Wapi Lowassa?

msnajo

JF-Expert Member
Jan 20, 2011
3,066
1,136
Saluti kwa wana jf wote. Wakuu ni siku nyingi sijamsikia mpambanaji EL, nini kimemkumba? Huyu bwana pamoja na makashfa yaliompata hadi kujiuzulu, alikuwa bora kuliko Pinda. Nina kila sababu ya kusema haya. Ukitaka kuamini haya, tazama hoja za Pinda mjengoni na kauli zake juu ya maswala muhimu kuhusu Taifa letu. He is very hopeless, sijui ni kigezo gani kilitumika kumpatia u-PM! Ningependa kumsikia Lowassa akisema lolote hususani kipindi hiki ambapo Taifa limekosa mwelekeo kabisa.
Ni mawazo tu wadau, karibuni kwa mjadala. Thanx.
 
Mwisho kabisa tutakuja kuanzisha ligi ya hivi

Kati ya mwizi asiyetaka wengine waibe na Mwizi wa kawaida ni yupi bora?
 
Unamtakia nini? Kamtafute kwake Monduli.

Mkuu yuko safarini akiongoza kamati yake ya Ulinzi na Usalama kutembelea balozi za Tanzania katika nchi tajiri (hakuna hata moja masikini), yeye anaongoza kamati iliyokwenda Canada, New York na Washington DC, na ameambatana na mkewe Regina Mumba Lowassa (si mbunge) na walinzi wawili na wamesafiri daraja la kwanza na yeye atakaa siku 21: wenzake wengine akiwamo Chiligati, Zungu, Anna Abdalah, Mohammed Seif Khatib watakaa siku 14 katika nchi za Ulaya na Asia, ziara ambayo imezua maswali mengi kuliko majibu. Bahati mbaya ameondoka Juni 26, siku ambayo kumetokea mambo ya aibu kwa Taifa letu. More to come, je, amekwenda kumchimba Membe? Je, amekwenda kufuatilia vijinsenti (yale madola Uswisi), ama wastaafu wamekimbia bajeti na wao kwenda kupumzika? Bejeti yao ya safari imetoka wapi? Ama ndio kuwahi kumalizia mabaki ya bajeti ya mwaka unaoisha wakwangue sizirudi?
 
Aaah, kwa hiyo sisi huku Marekani tukae mkao wa kula, eeh? Hata mkewe ni mjumbe wa kamati ya bunge. Na je, ofisi zetu za ubalozi barani Afrika nani anazitembelea?
 
Yeye kama X-Pm (sijui kama ni mstaafu ama mjiuzulu) anakuwa na stahili ya kusafiri na mkewe na walinzi kwenda nje! Sasa kwa ziara za Kibunge hilo ndio swali zito. Huko nyie nadhani tayari yupo huko. Tusaidieni kutupa vionjo, kama wanatalii ama kikazi... Lakini ingekuwa Bunge makini wangerudishwa ili waende baada ya bajeti
 
Mada ni alipo Lowassa, na mtoa mada alitarajia tuanze kumpamba maana kaondoka siku aliyotekwa Ulimboka na wanaotajwa kuhusika ni serikali, na yeye ni Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama!!! Patamu sana hapo, maana hata Pinda alipotaka kung'olewa bungeni Lowassa hakuwapo kabisa alikuwa Hanang kwenye msiba wa mzazi wa Marry Nagu..
 
yupo mbona, huwa humuoni kwenye vyombo vya habari. anajihusisha zaidi na shughuli za kijamii kama juzijuzi alikuwa kule kipawa akihamasisha harambee ya kukarabati shule za kata hiiyo
 
lowasa yupo ulaya na marekani akitumbua kodi za watz maskini huku akienda kumchimba membe katika fukuzia yao ya urais
 
Saluti kwa wana jf wote. Wakuu ni siku nyingi sijamsikia mpambanaji EL, nini kimemkumba? Huyu bwana pamoja na makashfa yaliompata hadi kujiuzulu, alikuwa bora kuliko Pinda. Nina kila sababu ya kusema haya. Ukitaka kuamini haya, tazama hoja za Pinda mjengoni na kauli zake juu ya maswala muhimu kuhusu Taifa letu. He is very hopeless, sijui ni kigezo gani kilitumika kumpatia u-PM! Ningependa kumsikia Lowassa akisema lolote hususani kipindi hiki ambapo Taifa limekosa mwelekeo kabisa.
Ni mawazo tu wadau, karibuni kwa mjadala. Thanx.

Haujui yuko Nje anatembelea Balozi zote za Tanzania kula pesa za nchi na hapo hapo kukagua balozi? wakati ni huu,

anajiamulia chochote Utamu ndio huo kwahiyo ni miezi miwili na alikuwa nje mwezi mmoja uliopita, yaani wanakula pesa za

nchi kama zao.
 
BORA YA LOWASA KULIKO HUYU WA SASA. Edward jembe sana! Ngoja tungoje kipyenga cha 2015 cha urais wa nchi. Nahisi ntakuwa kampeni menej wake.
 
Saluti kwa wana jf wote. Wakuu ni siku nyingi sijamsikia mpambanaji EL, nini kimemkumba? Huyu bwana pamoja na makashfa yaliompata hadi kujiuzulu, alikuwa bora kuliko Pinda. Nina kila sababu ya kusema haya. Ukitaka kuamini haya, tazama hoja za Pinda mjengoni na kauli zake juu ya maswala muhimu kuhusu Taifa letu. He is very hopeless, sijui ni kigezo gani kilitumika kumpatia u-PM! Ningependa kumsikia Lowassa akisema lolote hususani kipindi hiki ambapo Taifa limekosa mwelekeo kabisa.
Ni mawazo tu wadau, karibuni kwa mjadala. Thanx.

kamuulize mkewe
 
kamuulize mkewe

Nashukuru mkuu. Huu nao ni mchango wako wa mawazo kwenye hii thread. Mchango ni mchango hata kama ni finyu kiasi gani! Ila kama GT sio lazima upokee kila mawazo. Asante kwa kushiriki kutoa mawazo.
 
nchi iko pabaya,pinda kapinda kweli amepwaya hajulikani kama ni pm,afadhali el jamani,alikuwa na uwezo wa kutoa maamuz magumu,ni waziri mkuu pekee aliyekuwa anamfuatia edward moringe sokoine kwa uchapa kazi
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom