Wanyama na Rangi

Judgement

JF-Expert Member
Nov 13, 2011
10,327
4,776
Wadau,
Ni imani yangu hapa Jf tuko members wa aina na wa fani tofautitofauti.
Kwa faida ya fani zenu ninawaomba sana mnitendee haki, kunijuza hili.
Hawa wanyama mf. Ng'ombe , Mbuzi , Kondoo , Paka, na hasa husussan Mbwa mnyama ambae inasadikika ni mwenye kuwa na utambuzi wa akili ya hali ya juu, kuwazidi wanyama wengi.
Je ? Wanyama hawa wanao uwezo wa kutambua hii ni nguo ya rangi nyekundu, ile ni gari ya njano, au akajua leo mmiliki wake kavaa nguo za Kijani.
Tumkichukulia sana Mbwa anao utambuzi huo ? Wa kupambanua rangi? Majibu yenye ushahidi wa kisayansi nitayapa mapokeo makubwa.
Nawasilisha.
 
Mbwa, kama baadhi ya vinyama, hawatambui rangi. Ila kuna sauti mbwa anasikia na binadamu hatuwezi kusikia. Mungu aliwapa viumbe wote what they need to survive in this world.
 
Mi naomba kujua umefikiria nini hadi kuuliza hili swali?

Kilichopelekea nifikirie kulileta hili, nadhani hata wewe kuna wkt inakutokea uka'create Thread accordingly enviroment around.
Tulikua tumekaa sehemu mimi na wenzangu wa4, eneo ambalo tunakaa mara kwa mara ku'buz time.
Katika eneo hilo hua kuna paka wengi wanaozungukazunguka, na inapofika saa 12 Mbwa wa hapo hufunguliwa.
Mbwa wakishafunguliwa Paka hukosa amani kwn haipiti muda Paka wanakurupushwa.
Hasa yupo Mbwa mweupe dume mtemi kwelikwl, yeye ndiyo hua hakubali kumuona Paka upeo wa macho yake.
Leo kuna Paka mmoja wa Rangi michirizi kama njano au kahawia hivi, akamdindia mtemi huyo Mbwa. Paka yule alijitunisha akapanda juu karibu akaribie urefu wa Mbwa, (wakati huo sisi wote tukawa makini kuangalia ligi hiyo )
Kilichofata wakaungurumiana kisha mtemi Mbwa ndiyo alianza kuondoka, na akatambaa.
Kupita kama nusu saa hivi, Mbwa mtemi akarudi tena eneo hilohilo palipotaka kutokea ugomvi.
Mara hii akamkuta Paka mweusi.
Akamvagaa Paka black akaumwaga.
Hapo ndy sisi tukaanza kujadili, baadhi yetu wakawa wakisema yule Mbwa alidhani ni Paka yule wa kwanza, wengine wakakataa, kua hapana Mbwa ana utambuzi wa kutambua rangi kua yule Paka wa kwnz ni rangi nyingine na huyu rangi nyingine.
Inshort pale hatukupata ufumbuzi which is which !
Ndiyo nikashawishika nililete huku kwa watu waliokwenda Shule .
 
Mbwa ana uwezo wa kuona rangi nyeupe na nyeusi tu, hakuna zaidi ya hapo
 
Mbwa, kama baadhi ya vinyama, hawatambui rangi. Ila kuna sauti mbwa anasikia na binadamu hatuwezi kusikia. Mungu aliwapa viumbe wote what they need to survive in this world.
Respect mkuu...sikujua hili
 
  • Thanks
Reactions: Taz
niliwahi kusikia kuwa eti..wanyama kama ng'ombe na mbuzi wanatambua rangi moja tu ya kijani..hasa katika kula nyasi...na ndio maana muda mwingine hao wanyama wanakula karatasi au nailoni..sina uhakika..mwenye kujua atusaidie na hili
 
ngo'mbe anajua hata nyekundu....sijui aliijuaje......
lakini....nitajuaje kama mnyama ametambua rangi.....
au na wao wana majina yao ya rangi......?

ngo'mbe anajua hata nyekundu....sijui aliijuaje......
lakini....nitajuaje kama mnyama ametambua rangi.....
au na wao wana majina yao ya rangi......?

Dah..umenikumbusha ule mchezo wa ng'ombe kule zanzibar,na spain...unatega kitambaa chekundu..kisha ng'ombe anakuja kasi wewe unamkwepa....thanx..kwa kuniongezea ufahamu
 
Mbwa hawana uwezo wa kutofautisha rangi. Wanaona rangi nyeusi na nyeupe tu. Kama ktu ni cha rangi nyeupe ataona ni cheupe, kama ni cha rangi nyingne ataona ni cheusi. Kuhusu yule paka mweusi, mbwa alimtambua kuwa ni paka mwngne kwa kutumia harufu, hata kama yule paka wa kwanza angekua na pacha wake, mbwa alikua na uwezo wa kutambua kua ni mwingne.
Mbwa pia ana uwezo mkubwa sana wa kusikia, kwanza angalia tu masikio yake, pinna ni kubwa hvyo kumpa uwezo mkubwa wa kukusanya mawimbi ya sauti.
 
Preta, N'gombe hajui nyekundu. Wale wanao chezea n'gobe in arenas (Toreadors) wanatumia kitambaa chekundu kwa kuficha rangi ya damu ya n'gombe. Kinacho wakera n'gobe pale ni kule kutikisa kitambaa, wala sio rangi nyekundu.
Alafu kusema kua wanaona rangi ya kijani pia sio kweli. wanaona tu black, white and all the grey variations in between.
tukirudi kwa mtoa mada, lazima yule mbwa alijua kua sio yule paka wa mwanzo sababu huyo wa njano ataonekana light grey na huyo mweusi ni black.
ngo'mbe anajua hata nyekundu....sijui aliijuaje......
lakini....nitajuaje kama mnyama ametambua rangi.....
au na wao wana majina yao ya rangi......?

ngo'mbe anajua hata nyekundu....sijui aliijuaje......
lakini....nitajuaje kama mnyama ametambua rangi.....
au na wao wana majina yao ya rangi......?

Pretta, hichi ulichokisema hapa ndiyo cha kufanyia utafiti, mimi nina uthibitisho kabisa kua Ng'ombe hapatani na Red ! Na kama kuna anaebisha ktk hili avae nguo Nyekundu then akavinjari maeneo karibu na Ng'ombe aone mziki wake !
Hata wale wanaocheza Bull game , game huanzishwa kwa Ng'ombe kuoneshwa kitambaa nyekundu . Lazima ipo relation isiyo ya kawaida b'twin Ng'ombe na Red coular.
 
Preta, N'gombe hajui nyekundu. Wale wanao chezea n'gobe in arenas (Toreadors) wanatumia kitambaa chekundu kwa kuficha rangi ya damu ya n'gombe. Kinacho wakera n'gobe pale ni kule kutikisa kitambaa, wala sio rangi nyekundu.
Alafu kusema kua wanaona rangi ya kijani pia sio kweli. wanaona tu black, white and all the grey variations in between.
tukirudi kwa mtoa mada, lazima yule mbwa alijua kua sio yule paka wa mwanzo sababu huyo wa njano ataonekana light grey na huyo mweusi ni black.

Mkubwa ! Nashkuru kwa mchango huu, na bado naendeleza tafiti
 
Similar Discussions

0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom