Wapenzi wa Simba Sports Club nao wasusie IPP Media?

Mimi sijasusa, ila automatically nimejikuta siangalii kabisa ITV kwa sababu ya viwango vyao vibovu, vipindi hovyo na watangazaji wenye uelewa na upeo mdogo kabisa, inaboa hata kuangalia ule upuuzi, TBC1 kiwango kwa sasa.
Magazeti yao nlijikuta tu baada ya Magazeti yalioenda shule katika uchambuzi kama Mwananchi na Mwanaspoti kuingia.Zamani nlikuwa sikosi Lete Raha, lakini these days hata sijui kama bado lipo.
 
Natofautiana nanyi katika kuuelezea ukweli juu ya jambo hili....
si vyombo vyote vya IPP vimegomea ama kususia habari za Simba SC, NIJUACHO MIMI ni kuwa , Radi One na ITV ndio waliosusia kutangaza habari za mnyama. Nipashe na The Gurdian wao wanaendelea kama kawa, maana hata Nipashe la leo ndio kwaanza linafika hapa Iringa lina habari yenye Kichwa cha habari Phiri : Kipigo cha Zimbambwe Chawajia Yanga, HABARI hii ipo ukurasa wa 23 wa gazeti la nipashe la Tarehe 22,Machi 2010.
ninachotaka kusema ni kuwa mjadala ujiegemeze kwenye ukweli na sio Tetesi....na ukweli wenyewe ni kuwa Radio One na ITV Wamesusia habari za mnyama na si vyombo vyote vya IPP......nawatalia mjadala mwema....Iringa ni baridi kiasi.
 
"Timu ya Twiga Stars IMEWEZA kupata ajali na mchezaji mmoja AMEWEZA kujeruhiwa" - By Isack Gamba.....Kipindi cha JARIDA LA MICHEZO Jumamosi 20/3/2010

Too low.

Mtu mzima hajui jinsi ya kuunda sentensi na matumiza ya maneno. I changed channel hapo hapo baada ya hiyo sentensi
 
"Timu ya Twiga Stars IMEWEZA kupata ajali na mchezaji mmoja AMEWEZA kujeruhiwa" - By Isack Gamba.....Kipindi cha JARIDA LA MICHEZO Jumamosi 20/3/2010

Too low.

Mtu mzima hajui jinsi ya kuunda sentensi na matumiza ya maneno. I changed channel hapo hapo baada ya hiyo sentensi

Ni aibu! Hao ndio wanajidai kususia kutangaza habari za wakali SIMBA! Ni afadhali waendelee kususia milele ili tusahau kabisa kwamba kuna kitu kinaitwa Radio One au ITV.
 
Ni aibu! Hao ndio wanajidai kususia kutangaza habari za wakali SIMBA! Ni afadhali waendelee kususia milele ili tusahau kabisa kwamba kuna kitu kinaitwa Radio One au ITV.
ITV na Radio one wanakosa watangazaji wenye mawazo ya kisasa, wenye uwezo wakubuni vipindi vya micheza katika namna ya kumvutia msikilizaji, kina Gamba, kitenge na Rweyeyunga wamekuta vipindi vya michezo vilivyobunia na kusanifiwa na kina Abdalah Majura, Abuubakary Lyongo, Mikidadi Mahamudu.....wameshindwa kuvitengeneza vikaw vipindi maridadi kwa wasikilizaji wakileo.
Gamba kwangu nimejua kuwa ni mchoovu sikunyingi tu, uwezo wake wakutangaza uko chini ya kiwango, kwakweli sidhani kama wataifikisha ITV/Radio one mbali.
kuacha kutangazia Simba habari zao, hapo ndipo palipoongezea wigo waujinga wa watangazaji na management ya vituo hivyo,.
 
..simba sports ilikuwapo na itakuwepo..

ni kweli mengi ana bifu na simba kwa sababu walimuambia kweli kuwa kama anataka kuonesha meshi zao live ...basi alipie kwa kuwa naye analipwa...mengi akagoma na kuamua kuwawekea simba vikwazo....

sio simba tu hata baadhi ya wanasiasa asioelewana nao huwa hawaoneshi kwenye tv zake..ndio maana naunga sheria ya kudhibiti vyombo kama IPP kwani iwapo wakigombana na mtu ..inakuwa vikwazo ..basi ni hatari iwapo akiachiwa ukiritimba..
 
Hakuna haja ya kusumbua kichwa kufikiria vyombo vya IPP na coverage ya Simba,after all kuna media nyingi zenye akili kama Star TV ambao nao walifanyiwa vurugu na Simba lakini wakamaintain profession.Tabia za kususa zimezoeleka IPP si unakumbuka waliwahi kuisusa Yanga kisa Manji kuwa mfadhili wa klabu hiyo?Hakuna cha kupoteza IPP waendelee na ukanjanja wao Simba tuendeleze mapambano hakuna wanachoathiri kwetu.
...Nachelea kusema kuwa yale aliyokuwa akiponda Masanja wa Ze Comedy ndio yanathibitika hapa sasa. Hivi inawezekana vipi mtu mwenye pesa zako na unafanya biashara za uhakika katika media indistry eti mnawekeana bifu na Simba? Uswahili mtupu...Iko siku wenyewe watarudi kundini na watarusha habari za wekundu wa Msimbazi na tutawazodoa tu..!!!
 
Back
Top Bottom