Wapi John Dilinga Matlou

binafsi ni shabiki wake long time,kwa sasa amekuwa mtu mzima mkuu,anafanya shughuli zake binafsi ila muziki upo kwenye damu akipata nafasi hata kidogo tu anashusha burudani ya nguvu.
 
pamoja na umri kwenda kidogo lakini bado yuko vizuri sana kiuwezo wa kutangaza na kupiga muziki ila inasemekana haimlipi kivile na anafanya kwa kupenda tu muziki na ndio ameamua kuzama kwenye issue zingine.
 
John Mkimbizi anapiga business zake, kuna wakati alikuwa pale times Fm lakini ghafla akabwaga mzigo!
Ni Moja kati ya maDj wakali sana Bongo wakati fulani alikuwa na akina DJ Rico na kundi lao la the powerfull four.
Nakumbuka nimecheza Disco lake pale Ukumbi wa shimoni-Morogoro Hotel!
 
mimi nimeruka kwanja lake sana tu pale bilicanus miaka ya tisini mwishoni na vipindi vyake vingi hasa kipindi bora cha r&b na hiphop kuwahi tokea tz cha the cruz pale East africa radio
 
Mkatabaka wake Times fm uliisha,anafanya mambo yake kwa sasa,ila soon ataendelea na shughuli za u dj ktk kumbi za burudani..
Ni Dj mkali pekee aliyetoa albam collection iliyojaa scrtch za ujazo..KALI ZA JD! Unakumbuka?
 
huyu jamaa ni entertainer acha mchezo,jd wa redioni sio wa club!anaipenda kazi yake kutoka damuni na ana displine ya kazi haswa,pamoja na kazi ya u dj hatumii kilevi! Nafikiri imemsaidia kudumu kwenye kiwango chake
 
Big ups JD, kuna wakati pia alikuwa anakwenda kupiga pale triple A Arusha, he was trying to promote the club
 
Dah! Umenikumbusha huyu jamaa alitaka kusababisha maafa Mzumbe University mwaka 2002 kwa mautundu yake. Kwa wale wanaokumbuka ilikuwa ni welcome 1st year!
 
aliwahi kuitwa kutoa burudani kwa wanajeshi kambi moja ilikuwa balaa tupu kwa maafisa wa jeshi mpaka wakataka disko lisizimwe!
 
huyu jamaa arudi redioni bana labda tutaanza tena kusikiliza radio hasa entertainment programs,hawa watoto wa siku hizi sijui B kumi na ngapi wanaboa tu,nafuu Ml Chriss kule Choice Fm nasikiliza kidogo.
 
Msimsahau dj majey a.k.a majizo.hata yeye alikuwa noma,sijui yuko wapi!!
 
Huyu jamaa nilikuwa namkubali sana EA radio...one of those guys by the time nilidhani ni Mwamerika the way anashusha Lugha duhh!
 
DJ JD nakumbuka mara ya mwisho nilimuona Mwanza mwishoni mwa Mwaka jana alialikwa kupiga show Stone Club Mwanza Hotel.
 
jamaa anaujua mziki na anapenda watu wajue nini anakijua
 
Enzi zile wasanii walikuwa wanapanga foleni pale Ipp kupeleka CD zao kwake,walikuwa hawataki kuziacha pale tu ili apige nyimbo zao,wengine inasemekana hadi walikuwa wanavizia nje ya geti akitoka wampe CD! The cruz EA radio was hot!
 
huwa nasikitika sana baadhi ya madj maarufu sana wa zamani wanapiga muziki kwenye mabaa ya mitaani tena kwa ujira mdogo sana na wakionekana wamechoka kabisa,mmoja yuko palee fairway tegeta,nafikiri mnamfahamu!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom