urambo enzi hizo (1951)!
View attachment 40603iyo staili ya nywele ya uyo jamaa wa kushoto ilikuwa inaitwa "way" yaani nywele ziachane kama za mzungu vile!
View attachment 40604hata enzi hizo miembe ilikuwa mingi. Waafrica wanachimbua tairi wakati wazungu wameshika mikono. Kama inavyokuwa sasa (historia inajirudia)!
Mwaka 1951 tulikuwa hivi, miaka 60 baadae hata kiberenge hatuna!! Picha kama hizi zinakufanya una sympathise na watu wanaosema bora mkoloni angeendelea kututawala.View attachment 40643Stesheni ya treni ya Urambo (1951). Asali kwa wingii sehemu hizo!!!
Mambo land Rover 109 hilo
Hakika wa Tz wengi ndivyo tulivyo.Ndugu yangu hii picha ya stesheni karibu initoe machozi. Hakuna kilichobadilika hata rangi ya jengo ni ile ile aliyoiacha mkoloni. Ile barabara ya kuelekea sokoni nayo ni hivyo hivyo. Nasikia uchungu sana kuona kwetu hakukui hakubadiliki. Kuna mwana jamii mmoja baada ya uchaguzi wa Igunga aliandika anaona aibu kuzaliwa mnyamwezi, mimi najihisi vibaya sana kuona Urambo yetu iko vile miaka yote, watu wanaondoka hawarudi , tena wanaume wa urambo ndio kabisaa tukiondoka huko hata kurudi kuoa wa kwetu hatutaki, tunazidi kupotea
Ndugu yangu hii picha ya stesheni karibu initoe machozi. Hakuna kilichobadilika hata rangi ya jengo ni ile ile aliyoiacha mkoloni. Ile barabara ya kuelekea sokoni nayo ni hivyo hivyo. Nasikia uchungu sana kuona kwetu hakukui hakubadiliki. Kuna mwana jamii mmoja baada ya uchaguzi wa Igunga aliandika anaona aibu kuzaliwa mnyamwezi, mimi najihisi vibaya sana kuona Urambo yetu iko vile miaka yote, watu wanaondoka hawarudi , tena wanaume wa urambo ndio kabisaa tukiondoka huko hata kurudi kuoa wa kwetu hatutaki, tunazidi kupotea
Hapo utagundua kuna maeneo Tanzania haipigia hatua. Mwaka jana nilipita hapo stesheni yaani panafanana hivihivi. Hakuna mabadiliko yeyote.
Hata ndani bado mambo yaleyale ya zamani hata compyuta hamna