Wapi Lowassa?

Mheshimiwa lowassa ni dad pia kama tunaeshimu wazazi wetu kuvunjia heshima wa wengine ni ujinga tuweni na heshima si mtu unakurupuka na kuleta hoja ya viongozi wetu bila kuwa na lamaana

Kumwita mtu Fisadi si tusi na unajuaje aliyeleta mada ni mzee kuliko Lowassa. Jadili hoja si umri
 
Tumsubiri Pasco hapa kama ana la nyongeza.

Usimchokoze Mkuu Pasco, lakini tatizo la watetezi wa Lowassa wataibuka baada ya kupata maelekezo maalumu na wao kuingia 'kazini' sio wengine wanaibuka tu na kujitolea kupambana kama vita ya majimaji, wenzenu wanatumia 'bunduki' (fedha) nyie munaimba 'maji..maji' eti risasi (fedha) zitageuka maji.... Ila vita ya majimaji imetukomboa kwa kupeleka salamu kwamba, mabavu hayashindi matakwa ya wengi na kwa Tanzania mafisadi watumie tu fedha zetu walizochota na wanaopata nafasi wazichote hadi zikiisha nchi itakombolewa kutoka mikononi mwa mafisadi wanaoipelekesha nchi kusiko.
 
haya ndo baadhi ya mambo yanayotia hasira...serikali inasema haina hela wakati wengine wanazitumbua 2
 
]Unamtakia nini?[/COLOR] Kamtafute kwake Monduli.

Kama mwenyekiti wa Kamati ya Bunge inayohusika, pamoja na mambo mengine, Usalama wa Raia, AFUNGUKE kuhusu utekwaji wa Dr. Ulimboka. Tunapenda kupata maoni yake kama alivyotoa kuhusu JANGA la UKOSEFU wa AJIRA kwa VIJANA.
 
Haujui yuko Nje anatembelea Balozi zote za Tanzania kula pesa za nchi na hapo hapo kukagua balozi? wakati ni huu,

anajiamulia chochote Utamu ndio huo kwahiyo ni miezi miwili na alikuwa nje mwezi mmoja uliopita, yaani wanakula pesa za

nchi kama zao.

Sasa hela ambazo hii kamati ya ulinzi ya lowasa wanayotumia kusafiri huko nje si ingetosheleza kuwalipa madaktari? Hii serikali inasema haina uwezo lakini hela za safari za viongozi zipo.
 
Bunge letu limeangukia mikono mwa Lowasa na Chenge kirahisi kabisa. Wote wawili sasa ni wenyeviti wa kamati nyeti za mhimili huu muhimu na kwa maana hiyo wanaunda kile kinachoitwa Kamati ya Uongozi ya Bunge ambayo ina nguvu nyingi tu. Spika wetu amezingirwa kiaina na hawa jamaa wakisaidiwa kwa karibu na akina Serukamba, MomoseCheyo,...
Kwa maana hiyo wakati KIkwete anajitenga nao huku CCM na serikalini wao wamepata pa kupumulia.
 
Haya mambo hayatokei kwa bahati mbaya.Ndo style ya JK hiyo ya double standards...Kung'ata na kupuliza.Anafahamu fika nguvu za muhimili wa bunge, na hao kina EL na Chenge vijisenti, hawako hapo eti kwa bahati mbaya. Nape yeye ndo vuvuzela la "illusionist" mbele ya pazia la shows za "abra cadabra" for distraction purposes...

Huwezi kusema JK anawatenga kina EL na Vijisenti ccm, na wakati nafasi walizonazo ndani ya bunge, zinatolewa na hao hao chama tawala cha ccm chini ya usimamizi wa mwenyekiti wao!
 
Mh! Sidhani. Bunge lenyewe lina wafuasi wao wengi tu. Watu wanachaguliwa kuwa Wabunge kifisadi sana. Spika wetu mwenyewe ameipata nafasi hii kwa msaada mkubwa wa hawa jamaa. Unakumbuka Chenge alivyomng'ang'ania Sittta?
 
Hilo la kudoubt kwako, naliacha kwasababu tu ya upande wa "JK kujitenga nao kwenye serikali yake". Hata hivyo bado hilo alishasema ilikuwa "ajali ya kisiasa", na Chenge alishasema yeye mwenye vijisenti wala hana wasiwasi, na ni kweli tupu tumeshagunduwa!

Ila kwa upande wa bunge, unakubaliana na mimi kuwa kauli ya kwamba "JK anajitenga nao ccm" haina mantiki? Hizo nafasi za uongozi bungeni zinatolewa na nani?
 
Utakumbuka kwamba Lowasa na Chenge walikuwemo kwenye Cabinet ya kwanza ya Kikwete. Sasa hivi hawamo. Tena waliondoka kwa aibu. Utakumbuka pia wote wawili walikuwa kwenye CC ya CCM. Huko nako hawapo tena ingawa wameng'ang'ania kwenye NEC ya CCM. Huku kulikamata Bunge wanasaidiwa na Wabunge wenzao. Wakati mahasimu wao akina Mwakyembe, Sitta wanapelekwa serikalini wao wanajiimarisha huku Bungeni ambako Spika ni mtu wao sana tu.
 
Mkuu please usipotoshe umma, nani aliondoka kwa aibu?Ama hutaki kukumbuka kuhusu "ajali ya kisiasa"?

Waliondoka kwa shinikizo, tena EL alijiuzulu na hakufukuzwa kazi.

Ndo maana ninasema kuwa kama kweli JK angeamuwa kuwaondoa kabisa angeweza, alifunika kombe kwa kumpachika Nape kimazingaombwe ili kuwe na vuvuzela la kudanganya watu kuwa ufisadi unapigwa vita, tena kwa usanii wa "kuvuana magamba", we shahidi magamba yamegoma!

Ndo maana nikasema ni kama illusions.
 
Waliondoka kwa aibu kubwa. Kama ulimsikiliza Lowasa siku anaaga Bungeni wala hauwezi kubisha. Tayari ni historia na hakuna kitakachoibadili. Chenge yeye alimuaga bosi wake kiaina wakiwa kule China.
 
Hivi uwizi wa Richmond na kujiuzulu ndo kaondoka kwa "aibu kubwa"?

Mkuu aibu kwa kujiuzulu kama kweli ni mtuhumiwa badala ya jail?

Hotuba ya kujiuzulu ndo aibu kivipi na mtu bado ni powerfull?Hivi mbona huzungumzii kuwa JK alisema ni "Ajali ya kisiasa" Ajali toka lini ikawa aibu mkuu?

Pia aibu kivipi na wakati alisema hakuhojiwa?Hizi stori za aibu ni za watoto wa kindergaten.
 
Lowasa angefaa sana kuwarais, lakini si kwa hakati huu ambapo nchi inaliwa na chama chake, tunataka raisi ambaye hafungamani na uongozi uliopo madarakani ili atakapoanza kuchukua hatua asikumbushwe fadhila alizotendewa.
 
Hivi uwizi wa Richmond na kujiuzulu ndo kaondoka kwa "aibu kubwa"?

Mkuu aibu kwa kujiuzulu kama kweli ni mtuhumiwa badala ya jail?

Hotuba ya kujiuzulu ndo aibu kivipi na mtu bado ni powerfull?Hivi mbona huzungumzii kuwa JK alisema ni "Ajali ya kisiasa" Ajali toka lini ikawa aibu mkuu?

Pia aibu kivipi na wakati alisema hakuhojiwa?Hizi stori za aibu ni za watoto wa kindergaten.
Kile kitendo cha kuutema UwaziriMkuu uliokuwa umemnogea kiasi kile tena kwa kipindi kifupi namna ile ilikuwa ni AIBU kubwa. Ni doa kubwa kwake. Ile kitu ilim-derail sana tu. Unajua malengo ya Lowasa hayakuwa UwaziriMkuu peke yake.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom