Wanyama mikumi wamewekewa matuta sembuse wanafunzi jamani???

Pdidy

JF-Expert Member
Nov 22, 2007
50,956
22,138
Hili bado alijaniingia akilini,....yaani hii nchi imejaa ma bogasi serikalini
mpaka watoto wanaenda kuandamamana na kutuonyesha nini cha kufanya
huu ni ujinga ama upotevu wa ufahamu...inashangaza wanyama wa pale mikumi walikufa ovyo gafla leo hii tunapita kwenye matuta...hawa watoto wameuwawa mpaka majuzi wanaamua kuwaonyesha wapuuzi wa lio serikalini nini cha kufanya...je watu kama hao wanaitaji mshahara kweli??kwa nini tusipeleke pesa zao za mishahara kwenye ada za watoto creative kama hawa

JE WANYAMA NI BORA KULIO BINADAMU???
 
Hii nchi si mpaka uandamane au Ugome ndo utekelezewe unachotaka!! mi kinacho nshangaza ni pale ukishagoma viongozi wanakuja na wimbo wa mnachofanya ni against the law so why not come and discuss in my office!! yaani upupu mtupu! May be pale mikumi kabla ya matuta kuwekwa wanyama noa walilala barabarani maana "Action speakes louder than words"
 
Mimi naomba niende hatua moja zaidi mbele, hizi ajali za barabarani sasa zimekuwa tishio. Kila barabara inapokuwa nzuri na madereva wetu ndio wanapata kichaa, ila matuta naona ni hatua ya kurudi nyuma hasa ukizingatia hili ni tatizo la maeneo yate kama si nchi nzima. We tazama barabara inapofunguliwa, wananchi wanashangilia kuona wamepata ukombozi lakini baada ya muda mfupi kilio cha watoto kugongwa na magari kutokana na kasi ya madereva. Wazo langu tujaribu kuihamasisha serikali au hata sisi jamii tujenge MADARAJA YA KUVUKIA BARABARA. Naamni tukiamua tunaweza hata kuchangishana kama vile kujenga madarasa, ili kujinusuru na hawa wendawazimu wanaokaa nyuma ya usukani. Maisha ni yetu, tusipofanya jitihada sisi wenyewe ya kuyalinda wale tuliowapa dhamana hawatajali.
 
ila nchi hii inaboa sana

TUAME NDUGU YANGU??
 
Back
Top Bottom