Wapenda soka amkeni

Jecha A. Makame

New Member
Jan 23, 2011
1
0
Ndugu zangu wapenda soka hasa wale wanachama wa Simba na Yanga inatubidi tuwe makini sana katika maamuzi tunayoyafikia pale ambapo tunagusa maendeleo ya vilabu vyetu. mimi kwanza natoa sifa kubwa sana kwa wakurugenzi watendaji wa mtandao wa jamii forum kwa kutuwezesha kutumia mawasiliano haya rahisi ya kuwasiliana kwa njia ya mtandao.
Mimi naitwa Jecha Abdalah Makame naishi unguja maeneo ya Bububu, lakini pia ni mwanachama wa Yanga. Tukio kubwa ambalo nimelishuhudia mimi mwemnyewe kwa macho yangu ni ule mchezo wa Yanga na Simba ambapo katika mchezo huo Yanga ilifungwa goli mbili, cha ajabu zaidi ni kuona mmoja wa viongozi wangu tena wa cheo cha juu kabisa (Makamu wa mwenyekiti) yeye alikuja Zanzibar na alipofika tu alielekea kulikokuwa na kambi ya Yanga na kwa bahati mbaya sana kwake hakujua watu waliokuwa hapo hivyo ikawa bahati nzuri kwangu kuwepo pale na kujionea yale yaliyojitokeza. Bwana mkubwa huyu alipofika tu alimuuliza mmoja wa walinzi wa kambi mahali alipo mwanyekiti naye alimjibu kwamba ametoka na Mdhamini pamoja na Mbunge wa Temeke Ndg. Abass Z. Mtemvu, wallah alitukana matusi ya nguoni ya mwanamke akimtuhumu mwenyekiti wake kwamba kwanini aende na Zuberi Mtemvu. unajua siku hiyo ndipo nilipojua kuwa kumbe ustarabu si kuvaa nguo nzuri maana kamwe sikutarajia mtu kama Mosha kumtukana Mwenyekiti wake na nikasema je hata huko Dar Es Salaam ndivyo mnavyotukanana. Naomba mjadala huu uwekwe hadharani ili watu mbalimbali waujadili na lengo langu hapa ni kutengeneza maadili katika kila nyanja za kijamii.

Ni mimi J.A.Makame
 
Jitahidi ujijengee khulka ya kumuomba Muumba akujaalie HEKIMA, BUSARA, SUBRA, NA UDHIBITI NDIMI. Matusi ni sehemu ya kumkasirisha Muumba hivyo jiepushe na matumizi bora ya lugha na uwe ni kiumbe mwenye KAULI NJEMA.
Kwetu huku Bara wigo mpana wa mambo kadha wa kadha ya kidunia, kiukuaji, kimalezi bali pia kimjumuiko. Hivyo kuna baadhi wapo wenye mlengo huo wa khulka lakini tupo pia tuliostaarabika na tunaojizuia kwa ndimi zetu.
YANGA & SIMBA...huwa hakuna lugha njema kwa pande zote hizo, mifano ni kuangalia hali ya migogoro inayojiri kila mara kwa vilabu hivyo viwili vya soka hapa nchini. Hiyo ni ishara tosha kuwa ukiwakaribia hao...basi nawe uwe kidooogo ni mithili ya MWENDAWAZIMU.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom