya kula nao sahani moja maana ndo wanaelekea kuziba hilo ombwe la Uongozi lililopo CCM sasa. Sijui utakimbilia wapi?

Chadema ulishawakorofisha, labda ukimbilie kwa Dovutwa Fahmi.

Pole sana.
 
CCM itampoteza kisiasa huyu Bwana asipo kuwa makini, hawezekani muuza sera za KITAIFA chama apigwe stop kwenye kampeni
 
Back
Top Bottom